Wafu Katika Kristo
(1 Wathesalonike 4 :13 - 18)
Swahili
Year:
2012
Quarter:
3
Lesson Number:
8
Utangulizi: Je, nini kinachotokea tunapokufa? Kuna mitazamo miwili mikuu katika Ukristo. Mtazamo wa watu wengi ni kwamba “nafsi” au “roho” yako (sehemu ya fikra yako) inarudi mbinguni kusubiria ufufuo (ujio wa Yesu wa Mara ya Pili) wakati ambapo fikra zako na mwili wako vitaungana tena. Mtazamo wa watu wachache ni “kulala kwa roho,” ambapo mwili wako na roho yako vinakuwa havina ufahamu kaburini hadi siku ya ufufuo. Inaonekana Wathesalonike walikuwa na mtazamo wa tatu, na wenye kukatisha tamaa zaidi. Walionekana kufikiri kwamba kama mtu alikufa kabla Yesu hajarejea basi alikuwa amepotea milele. Hebu tuzame kwenye mwongozo wetu wa kujifunza Biblia ili tuweze kuchunguza kile anachokisema Paulo kwa Wathesalonike kuhusu hali ya wafu!
- Matumaini
- Soma 1 Wathesalonike 4:13. Je, tatizo la fikra ya Wathesalonike ni lipi? (Walikuwa kama watu waliohuzunikia vifo vya watu wengine kwa sababu “hawakuwa na matumaini.”)
- Je, Paulo anaiitaje aina hiyo ya fikra ya “hakuna matumaini?” (Ujinga. Anasema kwamba Wakristo wana mtazamo mpana ulioelimika kuhusu kifo.)
- Soma 1 Wathesalonike 4:14. Nini kilimtokea Yesu baada ya kuwa amekufa? (Alifufuka.)
- Je, imani hiyo inamaanisha nini kwetu? (Inamaanisha kwamba tukilala katika Yesu, Mungu atatufufua pia!)
- Utabaini kuwa fungu linasema, “Mungu atawaleta pamoja naye (Yesu).” Paulo anazungumzia jambo gani, je, ni kuhusu eneo la kijiografia? Je, ni kwamba Yesu (ambaye yupo mbinguni) atawaleta watu kutoka mbinguni kuja duniani wakati wa ujio wa Mara ya Pili? (Sidhani kama hicho ndicho kilichokusudiwa. Paulo haandiki kuhusu eneo la kijiografia, anaandika kuhusu uwezo na mamlaka. Kama vile Mungu alivyomtoa Yesu kaburini, vivyo hivyo Mungu atatutoa (kwa sababu ya ushindi wa Yesu) kaburini.)
- Soma 1 Wathesalonike 4:13. Je, tatizo la fikra ya Wathesalonike ni lipi? (Walikuwa kama watu waliohuzunikia vifo vya watu wengine kwa sababu “hawakuwa na matumaini.”)
- Dosari
- Soma 1 Wathesalonike 4:15. Ilhali tukiwa hatuelewi kwa ukamilifu mtazamo wenye dosari wa Wathesalokine, hii inatupatia mwangaza fulani kwenye hizo dosari. Je, Paulo anasahihisha dosari gani? (Kwamba wale watakaokuwa hai wakati wa ujio wa Yesu Mara ya Pili watakwenda mbinguni kabla ya wale waliokufa.)
- Je, hili lilikuwa ni suala la muda tu? (Sidhani. Paulo anaanza kwa kusema “Msifikiri kama watu wasiokuwa na matumaini.” Hiyo inaniambia kuwa Wathesalonike walidhani kwamba kama wasingeishi kuushuhudia ujio wa Yesu wa Mara ya Pili, wasingekwenda mbinguni. Ingewapasa kuishi ili waweze kwenda mbinguni.)
- Je, ukweli ni upi kwenye suala zima la muda? (Kwamba watu watakaokuwa hai hawatakwenda mbinguni kabla ya wale waliokufa katika Yesu.)
- Jiweke kwenye nafasi ya mshiriki wa kanisa la Thesalonike. Je, ungewezaje kuwa na huo mtazamo wenye dosari? (Je, hivyo sivyo mambo yalivyo maishani? Tuna matumaini ya kuishi ili tuone mambo mazuri!)
- Soma 1 Wathesalonike 4:15. Ilhali tukiwa hatuelewi kwa ukamilifu mtazamo wenye dosari wa Wathesalokine, hii inatupatia mwangaza fulani kwenye hizo dosari. Je, Paulo anasahihisha dosari gani? (Kwamba wale watakaokuwa hai wakati wa ujio wa Yesu Mara ya Pili watakwenda mbinguni kabla ya wale waliokufa.)
- . Ufufuo
- Soma 1 Wathesalonike 4:16. Je, nani atayekuja kutuchukua? (Yesu!)
- Je, atakuja kimya kimya? (Yesu atatoa mwaliko mkubwa. Sauti ya malaika mkuu itaungana na Yesu, na parapanda za Mungu zitapiga!)
- Je, mpangilio wa uendaji wetu ukoje? (Wale waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza! Sio tu kwamba Wathesalonike wamekosea kwa kufikiri kuwa hakuna matumaini, bali mpangilio sio sahihi – wale waliokufa watakuwa wa kwanza.)
- Mtazamo uliozoeleka ni jambo linaloitwa “shauku ya kisiri.” Dhana hapa ni kwamba Wakristo wengi walio hai watachukuliwa kwa siri kwenda mbinguni. Wengine watakapobaini, watapewa nafasi nyingine ya kwenda mbinguni. Je, fundisho hili linajipimaje dhidi ya mafungu tuliyoyasoma hivi punde? (Kwanza, muda umekosewa. Kwenye suala la kuchukuliwa kisirisiri Wakristo walio hai wanakwenda mbinguni kabla ya ufufuo wa jumla wa wafu. Paulo anasema kwamba hiyo sio kweli. Pili, hakuna siri yoyote kuhusiana na Yesu kuwachukua walio hai na wafu kwenda mbinguni pamoja naye. Kuna aina zote za kelele!)
- Soma 1 Wathesalonike 4:17. Je, tutakutana na Yesu wapi? Duniani? (Hapana, tutakutana na Yesu mawinguni. Yesu hatarandaranda duniani, vivyo hivyo nasi pia.)
- Ninapokuwa ninasafiri kwa ndege, na ikatokea kuwa tumechelewa kuondoka, mara nyingine rubani huwa anasema kuwa tutafidia muda tutakapokuwa hewani. Je, hii dhana inaendanaje na wafu watakaofufuliwa na watakaokuwa hai? (Sisi tulio hai tutaendana nao. “Tutachukuliwa pamoja nao mawinguni.”)
- Je, tutakuwa na Yesu kwa muda gani? (Milele!)
- Soma 1 Wathesalonike 4:18. Je, maelezo yana upungufu (hayana ukweli wote)? (Ninaposoma maneno haya ninajisikia kutoa kicheko kikubwa cha furaha! Je, hii inafurahisha kwa namna gani! Inatia moyo kwa namna gani! Bwana apewe sifa!)
- Je, yupo mtu aliyefariki ambaye ungependa ukutane naye mawinguni?
- Soma 1 Wathesalonike 4:16. Je, nani atayekuja kutuchukua? (Yesu!)
- Kulala Kiroho?
- Pasipo na utata kabisa Paulo anatuambia kwenye mafungu tuliyoyasoma hivi punde kwamba kwa sababu Yesu alifufuka, atawafufua wale waliokufa katika yeye. Paulo hasemi jambo lolote moja kwa moja kuhusu mustakabali wa sasa unaohusiana na mkanganyiko wa wafu kwenye haya mafungu. Bali, anatupa muktadha hasi tunaopaswa kuuchukulia.
- Jiweke kwenye nafasi ya Paulo. Kama Wathesalonike walidhani kwamba wale waliokufa kabla ya ujio wa Yesu wa Mara ya Pili waliikosa mbingu, je, jibu gani litakuwa na mantiki kama ilikuwa kweli kwamba roho au nafsi zao tayari zilikuwa mbinguni? (Ningesema kwamba, “Unadhani kwamba wafu wanaikosa mbingu? Unadhani wafu wameachwa nyuma? Roho zao zipo mbinguni kabla yenu!)
- Je, kwa nini Paulo hakusema hivyo? Kwa nini alizungumzia ufufuo wa jumla wa walio hai na wafu? (Hii inadokeza kwamba roho au nafsi za Wakristo waliofariki hazipo mbinguni.)
- Nilipokuwa mdogo, nilifundishwa kuhusu kulala kwa roho. Lakini baba yangu alipofariki, sikuwaruhusu watu wengine wafikirie kwa niaba yangu, kwa hiyo nilisoma kila fungu la Biblia linalohusiana na hii mada. Hebu tufanye uchunguzi kidogo kuhusu mada inayohusika. Soma sehemu ya kwanza ya Mhubiri 9:5. Je, kifungu hiki kinasema nini kuhusu hali ya wafu? (Hawajui jambo lolote.)
- Soma Mhubiri 9:1-2. Je, mafungu haya yanasema nini kuhusu wenye haki? (Wana mustakabali mmoja na waovu. Haijalishi unaungama dhambi zako au la, mustakabali wenu ni mmoja.)
- Soma Mhubiri 9:5-6. Je, wenye haki watapata thawabu gani? (Hawatapata thawabu yoyote!)
- Unapokuwa unasoma mafungu haya katika Mhubiri, je, unapaswa kuhitimisha kwamba hakuna kabisa maisha baada ya kifo? (Watu wanaoshadadia “kulala kwa roho” wanaonukuu Mhubiri 9:5 kwa mtazamo wao wanapaswa kupata zawadi ya “akili iliyolala!”) Sulemani ama ana msongo wa mawazo au anaandika tu kuhusu faida ya kuishi. Kama anatoa maoni yake kuhusu maisha baada ya kifo, basi anatofautiana kabisa na Agano Jipya.)
- Soma Mathayo 27:52-53, Yuda 9 na Mathayo 17:1-4. Je, hii inatuambia nini kilichojiri baada ya kifo cha Musa? (Yupo mbinguni! Alikwenda mbinguni kabla ya ujio wa Mara ya Pili. Mathayo 27 inadokeza kwamba hii ilitokea kwa watu wengine pia tofauti na Musa.)
- Je, ni sehemu gani za Musa zilizo mbinguni? (Utabaini kwamba Yuda anatuambia kuwa walikuwa wanagombania mwili wa Musa. Hii inaweka bayana kwamba sehemu ya fikra na mwili wake vipo mbinguni.)
- Soma Ufunuo 6:9-11. Je, wakati wa kufanyika hili ni upi? (Kabla ya ujio wa Mara ya Pili, kwa sababu Wakristo bado wanateseka (mashahidi wa dini) duniani.)
- Je, taswira ya roho kuvaa mavazi meupe inadokeza jambo gani? (Ufahamu, nafsi zenye haki zilizopo mbinguni kabla ya ujio wa Mara ya Pili. Kimsingi, jambo kubwa lililopo kwenye kitabu cha Ufunuo ni la kiishara, sio halisia.)
- Je, tutoke na hitimisho gani kutokana na kile anachotufundisha Paulo pamoja na haya mafungu machache tuliyoyapitia kuhusu hali ya wafu? (Habari njema ni kwamba kwa kuwa Yesu aliishinda dhambi na alifufuka kutoka katika wafu, wale waliomwamini wanaweza kuutazamia uzima wa milele, hata kama wamekufa. Kama ilivyo kwenye suala la kulala kwa nafsi/roho, nimegusia tu suala hilo kwa juu juu. Kutokana na kujifunza kwangu, nimefikia hitimisho lifuatalo. Kwanza, nimetambua kwamba kile nilichofundishwa kuhusu suala la kulala kwa nafsi/roho nilipokuwa mtoto ilikuwa ni sahihi – walao kwa watu wengi. Pili, hakuna mwenye haki ya kujigamba/kujisifu kuhusiana na mada inayohusika, kwa sababu Biblia ina mitazamo yote miwili. Nikijikuta mbinguni mara tu baada ya kufariki, nitashangaa, lakini sitashtushwa. Tatu, Biblia iko wazi kabisa kwamba Mungu anaweza kufanya jambo lolote analolitaka. Watu wengine anawafufua kabla ya ujio wa Mara ya Pili.)
- Rafiki, swali kwenu halilengi zaidi kuhusu “Lini utakwenda mbinguni” au “kama utakwenda mbinguni?” Je, utampokea na kumkubali Yesu kama mwokozi wako hivi leo ili kwamba swali la “kama” lijibiwe kwako?
- Juma lijalo: Matukio ya Mwisho.