Maisha ya Mkristo
Utangulizi: Je, unaipenda sana sheria? Juma lililopita tulijifunza kwamba sheria sio adui wetu, bali ni kitabu cha mwongozo cha Mungu kwa ajili ya maisha bora. Tuliona kwamba ni pale tu tutakaposhindwa kudhibiti ubinafsi kwa ajili ya manufaa yetu binafsi ndipo sheria itakapokuwa mpinzani wetu. Kama hiyo ni kweli, ni kwa nini basi Paulo anaashiria kwamba sheria ni tatizo kwetu? Je, hii ndio sababu sote tunashindwa kudhibiti ubinafsi kwa ajili ya manufaa yetu binafsi? Tunahitajika kujifunza zaidi! Juma hili tutazama zaidi kwenye wazo linalosema kwamba tunapaswa kujifunza upya fikra zetu ili tuweze kuelewa kwamba sheria ni rafiki na mfadhili wetu. Tunapaswa kuwa watu wenye ushawishi wa sheria! Kama suala hilo linaonekana kuwa la ajabu, hebu tuzame kwenye neno la Mungu na kuona kile anachokisema kuhusu sheria!
- Sheria ya Manufaa
- Soma Kumbukumbu la Torati 28:1-6. Je, utii unatufanyia jambo gani maishani mwetu? (Unanyesha mibaraka juu yetu. Ukitaka kujifunza suala kamili la mibaraka, soma Kumbukumbu la Torati 28:7-14.)
- Soma Kumbukumbu la Torati 28:15-20. Je, kutoitii sheria kunatutendea jambo gani? (Kunasababisha matatizo yasiyokuwa na mwisho. Ukitaka kusoma muktadha wote wa laana, soma Kumbukumbu la Torati 28:21-68.)
- Soma Malaki 3:8-12. Je, nini hutokea tunapotoa zaka? (Mibaraka inatumwagikia kiasi kwamba hatuna mahala pa kutosha pa kuihifadhi.)
- Soma Waefeso 5:28. Nini hutokea tunapowapenda wenzi wetu? (Unabarikiwa na mwenzi anayekupenda kama jinsi unavyompenda. Kumpenda mwenzi wako ni sawa na kujipenda wewe mwenyewe.)
- Soma Ufunuo 21:10-11 na Ufunuo 21:18-21. Je, Yerusalemu mpya ni mahala pa namna gani? Kamwe hatujawahi kuona mahala penye utajiri kama huo. Ni suala la kuogelea kwenye dhahabu na vito vya thamani.)
- Kwa nini anatupa ahadi yenye ukarimu kiasi hicho? Je, anajaribu kutuhonga? Au, je, utajiri na mafanikio ni suala la asili tu linalotokana na utendaji wa sheria yake? (Je, yote hapo juu ni majibu? Hatuwezi kukana kwamba Mungu ana kauli mbiu thabiti inayosema kwamba utii wa sheria unalipa gawio kubwa.
- Je, nini kimetokea kwenye kaulimbiu ya injili inayohusu kujikana nafsi? Je, tunaelezeaje suala la Yesu kumwambia yule kijana mdogo tajiri kuuza vyote alivyonavyo (Luka 18)? (Vipi kama tulisema kwamba kujikana nafsi (utii) kunaleta mibaraka mikubwa? Hatma ya kujikana nafsi ni kinyume tu cha kujikana nafsi?)
- Kuvunja Mkataba
- Soma Ayubu 9:32-35 na Ayubu 13:17-23. Je, Ayubu anaomba kitu gani? (Hukumu ya haki dhidi ya Mungu. Ayubu ana kesi, anayo hoja, na anahitaji kumtafuta hakimu aliye juu ya Mungu ili kwamba aweze kutendewa haki.)
- Je, ni madai gani ya kisheria atakayoyaleta Ayubu dhidi ya Mungu? (Kuvunja mkataba. Ayubu anaifahamu sheria ya Mungu inayohusu manufaa. Ukiwa mtiifu, unafanikiwa. Hiyo ndio habari. Suala hilo halitumiwi vizuri kwenye kesi ya Ayubu, na anataka kumshtaki Mungu.)
- Soma Ayubu 1:8-11. Je, Shetani anataka nini? (Yu kinyume na sheria! Anapingana na na dhana ya “tii na ufanikiwe.” Hebu tafakari jambo hilo – la Shetani kuwa kinyume na sheria!)
- Soma Ufunuo 12:12-13 na Ufunuo 12:17. Je, Shetani anamlenga nani? (Anawalenga wale wanaoamini kwamba Yesu ni Mungu na Mwokozi, ambao pia wanazishika sheria za Mungu.)
- Je, kisa cha Ayubu kinatufundisha sababu ya kwa nini Shetani amewalenga watunza amri na kile alicho nacho akilini mwake kwa ajili yao? (Anataka awafanye waachane na utiifu kwa Mungu. Ayubu anatuonyesha kuwa njia mojawapo anayoitumia Shetani ni kwa kuivuruga sheria ya manufaa.)
- Hebu tafakari jambo hili kidogo. Kama ungekuwa Shetani, je, mkakati wako pekee ungekuwa ni kuvunja kiungo kinachounganisha utiifu wa sheria na mibaraka mikubwa? (Hapana. Ningejaribu kuchombeza uongo kwamba kutokuwa na utiifu wa sheria huleta mibaraka mikubwa.)
- Je, tunaliona jambo hili hivi leo?
- Je, Shetani ana hoja halali kwenye mgogoro wa Ayubu? Ya kwamba Mungu anampa hongo Ayubu? (Hapana. Shetani haupendi mfumo huo, kwa sababu unamfanya awe mwenye hatia. Sheria ya Mungu inalenga kuwabariki na kuwalinda watu wake. Shetani anawezaje kuwakengeusha wafuasi wa Mungu kama wanadhani (wanafahamu) kuwa kumfuata Mungu huwapa mibaraka mikubwa na kuwalinda dhidi ya uovu?)
- Soma Ayubu 1:12. Je, unawezaje kuelezea jambo hili? Kwa nini Mungu hamwambii tu Shetani kuwa, “Unaifahamu sheria, na inatenda kazi vyema hapa. Nenda zako ukacheze huko mtaani!”
- Rafiki, hili ni jambo la muhimu sana. Kwa nini Mungu alianzisha sheria ambayo mara zote huwapa faida wale wanaotii? (Kwa sababu Mungu anatupenda. Upendo ndio upo nyuma ya manufaa. Ni kama vile upendo ulivyo nyuma ya zawadi zetu kwa watoto wetu.)
- Swali ni kwamba, je, watoto wetu wanachanganyikiwa na kudhani kwamba zawadi ndio mwisho wa kila kitu? Hiyo ndio changamoto ya Shetani hapa: je, Ayubu anatambua kwamba unampa vitu kwa sababu unampenda (Mungu)? Au, je, Ayubu anapenda vitu tu?
- Je, hii inatufundisha nini kuhusu namna ambavyo sheria ya manufaa inatenda kazi? (Kama ilivyo kwa mvutano, ni sheria. Tukiwa na utii, tunabarikiwa. Shetani anatafuta namna ya kuvuruga hii sheria, na anafanya hivyo kwa ridhaa/idhini ya Mungu, kwa sababu Mungu anatutaka tuielewe taswira pana ya upendo wake kwetu.)
- Rafiki, hili ni jambo la muhimu sana. Kwa nini Mungu alianzisha sheria ambayo mara zote huwapa faida wale wanaotii? (Kwa sababu Mungu anatupenda. Upendo ndio upo nyuma ya manufaa. Ni kama vile upendo ulivyo nyuma ya zawadi zetu kwa watoto wetu.)
- Soma Ayubu 9:32-35 na Ayubu 13:17-23. Je, Ayubu anaomba kitu gani? (Hukumu ya haki dhidi ya Mungu. Ayubu ana kesi, anayo hoja, na anahitaji kumtafuta hakimu aliye juu ya Mungu ili kwamba aweze kutendewa haki.)
- . Fikra Yenye Taswira Pana
- Hebu turejee kwenye masuala ya msingi. Tunaokolewa kwa neema pekee, sio kwa matendo yetu yoyote. Je, tunapaswa kuichukuliaje sheria? Je, kama adui? Je, kama kitu kisichokuwa cha msingi? (Hapana! Sheria ni rafiki wetu wa karibu sana kwa sababu utiifu wa sheria hubeba mibaraka mikubwa.)
- Je, hivi ndivyo unavyojisikia kweli?
- Rejea kwenye Ufunuo 12:17. Je, Shetani anapambana peke yake katika upande wake? (Malaika walioangushwa na wanadamu walioanguka wana lengo moja – kwamba wavunje kiungo kilichopo kati ya utii na mibaraka. Wanataka kuonyesha taswira kwamba kutokuwa na utiifu ndio njia ya kupata mibaraka.)
- Kama tunavutwa zaidi kutokuwa watiifu badala ya kuwa watiifu, je, hiyo inamaanisha nini? (Inamaanisha kuwa hatuna mtazamo sahihi wa sheria. Inamaanisha kuwa Shetani na washirika wake wametubadilisha ili kuendana na namna yao ya kufikiri. Inamaanisha kuwa moyo wa asili unaibua kichwa chake kibaya.)
- Hebu tujaribu kile tulichokuwa tukikijadili. Kama kwa sasa una tatizo kubwa maishani mwako, je, nini chanzo cha tatizo hilo? Kama una mambo yaliyokupata zamani yanayokuumiza, je, chanzo cha maumivu hayo ni kipi? (Somo letu linasema kwamba kimantiki inapaswa yatokane na muunganiko wa sababu tatu:
- Hukumtii Mungu, umevunja sheria ya manufaa;
- Mtu fulani hakumtii Mungu, na kwa hiyo amevuruga sheria ya manufaa kwako; au,
- Shetani kwa nguvu za miujiza (Kama Ayubu) amevuruga sheria ya manufaa maishani mwako.)
- Soma Warumi 7:10-13. Je, ni kwa namna gani sheria nzuri ajabu ya manufaa inasababisha mauti? (Sheria ina kipengele cha kiroho na kipengele cha asili (kawaida). Dhambi (kushindwa kuishika sheria) huleta mauti. Siwezi kuitii sheria, kwa hiyo nastahili kifo. Hiyo ndio sababu tunahitaji neema. Hicho ndicho kipengele cha kiroho. Kwa upande mwingine, sheria ni “takatifu, ya haki na nzuri,’ na tukitaka kunufaika na kubarikiwa, tutajitahidi kwa kufanya kila tuwezalo kuitii sheria.)
- Je, tulifikiaje kwenye suala la kwamba sheria nzuri ajabu ya manufaa ingeniua bila uwepo wa Yesu? (Angalia tena Warumi 7:11. Kuingia kwa dhambi ndio sababu.)
- Rafiki, je, somo hili limekushawishi kwamba kwa mujibu wa neema, sheria ni rafiki wako? Katika pambano la wema na uovu, ni muhimu sana kuelewa manufaa ya sheria. Wale waliookolewa wanaelewa kiungo hiki chanya cha sheria. Je, utaamua hivi leo kuwa mshawishi wa ukweli kwamba sheria inatubariki, na dhambi haina manufaa?
- Hebu turejee kwenye masuala ya msingi. Tunaokolewa kwa neema pekee, sio kwa matendo yetu yoyote. Je, tunapaswa kuichukuliaje sheria? Je, kama adui? Je, kama kitu kisichokuwa cha msingi? (Hapana! Sheria ni rafiki wetu wa karibu sana kwa sababu utiifu wa sheria hubeba mibaraka mikubwa.)
- Juma lijalo: Mambo ya Mwisho: Yesu na Watu Waliookolewa.