Somo la 12: Shiriki Habari Zake
Somo la 12: Shiriki Habari Zake
(Mathayo 10 & 28, Ufunuo 14)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Je, umewahi kuona mifano mibaya ya kuwashuhudia wengine? Kanisani kwangu, mtu mmoja aliyekiri mapambano yake ya kupunguza uzito alitaarifu alichokishuhudia kwa urekebishaji tabia ya ulaji wa mtu asiye mshiriki wa kanisa. Hata yeye alitambua tatizo kwa kukiri, “Ninaweza kupunguza kilo kadhaa.” Je, umewahi kushuhudia mifano mizuri ya ushuhudiaji? Katika miaka ya nyuma, washiriki wa kanisa walifanya ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba. Biblia haijaandika chochote kuhusiana na habari kwamba Yohana Mbatizaji au Yesu alikwenda nyumba kwa nyumba kupeleka injili. Watu waliwaendea. Tunapaswa kupelekaje injili? Mifano ipi ya ushuhudiaji ni mizuri? Je, tuwasubiri watu watujie? Tufanyeje ili waje? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Utume
-
- Soma Mathayo 28:18-20. Yesu aliwataka wanafunzi wake wafanye nini? Na kwa kuongezea, anatutaka tufanye nini? (1. Enendeni. 2. Mkawafanye kuwa wanafunzi. 3. Wabatizeni wanafunzi wapya. 4. Wafundisheni wanafunzi wapya.)
-
-
- Kazi gani kati ya hizo nne inaonekana kuwa ngumu zaidi? (Kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Kazi ya kwanza, tatu na ya nne zinaonekana kuwa na urahisi kwa kiasi fulani. “Enendeni” inaonekana kututaka tusonge mbele. Kama watu wanatafakari juu ya kubatizwa au kuwa na hitaji la kufundishwa, wanaonekana tayari wameridhia baada ya kushawishiwa na injili.)
-
-
- Angalia tena Mathayo 28:19 na amri ya “kuwafanya kuwa wanafunzi.” Una maoni gani juu ya kitendo cha kwenda nyumba kwa nyumba bila kukaribishwa ili kufanya ushuhudiaji? (Sikuwahi kujisikia vizuri kufanya hivyo. Sehemu ya tatizo ni kwamba nilikuwa ninaingilia uhuru wa mmiliki wa nyumba. Mwenye nyumba hakunikaribisha kuingilia ratiba yake ya siku. Hakuwa na shauku yoyote ya kujifunza zaidi habari za Mungu.)
-
-
- Nilikuwa na kawaida ya kusafiri kwa ndege sana. Mara kwa mara nilikuwa nikijiuliza kama ninaweza kumshuhudia aliyekaa pembeni yangu. Je, hii ni bora zaidi au inafanana sana na kwenda nyumba kwa nyumba kufanya ushuhudiaji? (Labda ni mbaya zaidi kwa sababu walilazimika kukaa karibu na mimi. Ningesubiri mtu huyo aseme jambo ambalo lingefungua fursa ya kuzungumzia masuala ya kiroho kwa njia ya kawaida.)
-
-
-
- Katika safari moja nilikuwa na mke wangu. Tulikuwa tumekaa kwenye msitari mmoja lakini mtu mwingine alikuwa amekaa katikati yetu. Mara moja aliuliza kama mke wangu angependa kubadilishana naye kiti kwa sababu hakutaka kusumbuliwa na mazungumzo ya watu wengine. Mke wangu alikubali, na mke wangu pamoja na mimi (sasa tukiwa tumekaa kwa viti vinavyopakana) akaanza kujadili kesi ya uhuru wa kuabudu niliyokuwa nikiendesha mahakamani. Ikatokea kwamba mtu huyu aliyebadilishana kiti na mke wangu alikuwa anasikiliza mazungumzo yetu na ghafla akamwomba mke wangu kama wanaweza kubadilishana naye kiti tena kwa kuwa alikuwa na shauku kubwa kuhusu kesi niliyokuwa nikiendesha mahakamani. Je, hii ni kazi ya Roho Mtakatifu?
-
-
-
- Je, Yesu anafafanua jinsi ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi? (Si hapa. Tutaliangalia hilo katika sehemu inayofuata.)
-
-
- Soma Mathayo 10:5-6. Hayo hayaonekani kuwa maelekezo kwa zama za leo, lakini je, kuna fundisho lolote katika hili kwa ajili yetu? (Tunatakiwa kuuelekeza uinjilisti wetu kwa wale ambao Roho Mtakatifu anatupendekezea. Kwenda nyumba kwa nyumba kwa kiasi kikubwa kunaongozwa na suala la kijiografia, si Roho Mtakatifu.)
-
- Soma Mathayo 10:7. Tulijadili maana ya maneno haya majuma mawili yaliyopita. Tulifanya uamuzi gani? (Nilipendekeza kuwa hadhira ya Kiyahudi ilidhani hii ilimaanisha Masihi alikuja na kwamba atauchukua ulimwengu. Leo tunaufahamu utume wa Yesu duniani.)
-
-
- Kwa kulizingatia hilo, ipi inayopaswa kuwa mada ya uinjilisti wetu? (Yesu alikuja duniani kama Masihi wetu. Yesu anakuja tena.)
-
-
-
-
- Je, njia nyingine itakuwa bora zaidi kwa kuzingatia kuwa muda mrefu umeshapita na uwapo wa uelewa mpana wa Yesu?
-
-
-
- Soma Ufunuo 14:6-7. Je, hili ni jambo “lililosasishwa” kutoka Mathayo 10:7? (Ndiyo, ni sasisho, na linahusu injili.)
-
-
- Ni nini kinacholifanya liwe jambo linalohitaji kushughulikiwa kwa haraka? (Rejea ya hukumu!)
-
-
- Soma Ufunuo 14:8-10. Hii inafafanua nini kuhusu hukumu? (Kwamba tunatakiwa kuwa makini ni nani tunayemwabudu. Tusingependa kupokea alama.)
-
- Soma Mathayo 10:8. Tunapaswa kulielewaje hili leo? (Yesu anawaambia wanafunzi wake kutenda mambo yaliyovuviwa na Roho Mtakatifu ambayo yatawafanya watu wawaendee. Ukifanya mambo kwa namna hii, huna haja ya kwenda nyumba kwa nyumba.)
-
-
- Je, hili linatuzuia kabisa kuendelea? Je, tutarajie kutenda miujiza hii, au tunapaswa kutafuta mbadala?
-
-
-
- Tafakari tena kuhusu Ufunuo 14. Je, kuzungumzia juu ya mwisho wa dunia na jinsi ya kuepuka alama ni jambo litakalovuta usikivu wa wasikilizaji?
-
-
-
- Je, maelekezo ya, “Toeni bure,” yanatoa njia nyingine? Ikiwa maisha yetu yamenufaishwa na injili, je, tunapaswa kushiriki na wengine manufaa hayo kama “ndoano” ya kuwaleta wasikilizaji kwenye mawasilisho yetu?
-
-
- Soma Mathayo 10:9-10. Tunapaswa kulielewaje hili? (Yesu anafafanua kuwa wasikilizaji wa injili wanapaswa kuchukulia gharama ya uinjilisti.)
-
-
- Je, hiyo inamaanisha kuwa tunapaswa kuwalipisha watu ili kuhudhuria mikutano yetu? (Nimegundua kwamba mtu akitakiwa kulipia kitu fulani, anakitunza vizuri zaidi. Anakithamini zaidi.)
-
-
- Soma Mathayo 10:11-13. Je, wazo la kukaa katika nyumba ya mtu usiyemfahamu limepitwa na wakati?
-
-
- Soma Luka 10:34-35. Hii inabainisha kuwa “nyumba za wageni” zilikuwepo wakati Yesu alipotoa maelekezo yake kwa wanafunzi wake. Je, hiyo inafanya uwepo uwezekano kwamba hilo linahusika kwetu katika zama za leo? Tunapaswa kukaa nyumbani?
-
-
-
- Au je, kawaida ya kutembea-tembea mijini, kukaa nyumbani, na kupeleka injili mtu kwa mtu limepitwa na wakati kutokana na kuwapo kwa Intaneti? Vipi kuhusu dhana ya ushuhudiaji wa uso kwa uso?
-
-
-
- Miongo kadhaa iliyopita, nilipata njozi ya mchana kuhusu kustaafu kazi yangu ya siku zote, kubadili basi kuwa basi la kutembelea lenye nyumba, na kusafiri kutoka kanisa moja hadi jingine kufundisha na kuhubiri. Tuseme kwamba nilikuwa na ratiba kamili na kutembelea makanisa 50 kwa mwaka. Hebu kwa ukaribu tuseme kuwa watu 200 walijitokeza katika kila kanisa ili kunisikiliza. Hadhira yangu yote kwa mwaka ingefikia watu 10,000. Somo hili linawafikia zaidi ya watu 24,000 waliojisajili kwa juma. Hii haiwajumuishi wale wanaoingia kwenye tovuti ya GoBible au kusoma somo hili katika mojawapo ya tafsiri nyingi zilizopo. Si kila aliyejisajili kwa njia ya barua pepe analifungua somo au kulisoma, lakini si kila aliyepo kanisani ni msikivu kwa yanayohubiriwa. Je, itakuwa na mantiki kwangu kwenda nyumba kwa nyumba au kanisa kwa kanisa?
-
-
- Soma Mathayo 10:14. Hii inatufundisha nini kuhusu kuwang’ang’aniza watu kuipokea injili?
- Roho Mtakatifu
-
- Soma Yohana 20:20-22. Takwa la kwanza la kupeleka injili ni lipi? (Kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu.)
-
- Soma Yohana 20:23. Je, Yesu anatupatia mamlaka ya kusamehe dhambi? Je, mamlaka hayo si ya Mungu pekee?
-
-
- Vipi kuhusu mamlaka ya kukataa msamaha wa dhambi? Je, ushuhudiaji wetu unajumuisha mamlaka ya kuwafungia wengine mbingu?
-
-
- Soma Mathayo 16:18-19. Kama kuna mwanafunzi ambaye angeweza kusamehe au kukataa kusamehe, huyo angekuwa Petro. Watu wangapi wanaweza kuja kwenye mkutano kama ungeahidi kuwa endapo wangekuja wangesamehewa dhambi zao na wangeweza kuwa na uhakika wa kuingia mbinguni?
-
- Soma Matendo 2:38. Yesu aliyaelewaje mamlaka ambayo Yesu alimpa? (Mamlaka ya Petro ilikuwa ni kupeleka injili. Vinginevyo, kifungu cha 38 kingesema, “Ninakusamehe dhambi zako.” Ufahamu wa Petro kuhusu kile Yesu alichomwambia unapaswa kuwa wa mwisho na wa kuhitimisha jambo hilo. Kimsingi, hatumwoni mwanafunzi yeyote akidai haki ya kusamehe au kuzuia msamaha wa dhambi.)
-
-
- Hivyo, tunapaswa kuzielewaje kauli za Yesu kuhusu kutoa au kuzuia msamaha? (Nadhani Yesu anasema kuwa kupeleka injili ni muhimu kwa ajili ya wokovu wa wasikilizaji wetu.)
-
-
-
-
- Je, hiyo inamaanisha kwamba uvivu au woga wetu unaweza kuzuia mtu mwingine kupata fursa ya kuisikia injili?
-
-
-
- Vipi kuhusu ahadi ya msamaha kama ‘ndoano’ ya kuwaleta watu kwenye mkutano ili kusikiliza injili? Je, hii ni njia bora kabisa ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi?
-
- Rafiki, je, utafanya uamuzi wa kudhamiria juu ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi? Kama jibu lako ni “Ndiyo,” basi jambo la kwanza kulifanya ni kumkaribisha Roho Mtakatifu mawazoni mwako na kutafuta mwongozo wake wa njia nzuri ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi.
- Juma lijalo: Kuingia Katika Umilele.
