Somo la 4: Mataifa: Sehemu ya 1
Somo la 4: Mataifa: Sehemu ya 1
(Mwanzo 10, 12, Wagalatia 3, 1 Samweli 8)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kama ungekuwa unataka kuanzisha taifa, ungelipa serikali ya namna gani? Je, itakuwa serikali ya kidemokrasia? Je, mfumo wake wa utawala utakuwa ni wa serikali ya makasisi? Je, itatawaliwa na mfalme? Vipi kuhusu kuwa na kundi dogo la viongozi? Au hutakuwa na serikali kabisa? Marafiki wangu wa Kikristo wananiambia kuwa wana wasiwasi juu ya kuwa na serikali inayotekeleza kanuni za Kibiblia. Swali langu kwao ni, “Mnapenda serikali inayozingatia sheria zipi?” “Je, mnapenda sheria zinazomkana Mungu?” Biblia ina jambo la kulizungumzia kuhusu serikali, hivyo hebu tuzame kwenye somo letu na tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Mungu na Serikali Mbaya
-
- Soma Mwanzo 10:1. Aina gani ya serikali ilitawala ulimwengu kabla ya gharika? (Soma Mwanzo 6:4-7. Wanadamu walikuwa wanajikita katika kutenda uovu. Lazima serikali iliruhusu jambo hili kwa sababu Mungu aliamua kwamba suluhisho pekee ilikuwa ni kuwaangamiza.)
-
-
- Baadhi ya watu hawa waovu waliitwaje? (“Watu hodari,” “watu wenye sifa.”)
-
-
- Soma Mwanzo 6:8. Kama unaifahamu Biblia, upendeleo huu kutoka kwa Mungu ulikuwa na matokeo gani? (Nuhu na familia yake ya karibu walipona gharika ile iliyotokea duniani kote ambayo iliwaangamiza wanadamu wote waliosalia.)
-
- Soma Mwanzo 10:6-9. Huu ni uzao wa mwana wa Nuhu, Hamu. Kifungu kinasema kuwa Nimrodi alikuwa wa kwanza duniani kuwa mtu hodari, lakini tuliona kwamba kabla ya gharika walikuwepo watu hodari. Unalielezeaje hili? (Maoni ya The Finis Dake Commentary yanatuambia kuwa Nimrodi alikuwa anamuasi Mungu, na kwamba uhodari wake kama mwindaji (“mbele za Bwana”) unaashiria kuwa pia aliwawinda wanadamu na alifanya hivi hadharani katika kumwasi Mungu. Katika dunia mpya baada ya gharika, tunaona moyoni mwa Nimrodi aina ya mtazamo wa kuasi uliobainisha tabia za wale watu hodari kabla ya gharika.)
-
- Soma Mwanzo 10:10-12. Je, hii ni miji mizuri iliyojengwa na Nimrodi? (Hapana, kwa ujumla miji hii inachukuliwa kuwa na uhasama kwa watu wa Mungu.)
-
- Soma Mwanzo 11:1-4. Kwa nini watu wanaoishi katika mji wa Nimrodi wanataka kujenga mnara ambao “kilele chake kitafika mbinguni?” (Wanataka “kujikinga dhidi ya gharika.” (Huu ni usasa unaoishi kwa kumwasi Mungu.)
-
-
- Soma Mwanzo 9:8-11. Hii inakuambia nini kuhusu wale waliojenga mnara wa Babeli katika nchi ya Shina? (Hawakumwamini wala kumtumaini Mungu.)
-
-
- Hebu turudi nyuma kidogo na tutafakari mambo ya kujifunza kuhusu serikali chini ya Nimrodi. Watu walikuwa na mtazamo gani kwa Mungu? (Waliasi. Hawakumwamini wala kumtumaini Mungu.)
-
-
- Hii inaashiria kuwa matokeo ya kuwa na wananchi wengi ambao hawamwamini wala kumtumaini Mungu ni yepi?
-
-
-
-
- Watamtumaini nani? (Watajitumainia wenyewe.)
-
-
- Mungu na Serikali Nzuri
-
- Soma Mwanzo 12:1-2. Je, Mungu anamtuma Abramu kama mmisionari, au anafanya jambo jingine kabisa? (Jambo jingine. Mungu anasema atamfanya Abramu kuwa “taifa kubwa.” Hiyo inamaanisha serikali.)
-
- Soma Mwanzo 12:3. Ni kwa msingi gani taifa hili litajengwa? (Wale watakaombariki Abramu watabarikiwa na wale wasiomheshimu watalaaniwa.)
-
-
- Hiyo inamaanisha nini? Abramu si mungu. Kwa nini baraka na laana zitoke kwa mtazamo wa mtu kwenda kwa Abramu? (Abramu ni mshirika wa Mungu. Anawakilisha taifa lijalo lililojitoa kwa Mungu. Ndio maana Mungu kwa nguvu isiyo ya kawaida anambariki au kumlaani mtu kutegemeana na njia watakayomwendea Abramu na taifa lake.)
-
-
- Angalia sehemu ya mwisho ya Mwanzo 12:3. Inamaanisha nini? (Soma Wagalatia 3:8. Hebu tuchimbue kwa kina Wagalatia 3 ili tuweze kuwa na uelewa mzuri zaidi.)
-
- Soma Wagalatia 3:1-5. Kuna tatizo gani kwenye fikra ya Wagalatia? (Wanaamini kuwa matokeo ya matendo yao ni kwa wao kuwa na Roho Mtakatifu na kuokolewa.)
-
-
- Je, huu unaonekana kama ndio mtazamo wa Nimrodi? (Wagalatia hawako kwenye uasi kama ilivyo kwa Nimrodi, lakini wana tabia zinazofanana ambapo wanaamini katika matendo yao kwa ajili ya kupata mafanikio.)
-
-
- Soma Wagalatia 3:6-9. Tunaona nukuu kutoka Mwanzo 12:3. Mwanzo 12:3 inarejelea jambo gani? (Inarejelea tukio lijalo la Yesu kufanyika kuwa mwili na kwamba maisha na kifo chake kwa ajili yetu ndio njia pekee ya wokovu.)
-
- Hebu turejee nyuma kidogo na tutafakari mambo ya kujifunza kuhusiana na serikali chini ya Abramu. Aina gani ya serikali inabarikiwa? (Ile inayomwangalia Mungu kwa uchanya. Kwa kuwa baraka kubwa ilikuwa ni kutabiriwa kwa ujio wa Yesu, hii inatuambia kuwa serikali inayobarikiwa zaidi ni ile iliyojengwa juu ya kanuni za Kikristo.)
-
-
- Endapo hukubaliani na hitimisho langu la awali, je, hukubaliani kwa msingi gani? (Kwa uzoefu wangu baadhi ya watumishi katika kanisa langu hawatakubaliana kutokana na uelewa wao wa Katiba ya Marekani. Naiona hii kama kejeli. Katiba ni nyaraka iliyotengenezwa na wanadamu. Je, kuitegemea, tofauti na kuitegemea Biblia, ni sawa na kujenga mnara?)
-
-
-
- Mwisho, unadhani kauli ya Mungu aliyoitoa katika kitabu cha Mwanzo 12:3 kuhusu baraka na laana inatumika kwenye chuki dhidi ya Wayahudi inayoendelea kuongezeka katika zama za leo?
-
- Serikali ya Makasisi Dhidi ya Ufalme
-
- Soma 1 Samweli 8:1-3. Ni kosa la nani kwamba watoto wa Samweli ni waamuzi wasio waaminifu? (Samweli alikuwa mtu mwema, hivyo sitamlaumu kwa wana waliokengeuka. Lakini anawajibika kwa kuwapa mamlaka wanaye wasio waaminifu.)
-
- Soma 1 Samweli 8:4-5. Je, unakubaliana na Wazee wa Israeli? (Mfumo wa sasa wa serikali haukuwa unakubalika kutokana na vitendo vya rushwa. Samweli alikuwa mtu wa Mungu na Wazee walimwendea ili kupata serikali nzuri.)
-
- Soma 1 Samweli 8:6. Unadhani kwa nini Samweli hakufurahishwa? Kwa sababu wanaye walikataliwa? Kwa sababu Wazee waliashiria kwamba alikuwa mzee sana kiasi cha kushindwa kutenda kazi yake?
-
- Soma 1 Samweli 8:7-8. Mungu analichukuliaje ombi la Wazee? (Si kama ambavyo ningebashiri. Mungu anasema kuwa wanamkataa Yeye!)
-
-
- Wazee walipaswa kuomba nini kama wangekuwa waaminifu kwa Mungu? (Kuwaondosha wana wasio waaminifu si kitendo cha kumkataa Mungu. Ambacho wazee wangepaswa kukiomba ni kwamba Samweli afanye kazi pamoja na Mungu ili kuwapatia waamuzi wapya.)
-
-
-
- Kwa nini Mungu anahusianisha nia zisizo sahihi na Wazee wakati vifungu vilivyotangulia vinafanya ombi lao lionekane kuwa na mantiki? (Mungu anasema kuwa watu wana historia ya kumkataa. Inaonekana kwamba Mungu alidhani kuwa jambo bora kwa sasa ingekuwa ni kukaa na Samweli. Mungu angeweza kufanyia kazi suala la kupatikana kwa nabii mpya kwa wakati sahihi.)
-
-
- Soma 1 Samweli 8:9. Kwa nini Mungu anakubali ombi la Wazee? Anadhani kuwa linatisha! (Kuwa makini kwa kile unachomwomba Mungu.)
-
- Soma 1 Samweli 8:11-17. Mangapi kati ya mambo haya unaweza kuyatarajia kutoka katika serikali ya kisasa?
-
-
- Hii inazungumzia nini kuhusu mtazamo wa Mungu juu ya serikali? (Inaonekana Mungu anadhani kuwa kadiri serikali inavyokuwa ndogo ndivyo inavyokuwa bora zaidi.)
-
-
- Soma 1 Samweli 8:18-20. Sasa tunaona taswira kamili juu ya mtazamo wa watu. Je, wamemkataa Mungu? (Wanaonekana kufanana kabisa na watu wa mnara wa Mwanzo 11:4.)
-
- Hebu turejee tena nyuma kidogo na tutafakari juu ya taswira pana zaidi. Unahitaji nini ili kuwa na serikali inayoongozwa na kanuni za Kibiblia? (Unahitaji watu wakubaliane nayo.)
-
-
- Je, serikali kama hiyo inawezekana kuwapo katika zama za leo?
-
-
-
- Ninachukulia kwamba watu wengi watajibu swali lililotangulia kwa jibu la “Hapana.” Tunapaswa kufanya nini basi ili tuwe na serikali bora kabisa? (Kuchagua viongozi wanaoelewa kanuni za Kibiblia na wanaozifuata katika kuongoza.)
-
-
- Soma Mathayo 20:25-28. Viongozi wa namna gani ni bora?
-
-
- Je, hii ni kweli kwa kanisa peke yake? Au ni kweli pia kwa serikali? (Yesu anatumia “watawala wa Mataifa” kama mfano mbaya. Hiyo inaashiria sheria ambayo Yesu anaitoa hapa inatumika kwa kanisa na kwa serikali.)
-
-
- Rafiki, je, utatafakari kwa kusali kile tulichokijadili na kukitumia kwenye matendo yako katika kuchagua na kuiunga mkono serikali?
- Juma lijalo: Mataifa: Sehemu ya 2.