Mungu Mtakatifu na Mwenye Haki (Yoeli)
(Yoeli 1 & 2)
Swahili
Year:
2013
Quarter:
2
Lesson Number:
3
Utangulizi: Chukulia kwamba unapata maafa maishani mwako. Je, lengo lako la msingi sana ni lipi? Kupona janga hilo, na ikiwezekana, kulibadilisha kuwa la manufaa kwako. Biblia ina ahadi za Mungu kutusaidia. Juma hili tunaangalia unabii wa Yoeli, nabii mdogo ambaye sio tu kwamba alitabiri maafa, bali pia alitabiri mwisho wa dunia. Pia alitabiri kile atakachokifanya Mungu ili kutusaidia. Hebu tuzame kwenye kitabu cha Yoeli ili tuone kile alichonacho Mungu kwa ajili yetu katika nyakati za dhiki!
- Mapigo
- Soma Yoeli 1:1-3. Je, ni tukio gani linakuja? Jambo ambalo halijawahi kutokea. Jambo linalopaswa kukumbukwa vizazi na vizazi.)
- Soma Yoeli 1:4 na Yoeli 1:6-7. Jambo gani linaelezewa? (Pigo la nzige.)
- Je, uharibifu wa mazao upo katika hali gani? (Mazao yote yameharibiwa.)
- Soma Yoeli 1:5. Kwa nini walevi waonyeshe kujali? (Kwa sababu hawana cha kunywa.)
- Soma Yoeli 1:9. Kwa nini makuhani wajihusishe? (Kwa sababu sadaka za hekaluni zimeliwa.)
- Kwa nini Biblia ijikite kwa walevi na makuhani? (Hii inaonyesha kwamba majanga yanawapata watu wote – wema na wabaya. Wale wanaoharibu mvinyo na wale wanaoutumia kwa huduma ya Mungu – wote wanataabika.)
- Soma Yoeli 1:12. Je, ni janga gani jingine limekuja? (Inaonekana kwamba kuna ukame pia.)
- Ni kitu gani kinachokupa furaha? (Kula – kupo hata kwenye Biblia. Uharibifu wa chakula na vinywaji umefanyika vibaya sana kiasi kwamba watu hawana furaha.)
- Unafuu wa Janga
- Soma Yoeli 1:13-14 na Yoeli 1:19-20. Je, jibu kwa janga hili ni lipi? (Kufunga na kuomba. Kwenda kwenye nyumba ya Mungu kumlilia Mungu.)
- Soma tena Joel 1:6. Je, Mungu analilinganisha janga hili na kitu gani? (Inaonekana ni kama kuvamiwa na jeshi la adui lenye nguvu kubwa.)
- . Siku ya Bwana
- Soma Yoeli 2:1. Jambo gani linakuja? (“Siku ya Bwana.”)
- Je, hiyo inamaanisha nini? (Inarejea ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
- Soma Yoeli 2:2. Fikiria kuhusu mwenendo wa kitabu cha Yoeli. Je, ni rejea gani ya kipekee tunayoiona mara mbili? (Rejea ya kuvamiwa na taifa la kigeni – jeshi kubwa lenye nguvu kubwa.)
- Je, Mungu pamoja na Yoeli wapo kwenye mada ya “Mambo Mabaya Yanayoweza Kutokea?” Au, je, unaona sababu nyingine ya kuunganisha pigo baya na ujio wa Mara ya Pili? (Ahadi ya kuokolewa kutoka maovuni anayotupa Mungu ni ujio wake wa Mara ya Pili. Wakati huo atawaokoa watu wake na kuanza uangamizi wa mwisho wa uovu.)
- Soma Yoeli 2:3. Je, jeshi la Mungu linafanyaje kazi? (Linaunguza kilichopo kwenye njia yake.)
- Soma Ufunuo 18:8-10 na 2 Petro 3:10. Je, unabii wa Yoeli unaendana na unabii wa Agano Jipya wa nyakati za mwisho? (Ndiyo, unabii wote unatuambnia kwamba dunia itaangamizwa kwa moto.)
- Soma Yoeli 2:4-6. Tunapoteza maaana kubwa ya hili fungu kwa sababu ya maarifa yetu ya kisasa ya kivita. Fikiria kwamba jeshi pekee ulilowahi kuliona lilijumuisha maaskari wa ardhini wakiwa na silaha za mikuki, upinde na mishale. Kama ungekuwa mmojawapo wa hao askari, je, ungejisikiaje kupambana na askari wenye farasi? Vipi kuhusu farasi wanaokokota magari ya kijeshi? Vipi kama kamwe ungekuwa hujawahi kuona farasi? (Kiwango cha hofu na mshangao unaelezewa kwa ufupi katika “kuruka juu ya vilele vya milima.” Mungu huleta hofu kwa waovu.)
- Soma Yoeli 2:10-11. Je, ujio wa Mara ya Pili ni mkuu na unaogofya kwa kiasi gani?
- Je, vifungu hivi vinaashiria nini kuhusu uwezo wa Mungu? (Unavuka hadi kwenye nyota!)
- Je, jibu kwa swali la mwisho: “Nani awezaye kustahimili” ni lipi? (Soma Yoeli 2:12-13. Wale wanaomrudia Mungu wanaweza kustahimili.)
- Hatutajifunza Yoeli 2:14-27. Mkanganyiko uliopo ni kwamba mafungu haya yanaonekana kuelezea ujio wa Mara ya Pili na wokozi wa Mungu wa watu wake katika siku za Yoeli. Maelezo yangu pekee katika jambo hili ni kwamba Yesu alifanya jambo linalofanana na hilo katika Mathayo 24 alipoelezea uangamivu wa Yerusalemu na ujio wa Mara ya Pili kwa namna iliyoyaunganisha matukio yote mawili.
- Soma Yoeli 2:1. Jambo gani linakuja? (“Siku ya Bwana.”)
- Uwezo wa Roho Mtakatifu
- Soma Yoeli 2:28. “Hata itakuwa baada ya hayo.” Baada ya kitu gani? Ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Hiyo haiwezi kuwa maana, kwa sababu katika Matendo 2 Paulo anasema kuwa kile kinachotokea wakati wa Pentekoste ni utimilifu wa maneno yaliyopo kwenye Yoeli 2.)
- Unadhani Mungu anamaanisha nini kwa kusema “baada ya hayo?” (Rejea mwendelezo wa kitabu hadi hapa tulipofikia. Janga lilifuatiwa na ujio wa Mungu na wokovu. Yesu alikuja duniani na kulishinda janga la dhambi – na “baada ya hayo” Roho Mtakatifu alikuja kwa uwezo.)
- Je, itakuwa haki kuhitimisha kwamba zawadi ya Roho Mtakatifu ni sehemu ya msingi ya ushindi dhidi ya janga? (Ndiyo! Ni kiini cha ushindi dhidi ya dhambi.)
- Je, zawadi ya Roho Mtakatifu imeenea kwa kiasi gani katika Yoeli 2:28-29? (Ni zawadi iliyotolewa kwa watu wote. Jinsia sio jambo la msingi. Umri sio jambo la msingi. Hadhi katika jamii sio jambo la msingi.)
- Unadhani ni kwa nini Mungu anasisitiza jambo hili la usawa kupitia kwa Yoeli – mtu aliyetabiri kipindi ambacho ukuhani ulikaliwa na wanaume pekee? (Roho Mtakatifu ni uwezo wa Mungu. Jambo la msingi ni kwamba katika pambano la mwisho kumalizia ushindi wa Mungu, watu wote wa Mungu wana fursa sawa katika kukamilisha jambo hilo.)
- Soma Yoeli 2:30. Je, ni kitu gani hasa tunachopaswa kukifanya sote kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu? (Mafungu ya awali yalisema unabii, ndoto na maono. Fungu hili linasema “maajabu” na linasema kwamba yanafanyika duniani.)
- Hebu tulichunguze hili zaidi katika kitabu cha Matendo. Soma Matendo 2:1-3. Je, jambo hili linatufundisha kwamba tutarajie kitu gani? (Upepo, kelele, moto na kunena kwa lugha.)
- Hebu tulichunguze hili zaidi katika kitabu cha Matendo 5:12-16. Je, jambo hili linatufundisha kwamba tutarajie kitu gani? (Ishara za maajabu na uponyaji.)
- Soma Mathayo 24:24. Je, ni maonyo gani tunayopewa kuhusu matukio kama hayo katika nyakati za mwisho? (Kwamba Shetani atawafanya mawakala wake kutenda ishara kuu na miujiza.)
- Hebu tuangalie kwa undani zaidi suala hili kwa kuuchunguza muktadha. Soma Mathayo 24:23-26. Je, ni katoka muktadha upi tunaona hizi ishara za Kishetani? (Zinaunganishwa na mtu fulani anayedai kuwa yeye ni Yesu.)
- Je, hii ni njia ya kuitegemea sana kutenganisha kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya Shetani – ya kwamba mtu huyo anadai kuwa yeye ni Yesu?
- Hebu tuangalie kwa undani zaidi suala hili kwa kuuchunguza muktadha. Soma Mathayo 24:23-26. Je, ni katoka muktadha upi tunaona hizi ishara za Kishetani? (Zinaunganishwa na mtu fulani anayedai kuwa yeye ni Yesu.)
- Katika Mathayo 12 Mafarisayo wanahusianisha miujiza iliyotendwa na Yesu na uwezo wa Shetani. Soma Mathayo 12:25-28. Je, Yesu anajibu nini dhidi ya mashtaka hayo?
- Soma Mathayo 12:31-32. Je, dhambi isiyosamehewa ni ipi? (Kuuhusianisha uwezo wa Roho Mtakatifu na Shetani.)
- Je, kazi yetu kutambua ishara za nyakati za mwisho na maajabu imekuwa ngumu zaidi? (Nadhani hili ni onyo madhubuti kwetu sisi kuwa makini sana katika kulaumu utendaji wa miujiza (au udhihirishaji wowote wa wazi wa Roho Mtakatifu) unaofanywa na Wakristo wenzetu.)
- Rafiki, katika dunia hii tunakabiliana na matatizo na hata mara nyingine maafa. Mungu anaahidi kwamba atatenda kila jambo kwa usahihi. Sehemu ya hii ahadi ni kwamba atamtuma Roho Mtakatifu awe pamoja nasi na kutuwezesha kutenda mambo makuu. Je, Roho Mtakatifu yu maishani mwako? Je, ungependa kumwomba Roho Mtakatifu akujie kwa nguvu kabisa?
- Soma Yoeli 2:28. “Hata itakuwa baada ya hayo.” Baada ya kitu gani? Ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Hiyo haiwezi kuwa maana, kwa sababu katika Matendo 2 Paulo anasema kuwa kile kinachotokea wakati wa Pentekoste ni utimilifu wa maneno yaliyopo kwenye Yoeli 2.)
- Juma lijalo: Bwana wa Mataifa Yote (Amosi).