Somo la 9: Katika Zaburi: Sehemu ya 2
Somo la 9: Katika Zaburi: Sehemu ya 2
(Zaburi 46, 47, 75, Yeremia 4)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Maisha yako yanaendeleaje? Je, utajibu kuwa, “kwa ujumla yanaendelea vizuri” au “mambo ni mabaya?” Je, kuna namna ambayo tunaweza kuboresha jinsi maisha yetu yanavyoendelea? Mungu anatuambia kuwa kuna njia bora zaidi. Njia ambayo hatma yake ni ushindi. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze juu ya njia bora zaidi!
- Kupandishwa Cheo
-
- Soma Zaburi 75:6-7. Tunapaswa kujishughulisha na nani zaidi katika eneo letu la kazi? Bosi? Wafanyakazi wenzetu? Wateja?
-
-
- Kifungu cha 7 kinaposema kuwa Mungu “ndiye ahukumuye,” aina gani ya hukumu inarejelewa? (Lazima rejea ya “kumwinua” inarejelea angalao kupandishwa cheo katika eneo la kazi. Inaweza kurejelea aina nyingine za heshima ambazo mwajiriwa anaweza kutaka kuzipokea.)
-
-
-
- Inamaanisha nini kusema “humdhili huyu?” (Mungu anaweza kukupandisha cheo au kukushusha cheo katika eneo la kazi.)
-
-
-
- Hii inatufundisha nini kuhusu jinsi ya kuboresha maisha yetu katika eneo la kazi?
-
-
- Soma Zaburi 75:4-5. Waajiriwa wanapaswa kuepuka nini? (Kujivuna. Usiwe na maringo. Nadhani tunakabiliana na aina mbili tofauti za waajiriwa. Aina ya kwanza inafanya vizuri na kwa kawaida inatarajiwa kujivuna. Aina ya pili haistahili kujivuna. Wana mtazamo wa majivuno hata kama hawana chochote cha kujivunia.)
-
- Soma Zaburi 75:8. Unadhani mvinyo unaotoka povu ni kinywaji kizuri kunywewa? (Hapana. Hii inaonekana kuwa hasi sana.)
-
- Soma Zaburi 75:9-10. Je, wema na wabaya wanapiga vyombo vya muziki? Rejea ya “pembe” inamaanisha nini? (“Pembe” inawakilisha nguvu ya mnyama. Hii inatuambia kuwa nguvu ya waovu itakoma. Nguvu ya wenye haki itaongezeka!)
- Kupitia Nyakati Ngumu
-
- Soma Zaburi 46:1-3. Ukanda wa kati wa Marekani umekuwa ukipitia hali mbaya sana ya hewa. Fikiria kwamba mahali unapoishi kuna tetemeko la ardhi la kutisha ambapo “milima” inatetemeka “moyoni mwa bahari.” Fikiria mafuriko hayo ya kutisha kiasi cha dunia kutetemeka wakati maji yanaunguruma. Je, umewahi kupitia mateso ya balaa la hali ya hewa?
-
- Soma Zaburi 46:4-5. Hii ni taswira tofauti kabisa. Mahali hapa pazuri pa kuishi pako wapi? (Hii inaonekana kama dunia mpya na mto wa uzima.)
-
-
- Kwa nini kutofautisha hali hizi mbili?
-
-
- Soma Zaburi 46:6-9. Mtunga Zaburi anamaanisha nini kuhusiana na hali hizi mbili? (Mungu ndiye yupo katika udhibiti!)
-
- Soma Zaburi 46:10-11. Unapaswa kufanya nini kama unataka kuishi maisha mazuri yenye amani tele? (Kumjua Mungu! Amini kwamba yuko pamoja nawe. Ukifanya hivyo, atakuwa ngome yako.)
- Hakuna Tumaini
-
- Soma Yeremia 4:23. Hii inakukumbusha kitu gani? (Soma Mwanzo 1:2. Hii imekusudiwa kutukumbusha juu ya hali ya dunia kabla ya Uumbaji.)
-
- Soma Yeremia 4:24-26. Je, hii inatukumbusha kile tulichokisoma muda mfupi uliopita katika Zaburi 46? (Inaonekana kufanana sana na kutisha sana.)
-
-
- Kuna njia gani ya kutoka kwenye mazingira haya ya “hakuna tumaini?”
-
-
- Soma Yeremia 4:1-2. Mwanzo wa sura hii unaeleza njia ya kuepuka tatizo hili la kutisha. Ni njia gani hiyo?
- Njia Ielekeayo Ushindi
-
- Soma Zaburi 67:1-2. Je, Mungu ana sababu ya “ubinafsi” kuwabariki wale wanaomfuata? (Inaboresha taswira ya Mungu. Mungu anapowabariki wale wanaomfuata, kunaifanya “njia yake ijulikane duniani.” Inawafanya wengine wahitimishe kwamba hii ndio njia ya kuwa na maisha mazuri.)
-
- Soma Zaburi 67:3. Kumsifu kwako Mungu kuna wajibu gani katika kuboresha hadhi yake? (Kuhusianisha baraka zako kwa Mungu tofauti na juhudi zako mwenyewe humwinua Mungu mbele ya watu wengine.)
-
-
- Kuna athari gani ikiwa unakiri kuwa mfuasi wa Mungu hadharani lakini unakamatwa kwenye matendo machafu/yasiyofaa?
-
-
- Soma Zaburi 67:4. Angalia neno ambalo tafsiri ya Biblia ya ESV inalitafsiri kama “haki” (equity). Tafsiri ya KJV inalitafsiri kama “righteously” na kwa Kiyunani linamaanisha kitu kilicho na usawa (level) au “kinyoofu” (straight). Hii leo maana maarufu ya “usawa” (equity) ni kuwabagua baadhi ya watu ili kupata matokeo ambayo wanadamu walio katika udhibiti wanadhani kuwa ni matokeo bora. Hicho si kinachomaanishwa kwenye kifungu hiki. Unadhani kifungu hiki kinamaanisha nini? (Mungu anatenda kilicho bora kwa ajili yetu. Mungu anawainua wale wanaomfuata.)
-
-
- Je, huo si ubaguzi? (Ni ubaguzi, lakini ni ubaguzi uliojengwa juu ya ustahili. Tumemchagua Mungu.)
-
-
- Soma Zaburi 67:5-7. Ni nini sehemu ya ushindi wa wale wanaomfuata Yesu? (Baraka hapa duniani.)
- Ukumbusho
-
- Soma Mathayo 26:26-29. Jifikirie kwamba upo katika chakula hiki cha jioni. Je, huu unaonekana kuwa wakati mzuri wa furaha?
-
-
- Utaona kwamba kifungu cha 27 kinarejelea kunywea kikombe. Kifungu cha 29 kinauita “uzao huu wa mzabibu.” Katika sehemu ya kwanza ya somo hili tulisoma kuhusu “mvinyo unaotoa povu” katika Zaburi 75:8. Tofautisha mambo haya mawili.
-
-
- Soma Ufunuo 14:14-15. Unadhani inamaanisha nini kusema kwamba “mavuno ya nchi yamekomaa?” (Hili ni pambano la mwisho dhidi ya maadui wa Mungu. Wakati wa mwisho umewadia.)
-
- Soma Ufunuo 14:19-20. Je, tunazungumzia kuhusu tunda la mzabibu au kitu kingine? (Tunazungumzia kuhusu damu ya waovu katika pambano hili la mwisho.)
-
- Angalia tena anachokisema Yesu katika Mathayo 26:27-28. Biblia inaiendeaje ishara ya tunda la mzabibu? (Inaashiria damu ya wanadamu.)
-
- Soma 1 Wakorintho 11:25-26. Hii inatueleza kuwa kukinywea “kikombe” kunapaswa kututendea nini? (Kunapaswa kutukumbusha juu ya kifo cha Yesu kwa ajili yetu.)
-
-
- Unadhani hilo linapaswa kutusikitisha? (Hii ndio njia ambayo Yesu aliishinda dhambi na kutupatia uzima wa milele.)
-
-
-
- 1 Wakorintho 11:25 inasema, “kila mnywapo.” Unadhani hii inarejelea ushirika (meza ya Bwana) peke yake? Au litakuwa jambo jema kumfikiria Yesu kila mara tunapokunywa tunda la mzabibu?
-
-
-
-
- Kwa kuwa muktadha katika somo hili ni kuushinda uovu, je, tunapaswa pia kutafakari kuhusu kushindwa kwa uovu?
-
-
-
- Rafiki, wito wangu wa mwisho unafahamika. Je, ungependa kuishi maisha bora? Je, ungependa kupata ushindi juu ya changamoto zote za uovu? Mgeukie Yesu na atakupati baraka na ushindi. Kwa nini usiamue kufanya hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Tuliofikiwa na Miisho.