Somo la 10: Tuliofikiwa na Miisho
Somo la 10: Tuliofikiwa na Miisho
(Mathayo 24, Mwanzo 18, 2 Petro 2)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Karibia kila mtu anaamini katika hukumu itakayotolewa wakati fulani katika siku zijazo. Lakini watu wangapi wanatumia muda wao kufikiria juu ya Mungu kutekeleza hukumu? Hususan hukumu hiyo kutekelezwa kwao? Biblia ina kumbukumbu ya hukumu kubwa zisizo za kawaida zinazotokea muda mrefu kabla ya hukumu ya mwisho. Hukumu hizi zisizo za kawaida (supernatural) za kale zinatufundisha nini kuhusu hukumu ya mwisho? Hebu tuzame kwenye somo letu linalohusu hukumu mbili kati ya zile za kale katika Biblia na tujifunze zaidi!
- Mifano
-
- Soma 2 Petro 2:1-3. Petro anaonya dhidi ya nini? (Waalimu wa uongo mafisadi na walafi.)
-
- Soma 2 Petro 2:4-6. Kuna mifano ipi ya utayari wa Mungu kutekeleza hukumu kwa waovu? (Ipo mitatu: Mungu aliwatupa malaika waovu kutoka mbinguni, Mungu akaleta gharika, na Mungu akaigeuza Sodoma na Gomora kuwa majivu.)
-
-
- Biblia inafikisha ujumbe gani? (Mungu anaweza kuwaadhibu waovu kabla ya muda wa hukumu ya mwisho. Adhabu hizi za awali ni mifano ya kile kitakachotokea kwa watu wasio wacha Mungu.)
-
- Gharika
-
- Soma Mathayo 24:36-37. Je, mtu amewahi kukwambia, “Siwezi kukwambia, lakini ninaweza kukudokeza?” Je, hicho ndicho kinachosemwa katika vifungu hivi?
-
-
- Unawezaje kutoa vidokezo halali ikiwa hujui “siku na saa” ya kurudi kwa Yesu Mara ya Pili? (Yesu anasema kuwa matukio yanayofanana na hayo yanaweza kutupatia ishara tu.)
-
-
- Soma Mathayo 24:38-39. Je, hizi ni shughuli za kawaida? (Ndiyo.)
-
-
- Watu wanaoishi maisha yao ya kawaida wanashitukizwaje (surprised) na gharika? (“Hawakutambua.”)
-
-
- Soma 2 Petro 3:10. Mtu wa kawaida anafahamu kwa kiasi gani habari za wezi? Je, wanadhani kuwa wanaweza kufanyiwa vitendo vya unyang’anyi? (Ndiyo. Hawadhani tu kuwa kitendo hicho kitatokea hivi karibuni. Hebu tuchunguze jambo hili zaidi.)
-
- Soma Mwanzo 6:5-8. Wanadamu ni wabaya kiasi gani? (Dhamira zao zilikuwa ovu tu wakati wote.)
-
-
- Mungu anakuwa na mwitiko gani katika hilo? (Anajutia kuwaumba wanadamu na anaamua kuwaangamiza.)
-
-
- Soma Mwanzo 6:3. Mungu anasema nini? Wanadamu wataishi kwa muda mfupi? Au ndani ya miaka 120 maisha ya watu duniani yatakoma? (Ukisoma maoni ya Mungu katika 1 Petro 3:20 kifungu hicho kinasema kuwa Mungu aliwavumilia wanadamu wakati wa ujenzi wa safina. Hiyo inaonekana kama miaka 120 ndio kipindi cha uvumilivu wa Mungu.)
-
- Soma 2 Petro 2:5. Tafsiri ya ESV inamwita Nuhu “mjumbe wa haki.” Soma Mwanzo 6:13-14, inayotwambia kuwa Nuhu alijenga safina ili kufanya ulinzi dhidi ya gharika inayokuja. Ikiwa Nuhu anajenga meli hii kubwa kabisa ambayo haijawahi kutokea, ikiwa Nuhu anahubiri (anatangaza) habari njema ya hukumu inayokuja, Mungu anawezaje kuwaambia watu wa kipindi hicho kuwa “wasio na ufahamu?”
-
- Hebu tuchambue kwa kina usuli wa kauli ya Yesu. Soma Mathayo 24:30. Ni nini iliyo mada ya mjadala wa Yesu? (Ujio wake wa Mara ya Pili.)
-
- Soma Mathayo 24:32-35. Hiki ndicho alichokisema Yesu kabla ya kauli yake katika Mathayo 24:36 kwamba hakuna anayejua muda wa ujio wake wa Mara ya Pili. Tunaweza kujua nini kuhusu muda wa ujio wa Mara ya Pili? (Kuna ishara. Unaweza kuwa na uelewa wa jumla kwamba hukumu ya mwisho inakaribia kutekelezwa.)
-
-
- Sasa fikiria, kama alivyofafanua Yesu, ndoa katika kipindi ambacho Nuhu alikuwa anajenga safina. Je, bwana na bibi harusi wangeweza kuwa na ufahamu wa meli kubwa na onyo dhidi ya gharika inayokuja? (Ndiyo. Lakini wamejikita kwenye maisha yao sasa hivi. Hawajajikita kwenye mwisho wa dunia yao.)
-
-
-
-
- Je, utawaita kuwa “wasio na ufahamu?”
-
-
-
- Hebu tukae pembeni kidogo. Mada yetu ni juu ya jinsi hizi hukumu za awali zinachoweza kutufundisha kuhusu hukumu ya mwisho. Je, Roho Mtakatifu atawapa wale wanaotenda uovu concern ya jumla kuhusu hukumu?
-
- Soma Mathayo 24:40-42. Tunapaswa kuwa tukifanya nini ili kujiandaa kwa ujio wa Mara ya Pili? (“Kukesha.” Kuwa macho.)
-
- Soma Mathayo 24:43-44. Kumbuka rejea ya Petro ya kufanyiwa vitendo vya unyang’anyi. Je, bwana angefanya nini tofauti kama angejua mwivi anakuja muda fulani? (Angekaa macho.)
-
-
- Mojawapo ya matatizo makubwa ya msingi katika kufundisha Biblia ni kuifanya iwe ya muhimu na kueleweka. Utafanya nini katika kujibu maelekezo ya “kukesha?” “Kuwa macho?”
-
-
- Soma Mathayo 24:44-46. Ni jambo gani hasa linafanywa na mtumishi huyu? (Anajishughulisha na kazi aliyopewa na bwana wake.)
-
- Soma Mathayo 24:48-49. Kinyume chake, mtumishi mwovu anafanya nini? (Anajihusisha na shughuli ambazo si sehemu ya kazi yake.)
-
- Sote tunahitaji kulala, tunatakiwa kuwa “macho” kwa wezi, na hatujui mwizi atakuja lini. Tunapaswa kuwa tunafanya nini? Kujaribu kubashiri kwa umahsusi zaidi muda atakaokuja mwizi? Au kuwa waaminifu katika kazi yetu ya kuifanya nyumba kuwa salama kadiri tunavyoweza? (Yesu anatwambia kufanya kazi aliyotupatia. Kuwa waaminifu katika juhudi zetu za kuutangaza Ufalme wa Mungu. Hatuambii kuwa tujaribu kubainisha muda wa kuibiwa.)
-
-
- Utaona kwamba mtumishi anaihudumia “familia.” Kuwa mama mwaminifu. Kama una kazi kanisani kwako, itende kwa uaminifu. Huko ni kuwa macho.
-
- Sodoma na Gomora
-
- Soma Mwanzo 18:20-22. Mungu anajadiliana na nani kuhusu mustakabali wa Sodoma? (Ibrahimu. Hatutasoma vifungu vinavyofuatia, lakini Ibrahimu anashauriana na Mungu kipimo cha kuangamizwa kwa Sodoma. Kama kuna watu kumi waaminifu katika mji wote, Mungu hatauangamiza.)
-
- Soma Mwanzo 19:1-3. Lutu anajenga hoja “kwa nguvu” kwamba malaika hawa wawili wasikae uwanjani usiku kucha. Kwa nini?
-
- Soma Mwanzo 19:4-5. Hili ni jibu la swali la awali. Wanaume wote wa Sodoma wanataka kuwafanyia nini kwa uthabiti wageni wa Lutu? (Wanataka “kuwajua.”)
-
-
- Je, wanataka tu kufahamiana na wageni hawa? (Soma Mwanzo 19:6-7. Lutu anawarejelea watu wa mji ule kuwa “wabaya.” Wanadai kwamba wapewe wageni ili wawabake.)
-
-
- Soma Mwanzo 19:8-9. Kama tutakavyoona, Lutu anaokolewa na Mungu kama mmojawapo wa watu wenye haki katika Sodoma. Je, inakuwaje haki kuwatoa mabinti wako ili wabakwe badala ya wageni ambao umekutana nao punde tu? (Kwa dhahiri, kitendo hicho hakitakuwa cha haki. Lakini Lutu anajua jambo ambalo ana uhakika litawaepusha na kuwafanya mabinti wake kuwa salama – wanaume hawa ni mabasha/wasenge (homosexuals).)
-
- Soma Mwanzo 19:10-11. Malaika wageni waliwashindaje wasenge wabakaji watarajiwa?
-
- Hivi punde tu Ibrahimu alikuwa na mjadala na Mungu kuhusu kuiangalia asili ya watu wa Sodoma. Hiyo inafuatiwa na kisa hiki. Biblia inafikisha ujumbe gani? Dhambi ya Sodoma ni ipi?
-
- Soma Yuda 6-7. Yuda anaielezeaje dhambi ya Sodoma na Gomora? (Anaiita “uasherati” na “mambo ya mwili yasiyo ya asili.”)
-
- Soma Ezekieli 16:49-50. Hii inaelezeaje dhambi za Sodoma? (Kiburi na kutowasaidia maskini na wahitaji ingawa walikuwa na chakula cha kutosha na muda wa kutosha. Kifungu pia kinabainisha kufanya “machukizo.” Kuna watu wengi katika zama za leo wanaohoji, kutokana na kifungu hiki, kwamba tatizo la Sodoma lilikuwa dhambi ya jumla, na kwa umahsusi kutowasaidia maskini. Lakini vitabu vya Mwanzo na Yuda vinabainisha asili ya dhambi ya Sodoma. Ukweli kwamba watu wa Sodoma pia walijihusisha kwenye dhambi nyingine hakuiondoi dhambi iliyobainishwa.)
-
- Soma Mwanzo 19:24-25 na Mwanzo 19:28. Kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora kunatufundisha nini kuhusu hukumu ya mwisho?
-
- Soma 2 Petro 2:5 na 2 Petro 2:7-9. Tunaona tumaini gani kwenye vifungu hivi? (Mungu anajua jinsi ya kutuokoa kutoka kwenye majaribu!)
-
-
- Kifungu cha 8 kinatuambia kuwa Lutu aliteseka kwa dhambi iliyomzunguka kote. Kwa nini hakuondoka? Nuhu hakuwa na uchaguzi kama huo. (Hili linatuliwaza. Mungu anamrejelea Lutu kwa uchanya hata kama alikuwa na dosari za dhahiri.)
-
-
-
- Kifungu cha 9 kinatuambia kuwa Mungu anawaweka wasio na haki “katika hali ya adhabu” kabla ya hukumu ya mwisho. Unadhani hiyo inamaanisha nini?
-
-
- Rafiki, je, utayatafakari maisha yako kwa dhati kabisa? Matendo yetu yanahusika, na si mara zote Mungu anasubiria hadi kwenye hukumu ya mwisho ili kufanya uamuzi juu ya maisha yetu. Kwa nini usimgeukie sasa hivi? Kwa nini usifanye uamuzi wa kuwa mtumishi mwaminifu wakati ukimsubiria Yesu kurudi?
- Juma lijalo: Ruthu na Esta.