Somo la 2: Kumjua Mungu
Somo la 2: Kumjua Mungu
(Mwanzo 1-3, 1 Yohana 4)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Baba wangu alikuwa mtu mzuri. Alikuwa mwerevu, mwenye upendo, mwenye mafanikio, na alitupeleka kanisani kila Sabato. Baba wake, yaani babu wangu, alifariki kabla sijazaliwa. Hilo lilinifanya nitake kujua habari za babu wangu. Lilikuwa jambo la kukatisha tamaa. Kamwe baba wangu hakusema jambo lolote jema kumhusu baba wake na bibi wangu hakuwa na msaada wowote. Usiku mmoja, wakati mimi na baba wangu ambaye sasa amezeeka tulikuwa tumeketi kwenye bembea ya ukumbini nyumbani kwangu, nilimuuliza kama anaweza kuniambia jambo lolote chanya (jema) kumhusu baba wake. Alitafakari kidogo kisha akaniambia kuwa babu wangu alijenga makanisa mawili na kuyahudumia kama mchungaji. Nilifurahi sana na kushangaa kwamba sikuwa nimewahi kujua hili hapo awali. Je, kuna mambo kumhusu Baba wetu wa mbinguni ambayo yanatufurahisha sana na kutushangaza kuyafahamu? Hebu tuzame kwenye somo letu linalohusu kumjua Mungu vizuri zaidi!
- Mungu Muumbaji
-
- Soma Mwanzo 1:1-3. Nani anawajibika na uumbaji tunaouona mahali kote? (Mungu. Biblia haisitisiti. Haikuwa “upandikizaji wa viumbe kutoka anga za mbali.”)
-
-
- Nukuu ya “Roho ya Mungu” katika kifungu cha 2 inatufundisha nini kumhusu Mungu? (Hii inatuambia kuwa Mungu ana “Roho” ambaye ana uwezo wa “kutulia.” Hii inaunga mkono fundisho la Utatu Mtakatifu.)
-
-
-
- Mchakato gani unafanyika ili kutengeneza nuru? (Mungu ananena tu.)
-
-
-
-
- Hii inazungumza nini kuhusu nadharia ya uibukaji? (Inaikanusha. Kama unaamini kuwa Mungu aliumba nuru kwa kunena tu, alikuwa na sababu gani ya kuumba kwa njia ya bahati (chance) na mpangilio wa asili (natural selection)?)
-
-
-
-
-
- Hii inazungumza nini kuhusu uwezo kamili wa Mungu? (Ukweli kwamba baadhi ya Wakristo wanaamini katika chanzo cha nadharia ya uibukaji inaonesha kuwa si tu kwamba hawaiamini Biblia, bali pia hawaamini katika uwezo wa Mungu – ni kushindwa kwa muda mrefu kwa wanadamu.)
-
-
-
- Soma Mwanzo 2:7. Je, Mungu angeweza kumuumba mwanadamu kwa kunena tu? (Naam.)
-
-
- Unadhani kwa nini Mungu “alimtengeneza” mwanadamu kutoka ardhini na “kumpulizia pumzi ya uhai” ndani yake? (Inaonesha kuwa mwanadamu alikuwa wa pekee. Kitu kilichotengenezwa kwa mkono kinachukuliwa kuwa cha pekee (unique).)
-
-
-
- Je, ukweli kwamba Mungu hakunena ili wanadamu wawepo unatoa msingi kwa ajili ya nadharia ya uibukaji? (Hapana. Hii ni kinyume na bahati na mpangilio wa asili.)
-
-
- Soma Mwanzo 1:27. Wanadamu wanatufundisha nini kuhusu asili ya Mungu? (Tuliumbwa “kwa mfano wake.” Ukiunda taswira ya kitu kingine, hilo hukufundisha jambo fulani kuhusu kile cha asili.)
- Kampeni ya Kumpinga Mungu Hadharani
-
- Soma Mwanzo 3:1-4. Unaweza kuelezeaje kwa ufupi ujumbe wa nyoka kuhusu Mungu? (Si mkweli.)
-
-
- Tumekutana na tafakari ya muhimu sana katika kumjua Mungu. Ni ipi hiyo? (Kwamba nguvu kubwa sana inataka kudhuru hadhi ya Mungu.)
-
-
- Soma Ufunuo 12:9 na uniambie hii “nguvu kubwa” inayopingana na Mungu ni nani? (Shetani.)
-
- Angalia tena Mwanzo 3:4. Je, unagundua majaribio ya kila mara ya kukudanganya? (Kwa zaidi ya miaka arobaini nimetambua kwamba siwezi kuziamini habari. Mwaka 1980 nilishinda kesi ya muhimu sana ya uhuru wa maoni ya mwajiriwa mbele ya Mahakama Kuu ya Massachusetts. Gazeti/jarida la Boston Globe lilichapisha makala kuhusu uamuzi huo ambao ulikuwa upotoshaji wa dhahiri kabisa. Kichwa cha habari kilikuwa cha uongo. Gazeti/jarida la Globe lilikataa kusahihisha uongo huo.)
-
- Soma Mwanzo 3:5. Je, huu ni uongo?
-
-
- Nilidhani Mungu alisema (katika Mwanzo 1:27) kwamba wanadamu tayari “walifanana na Mungu.” Ni nini madai ya nyoka? (Si kweli kwamba “walifanana na Mungu.” Mungu alidanganya.)
-
-
-
- Je, ujumbe wa nyoka ni uongo kamili? (Hapana. Adamu na Hawa wataweza kuujua uovu. Kwa mfano, waliweza “kujua” kwamba mzaliwa wao wa kwanza alimwua mtoto wao wa pili. Kuna wimbo maarufu ulioimbwa na Toby Keith wenye maneno, “Ninatamani nisingejua sasa kile ambacho sikukijua awali.” Hawa na Adamu wangekubali.)
-
-
-
-
- Je, kuchanganya uongo na ukweli ni njia ya kawaida ya kudanganya?
-
-
-
-
- Ni jambo gani kwa umahsusi linalopaswa kuwa hitimisho tunalotoka nalo kutokana na mfano huu wa kampeni ya Shetani ya kumpinga Mungu hadharani? (Lengo lake ni kutufanya tusimtumaini Mungu kwa kuamini kuwa Mungu hatuwazii mambo mema.)
-
- Mungu Wetu wa Upendo na Utakatifu
-
- Soma Isaya 57:14-15. Mungu anajielezeaje? (Anasema jina lake ni “Takatifu,” kwa sababu anakaa “mahali palipoinuka na palipo patakatifu.”)
-
-
- Mungu amekuwepo tangu lini? (Milele.)
-
-
-
- Mungu anakaa mahali gani pengine? (Anakaa nasi ikiwa tuko radhi kumpokea. “Utayari” inamaanisha kuwa tuna “majuto” – hatujajawa kiburi chetu wenyewe.)
-
-
-
- Ni nini lengo la Mungu kukaa pamoja nasi? (Anataka kutuinua. Anataka kufufua/kuamsha mioyo yetu. Kifungu cha 14 kinatuamnbia kuwa anataka kuondoa vikwazo maishani mwetu.)
-
-
- Soma 1 Yohana 4:9. Mungu ametufanyia nini kinachodhihirisha upendo wake? (Alimtuma Yesu ili aishi na kufa kwa ajili yetu “ili tupate uzima kwa yeye.”)
-
- Soma 1 Yohana 4:10. Nimeelezea kisa hapo kabla kuhusu kulitembelea kanisa na kukaribishwa nyumbani kwa mshiriki ambaye pia aliwakaribisha wanandoa waliokuwa na maswali kumhusu Mungu. Watoto wao na wazazi wao walifariki kwenye ajali moja ya gari. Je, niwaelezee wanandoa hawa juu ya Mungu kuwapenda? Unaweza kuwaelezeaje jambo hili?
-
-
- Ufafanuzi wako utaendanaje na ukweli kwamba hatimaye Mungu ndiye mdhibiti wa mambo yote? (Sisi si Mungu. Hatujui mambo yote (au chochote kuhusu kweli za msingi), hivyo sidhani kama tunapaswa kuelezea matumizi ya upendo wa Mungu katika muktadha wa janga la kutisha. Badala yake, tunatakiwa kurejea kwenye ukweli kwamba Yesu aliteswa hadi kufa katika tendo la upendo ili kutuokoa. Yesu anachukua dhambi zetu na kutufungulia uzima wa milele.)
-
- Uhusiano Chanya wa Mungu Hadharani
-
- Soma Yohana 14:8-11. Hoja gani yenye nguvu tunayotakiwa kuijenga jinsi tunavyopaswa kumchukulia Mungu? (Tunayaangalia maisha ya Yesu. Tunaangalia kafara ya Yesu kwa ajili ya dhambi zetu.)
-
- Soma Yohana 14:12. Kampeni ya Mungu ya uhusiano chanya hadharani inaendeleaje? (Kupitia kwetu.)
-
- Angalia tena nyuma kabisa kwenye 1 Yohana 4:11-12. Yohana anamaanisha nini anaposema, “Hakuna mtu aliyemwona Mungu?” (Ni vigumu kuhusiana na mtu ambaye hujawahi kumwona.)
-
-
- Ni lipi suluhisho la Yohana kwenye tatizo hili halisi? (Watu wengine watauona upendo wa Mungu kupitia kwetu. Upendo wa Mungu unakamilishwa ndani yetu pale Roho wake anapokaa ndani yetu.)
-
-
-
- Je, hili ni rahisi? Je, kuna nyakati unapata msukumo wa kuwapiga au kuwakejeli wale wanaohimiza maadili na mitazamo ya Shetani? (Kwa dhahiri sijiingizi kwenye mapigano ya ngumi, na ninatumaini nawe pia hufanyi hivyo. Lakini uhasama na mabezo (dharau) ni majaribu ya mara kwa mara. Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kubadilisha (replace) uhasama na mabezo kwa upendo.)
-
-
- Soma 1 Yohana 4:13. Je, hii ni njia ya kupima kama upendo wa Mungu u ndani yetu? (Ndiyo. Yohana anasema tunajua kuwa tu ndani ya Mungu kwa kuwa ametupatia Roho wake.)
-
- Soma 1 Yohana 4:14-18. Kuna uhusiano gani kati ya upendo wa Mungu kuwa ndani yetu na “ujasiri” wetu katika hukumu ya mwisho? (Kuuelewa upendo wa Mungu, kuwaonesha wengine upendo wa Mungu, hutupatia uhakika kwamba Mungu anatutendea jambo la upendo. Hatuna haja ya kuogopa adhabu kama upendo wa Mungu unakaa ndani yetu.)
-
- Soma 1 Yohana 4:19. “Tunauuzaje” upendo wa Mungu kwa wengine? Tunakanushaje kampeni ya upotoshaji wa Shetani? (Hoja kuu ni kwamba Mungu alitupenda kwanza. Alitupenda katika uumbaji. Anatupenda katika kumtuma Yesu kutuokoa kutoka dhambini mwetu na kushindwa kwetu.)
-
- Rafiki, je, umemwomba Roho Mtakatifu alete upendo moyoni mwako? Je, utakuwa balozi kwa ajili ya upendo wa Mungu? Je, utafanya kazi kupinga kampeni ya upotoshaji wa Shetani kuhusu upendo wa Mungu? Kwa nini usijitoe kufanya hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Kiburi Dhidi ya Unyenyekevu.
