Kujiandaa kwa Ajili ya Uinjilisti na Ushuhudiaji
Utangulizi: Je, umewahi kuwa na maamuzi ya haraka kufanya jambo fulani? Je, maamuzi hayo yalikuwa na matokeo gani? Mara kwa mara, maamuzi yanayofanywa dakika za mwisho sio mazuri kwa sababu yanatupatia muda mfupi wa kujiandaa. Tunapokuwa tunakwenda kwenye matembezi marefu, inabidi tuangalie aina ya mavazi ya kuvaa, aina ya viatu tutakavyovihitaji, na pia kama tutahitaji kitu cha kuzuia wadudu au jua. Yumkini pia tukahitaji kifaa kinachotumika kuonyesha uelekeo (GPS)! Kama tuna kazi ya mradi, tutatafuta zana na vifaa vinavyohitajika ili kukamilisha kazi hiyo. Tukiamua kuwa na taaluma fulani, basi tutakwenda shule ili kujiandaa kuwa na taaluma hiyo. Je, ushuhudiaji na uinjilisti una tofauti yoyote? Tukitaka kuwa na ufanisi zaidi, basi tunahitajika kujiandaa. Waefeso 6 ni sura nzuri sana kuhusu jinsi ya kujiandaa. Lakini, juma hili tutaangalia njia nyingine za jinsi ya kujiandaa. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Wavuvi wa Watu
- Soma Marko 1:14-18. Kama wewe ungekuwa Yesu, na muda ulikuwa umetimia wa kuhubiri habari njema ambayo ilikuwa imekuleta hapa duniani, je, ungewachagua hawa wawili? Je, wanaonekana kama wapo “tayari?”
- Je, vipengele chanya (vizuri) vya kuwachagua wavuvi ni vipi? (Kwa mantiki ya ujumla, walikuwa kwenye shughuli ya “uvuvi.” Pia walikuwa radhi.)
- Je, vipengele hasi (visivyo vizuri) vya kuwachagua wavuvi ni vipi? (Hakuna mavunzo ya kiteolojia. Walionekana kutofahamu chochote kuhusiana na shughuli ya kufanya uinjilisti.)
- Je, Yesu aliahidi kuwatendea nini? (Kama wakimfuata, “atawafanya kuwa wavuvi wa watu.”)
- Je, historia ya kisa hiki inatupa tumaini gani? (Huko nyuma tulijadili suala la karama za asili na karama za roho, lakini hii inatuonyesha kuwa Yesu anaweza kutufundisha kwa ajili ya ushuhudiaji na uinjilisti. Yesu atatuandaa.)
- Soma Marko 1:14-18. Kama wewe ungekuwa Yesu, na muda ulikuwa umetimia wa kuhubiri habari njema ambayo ilikuwa imekuleta hapa duniani, je, ungewachagua hawa wawili? Je, wanaonekana kama wapo “tayari?”
- Mafunzo ya Mtazamo Mpana
- Soma Mathayo 14:14-15. Je, unaweza kutoa pendekezo kama hilo? Hii ni sawa na kuwa mtu mwenye kufanya mambo kiuhalisia/kivitendo, sawa? Huyu ni mtu anayejali sana uhalisia. Mtu ambaye hajali sana mambo ya kimbingu kiasi kwamba hana umuhimu wowote duniani (hapa ni katika kujaribu kuelezea kwa ufupi msemo ulio maarufu). Sawa?
- Je, kuna ubaya wowote na hili pendekezo? (Hapana. Linaleta mantiki.)
- Soma Mathayo 14:16. Kumbuka kwamba Yesu aliwaambia kuwa atawafanya kuwa wavuvi wa watu. Je, haya ni mafunzo ya uvuvi wa watu – kutakiwa kuchukua sehemu ya jukumu la kuwasaidia watu wengine?
- Soma Mathayo 14:17. Je, haya ni mafunzo ya uvuvi wa watu – kutakiwa kuwa mtu mwenye kuchukulia mambo kimantiki na kutafakari kwa kina?
- Angalia tena jibu walilolitoa wanafunzi kwa Yesu. Je, “wanamfuata Yesu?” (Kumbuka, Yesu alisema “nifuateni” nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Hawamfuati Yesu, wanamuuliza Yesu maswali.)
- Soma Mathayo 14:18-21. Je, ni somo gani walilopaswa kujifunza wanafunzi kuhusu kuwa wavuvi wa watu? (Miujiza ya Yesu inajielekeza kwenye utekelezaji wa vitu kivitendo. Kimantiki kabisa Yesu angeweza kuwaruhusu makutano waende zao kula. Lakini, Mungu anatutia moyo “tufikiri kwa mapana zaidi” – hata pale yanapokuja masuala ya utekelezaji wa kivitendo ambayo hayahitajiki kwa umuhimu mkubwa, lakini ambayo yanasaidia kuuendeleza Ufalme wa Mungu.)
- Soma Mathayo 14:14-15. Je, unaweza kutoa pendekezo kama hilo? Hii ni sawa na kuwa mtu mwenye kufanya mambo kiuhalisia/kivitendo, sawa? Huyu ni mtu anayejali sana uhalisia. Mtu ambaye hajali sana mambo ya kimbingu kiasi kwamba hana umuhimu wowote duniani (hapa ni katika kujaribu kuelezea kwa ufupi msemo ulio maarufu). Sawa?
- . Kufanya Suala la Msingi kuwa Suala la Msingi
- Hebu tuendelee na mafunzo! Soma Mathayo 15:1-2. Tumaini langu ni kuwa wanafunzi walinawa mikono kabla hawajaanza kushughulika na mkate na samaki! Je, unakubaliana na viongozi wa kidini?
- Soma Mathayo 15:3-6. Je, umewahi kufanya kile anachoonekana kukifanya Yesu? Mtu anakukosoa na katika kumjibu unawakosoa kwa kile wanachokifanya kimakosa?
- Je, umewahi kusikia kuwa makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sahihi?
- Je, una utetezi wowote kwa ajili ya utetezi wa Yesu? (Suala la kunawa mikono ni utamaduni wa wanadamu. Kushindwa kuwasaidia wazazi wako ni ukiukaji wa sheria ya Mungu - Amri Kumi. Yesu anasema kuwa unawakosoa wafuasi wangu juu ya vitu vidogo, wakati ambapo unawafundisha watu kukiuka Amri Kumi.)
- Soma Mathayo 15:7-11. Je, ni somo gani analolifundisha Yesu kwa wale wanaotaka kuwa wavuvi wa watu? (Kwamba hatupaswi kuburuzwa na mafundisho ya wanadamu. Tunahitajika kuyashika matakwa ya Mungu mara zote.)
- Je, tunatimizaje hilo? (Yesu anafundisha kuwa hili ni suala la “moyo.” Moyo kwa ajili ya watu wengine hauburuzwi na matakwa ya kidini yaliyoanzishwa na wanadamu.)
- Soma Mathayo 15:12-14. Kwa nini wanafunzi walijali kuhusu kuwachukiza watu? (Sipendi kuwachukiza watu. Kwa ujumla Yesu alikuwa kinyume kabisa na uchukizaji (Mathayo 17:27). Lakini, mtu anapowaongoza watu wengine upotevuni, unaweza (na unapaswa) kuachana nao. Samaki wengine hurudishwa majini kwa sababu ni hatari kwa samaki wengine waliomo kwenye mtumbwi.)
- Soma Mathayo 15:15-20. Petro anamwomba Yesu atoe ufafanuzi wa suala hili, na Yesu anasema, “Mu mabubu (hamna akili) kwa kiasi gani?” Je, kuna somo lolote katika hili kwa ajili yetu? (Kitu tunachotaka kijifunza hivi punde sio suala linalokaribiana na teolojia. Kama hukubaliani na hitimisho la Yesu, basi wewe ni mpumbavu.)
- Je, nini kinapaswa kuwa lengo la juhudi zetu kwenye uinjilisti wetu? (Akili.)
- Kwa nini? (Ndio chanzo cha uovu maishani mwetu.)
- Kwa nini unadhani kuwa kitu cha kwanza anachokiorodhesha Yesu ni “mawazo maovu?” (Mawazo yetu ndio msingi wa matendo yetu maovu.)
- Je, utafanya kitu gani katika kuilenga akili? (Tunatakiwa kufanyia kazi suala la kubadili mitazamo/mawazo, sio kubadili mwonekano wa nje. Lengo letu kuu ni kubadili mioyo, sio kubadili vyakula au mavazi. Badiliko la moyo huleta mabadiliko ya nje.)
- Je, nini kinapaswa kuwa lengo la juhudi zetu kwenye uinjilisti wetu? (Akili.)
- Sehemu/Kijenzi cha Imani
- Soma Mathayo 17:14-16. Je, tuna taarifa gani kuhusu juhudi za uinjilisti za wanafunzi wa Yesu? (Walishindwa! Wanafunzi walijaribu kumponya yule kijana (mvulana), lakini walishindwa.)
- Soma Mathayo 17:17-18. Je, nani anayeelezewa hapa? Baba? Kijana? Wanafunzi? (Nadhani ni wanafunzi.)
- Soma Mathayo 17:19. Kwa nini wanafunzi walimwendea Yesu kwa faragha? (Hii inathibitisha kuwa wao ndio walikuwa walengwa wa maneno ya Yesu. Walimwendea kwa faragha kwa sababu hawakuelewa kuwa ni kwa nini walishindwa. Hawakuelewa ni kwa jinsi gani maneno ya Yesu yaliwahusu. Hawakutaka kudhalilishwa/kuaibishwa hadharani kwa mara nyingine tena.)
- Soma Mathayo 17:20. Tatizo lilikuwa ni nini? (Upungufu wa imani.)
- Je, tunaweza kulinganishaje hili na kisa chetu cha awali – kile kilichohusu kuwalisha makutano? (Yesu anaatutaka tuwe na imani, ya kwamba hakuna ambacho hakitawezekana kwetu. Kiasi kidogo tu cha imani kinaweza kufanya mambo makubwa. Kushindwa kwetu kuwa na imani kunatuonyesha kuwa kizazi “kisichoamini na kipotovu.”)
- Je, tuwianisheje maelekezo haya na matamanio yetu ya kuyatenda mapenzi ya Mungu? Je, kwa kawaida huwa tunasema, mtu anapokuwa ameshindikana kuponywa, “sio mapenzi ya Mungu?” Hatusemi kuwa, “Sisi ni kizazi kiovu na kipotovu kinachopungukiwa hata imani ya punje ya haladari – hiyo ndio sababu mtu huyu alifariki.” Je, tuseme kauli ipi?
- Je, panaweza kuwepo na shaka yoyote kuhusu mapenzi ya Mungu kwenye hali ya huyu kijana?
- Soma Yohana 15:5-7. Kwa mara nyingine tena Yesu anaahidi kutupatia tutakachomwomba, kama tukitimiza masharti fulani. Je, Yesu anayaelezeaje masharti? (Kusalia ndani ya Yesu huelezea imani. Tunatakiwa kuunganishwa na Yesu. Muungano huu unapaswa kutupatia utambuzi wa mapenzi yake.)
- Mara zote huwa ninakuwa na wasiwasi tunapotumia maneno kama vile “kuunganishwa” na Yesu. Kama suala la kiuhalisia (kivitendo) je, hiyo inamaanisha nini? Soma Yohana 15:26. Muunganiko huu ni uwepo wa “Msaidizi” - Roho Mtakatifu.)
- Je, maisha yako yamejawa Roho Mtakatifu? Je, unatafuta uongozi wa Roho Mtakatifu kwa yule anayetakiwa kuponywa?
- Rafiki, tunamhitaji Yesu kutufanya kuwa wavuvi wa watu. Sehemu ya mafunzo hayo ni kutafakari kwa mtazamo mpana, kuelewa na kujikita kwenye kile kilicho muhimu, na kushikilia imani thabiti iliyounganishwa na Yesu kupitia kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atatupatia uwezo na maelekezo kutenda mambo makubwa na ya muhimu katika kuuendeleza Ufalme wa Mungu.
- Juma lijalo: Kujielekeza Kwenye Utume.
