Somo la 11: Kukaa na na Kristo
Somo la 11: Kukaa na na Kristo
(Wakolosai 2)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Je, inajalisha jinsi unavyoishi? Je, mawazo yako yanajalisha? Majuma mawili yaliyopita, tulijifunza kwamba tukiendelea kuwa imara kiimani katika Yesu, na “tusihame” na kumwacha Yeye, tunaweza kuwa na uhakika kwamba tunaokolewa kutoka katika dhambi zetu. Hilo linatufanya tudhani kuwa haijalishi kile tunachokifanya ilimradi hatugeuki na kumwacha Yesu. Katika Wakolosai 3, Paulo anatuambia kuwa kile tutendacho na kukitafakari ni muhimu. Hatuko huru kutenda lolote tulitakalo, tukiwa na uhakika kuwa “Mungu atasamehe.” Mungu atasamehe, lakini hilo halipaswi kuwa msingi wa rejea yetu kwa ajili ya mawazo yetu. Hebu tuzame kwenye fundisho la Paulo kuhusu jinsi tunavyopaswa kutafakari na kuishi maisha yetu kama watoto wa Mungu!
- Kinachofuata?
-
- Soma Wakolosai 3:1. Paulo anapoanza kwa kusema, “Basi mkiwa mmefufuliwa,” anamaanisha nini? Kwa nini hili ni muhimu? (Paulo anawaandikia wale waliookolewa kwa imani pekee. Hawaandikii wale waliochanganyikiwa kuhusu endapo matendo yao ni sehemu ya ufunguo wa wokovu wao.)
-
-
- Ikiwa mko imara katika wokovu wenu, tunapaswa kutafuta nini? Mambo “yaliyo juu” ni yepi? (Mbinguni.)
-
-
-
- Ningekwambia “uitafute mbingu,” ungefanya nini? Ungenijibuje? (Ningejibu kuwa ninatakiwa kuiweka imani yangu katika Yesu. Lakini hiyo haionekani kama namna ambayo Paulo anatutaka tujibu.)
-
-
-
- Tafakari tena kauli ya Paulo ya “Basi, mkiwa.” Ikiwa mmeokolewa kwa neema, basi mnatakiwa kutafakari juu ya kuyapata (kuyatafuta) mambo ya kimbingu. Je, hivyo ndivyo unavyoielewa?
-
-
- Soma Wakolosai 3:2. Je, hii inakuelezea wewe? Mwitiko wangu wa awali ni kwamba kifungu hicho hakinielezei mimi. Ninayatafakari mambo yanayonizunguka. Ninatafakari juu ya ninachotakiwa kukitenda, ambacho ningependa kukitenda, na jinsi ambavyo ningependa kuboresha mambo.
-
-
- Fikra yangu ya pili ni kwamba kuyatafakari mambo yanayonizunguka kunaifanya akili yangu iyatafakari “mambo ya juu,” angalao kwa kiasi fulani. Kwa mfano, sasa hivi ninatafakari jinsi ninavyopaswa kuandika somo hili vizuri zaidi. Sasa hivi nipo Michigan ili kusaidia mustakabali wa Chuo Kikuu cha Andrews – chuo kikuu cha dhahiri cha Kikristo. Je, hii inatosheleza maelekezo ya Paulo ya kuyatafakari mambo “ya juu?” Au ukweli kwamba Andrews na mimi tupo duniani inamaanisha kuwa hili halihusiki?
-
-
- Soma Wakolosai 3:3-4. Paulo anatumia neno jingine la kiunganisho. Anasema “kwa maana” mlikufa – ikimaanisha kufa pamoja na Yesu pale mlipobatizwa. Angalia Wakolosai 2:12. Kifo chetu katika Kristo, na “kufichwa” katika kile ambacho Yesu ametutendea, vinahusianaje na mahali ambapo mawazo yetu yanajikita? (Kufichwa katika Yesu inamaanisha kuwa tuko salama katika Yeye. Tunaweza kujikita kwenye jambo jingine.)
-
-
- Kamwe sijawahi kuanzisha biashara, lakini ninachukulia kwamba biashara inapoanza mmiliki anafanyia kazi masuala ya msingi ya kuifanya biashara kuwa wazi. Vipi kama mwekezaji tajiri atamjia mmiliki na kusema, “Usiwe na wasiwasi juu ya kuiacha wazi milango yako, nitashughulika na hilo. Badala yake fanyia kazi jinsi unavyoweza kuboresha biashara.” Hilo linawezaje kuyafanya upya mazingatio ya mmiliki?
-
-
-
- Je, hii ni analojia ya haki? Kwamba badala ya kujikita kwenye kuzishinda dhambi katika maisha yetu, tujikite kuwaleta wengine kwa Yesu?
-
- Yaueni
-
- Soma Wakolosai 3:5. Niliposoma hili nikatafakari kile nilichokiandika hivi punde hakipo sahihi. Paulo anaandika juu ya kukabiliana na dhambi mahsusi. Inaonekana kama Paulo anatutaka tujikite kwenye dhambi katika maisha yetu. Je, nilikuwa ninakuelekeza katika uelekeo usio sahihi?
-
-
- Ikiwa mtu atayazika mambo hayo maovu anayoyataja Paulo, je, itaifanya akili iwe huru kutafakari na kupanga juu ya kuutangaza ufalme wa Mungu? (Tafakari nyuma kwenye kifungu cha 3 kinachosema kuwa “mlikufa.” Paulo anasema kuwa tunatakiwa kutoa hatima ile ile kwa dhambi hizi zilizoorodheshwa. Tunatakiwa kuzifanya zife.)
-
-
-
- Je, unaweza kuona namna ya kujikita kuzifanya dhambi hizi “zife” na bado kuziweka akili zetu kwenye mambo ya kimbingu? (Sehemu ya kuzifanya akili zetu zijikite mbinguni na kuutangaza ufalme wa Mungu si kuyaelekeza mawazo yetu kwenye mambo mabaya. Kwa muktadha huo “tunayaua” mambo ya “kidunia.”)
-
-
-
- Angalia orodha ya dhambi katika kifungu cha 5. Zina jambo gani la kufanana, tofauti na kuwa dhambi? (Ni dhambi za “tamaa.” Ni mambo unayoyataka, mengi ambayo yamefungamanishwa na tamaa ya ngono.)
-
-
-
-
- Tafakari mfano huu. Unakutana na mtu anayevutia sana wa jinsia tofauti. Je, mwitiko wako wa kwanza ni, “Ninawezaje kumfanya anipende? Au ni, “ninawezaje kumfanya aipende injili?
-
-
-
-
-
- Je, hii inafafanua jinsi tunavyoweza kujikita kwenye mambo ya kimbingu wakati huo huo kuua dhambi hizi za tamaa?
-
-
-
-
- Utaona kwamba tamaa inaitwa “sanamu.” Unafafanuaje hilo? Si kukisujudia kitu. (Huu ni ufafanuzi mwingine mzuri wa tofauti kati ya kuziweka akili zetu kwenye mambo ya kimbingu na kuziweka kwenye dhambi za tamaa. Kutamani kitu ni kutaka kitu cha mtu mwingine. Dhambi ni kupanga jinsi ya kujipatia kitu hicho. Kujikita kwenye mambo ya kimbingu itakuwa ni mpango wa kuandaa mambo yanayoutangaza ufalme wa Mungu.)
-
-
- Soma Wakolosai 3:6. Kwa nini dhambi hizi za tamaa zinasababisha hukumu ije? (Mkristo akijikita katika kuridhisha tamaa yake, na si kuutangaza ufalme wa Mungu, hakuna sababu ya Mungu kusubiri zaidi kurejea.)
-
- Soma Wakolosai 3:7-9. Angalia orodha hii mpya ya dhambi. Hizi si dhambi za tamaa. Ni dhambi zipi hizi? Zinafananaje? (Ni dhambi zinazowatenganisha watu.)
-
-
- Je, hii ni hoja ya kujaribu kuepuka kuwafedhehsha watu wengine? (Jambo fulani kuhusu kuamini kuwa unaufahamu ukweli husababisha mawazo thabiti. Sidhani kama kuna ubaya wowote kwenye mawazo thabiti, lakini tunatakiwa kuwa na ukomavu wa kihisia katika namna tunavyoyashiriki mawazo hayo na watu wengine.)
-
-
-
- Niliulizwa kuhusu makala niliyoiandika (si kwenye GoBible) ambapo nilitumia mbinu ya “kubomoa kabisa” hoja ya upande pinzani. Je, tunapaswa kila wakati kuwa waangalifu sana tusije kuwaudhi wengine? (Nitawaacha wengine wafanye uamuzi juu ya manufaa ya kutumia njia yangu katika hiyo makala. Lakini ninaona tofauti ya kujenga hoja kwenye mawazo na dhana zinazosukumwa kwa nguvu na makundi mengine, na kubishana kwa hoja na mtu mwingine. Angalia kile anachokifanya Paulo hapa: anaandika juu ya kuua njia fulani za fikra.)
-
- Ziponyeni
-
- Soma Wakolosai 3:10-11. Je, bado Paulo yuko kwenye mada ya kuepuka kuwatenganisha watu? (Ndiyo, sasa anaandika juu ya mitazamo inayotuleta pamoja. Tukiona kuwa makundi yote haya tofauti yako pamoja katika Yesu, itabadili mtazamo wetu kuhusu tofauti zilizopo.)
-
- Soma Wakolosai 3:12. Jambo gani linafanana kwenye mitazamo hii? (Inaponya tofauti zilizopo. Kuwa na mitazamo hii husaidia kuepuka migogoro.)
-
-
- Lakini vipi kama mtazamo wako uko sahihi? (Mambo mawili. Kuwa sahihi ni muhimu na jambo sahihi kimaadili halipaswi kutiwa matatani (compromised). Lakini una uhakika kwamba uko sahihi? Ni kwa jinsi gani “unyenyekevu, upole na uvumilivu” unaathiri jinsi unavyoshikilia mtazamo wako?
-
-
- Soma Wakolosai 3:13. Tunapofikiria gharama ya kumsamehe mtu aliyetujeruhi, tunapaswa kutafakari nini? (Ni kwa kiasi gani Yesu ametusamehe. Na msamaha wake ulimgharimu nini.)
-
- Soma Wakolosai 3:14. Upendo “unatufungaje” pamoja? (Unatoa nafasi zaidi kwa wale unaowapenda – angalao unapaswa kufanya hivyo.)
-
- Soma Wakolosai 3:15. Kama hauna mgogoro na watu wengine, je, maisha yako ni ya amani zaidi? (Naam. Hicho ndicho anachotupatia Paulo, maisha ya amani zaidi.)
-
-
- Sehemu ya mwisho katika kifungu hiki ni ya muhimu kiasi gani, ushauri wa kuwa na “shukrani?” (Mtazamo huu ni kinyume cha kuwa na tamaa. Nadhani kuwa na shukrani ni jambo la muhimu sana katika kuwa na maisha ya amani.)
-
-
- Soma Wakolosai 3:16. Tunapata mwongozo gani halisi wa kuwa na maisha ya amani zaidi, yaliyojikita katika masuala ya mbinguni? (Kufanya kile unachokifanya sasa hivi, ambacho ni kukaa ndani ya neno la Mungu. Kujifunza na kufundisha neno la Mungu.)
-
- Soma Wakolosai 3:17. Je, haya ni maisha yaliyojikita katika masuala ya mbinguni? Kwamba chochote tukifanyacho, tunakifanya kwa jina la Yesu?
-
-
- Ni kwa jinsi gani hasa utafanya hivyo? (Unapaswa kuutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu, na unapaswa kujiuliza, “Ni jambo gani la Kikristo la kulitenda hapa?”)
-
-
- Rafiki, je, una mawazo bora zaidi sasa hivi kuhusu jinsi ya kuyazingatia mawazo yako kwenye mambo ya kimbingu? Kwa nini usimwombe Roho amtakatifu, sasa hivi, akusaidia katika kipindi hicho cha mpito?
- Juma lijalo: Kuishi Pamoja Sisi kwa Sisi.
