Somo la 6: Kuielewa Kafara
Somo la 6: Kuielewa Kafara
(Isaya 1, Waebrania 10, Kutoka 12, Ufunuo 5)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unaweza kufafanua jinsi dhambi zilivyosamehewa na wokovu kupatikana katika Agano la Kale? Jibu ni mfumo wa kafara za wanyama. Mwanadamu alipotenda dhambi, mnyama alikufa. Kwenye mjadala kati ya wokovu kwa njia ya matendo na wokovu kwa njia ya imani, haya si matendo. Unafikiria nini kuhusiana na mfumo ule? Wanadamu wanapenda kuwalaumu wengine kwa kushindwa kwao. Kwa ujumla huwa tunashukuru pale mtu mwingine anapobeba lawama kwa ajili ya makosa yetu. Mfumo wa kafara za wanyama unaonekana kama vile kamwe wanadamu hawakuwa na haja ya kuwajibika kwa yale waliyoyatenda. Je, hilo linakuhangaisha? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu maana kamili ya kafara za wanyama!
- Maana ya Kafara?
-
- Soma Isaya 1:2-5. Kuna tatizo gani kwa watu wa Mungu? (Ni waovu na “wamefarakana” na Mungu.)
-
-
- Mungu anazungumzia kuhusu uwezo wa ng’ombe au punda kumjua bwana wake. Je, Mungu anasema kuwa watu wake ni wapumbavu kuliko ng’ombe au punda? (Hicho ndicho haswaa anachokisema Mungu.)
-
-
- Soma Isaya 1:6-9. Israeli imekaribia kiasi gani kuangamizwa kabisa? (Imekaribia sana. Manusura wachache wanadhihirisha kutokana na kile kilichotokea Sodoma na Gomora.)
-
-
- Wana tumaini gani kuhusiana na kuwa bora zaidi? (Kifungu cha 6 kinasema kuwa vidonda vyao havitibiwi.)
-
-
- Soma Isaya 1:11-13. Ikiwa kumtoa kafara mnyama ndilo jibu sahihi la dhambi maishani mwako, kwa nini Mungu anawaambia watu wake kuwa “imetosha?”
-
-
- Unadhani tatizo halisi ni lipi? (Kifungu cha 13 kinalielezea kwa ufupi – Mungu hataki “ubatili” na “makutano ya ibada.” Kama hujisikii kumtumikia Mungu, kwa nini basi ujiingize katika mienendo ya kumtumikia? Mungu hapendezwi na unafiki.)
-
-
- Katika Isaya 1:11 Mungu anasema kuwa hafurahii kafara za wanyama. Kwa kuwa hilo ni kweli, kwa nini Mungu aliweka mfumo wa kafara?
-
-
- Je, tunaweza kukiita kipindi cha mfumo wa kafara “kuhesabiwa haki kwa imani?” (Ndiyo. Njia ya kuondoa dhambi haikuhusisha mtu kulipa faini, kudhuriwa mwili, au hata kuadhibiwa kuwa ajili ya dhambi zake.)
-
-
-
- Kama Mungu alikuwa hafurahii kuchinjwa kwa wanyama, kama wanadamu walikuwa hawaadhibiwi kwa ajili ya dhambi zao, ninauliza tena, je, hili lilikuwa wazo baya? Kwamba Mungu hafurahii na wanadamu hawawi na nidhamu? (Palikuwepo na nidhamu kwa maana ya kwamba miji yao ilikuwa inachomwa moto na nchi yao inaliwa na wageni. Lakini haionekani kuwa adhabu binafsi kwa dhambi binafsi.)
-
-
-
-
- Ikiwa adhabu ya jumla ya dhambi ilitoka kwa wageni, kwa nini kutoa kafara wanyama wasio na hatia? (Kinadharia, kumwona mnyama asiye na hatia akifa kwa ajili ya dhambi zako kunapaswa kukufanya uzichukulie dhambi zako kwa umakini. Lakini ninadhani kikubwa alichokimaanisha Mungu ni kwamba kafara ilikuwa aina ya unabii wa Yesu ajaye. Hebu tujadili hili katika sehemu inayofuat)
-
-
- Unabii wa Yesu Ajaye na Pasaka
-
- Soma Waebrania 10:1-3. Waebrania inasema kuwa sababu moja ya kuwapo kwa kafara za wanyama ni ipi? (Kuwakumbusha wanadamu juu ya asili ya dhambi.)
-
- Soma Waebrania 10:4-5 na Waebrania 10:9-10. Sababu ni ipi ya Mungu kuanzisha mfumo wa kafara wa Agano la Kale? (Lengo lilikuwa ni kuwaelimisha wanadamu jinsi Mungu atakavyoshughulikia tatizo lao la dhambi. Ulikuwa ni unabii kwa njia ya vitendo.)
-
- Hebu rudi nyuma kidogo na ulitafakari hili. Chukulia kwamba Mungu alikuja duniani na wanadamu wakamuua. Ungepata fundisho gani kutokana na hilo? (Uovu ulishinda. Mungu alishindwa.)
-
- Soma Kutoka 12:3-6. Kama ulikuwa unamchinja kondoo huyu, kwa nini ijalishe kama alikuwa na hila? (Hii si sawa na wanyama wazaao. Hii ni sehemu nyingine ya msingi ya unabii kivitendo. Yesu alikuja duniani na kuishi maisha makamilifu kwa ajili yetu. Kwa sababu hiyo kondoo alitakiwa kuwa mkamilifu.)
-
- Hebu tujikite katika kitabu cha Kutoka 12:3 na Kutoka 12:6. Familia ilimtunza kondoo kwa muda gani kabla haijamtoa kafara? (Siku nne.)
-
-
- Mungu anamaanisha nini? (Wanaweza kumpenda kondoo. Hivyo kuifanya kafara kuwa binafsi zaidi.)
-
-
- Soma Kutoka 12:7-8. Kwa nini wanamla kondoo? (Yesu hakufa tu badala yetu, bali anatupatia uzima kwa njia ya kafara yake. Yohana 6:48 ina maneno ambayo Yesu anasema, “Mimi ndimi chakula cha uzima.”)
-
- Soma Kutoka 12:12-13. Kwa nini kupaka damu ya kondoo kwenye mlango wa mji wako? (Malaika aliyemwangamiza adui wa watu wa Mungu alipita juu ya nyumba zilizo na damu na hakuwaua wazaliwa wa kwanza wa wale waliofuata maelekezo ya Mungu.)
-
-
- Hiyo inamaanisha nini kwenye unabii huu kwa vitendo? (Mungu anaita “balls and strikes.” Kwa kusema hivyo ninamaanisha kuwa Mungu yuko makini kuhusiana na sisi kuyatenda mapenzi yake. Kufuata maelekezo kwa kuipokea kafara ya Yesu hutupatia uzima badala ya mauti.)
-
-
- Heu turejee nyuma kidogo tena na tulitafakari hili. Ni upi uliokuwa muktadha wa malaika mwangamizaji wakati wa Pasaka? (Wamisri waliwaweka utumwani watu wa Mungu kwa mamia ya miaka. Hawakuwaachia kutoka utumwani licha ya maonyo ya mapigo ya awali. Mungu si tu kwamba anatuonesha upendo na rehema, bali pia anasimama dhidi ya maadui wetu kwa namna kali kabisa. Hii ni sehemu ya unabii.)
- Unabii wa Ushindi
-
- Soma Ufunuo 5:5-7. Je, sasa Mwana-Kondoo amekuwa Simba?
-
-
- Kondoo huyu ni nani? (Rejea yake inayoonekana kuwa ni “kuchinjwa” ni uthibitisho kwamba huyu ni Yesu.)
-
-
- Soma Ufunuo 5:8-10. Yesu ametimiza nini kwa kuchinjwa kwake? (“Alimnunulia Mungu watu kutoka kila kabila na lugha na jamaa na taifa.” Hili ndilo hitimisho la utimilifu wa unabii kwa njia ya kumtoa kondoo kafara.)
-
- Soma Ufunuo 5:11-14. Je, bado ulimwengu umegawanyika?
-
-
- Nani anayemwabudu Yesu? (Kila mtu na kila kitu!)
-
-
- Soma Ufunuo 7:9-10. Hii inadhihirisha nini kuhusu idadi ya wale wanaookolewa? (Idadi kubwa inaokolewa. Idadi isiyoweza kuhesabika.)
-
- Soma Ufunuo 7:13-15. Mavazi meupe yanawakilisha nini? (Yanafanywa kuwa meupe kwa kuoshwa katika damu ya Yesu. Hii ni haki kwa imani pekee.)
-
-
- Utaona kwamba idadi hii ya watakatifu “inatoka katika dhiki ile iliyo kuu.” Ikiwa haya ni mateso ya mwisho, tunawezaje kuwa na kundi kubwa la watu? (Ninachokifikiria ni kwamba kwa kuwa wazee mbinguni hawawajui (angalia kifungu cha 13), hawa si wale ambao tayari wanakaa mbinguni. Kimantiki dhiki kuu inaweza kurejelea safari kuu katika sayari dunia. Hawa ni watakatifu waliopona uasi wa Shetani na malaika wake wapotofu alioanguka nao.)
-
-
- Soma Ufunuo 7:16-17. Hapa tunaona unabii gani mwingine wa Mwana-Kondoo? (Yesu pia ni Mchungaji wetu. Anatukinga na mateso yote na anatupatia furaha!)
-
- Rafiki, je, utakubaliana kwamba Yesu kufanyika mwili, maisha yake na kifo chake cha mateso makali vyote vilitabiriwa kupitia mfumo wa kafara? Je, utaipokea kafara yake kwa ajili yako na kufurahia katika ushindi ambao aliufanya uwezekane kwa ajili yako? Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Misingi ya Unabii.