Somo la 12: Watangulizi
Somo la 12: Watangulizi
(Danieli 2-3, Matendo 12)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Jaribu linakujiaje? Je, ni katika mambo makubwa au mambo madogo maishani? Somo letu juma hili linahusu visa viwili ambapo vijawa wawili walikabiliana na suala la kupoteza uhai wao kwa kuwa waaminifu kwa Mungu. Unaweza kuwa unatafakari, “Kamwe sijawahi kupitia kitu kama hicho, na ninatumaini sitakipitia!” Hata hivyo, kumbuka kuwa baadhi ya vijana hawa walianza na suala la uaminifu wao kwa Mungu lilipokuja suala la chakula. Je, inawezekana kwamba hatujakabiliana na chaguzi kubwa, za kuvutia kwa sababu tumeshindwa katika chaguzi ndogo? Au, tumepoteza muono wa taswira pana – kwamba masuala yote ya uaminifu kwa Mungu, makubwa kwa madogo, ni ya muhimu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu kuwa waaminifu kwa Mungu tunapokuwa katika shinikizo la kutisha!
- Ndoto
-
- Soma Danieli 2:1-3. Je, umewahi kuota ndoto iliyokuhangaisha? Je, ndoto hiyo ilikufanya ukose usingizi?
-
-
- Je, umewahi kudhani kuwa ndoto yako ilikuwa (au ingeweza kuwa) ujumbe kutoka kwa Mungu?
-
-
-
- Unadhani kwa nini Nebukadreza alifadhaika sana kuhusiana na ndoto yake? (Wafalme wanajua kuwa wao ni wa muhimu. Kwa hiyo, lazima ndoto zao zitakuwa za muhimu. Tafsiri ya The New Bible Commentary inatuambia kuwa katika zama za kale wafalme wa Mashariki ya Karibu waliamini kuwa miungu iliwapatia ujumbe kwa njia ya ndoto.)
-
-
-
-
- Je, Mungu wa kweli angeweza kumpa Nebukadreza ujumbe kwa njia ya ndoto? (Soma Danieli 2:29. Mungu alimpa Nebukadreza ndoto yake.)
-
-
-
- Soma Danieli 2:4-6. Nebukadreza alikuwa bosi wa namna gani?
-
-
- Je, unadhani kundi hili la wataalamu lilijutia kile walichokisema katika kifungu cha 4?
-
-
- Unadhani kwa nini Nebukadreza aliwasisitiza wataalamu wake wamwambie undani wa ndoto yake? (Soma Danieli 2:8-9. Nebukadreza aliamini kuwa wamekuwa wakimdanganya. Kama wanaweza kuelezea mambo yajayo kwa njia ya ndoto, basi linapaswa kuwa jambo dogo kuelezea yaliyomo kwenye ndoto yake. Hiki kilikuwa kipimo cha uaminifu wao na uwezo wao wa kuitafsiri ndoto kwa usahihi. Kama hawatamweleza ukweli, kulikuwa na haja gani ya wao kuendelea kuwapo? Tatizo la kutafsiri ndoto ilikuwa ni kwamba wangeweza kumwambia jambo lolote. Sasa Nebukadreza alikuwa na njia madhubuti ya kupima kile alichokuwa akiambiwa.)
-
- Hebu turuke vifungu kadhaa chini na tusome Danieli 2:17-18. Kwa dhahiri Danieli aliahidiwa muda zaidi na Mfalme. Kwa nini Danieli aliwahitaji marafiki wake waombe kuhusiana na jaribu hili? (Lazima Danieli aliamini kuwa sala ya kundi ni bora zaidi.)
-
-
- Je, unakubaliana kwamba sala ya pamoja (kwenye kikundi) ni bora zaidi? (Soma Mathayo 18:19-20.)
-
-
- Soma Danieli 2:19. Mungu anajitokeza! Danieli anafanya nini baada ya Mungu kufunua siri? (Anamtukuza Mungu!)
-
- Soma Danieli 2:27-28. Utaona kwamba Danieli hataji jina lake mwenyewe hata mara moja. Hasemi chochote kuhusu nafasi yake katika ufunuo huu. Kwa nini?
-
- Soma Danieli 2:29-30. Hatimaye, Danieli anabainisha wajibu wake katika mambo haya. Soma na kujifunza maneno ya Danieli katika vifungu hivi. Anaelezeaje wajibu wake, wajibu wa Mfalme, na wajibu wa Mungu katika mchakato huu?
-
- Soma Danieli 2:31-34. Hatutaingia kwenye undani wa ndoto hii ya kinabii, isipokuwa kusema kuwa inaelezea historia ijayo ya ulimwengu!
-
-
- Ulipoona picha ya msanii ikielezea taswira hii, je, ilionekana kuwa ya “kutisha?”
-
-
- Soma Danieli 2:46-47. Je, Nebukadreza alipata ujumbe wa kwamba habari hizi zilimhusu mtu gani? (Si kwa uhakika. Si tu kwamba Mfalme anaanguka chini mbele ya Danieli, bali pia anasema “wewe uliweza kuifumbua siri hii.” Hata hivyo, Nebukadreza anapata ujumbe kuwa Mungu mkuu wa Mbinguni ndiye “Mungu wa Miungu na Bwana wa wafalme.”)
- Tatizo Linalofuata
-
- Soma Danieli 3:1. The SDA Bible Commentary inabainisha kuwa sanamu hii ina urefu sawa na Mnara wa Uhuru uliopo katika bandari ya Jiji la New York. (Bila kujumuisha kiegemezo chini ya mnara.) Unadhani kitu gani kilimhamasisha Mfalme Nebukadreza kuagiza kazi hii ya kisanii ya ghorofa kumi? (Bila shaka haya ni matokeo ya ndoto ambayo Danieli aliitafsiri.)
-
-
- Mara moja ninaona leseni ya kisanii ikichukuliwa na sanamu iliyoonekana katika ndoto. Sanamu halisi inakengeukaje/inatofautianaje na sanamu ya kwenye ndoto? (Soma Danieli 2:37-38. Katika ndoto, kichwa pekee ndicho kilichotengenezwa kwa dhahabu. Kichwa ndio sehemu pekee iliyomwakilisha Nebukadreza.)
-
-
-
- Kama ungekuwa Nebukadreza, kwa nini ungetaka kutengeneza sanamu yote kwa dhahabu? Kuwa mwaminifu kwa ndoto kunaweza kukuokolea fedha nyingi! (Nani anayetaka kukumbushwa kwamba yeye (na ufalme wake) ni viumbe wenye kufa na wana siku chache tu za kuishi? Kimsingi, pia kuna suala la lile jiwe sumbufu (Danieli 2:34-35) ambalo linasahaulika.)
-
-
-
-
- Unadhani sanamu hii ilikuwa na sura ya nani?
-
-
-
- Soma Danieli 3:3-5. Je, watu walifahamu kabla kwamba hii ilikuwa sherehe ya kawaida ya kuweka wakfu – kwamba kimsingi hili lilikuwa tukio la kidini?
-
- Soma tena Danieli 2:46-47. Mfalme Nebudareza anawezaje kutoka nje ya msitari kiasi hicho?
-
- Soma Danieli 2:49. Je, unadhani Daniel alikuwa na uelewa kabla wa kile alichokiwaza Mfalme kwa ajili ya sherehe ya kuweka wakfu? (Danieli ndiye aliyetafsiri ndoto. Daniel ndiye aliyetumikia katika uga wa kifalme. Kimsingi alifahamu mnara huu mkubwa ulikuwa unajengwa katika uwanda wa Dura. Hata hivyo, inawezekana Nebukadreza alidhani, kutokana na ndoto halisi, kwamba ilikuwa vyema kutomwambia Danieli alichokuwa anakipanga mawazoni mwake na kumtuma Danieli kwenda safari ya kikazi. Inaonekana haikuwa jambo la kawaida kwa Danieli kuwa na uelewa wa kabla juu ya matakwa ya ibada, akapanga safari kwenda nje ya mji, na asiwaonye marafiki wake watatu.)
-
- Soma Danieli 3:6. Kwa nini tanuru ya moto ni sehemu ya amri hii? Je, palikuwepo na tatizo la uaminifu katika ufalme ule? (Huenda Danieli na marafiki wake watatu walikuwa wanapata waongofu kwa Mungu wa kweli.)
-
- Soma Danieli 3:8-12. Unadhani Wakaldayo (wenye hekima wa Babeli) walimchukuliaje Danieli na marafiki wake watatu? (Watumwa mateka wanapandishwa vyeo juu yenu? Suala hilo lilikuwa kashfa! Nina uhakika vijana hawa walisahau mapema kabisa kwamba maisha yao yaliokolewa na Danieli na kwamba walikuwepo watu wengi wenye wivu miongoni mwa “wenye hekima wa Babeli” juu ya uwezo na mamlaka ya hawa mateka wa Kiyahudi.)
-
- Soma Danieli 3:13-16. Unadhani kwa nini Nebukadreza aliwauliza marafiki hawa watatu kama jambo hili ni kweli? (Alipendezewa (appreciated) nao.)
-
-
- Unadhani kwa nini marafiki hawa watatu walijibu, “hamna haja kukujibu katika neno hili?” (Swali lilikuwa “mungu yupi” atakayewaokoa? Nebukadreza alifahamu kwa uhakika aliyekuwa Mungu wao.)
-
-
- Soma Danieli 3:17-18. Una maoni gani juu ya kauli ya marafiki watatu ya “bali kama si hivyo?” (Imani iliyoje!)
-
- Soma Danieli 3:22-26. Mungu gani aliyewaokoa?
-
- Soma Danieli 3:30. Je, unataka kuishi maisha yenye mafanikio?
- Petro
-
- Soma Matendo 12:1-3. Je, unakumbuka kisa cha mamaye Yakobo akimwendea Yesu kumwomba kwamba wanaye (Yakobo na Yohana) wakae mkono wa kuume wa Yesu katika ufalme wake? Kisa hicho kinapatikana katika Mathayo 20:20-23.)
-
-
- Soma Mathayo 20:22-23. Je, Yakobo amekinywea kikombe cha Yesu? Je, hiki ndicho alichokuwa anakiwaza mamaye Yakobo? (Hiki ni kielelezo kikamilifu cha ukinzani wa injili. Yesu anataka tubarikiwe. Amri zake zinalenga kutusaidia kuwa na maisha mazuri. Lakini kuwa mfuasi wa Yesu wakati mwingine inamaanisha kwamba tunateseka. Waebrania 11 inaelezea matendo haya tofauti kabisa, lakini inatuahidi kuwa hatimaye watu wote watapata kile ambacho Mungu amekiahidi.)
-
-
- Soma Matendo 12:4-6. Je, hii imepita kiasi? Askari kumi na sita kumlinda mhubiri mmoja ambaye amefungwa minyororo gerezani?
-
-
- Kama ungekuwa Petro, je, ungeogopa? Je, ungewafikiria marafiki watatu wa Danieli? Je, ungemfikiria Yakobo na kauli ya Danieli 3:17-18 ya “bali kama si hivyo” ya marafiki watatu? (Petro amelala!)
-
-
- Soma Matendo 12:7-10. Je, Petro anastaajabishwa (surprised) na Mungu?
-
- Soma Matendo 12:12-15. Je, wale wanaomwombea Petro wanashangazwa na Mungu? Wanashangazwa na jibu la maombi?
-
- Rudi nyuma na usome Matendo 12:11. Je, Petro alikuwa na uhakika kuwa ataokolewa? Je, anafanana na marafiki watatu?
-
- Rafiki, Ufunuo inatuambia kuwa mwisho wa dunia unapokaribia tutakabiliana na changamoto kubwa katika imani yetu. Je, utadhamiria, kama ilivyokuwa kwa Danieli na marafiki wake watatu, na kama ilivyokuwa kwa Petro, kusalia kuwa mwaminifu kwa Mungu na kumtumaini bila kujali chochote kitakachotokea?
- Juma lijalo: Taswira za Mwisho (Tamathali za Semi za Ule Mwisho.