Mpinga Kristo.
Utangulizi: Juma lililopita Paulo alitueleza kuwa mwisho wa mateso utakuja na Kuja kwa Yesu Mara ya Pili. Kumbuka kuwa hapo awali Paulo aliwaambia Wathesalonike kuwa, wakati wa Marejeo ya mara ya Pili, wangewaona wapendwa wao ambao walishafariki. Kiasili, walihitaji kujua zaidi kuhusu muda wa Marejeo ya Mara ya Pili! Lakini, badala ya kuwapatia ufafanuzi mkamilifu, Paulo aliwambia (1Wathesalonike 5:1-2) ya kwamba hakupaswa kuwaambia maana watashtukizwa. Ni jibu la aina gani hilo? Inavyoonekana, wathesalonike nao walikuwa na mtizamo huo kwa kuwa Paulo anarejea tena mada ya muda wa Marejeo ya Mara ya Pili. Lazima watakuwa walimwambia kuwa walihitaji kujua zaidi. Binafsi nina vutika na ufuatiliaji wakati wa Marejeo Mara ya Pili! Na wewe unavutika? Kama ndiyo, basin a tuzame pamoja kujifunza Paulo ana lipi la kusema juu ya matukio yanayozunguka Kuja Mara ya Pili kwa Yesu.
- Utulivu sasa
- Soma 2 Wathesalonike 2:1-2. Ni tatizo gani Paulo analizungumzia? (Wathesalonike wameshtushwa na uzingatiaji muda wa Marejeo ya Pili ya Kristo.)
- Ni nini sababu ya kushtushwa? (Mtu mmoja alisema limeshatokea. Wamelikosa!)
- Kwanini watu wafikiri kuwa wamekosa Kuja Mara ya Pili? (Inavyoonekana, mambo ya tetesi yalianza tangu zamani. Tetesi walizosikia Wathesalonike ni kuwa walikuwa wamekosa Marejeo ya Maara ya Pili na chanzo cha taarifa hiyo kudhaniwa kutoka kwa Paulo.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:3. Kwanini Paulo hasemi kuwa, “Sijawahi sema jambo hilo?”
- Anasema nini badala yake? (Paulo haridhiki na ukanushaji tu. Isipokuwa, anaeleza kiundani Marejeo ya Mara ya Pili kuonyesha kuwa isingewezekana kuwa limeshatokea.)
- Tunawezaje kupata ubashiri bora zaidi wa mpangilio wa mambo wa Marejeo ya Pili? (Ukengeufu unaanza kwanza. Mwana asiye na sheria (mwana wa uharibifu anafunuliwa. Huyu mwana “amewekewa uangamivu.”)
- Ni kwa namna gani mtu anaweza “akawekewa uangamivu?” Nilidhani ya kuwa neema ilikuwepo kwa wote waliokuwa na utayari?
- Soma Yohana 17:12. Endapo unahitaji kusoma muktadha kuelewa kauli hii ya Yesu, fanya hivyo. Ni nani Yesu anamuita “yeye aliyewekewa upotevu?” (Yuda. Adam Clarke katika uchambuzi wake anabaini kuwa kauli ya kulingana na hii kwa Kiebrania ilitumiwa na walimu kumwelezea Shetani au Adamu baada ya anguko. Yuda, shetani na Adamu wote walifanya chaguzi mbaya kabisa. Hivyo, huyu mtu amabaye Paulo amemuainisha amechagua uangamivu.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:1-2. Ni tatizo gani Paulo analizungumzia? (Wathesalonike wameshtushwa na uzingatiaji muda wa Marejeo ya Pili ya Kristo.)
- Mpinga Kristo
- Soma 2 Wathesalonike 2:4. Yatupasa kubaini kwa umakini tabia ya mtu huyu aliyewekewa uangamivu ni zipi? (Anampinga Mungu. Anajiinua juu ya Mungu. Anaweka makao yake makuu katika hekalu la Mungu. Anajatangaza yeye kuwa Mungu.)
- Awali tulimlinganisha na Adamu na Yuda. Ni jambo lipi mtu huyu analifanya linalomtofautisha na Adamu na Yuda? (Anajitangaza kuwa zaidi ya Mungu. Anajitangaza kuwa Mungu. Yuda yawezekana alifikiria kuwa mwerevu kuliko Yesu, na hiyo itamshinikiza Yesu kujitangaza kuwa mfalme. Lakini, Yuda hakuwahi kujitangaza yeye ni Mungu.)
- Ni nini kinachojidhihirisha katika fungu hili kama kielelezo bayana cha alama ya kihistoria? (Mtu huyu “anajiketisha katika hekalu la Mungu.”)
- Hekalu la Mungu ni nini?
- Paulo angeamini kuwa hekalu katika Yerusalemu pekee ndiyo” hekalu la Mungu,” sawa?
- Hekalu la Yerusalemu liliangamizwa baada ya muda huu. Je, alama yetu ya kihistoria imetoweka? (Pengine hekalu katika Yerusalemu litajengwa tena.)
- Soma 2 Wakorintho 6:16, 1 Wakorintho 3:16 na Waefeso 2:21-22. Ni namna zipi tofauti amabazo mafungu haya yanaibua katika kuelewa kauli “hekalu la Mungu?” (ya kwamba washiriki wa kanisa ni hekalu la Mungu.)
- Soma Ufunuo 3;11-12. Je, hii itatuongeza nini katika taswira yetu ya hekalu la Mungu? (Hata katikati ya Yerusalemu mpya kushuka duniani, Mungu bado anaita watu wake kama sehemu ya “hekalu la Mungu.”)
- Itakuwa ni vyema sana kutazamia huyu mtu wa uangamivu kujitokeza kwenye hekalu litakalojengwa tena Yerusalemu. Lakini haya mafungu mengine yanaonyesha uwezekano wa kuwa huyu mpinga kristo anajiinua juu ya kanisa la Mungu.)
- Tazama tena 2 Wathesalonike 2:4. Huyu mwana wa uangamivu, huyu mpinga kristo anajitangaza yeye kuwa Mungu. Je, tumewahi kuona mtu anayejiinua binafsi juu ya kanisa la Mungu na kujitangaza binafsi kuwa Mungu? (Ufafanuzi wa Barnes, mchambuzi mashuhuri wa kikristo anasema, “ni namna gani itatiliwa shaka hapa ya kuwa kinachozungumziwa hapa ni upapa?” Barnes alikuwa mchungaji wa kanisa la Presbetari katika Filadelfia. Mchungaji Barnes alifariki mwaka 1870. Ilikuwa ni kawaida kwa waprotestanti wa wakati wake kuamini kuwa Paulo alikuwa akizungumzia papa. Hata hivyo, hata Barnes hakuweza kupata uthibitishi wa papa kudai yeye ni Mungu. Ilibidi aupate katika maandishi ya wakatoliki wengine.
- Soma 2 Wathesalonike 2:5-7 Paulo anawadhihirishia Wathesalonike siri ambayo hajashiriki na sisi. Je, unafikiri ni ipi hii “siri ya kuasi?”
- Je, unafikiri ni kipi kinachomzuia?” (Paulo hatuambii. Lakini, nadharia iwayo yote tuundayo ya mpinga kristo, roho ya kufikiri tu bora kuliko Mungu, roho hii inazuiwa na nguvu fulani ya uungu.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:8. Je, utafika wakati ambapo mpinga kristo huyu atadhihirishwa? (Ndiyo. Katika muda fulani mpinga kristo atawekwa huru kujidhihirisha.)
- Ni kwa namna gani mpinga Kristo atakoma? (Hii ni muhimu. Mpinga kristo anakuja kabla ya Marejeo ya Pili ya Yesu na atashindwa wakati wa Marejeo ya Pili ya Yesu. Mpangilio wa mambo hapa upo wazi kabisa.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:9-10. Upi ni uthibitisho wetu ulio bayana (zaidi ya mpangilio wa muda wa matukio) wa mpinga kristo wa wakati wa mwisho? (Anafanya miujiza ya aina zote, ishara na maajabu. Anashirikiana na uovu.
- Kwanini anafanya aina zote za miujiza, ishara na maajabu? (Anaitenda kuwadanganya wakristo.)
- Kutudanganya kuhusu nini? (Ukirejea kile tulichokisoma, pendekezo bayana ni kuwa huyu mpinga kristo wa wakati wa mwisho ananuwia kutuaminisha ya kuwa yeye ndiyo Kristo ajaye. Anajaribu kuigiza Marejeo ya Pili.)
- Je hiyo inaonekana kuwa ni papa? (Hapana. Kama wale wanaosoma somo hili wajuavyo, mimi siyo mshikaji shupavu wa elimu ya dini juu ya tafsiri ya unabii. Badala yake, nafikiri ni muhimu sana kwetu kuwa macho na kupima matukio ya sasa dhidi ya Biblia. Isipokuwa labda kitu kitokee mbeleni, hakuna papa aliyepita aliyetimiza aidha mpangilio wa muda au kuonesha mambo yaliyofafanuliwa na Paulo. Hakuna papa aliyewahi kusema, “mimi ni Marejeo ya Pili ya Kristo.”)
- Kwanini anafanya aina zote za miujiza, ishara na maajabu? (Anaitenda kuwadanganya wakristo.)
- Muhimu zaidi, ni tatizo mara zote kunyooshea vidole waaminio wengine katika Kristo na kuwaita “mpinga Kristo.” Hii ni muhimu zaidi hasa tutazamapo mjumuiko wa dini katika dunia. Kuna Waislamu 1.6 billioni na Wakristo 2.2 billioni. Kwanini wakristo waitane mpinga kristo wakati kuna kundi kubwa bila ubishi lipingalo dhana kuwa Yesu ni Mungu?
- Shirika la Muhammadi kundi la kiislamu Marekani wanazungumza hili juu ya Imamu wa 12 ajaye wakati wa mwisho wa dunia, “Dunia haitofikia mwisho” anasema mtume Muhammad “mpaka mwanaume kutoka familia yangu (Ahlulbayt) na wa jina langu atakapokuwa bwana wa ulimwengu, muonapo bendera ya kijani ikija kutokea upande wa Khorasan, basi mjiunge nao, kwa kuwa Imamu wa Mungu atakuwa na bendera yeye atakayeitwa Al-Mahdi.”
- Endapo kama unataka kusoma zaidi juu ya imani ya waislamu katika kuja kwa Mahdi, soma habari hiyo kwenye Wikipedia. Si Wakristo wengi wanaelewa juu ya mtazamo wa waislamu wa matukio ya siku za mwisho unaotazamia ujio wa Mahdi punde kabla ya kile Waislamu wakiitacho siku ya ufufuo.
- Soma 2 Wathesalonike 2:4. Kama hekalu la Mungu ni kanisa lake hiyo inakubaliana vipi na nadharia ya kuwa Mahdi ndiye mpinga Kristo wa wakati wa mwisho? (Haikubaliani.)
- Tuhitimishe vipi kutokana na hili? (Hii inatupa dokezo ya nini tutizame katika siku za usoni. Kama Mahdi atajiinua mwenyewe katika hekalu lililojengwa upya Yerusalemu, basi Paulo itakuwa alikuwa anazungumzia hekalu halisi. Vinginevyo, yatupasa kutafuta mpinga Kristo mwenye kudai kuwa kichwa cha Ukristo.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:11-12. Paulo anaanza kwa kuwaonya Wathesalonike juu ya kudanganywa. Nini tufanye ili tuepuke kudanganywa na mpinga Kristo wa wakati wa mwisho? (Lazima tuwe na na nyoyo zilizoongolewa. Lazima tuamini ukweli wale wenye kudanganywa ni wale wenye “kujifurahisha katika udhalimu” na “hawakukubali kupenda ile kweli” wale wasiodanganywa ni wale wanaompenda Mungu na kamati yake.)
- Rafiki ni wapi unaposimama? Unapenda ukweli wa Mungu? Je, uko tayari kujifunza kwa dhati Biblia yako na kufungua macho yako kwa uwongo huu wakati wa mwisho? Omba kwamba Roho Mtakatifu akupe utambuzi na kukusonda juu ya kweli ya Mungu! Lakini, wakati ambapo mpinga Kristo huyu atakapokuja furahi ya kuwa Yesu ndiye anayefuatia.
- Soma 2 Wathesalonike 2:4. Yatupasa kubaini kwa umakini tabia ya mtu huyu aliyewekewa uangamivu ni zipi? (Anampinga Mungu. Anajiinua juu ya Mungu. Anaweka makao yake makuu katika hekalu la Mungu. Anajatangaza yeye kuwa Mungu.)
- . Juma lijalo: Kudumisha Kanisa katika Uaminifu