Somo la 7: Sasa Sikia Hili!
Somo la 7: Sasa Sikia Hili!
(1 Wakorintho 10, Hesabu 14, 21 & 25, Mathayo 23)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Paulo anaandika katika 1 Wakorintho 10:13 kuhusu majaribu yaliyo “kawaida ya wanadamu.” Je, umetafakari kwamba wale wanaokuzunguka wanakabiliana na majaribu yale yale unayokabiliana nayo? Je, umetafakari kwamba watu waliokuwepo katika zama za kanisa la awali walikabiliana na majaribu ya aina ile ile? Vipi kuhusu wale walioondoka Misri kwenda Kaanani? Baadhi ya watu wanafundisha kwamba wale walioondoka Misri walikuwa watu wasiostaarabika na kamwe hawafananishwi nasi katika zama za leo. Sikubaliani na hoja hiyo. Tangu zama za Adamu na Eva wanadamu wamekabiliana na aina ile ile ya majaribu. Tunatakiwa kujifunza jinsi watu wa zama za kale walivyokuwa na mwitiko kwenye majaribu ili tuweze kunufaika na mbinu hizo. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili lituongoze dhidi ya uovu!
- Maelekezo Yetu
-
- Soma 1 Wakorintho 10:1. Hawa akina “baba” waliokuwa chini ya wingu na kupita kati ya bahari ni wepi? (Paulo anarejelea safari yaw ana wa Israeli kutoka Misri. Hawa ni watumwa wa kiMisri waliowekwa huru na Mungu ili wasafiri katika nchi ya ahadi ya Kaanani.)
-
- Soma 1 Wakorintho 10:11. Nani anayepaswa kujifunza kutokana na kumbukumbu ya wale waliowekwa huru kutoka utumwani Misri? (Paulo anawaandikia wale waliopo katika kanisa la Korintho. Hawa ni washiriki wa kanisa la awali. Lakini utaona kwamba kumbukumbu hii pia ni kwa wale “waliofikiliwa na miisho ya zamani.” Hao ni sisi.)
-
-
- Somo hili ni sehemu ya mfululizo wa manabii. Ni kwa jinsi gani mapitio ya safari ya wana wa Israeli kutoka Misri inaendana na somo la manabii? (Kwa jambo moja, Musa kiongozi wao alikuwa nabii mkubwa. Zaidi ya hayo, wale walioshiriki katika safari ya wana wa Israeli walipitia uzoefu wa uongozi binafsi wa Mungu.)
-
-
-
- Je, umetafakari kuwa ingekuwa jambo jema kuwa na Yesu alipoishi hapa duniani? Unadhani uzoefu huo ungekusaidia kuepuka dhambi? (Sidhani kama hilo ni kweli kwa kuzingatia mambo matatu. Kwanza, watu wengi siku hizi wanapendelea mawazo yao kuliko mafundisho ya dhahiri ya Biblia. Pili, mara kwa mara manabii walikabiliana na chuki. Tatu, kama ambavyo tutajifunza hivi punde, wale waliokuwa kwenye safari ya wana wa Israeli walikuwa na uhusiano wa “hali ya juu” na Mungu na bado waliasi.)
-
- Kumbukumbu
-
- Soma 1 Wakorintho 10:2-4 ili tuanze uchunguzi wetu wa kumbukumbu ya safari ya wana wa Israeli. Wale waliokuwepo kwenye safari ya wana wa Israeli walikuwa na faida gani? (Walipitia uzoefu wa kuona muujiza mkuu pale walipovuka Bahari ya Shamu na jeshi la Misri halikuwadhuru. Waliongozwa na Musa. Mwamba wa kiroho uliokuwa pamoja nao ulikuwa Kristo mwenyewe. Walikuwa na mlo wenye afya. Walikunywa maji yaliyotolewa na Mungu.)
-
-
- Unadhani walipaswa kuwa watu wa namna gani? (Watu wazuri. Walikuwa na uthibitisho wa kujirudiarudia wa upendo na ulinzi wa Mungu.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:5. Tunaweza kuichukulia safari ya wana wa Israeli kama kambi ya kiroho, ikimaanisha kwamba yalikuwa mafunzo ya kiroho ya kina kabisa. Mambo yalikuwaje? (Hayakwenda vizuri. Mungu “hakupendezwa” na wengi wao.)
-
- Soma 1 Wakorintho 10:6. Ni nini lengo la kisa cha safari ya wana wa Israeli? (Kwa mara nyingine tunaambiwa kwamba tunapaswa kujifunza jambo fulani kutokana na hii safari. Safari ina mifano inayopaswa kutufanya tusitamani uovu.)
-
-
- Ikiwa walipitia uzoefu wa uongozi mzuri na miujiza mikuu, kwa nini bado walitamani uovu? (Chukulia kwamba watu wengi wanatenda dhambi kwa sababu wanadhani inawapa faida. Watu waliokuwepo kwenye safari ya wana wa Israeli walikuwa na faida mbalimbali za kiroho na bado walimuasi Mungu.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:7. Tukio gani katika kipindi cha safari ya wana waa Israeli kinaelezewa hapa? (Soma Kutoka 32:4-6. Hapa ni wakati Haruni alipotengeneza ndama wa dhahabu ili kumwabudu.)
-
-
- Je, “kucheza” ndilo tatizo hapa? (Angalia tena Kutoka 32:4. Sehemu mbaya kabisa ya tukio hili ni kuihusisha miujiza mikuu iliyotendwa na Mungu na huyu ndama wa dhahabu ambaye Haruni alimtengeneza!)
-
-
-
- Tunapata fundisho gani katika zama za leo? (Kuyahusisha mafanikio yetu na matendo yetu wenyewe badala ya kutoa sifa kwa Mungu ni uabudu sanamu.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:8. Tukio gani linaelezewa hapa?
-
- Soma Hesabu 25:1-2. Mwanzo wa kushindwa kwa watu wa Mungu ni upi? (Uzinzi.)
-
- Soma Ufunuo 2:14 na Hesabu 31:16. Je, unafahamu msingi wa kisa kilichosababisha ushauri wa Balaamu? (Balaki, mfalme wa Moabu, aliona kile ambacho watu wa Mungu walikifanya wakati wa safari yao ili kuyashinda mataifa ya mahali pale. Katika kitabu cha Hesabu 22-24 Balaki anawasiliana na Balaamu na kumwomba awalaani watu wa Mungu. Hilo halitimii. Vifungu hivi vinatuambia kuwa kisa kinaendelea katika kitabu cha Hesabu 25 ambapo Balaamu anampendekezea Balaki njia nyingine ya kuwaangusha watu wa Mungu.)
-
-
- Je, jaribu la uzinzi ndio njia ya Shetani kuwashinda Wakristo ambao hawawezi kushindwa na njia nyingine? (Hilo ndilo fundisho kwa ajili yetu.)
-
-
-
- Je, umewafahamu Wakristo wanaobadili uelewa wao juu ya kile Biblia inachokifundisha kuhusu tabia ya uzinzi na mwenendo ambao Biblia inaushutumu?
-
-
-
- Kuna tofauti gani kati ya kumpemda mtu ambaye anajihusisha na tabia ya dhambi na kuidhinisha mwenendo huo? (Tunapaswa kuwapenda wengine, ikiwemo watoto wetu, bila kuruhusu hisia binafsi ili kubainisha kile tunachokiamini kuwa Mungu amekisema.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:9-10 na Hesabu 21:5-6. Watu “walimjaribuje” Yesu? (Huu ni uongo wa dhahiri. Kwa upande mmoja wanasema hawana chakula, na kwa upande mwingine wanasema chakula ni kibaya. Kama Mungu angetaka wafe angeruhusu jeshi la Misri liwaue.)
-
-
- Kuna fundisho gani kwetu leo? Je, Wakristo wanasema uongo kuhusu mazingira yao kwa kukana baraka zao? Je, baadhi ya Wakristo ni walalamishi kila mara?
-
-
-
- Utaona kwamba Paulo anasema kuwa baadhi ya watu “waliangamizwa na Mwenye Kuharibu.” Huyu Mwenye Kuharibu ni nani? (Soma Kutoka 12:23 na Waebrania 11:28. Mwenye Kuharibu pia anajitokeza katika maelezo ya Pasaka. Kitabu cha Kutoka kinatuambia kuwa Mungu aliwalinda wale ambao miimo ya milango yao iliwekewa alama ya damu ya kondoo. Kama Mwenye Kuharibu alikuwa malaika mtiifu au malaika aliyeanguka akitenda kazi chini ya mamlaka makuu ya Mungu hakuelezewi kwa hakika.)
-
-
-
-
- Tunaona fundisho gani katika hili? (Usalama wetu umejengwa katika kutumaini ulinzi wa Mungu badala ya kujitegemea sisi wenyewe.)
-
-
-
- Soma 1 Wakorintho 10:12. Je, hii ni kauli ya nguvu inayounga mkono kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo? Je, ni kauli ya nguvu kuhusu utii? (Nadhani mjadala wa Paulo ni kauli ya nguvu kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani. Wana wa Israeli waliokolewa kutoka Misri kwa uwezo wa Mungu, si kwa uwezo wao. Mwenye Kuharibu hakuwagusa wale waliolindwa na damu ya kondoo. Lakini Paulo anaonya kwamba wale waliopitia uzoefu wa wokovu wa Mungu hawapaswi kujivuna kiroho. Lazima imani yao iendelee kuwekwa kwa Mungu badala ya kuwekwa kwao.)
- Majivuno Yetu ya Uongo
-
- Soma Hesabu 14:1-4. Kipindi ambacho kumbukumbu hii inaandikwa ni wakati watu wa Mungu walipokuja kwanza kwenye mpaka wa Nchi ya Ahadi. Je, huku ni kujizuia kunakofahamika?
-
-
- Je, watu hawajajifunza chochote?
-
-
- Soma Hesabu 14:6-9. Je, watu wanasikia tu taarifa za kukatisha tamaa? (Hapana. Yoshua na Kalebu wanatafuta kuwatia moyo kuwa na imani kwa Mungu.)
-
- Soma Hesabu 14:10-11. Uasi umekuwa mbaya kiasi gani? (Wanataka kuwapiga mawe wale wanaojenga hoja kumuunga mkono Mungu. Mungu anataarifu kuwa “wanamdharau.”)
-
-
- Je, sisi tu bora kuliko hilo? Je, tunamshambulia Mungu na viongozi wake pale mambo yanapoenda mrama?
-
-
- Soma Mathayo 23:29-30. Je, viongozi wa dini waliokuwepo katika kipindi cha Yesu walidhani walikuwa bora kuliko baba zao waliomuasi Mungu? (Ndiyo.)
-
- Soma Mathayo 23:23-25. Ni nini tatizo la viongozi wa dini? (Wanapuuzia haki, rehema, na uaminifu. Wamejaa ulafi na kujiendekeza.)
-
- Soma Mathayo 23:28. Viongozi wa dini wanatenda dhambi gani nyingine? (Hawafuati sheria na ni wanafiki.)
-
-
- Je, wanafanana na mambo yote haya kwa wakati mmoja?
-
-
-
- Je, haya yanaonekana kama kushindwa kwa watu wa Mungu katika safari ya wana wa Israeli? (Yanaonekana tofauti.)
-
-
- Baadhi ya viongozi wa dini leo wanahoji kwamba madai ya haki na rehema yanatutaka tupuuzie amri fulani za kibiblia. Wananukuu Mathayo 23:23 ili kuunga mkono msimamo wao. Kuna tatizo gani na hoja hiyo? (Yesu hakutenganisha haki na rehema na uaminifu. Alibainisha yote haya matatu kama mambo makubwa ya sheria.)
-
-
- Utaona kwamba Yesu pia anawashutumu viongozi wa dini kwa kutozingatia sheria na unafiki. Je, tunaweza kudai kwa usahihi kuwa wafuasi wa fundisho la Yesu kuhusu haki na rehema wakati tukilikataa fundisho lake kuhusu utii? (Yesu anafundisha kuwa haki, rehema, na uaminifu vinaendana. Hatuwezi kuhalalisha kutokutii kwa kusisitiza uelewa wetu binafsi kuhusu haki.)
-
-
-
- Je, kuna hatari iliyo kinyume? Je, tunaweza kujali zaidi kuhusu utii wa sheria fulani kiasi cha kupuuzia haki na rehema? (Hicho ndicho haswaa alichokishutumu Yesu kwa Mafarisayo.)
-
-
- Rafiki, tumeanza na ukweli kwamba tunakabiliana na majaribu ambayo ni kawaida kwa wanadamu wote. Katikati ya majaribu hayo, je, utauchukulia kwa dhati wito wa Mungu wa kumtegemea na si kuzitegemea hisia zako kuhusu kipi kilicho haki? Kwa nini usijitoe sasa hivi kufuata neno lake na kuutegemea uwezo wake wa kuyashinda majaribu?
- Juma lijalo: Kutafsiri Maandiko ya Kinabii.
