Somo la 1: Kuuhakiki Uhalisia
Somo la 1: Kuuhakiki Uhalisia
(Ufunuo 3, Yohana 15)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Kama unafanana na waajiriwa wengi, una (au ulikuwa nayo ulipokuwa ukifanya kazi) aina fulani ya tathmini ya kazi yako. Je, umewahi kusikia tathmini ya maisha yako ya kidini? Katika shule ya sheria ni kawaida kwa tathmini pekee ya mwanafunzi kuwa mtihani wa mwisho. Wengi wanayachukulia hivyo maisha ya Kikristo. Yesu atakapokuja utajua kama umefaulu! Somo letu juma hili linahusu kufanyia tathmini uhusiano wetu na Mungu na jinsi tunavyoweza kuuboresha. Hebu tuzame kwenye somo letu!
- Kanisa la Laodikia
-
- Soma Ufunuo 1:4-5. Makanisa mangapi yanapokea ujumbe kupitia kwa Yohana kutoka kwa Yesu na roho saba? (Saba.)
-
- Pitia kwa haraka haraka sura ya 1-3 ya kitabu cha Ufunuo na kisha usome Ufunuo 3:14. Kanisa lipi kati ya makanisa saba ndilo kanisa la Laodikia? (Kanisa la saba.)
-
-
- Tunafahamu kwamba kanisa la Laodikia lilikuwepo katika Bonde la Mto Lycus katika eneo la Frigia. Hiyo inatuambia kuwa lilikuwa kanisa halisi. Je, unadhani ujumbe unaofuatia ni kwa ajili ya washiriki wa kanisa hilo pekee? Kama umesema, “ndiyo,” kwa nini basi tunaliona kwenye Biblia? (Wasomi wengi wa Biblia wanajibu, “hapana.” John McArthur anatoa maoni kwamba makanisa haya saba pia yanawakilisha aina ya makanisa yaliyopo “kupitia kwenye umri wa kanisa.”)
-
-
-
- Unadhani kwamba kwa kuwa Laodikia ni kanisa la mwisho kati ya makanisa saba, linaelezea Wakristo wanaoishi katika siku za mwisho? (Huu ndio mtazamo wa watu wengi. Pia wanaamini kuwa tunaishi katika siku za mwisho na hivyo ujumbe kwa Laodikia unahusika kwetu.)
-
-
-
- Kimsingi, kuna uwalakini mkubwa katika jambo hili. Jambo moja ni kwamba, hatuna uhakika kwamba tunaishi katika siku za mwisho. Una maoni gani? Je, tunaishi katika siku za mwisho hapa duniani?
-
-
- Soma Ufunuo 3:15-17. Hebu tuendelee na assumption kwamba ushauri kwa Walaodikia unahusika kwetu. Mungu anasema kuwa mwitiko wake kwetu ni upi? (Anataka kututapika kutoka kinywani mwake. Kwa dhahiri hilo haliwezi kuwa jambo zuri.)
-
- Angalia tena Ufunuo 3:17. Mtazamo wa Walaodikia unalinganishwaje na uhalisia? (Ni kinyume kabisa. Wanadhani wao ni matajiri na hawahitaji chochote; kimsingi, wao ni maskini na wanahitaji kila kitu- hadi nguo.)
-
-
- Maoni yao yanawezaje kuwa ya uongo sana kiasi hicho? Mtu anawezaje kuwa uchi na mnyonge na kudhani kuwa yeye ni tajiri na hana haja ya kitu chochote? (Ama washiriki hawa wana tatizo la afya ya akili, au wana vigezo tofauti.)
-
-
- Soma Ufunuo 3:18. Hebu subiri kidogo! Kama watu hawa ni maskini, wanawezaje kununua dhahabu au mavazi meupe?
-
-
- Ni kwa jinsi gani kulipia dhahabu na mavazi kunaweza kuwafanya wawe matajiri? (Kwa dhahiri sana, tuna mitazamo miwili tofauti. Kubadili mali moja na nyingine hakuongezi utajiri. Tulicho nacho ni mitazamo tofauti wa kile ambacho Walaodikia wanakihitaji.)
-
-
- Soma Ufunuo 7:13-14 na Isaya 61:10. Ni nini gharama ya mavazi haya meupe? (Hayagharimu chochote. Yanatolewa na Mungu au yanasafishwa kwa damu ya Yesu. Yanatupatia haki yetu mbele ya Mungu.)
-
- Soma 1 Petro 1:6-7. Hii inaashiria kuwa nini kinamaanishwa kwenye rejea ya Ufunuo 3:18 ya “dhahabu iliyosafishwa kwa moto?” (Dhahabu iliyosafishwa kwa moto ni imani.)
-
-
- Hebu tuunganishe dhana hizi mbili kuhusu mavazi meupe na dhahabu iliyosafishwa ili kuelewa kuna kasoro gani kwa Walaodikia. Ni nini hitimisho lenye mantiki juu ya kasoro iliyopo kwao? (Wamekataa haki kwa imani pekee. Wamepungukia imani katika haki hiyo. Haki kwa imani ni jambo ambalo kila mtu anaweza kulimudu. Ni karama ya bure.)
-
-
-
- Ni nini msingi wa imani ya Walaodikia kwamba wao ni matajiri na hawahitaji chochote wakati kinyume chake tu ndio ukweli? (Soma Isaya 64:6. Sisi si wasafi. Haki yetu yote ni kama vazi lililochafuliwa. Walaodikia waliyategemea matendo yao mema ili kuonyesha kustahili kwao mbele za Mungu. Hivyo ndivyo walivyodanganywa vibaya sana na hawakuelewa hali yao halisi.)
-
- Kuipindua Laodikia
-
- Soma Ufunuo 3:19. Unamlaumuje mtu asiyeamini katika kuhesabiwa haki kwa imani pekee?
-
-
- Je, wale wanaoamini kuwa wanatenda mambo ambayo Mungu anataka wayatende wana uwezekano mdogo wa kudhani kuwa wanahitaji kutubu?
-
-
-
- Utaona kuwa kifungu kinasema, “uwe na bidii.” Je, kwa kawaida tunawachukulia wale wanaoitegemea imani pekee kama kundi lisilo na bidii?
-
-
-
- Utakuwaje na bidii kutangaza haki kwa imani pekee miongoni mwa watu wengine?
-
-
- Soma Ufunuo 3:20. Ni kwa jinsi gani neno hili la picha ya Yesu kuja katika mlango wa mbele wa nyumba yetu na kubisha linaendana na dhana ya kuhesabiwa haki kwa imani pekee? (Yesu anatujia. Hatufanyi kazi ili kustahili kumwendea Yesu.)
-
-
- Jambo gani linahitajika ili kumfanya Yesu ale pamoja nasi? (Kwanza, tunatakiwa “kuisikia” sauti yake. Hiyo inamaanisha tunatakiwa kuelewa fundisho la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani pekee. Pili, tunatakiwa kufungua mlango. Hii inamaanisha tunatakiwa kulipokea fundisho.)
-
-
- Soma Ufunuo 3:21. Ufunuo inatumia neno “kushinda.” Je, hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea uelewa na fundisho kwamba Yesu alifanya yote?
-
-
- Tunapotafakari kuhusu kujitahidi kutii, hilo linaonekana kuendana zaidi na dhana ya kushinda. Unalielezeaje hilo?
-
-
-
- Kibaya zaidi, Yesu anasema kuwa tunashinda kama alivyoshinda. Yesu hakuokolewa kwa neema pekee. Alitii kikamilifu. Aliteseka kiasi cha kutisha. Tunapaswa kuelewaje kwamba tunashinda kama alivyoshinda Yesu? (Soma Wakolosai 2:11-13. Tuna fursa ya kina sana. Kwa njia ya ubatizo tunashiriki maisha, kifo, na ufufuo wa Yesu, na katika yeye tunahesabiwa haki mbele ya Mungu.)
-
-
-
- Ngoja niulize tena: ni kwa jinsi gani ukubali wa neema kimantiki unaweza kuelezewa kama “kushinda?” (Majivuno yanafanya iwe vigumu kuitegemea neema pekee. Tunajivunia matendo yetu mema.)
-
-
- Soma Ufunuo 3:22. Je, una masikio ya kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia?
- Kuzishika Amri
-
- Soma Yohana 15:9-11 na Yohana 15:14. Je, hii inaonekana kama badiliko la mwelekeo la kisanii? Tunatoka moja kwa moja kwenye kuhesabiwa haki kwa imani pekee hadi kuambiwa kuwa sisi si marafiki wa Mungu ikiwa hatutii amri zake? Je, unaweza kupatanisha tunachokisoma kwenye Ufunuo 3 na kile tunachokisoma katika Yohana 15?
-
- Angalia tena Yohana 15:9. Yesu anataka nini kwa ajili yetu? (Kukaa katika pendo lake.)
-
-
- Yohana 15:10 inatuambia kuwa tunakaa katika pendo la Yesu ikiwa tutazishika amri zake. Je, hii inamaanisha kuwa Mungu hatatupenda ikiwa hatutazitii amri zake? Je, utii ndio kipimo cha upendo wetu kwa Mungu? (Jibu langu ni, “hapana.” Ninaelewa kwamba Mungu alitupatia amri zake ili kuyafanya maisha yetu yawe bora. Amri ni kitendo cha upendo. Tukitaka kukaa katika pendo la Mungu, tunazishika amri zake.)
-
-
- Rafiki, je, unajiamini katika matendo yako, au unaamini kwa ujasiri kuhesabiwa haki kwa njia ya imani pekee? Kwa nini usifanye uamuzi leo wa kupumzika tu kwenye kile alichokutendea Yesu?
- Juma lijalo: Kumjua Mungu.
