Somo la 3: Taswira za Ndoa
Somo la 3: Taswira za Ndoa
(Ufunuo 19 & 21, Waefeso 5, Ezekieli 16)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unapenda kutumia muda na watu wenye upendo kwako na wanaokutia joto? Mimi ninapenda! Tusingependa kutumia muda wetu na watu walio baridi na wako mbali. Kati ya mambo unayoweza kuyatarajia kutoka kwa mungu wa kipagani, kuwa na upendo na mwenye kutia joto si miongoni mwao. Mimi si mtaalamu wa miungu ya kipagani, lakini kwa jinsi ninavyoielewa upendo au kutia joto ni sifa ya mungu wa kipagani, na si hisia inayowaonesha wanadamu. Kwa mfano, Eros, mungu wa upendo, na Aphrodite, mungu mke wa upendo, ni taswira za huruma. Miungu hiyo inaweza kutia msukumo upendo, lakini haioneshi upendo kwa wanadamu. Hicho ndicho kinachomfanya Mungu wetu awe wa kipekee isivyo kifani. Mungu wa kweli wa ulimwengu anajidhihirisha kama mwenye mwingiliano mkubwa wa upendo na wanadamu. Yeye ni Baba wetu. Juma hili Yeye ni Mwenzi wetu. Tunapaswa kuwa na shukrani katika hilo! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi kuhusu Mungu kama Mwenzi wetu!
- Kufunga Ndoa na Mungu
-
- Soma Ufunuo 19:6-7. Mwana-Kondoo ni nani? Na anataka kufanya nini? (Soma Ufunuo 5:12. Yesu ni Mwana-Kondoo. Anakaribia kufunga ndoa.)
-
- Soma Ufunuo 19:8. Mwana-Kondoo anafunga ndoa na nani? (Soma Ufunuo 21:9-10. Hii inasema kuwa Mwana-Kondoo anafunga ndoa na mji.)
-
-
- Eti nini? Inawezekanaje Yesu akauoa mji? (Si tu mji wowote, bali ni mji mtakatifu, Yerusalemu Mpya.)
-
-
- Hebu turejee nyuma na tusome tena Ufunuo 19:8. Yerusalemu Mpya imevaa nini? (“Kitani nzuri,” inayotafsiriwa kama “matendo ya haki ya watakatifu.” Jengo linawezaje kuvaa matendo ya mtu?
-
- Soma Ufunuo 21:27. Nani anaishi katika mji huu? (Wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima.)
-
- Soma Waefeso 5:28-32. “Siri hiyo kubwa” ni kitu gani? (Kwamba Yesu ni Mume wa kanisa. Utaona kwamba kifungu cha 30 kinaeleza kuwa Wakristo ni “viungo vya mwili wake.”)
-
-
- Wakati hili linaweza kuonekana kama jambo la ajabu kwa mtu asiye na uelewa na Biblia, Wakristo wanahusianishwa na Kanisa ambalo ni bibi arusi wa Yesu. Hivyo, tumeolewa na Yesu. Hii inafafanua kwa nini mji umevaa matendo ya wenye haki na waliokombolewa wanaishi katika mji – Yerusalemu Mpya.)
-
-
-
- Hebu jiulize, kwa nini Mungu achague kutufanya tumwangalie kama Baba wetu na Mwenzi wetu?
-
- Kutokustahili Kwetu
-
- Soma Ezekieli 16:4-5. Umma una maoni gani juu ya mtoto huyu? (Wako radhi kumwacha afe. Hakuna aliyemsaidia.)
-
- Soma Ezekieli 16:6-9. Mungu amefanya nini kwa mtoto huyu asiyetakiwa?
-
- Soma Ezekieli 16:10-13. Je, Mungu anatenda mambo ya msingi tu kwa mtoto huyu asiyetakiwa? (Hapana. Anampa kila lililo la manufaa. Anamtendea kama mtoto wa kifalme.)
-
- Soma Ezekieli 16:14-15. Je, mwanamke huyu aliyekuwa mtu mzima bado hatakiwi? (Hapana. Sasa ni mrembo na wa kutamanika.)
-
- Ruka hadi chini na usome Ezekieli 16:32-35. Huyu ni mke wa namna gani? (Asiye mwaminifu, na kiukweli ni mke mpumbavu. Ni mrembo, lakini anawalipa watu kwa ajili ya ngono. Hata makahaba wana ufahamu wa kutosha kiasi cha kuomba malipo!)
-
- Hebu tafakari kidogo kisha unielezee kuhusu mwanamke huyu. Je, Mungu amemwokoa?
-
-
- Je, Mungu amemfanya atamanike?
-
-
-
- Je, Mungu amemtajirisha?
-
-
-
- Je, Mungu amemwoa?
-
-
-
- Wajibu wake kwa Mungu ni upi?
-
-
-
- Hebu niambie, Mungu anatufundisha nini kupitia kwenye kisa hiki cha kutisha na kuaibisha kuhusiana na ndoa? (Kwanza, Mungu anaizungumzia Israeli, lakini ninadhani kinahusiana na watu wa Mungu wa nyakati zote. Pili, kinachohusika kwenye majibu yetu ni kwamba kwa kuwa na uhusiano nasi wa “ndoa,” Mungu amejitoa kwa ajili ya aina zote za huzuni pale tunapokuwa si waaminifu.)
-
- Mfano Halisi
-
- Soma Mwanzo 24:1-4. Unadhani kwa nini ilikuwa muhimu kwa Ibrahimu kumfanya mwanaye aoe kutoka kwa “jamaa” wake tu?
-
- Soma Mwanzo 24:5-6. Wajibu wa pili wa mtumishi wake, Eliezeri ni upi? (Asimwache Isaka katika familia ya binti.)
-
- Soma Mwanzo 24:7-8. Je, hii inatupatia kidokezo cha kwa nini Ibrahimu hakutaka mwanaye amwoe Mkaanani au kutaka mwanaye akae na mkewe mpya? (Mpango uliokuwepo ni kwamba uzao wa Ibrahimu utawaangusha Wakaanani kutoka katika nchi. Isaka asingeweza kukaa na “ndugu” zake kwa sababu alikuwa sehemu ya msingi ya familia kuhama kwenda kukaa Kaanani.)
-
-
- Je, kuna fundisho hii leo kwa ajili ya ndoa za watoto wetu? (Hatutaki watoto wetu waoane na wapagani kwa sababu lengo ni kuepuka wao na wajukuu wetu kuwa wapagani.)
-
-
- Soma Mwanzo 24:10-14. Ni nini msingi wa mafanikio ya Eliezeri? (Maombi! Tunatakiwa kuwaombea wenzi watarajiwa wa watoto wetu. Tunatakiwa kuwafundisha kuomba ili wapate mwongozo wa kupata mwenzi sahihi.)
-
- Soma Mwanzo 24:15-19. Unadhani kwa nini Eliezeri alipendekeza kipimo cha mke mtarajiwa kuwa mwenye bidii ya kazi? (Inaelekea kuonesha kwamba alikuwa mwenye huruma na kuwafikiria wengine, na si mbinafsi, na si mvivu.)
-
-
- Je, mtu anapaswa kumwoa mwenzi mvivu? (Kwa uchunguzi wangu ndoa zinakuwa kwenye matatizo makubwa pale ambapo mwenzi mmoja (mwanamke au mwanaume) analalamika kuwa yeye ndiye anayefanya kazi zote.)
-
-
- Rebeka anamkaribisha Eliezeri nyumbani kwao, Eliezeri anasimulia kisa chote kwa baba na kaka wake Rebeka, na wanakubali Rebeka aondoke kwenda kuolewa na mwana wa Ibrahimu. Soma Mwanzo 24:57-58. Kwa nini Eliezeri anakubali kuwa Rebeka ndiye atoe uamuzi? (Hii inaonesha kuwa katika kipindi kifupi ambacho Eliezeri alikitumia kuwa na Rebeka alikuwa na ujasiri na uhakika naye.)
-
- Utafakari utangulizi. Soma Mwanzo 24:54-57. Je, Rebeka ndiye anayepewa fursa ya kusema neno la mwisho kuhusu ndoa? (Hapana. Ni suala tu la endapo atapewa siku kumi za kuiaga familia yake.)
-
-
- Utaona kwamba ni mama na kaka ndio wanaoonekana kufanya majadiliano ya mkataba wa ndoa. Una maoni yoyote kwa nini hilo linafanyika? (The Bible Knowledge Commentary inataarifu kuwa katika jamii ile kaka wa mwanamke ndiye aliyemtoa dada wake kwa ajili ya ndoa.)
-
-
- Soma Mwanzo 24:59-61. Hii ni baraka ya namna gani? Unadhani hii ilikuwa kuagwa rasmi (send-off) kwa bibi arusi? (John MacArthur analiita hili kama “ombi la desturi,” lakini kwa upande wangu inaonekana kama vile Eliezeri alielezea ahadi alizopewa Ibrahimu kuhusu uzao wake.)
- Chagua kwa Makini
-
- Soma Ufunuo 17:4-5. Tulichojifunza hadi kufikia hapa ni “ndoa” kamilifu kati ya wanadamu na Mungu. Na tumejifunza kinyume chake, kwamba wanadamu waliokuwa na uhusiano na Mungu walikuwa makahaba, badala ya wenzi waaminifu. Hii “mama wa makahaba” inaonekana kuwa kitu gani? (Haya ni mamlaka ya kidini ambayo hatimaye yanapingana na Mungu.)
-
-
- Tunaposoma kuhusu Israeli kuenenda kama kahaba, badala ya mke, Mungu alikuwa anaitafuta Israeli ili kumrudia Yeye. Kahaba wa Ufunuo 17:5-6 ana tofauti gani? (Haya si mamlaka yanayotamani kuwa na uhusiano na Mungu. Huu ni upinzani uliopangiliwa.)
-
-
- Soma Ufunuo 14:8. Hii ni sehemu ya Ujumbe wa Malaika Watatu (Ufunuo 14:6-11). Mamlaka haya ya kidini ya Babeli yanafanya nini? (Yanalazimisha uzinzi na uasherati.)
-
-
- Utaona kwamba Babeli inarejelewa kama “mwanamke” na kifungu cha 8 kinatumia maneno “uliowanywesha mataifa yote.” Je, hii ni nguvu halisi? (Soma Yeremia 51:7. Kwa kumwita Babeli kuwa ni Bwanamke, ikirejelea mvinyo, na kumwita kahaba, taswira ni ile ya kushawishi/kutamanisha, badala ya nguvu kamili.)
-
-
- Hebu tafakari kidogo. Tulimshangilia Mungu aliposema kuwa anataka kuwa na uhusiano wa karibu kabisa na sisi kwa sababu anaulinganisha na ndoa (na kwa yeye kuwa Baba wetu). Je, Shetani anatafuta kuwa na uhusiano na sisi ulio sawa na kinyume? (Hapana. Mungu anatoa mwelekeo kwa kutuita mabibi arusi wake. Kumgeukia Shetani inamaanisha “si bibi arusi wa Mungu.”)
-
- Soma Ufunuo 21:1-3. Hapo awali tulijadili kuhusu kuuita mji bibi arusi. Hapa tunaona kuwa rejea ya kweli ni ya watu wanaoishi katika mji. Je, hii inatupatia taswira kamili ya ndoa yetu na Yesu?
-
- Soma Ufunuo 21:4-7. Hatimaye huu utaishia kuwa uhusiano wa namna gani? Baadhi ya ndoa ni nzuri na baadhi ya ndoa zinatisha. Hii ni aina gani ya ndoa?
-
-
- Angalia pia rejea ya Mungu kuwa Baba wetu na sisi watoto Wake.
-
-
- Rafiki, Mungu anatamani kuwa na uhusiano wa karibu sana na wewe. Je, utakubali? Je, utasalia kuwa mwaminifu kwa Mungu aliyekuokoa na anataka kukupeleka mbinguni ili akawe pamoja nawe? Kwa nini usimpokee sasa hivi?
- Juma lijalo: Mataifa: Sehemu ya 1.