Watu Maalum wa Mungu (Mika)
(Mika 1, 2, 5 & 7)
Swahili
Year:
2013
Quarter:
2
Lesson Number:
7
Utangulizi: Je, kila mtu anahitaji tumaini? Jibu la dhahiri ni, “ndiyo.” Lakini, tumaini ni kitu cha kuchekesha sana. Huhitaji tumaini kama unaridhika na jinsi mambo yalivyo hivi sasa. Katika Ufunuo 3:16 Mungu anasema anataka kuwatapika watu walio vuguvugu. Mungu anapendelea tukiwa moto au baridi. Je, hiyo inamaanisha kuwa Mungu anataka kuwatapika watu wasiohitaji tumaini? Utakumbuka juma lililopita Mungu alipeleka mnyoo uliokausha mti uliompa Yona kivuli? Je, Mungu ataleta “minyoo” maishani mwetu ili kutuweka kwenye mkao ambao tunahitaji tumaini? Kama hivyo ndivyo, je, Mungu anatoa tumaini la aina gani? Hebu tuzame kwenye somo letu la kitabu cha Mika ili tujifunza zaidi!<\p>
- Unabii Kuhusu Adhabu
- Soma Mika 1:1. Je, nabii ni nani? (Mika.)
- Je, ujumbe wa unabii wake ni upi? (Mungu amempa maono kuhusu mustakabali wa Yerusalemu na Samaria.)
- Soma Mika 1:2-5. Hebu subiri kidogo! Huko nyuma tulijifunza kwamba Yuda ilijumuisha makabila mawili ya upande wa kusini na Israeli ilijumuisha makabila kumi ya kaskazini. Yerusalemu ilikuwa katika Yuda. Kwa nini Yuda inaadhibiwa kutokana na dhambi za Israeli? (Tayari Israeli imekwishashindwa na Ashuru. Sasa Mika anaziunganisha Yuda na Israeli pamoja. Utaona kwamba anarejea “dhambi ya Yakobo,” na Yakobo ni baba wa wana waliokuja kuwa makabila kumi na mawili yaliyoifanya Yuda na Israeli.)
- Soma Mika 2:3-4. Je, ni adhabu gani inayoonekana kuwa mbaya zaidi? (Dhihaka, kebehi. Sote tumeshatokewa na mambo mabaya maishani. Mambo hayo mabaya yanapoozwa na marafiki wanaotukumbatia ili kutuliwaza. Inakuwa rahisi zaidi kama watu wanakuwa wenye huruma. Hapa, wale wanaoteseka wanadhihakiwa na watu wengine.)
- Kwa nini Mungu aruhusu jambo hilo? Mungu ni Mungu wa Upendo! (Tuna viashiria fulani. Mungu anasema “hamwezi kujiokoa.” Katika sehemu inayofuata tutajifunza asili ya dhambi zao. Tutaona kwamba wanaweka tumaini lao kwao wenyewe, ama kupitia kwenye sanamu walizozifanya au kupitia kwenye mfumo wa haki wenye udanganyifu. Hayo ni majivuno ya uongo na Mungu anaikatilia mbali.)
- Soma Mika 2:5. Kumbuka kwamba katika fungu la 4 tatizo lilikuwa ni kwamba watu walipoteza mashamba yao, na watu wasiostahili (wasaliti) waliichukua. Je, inamaanisha nini kwa “kuyagawa mashamba yao kwa kura?” (Soma Mithali 16:33. Kupiga kura ilikuwa ni njia ya kubainisha mapenzi ya Mungu. Ilikuwa ni namna ya Mungu ya kuongoza. Badala ya Mungu kugawanya mashamba miongoni mwa watu wake, sasa maadui wa Mungu watafanya uamuzi huo.)
- Soma Mika 1:1. Je, nabii ni nani? (Mika.)
- Tatizo la Dhambi
- Soma Mika 2:6-7. Je, manabii wengine wanatabiri juu ya jambo gani? (Wanasema kuwa mambo mabaya hayatawatokea watu. Mungu hakasiriki na wala hafanyi mambo kama hayo.)
- Umewahi kuwasikia watu wakisema kuwa hukumu haiendani na Mungu mwenye upendo? Asili ya Mungu ya upendo haitoi mwanya wowote wa adhabu? (Sehemu ya tatizo la dhambi kwa watu hawa ni mtazamo wao: hawakuamini kwamba Mungu atatoa hukumu juu yao.)
- Soma tena Mika 2:7. Je, Mungu anatoa jibu gani kuhusu hukumu katika sehemu ya mwisho ya fungu la 7? (Mungu anatenganisha kati ya walio wema na walio waovu. Tunafahamu kutoka katika kitabu cha Ayubu na kutokana na uzoefu wetu maishani kwamba mambo mabaya mara nyingine huwatokea watu wema. Lakini, tunafahamu pia kwamba mambo mabaya mara nyingi huwatokea watu wabaya.)
- Soma Mika 2:8. Mara kwa mara Mungu huonya kuhusu matajiri kuwaonea masikini. Je, ni kitu gani kinachowatokea matajiri hapa? (Watu wa Mungu wanawaibia matajiri.)
- Je, Mungu analichukuliaje suala la kuwanyanyasa matajiri? (Wale wanaofanya hivyo ni maadui wa Mungu.)
- Soma Mika 2:9. Je, ni uovu gani mwingine unaofanywa na hawa watu? (Wanawafukuza wanawake na watoto kutoka kwenye nyumba zao. Wanawanyang’anya watu hawa mibaraka ambayo Mungu aliwapa.)
- Jambo hili linagusa sera ya umma iliyopo katika nchi nyingi. Watu wasio matajiri wanahoji kwamba matajiri wanapaswa kutozwa kodi kubwa sana kwa sababu tu wanaweza kuimudu. Je, mafungu haya yanatufundisha nini kuhusu jambo hili? (Mungu yu kinyume na vitendio visivyo vya haki. Kama matajiri wanawaibia masikini, Mungu yu kinyume na jambo hilo. Kama masikini wanawaibia matajiri, Mungu yu kinyume na jambo hilo. Mungu anasema “usichukue mibaraka yangu” kutoka kwa watu wangu.)
- Soma Mika 2:10. Je, maneno ya Mungu kuhusu mustakabali wa siku zijazo ni yapi? (Watu wa Mungu wanatakiwa kuondoka. Wameinajisi na kuiharibu nchi. Wanapaswa kuondoka.)
- Mungu anawaambia watu wake, kama unaiamini miungu mingine, kama huwatendei vizuri watu wengine, hukumu inakuja, amini usiamini. Je, watu hawa watalihitaji tumaini? (Ndiyo, dhambi zetu zinapoishia kwenye hukumu, tunakuwa makini sana na hitaji letu la tumaini. Hebu tuliangalie tumaini katika sehemu inayofuata.)
- Soma Mika 2:6-7. Je, manabii wengine wanatabiri juu ya jambo gani? (Wanasema kuwa mambo mabaya hayatawatokea watu. Mungu hakasiriki na wala hafanyi mambo kama hayo.)
- . Tumaini Kuu
- Soma Mika 5:1. Je, hukumu imeanza? (Ndiyo!)
- Soma Mika 5:2. Je, hapa tunalo tumaini gani? (Huu ni unabii kumhusu Yesu, aliyezaliwa Bethlehemu!)
- Je, una mashaka kwamba Yesu alikuwepo? Je, una mashaka kwamba Yesu ni Mungu? Angalia unabii wa Mika ulionyooshea kidole mahali alipozaliwa!
- Je, unaweza kuelewa ni kwa nini wanafunzi wa Yesu walidhani kwamba atawaangusha Warumi na kuitawala Israeli?
- Je, unaielewaje kauli ya “atakayekuwa Mtawala katika Israeli?” (Lazima hii iwe ni rejea ya ujio wa Mara ya Pili, kwa kuwa Yesu “hakutawala” kwa namna ya kawaida wakati wa uhai wake hapa duniani.)
- Soma Mika 5:3. Je, “yule aliye na utungu ambaye huzaa” ni nani? (Mariamu, mamaye Yesu. Jambo hili linatabiri namna ambayo Mungu anafanyika kuwa mwanadamu na kuishi pamoja nasi.)
- Kwa nini Israeli inatelekezwa hadi hapo baadaye? (Kama tulivyoona hapo kabla, watu wa Mungu walimwangusha. Licha ya kutokuwa waaminifu, Mungu alizindua mpango wake wa kishujaa wa uokoaji. Jambo hili linaleta tumaini!)
- Soma Mika 5:4. Yesu anatabiriwa kuwa atakuwa kama mchungaji. Je, jambo hilo linahamasishaje tumaini? (Mchungaji hulinda. Ulinzi huu huja na nguvu yenye uwezo wa Kimungu, na hutupatia usalama mkubwa kabisa.)
- Soma Mika 5:5-6. Nina uhakika wasomi waliokuwepo nyakati za Yesu waliyaona mafungu haya na kupigwa na butwaa kwamba ni kwa namna gani yalihusiana na suala la Yesu kufanyika kuwa mwanadamu. Huenda wanafunzi wa Yesu walidhani kwamba wao ndio walikuwa kati ya wachungaji wadogo/viongozi kati ya saba hadi kumi na tano. Unadhani mafungu haya yanahusianaje? (Hii inaonekana kuunga mkono mtazamo wa “mwokozi shujaa.” Lakini, kwa kuwa jambo hili halikutokea likihusianishwa na Yesu, basi jambo hili ama linarejea ushindi halisi wa Israeli katika kipindi cha mwisho wa wakati au linamaanisha ushindi wa kiroho wa watu wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu. Kama “Mwashuri” inarejea nguvu za uovu zinazopingana na watu wa Mungu, Yesu alipata ushindi dhidi ya dhambi na nguvu za uovu pale msalabani.)
- Soma Mika 5:7-8. Je, watu wa Mungu wametawanyika duniani kote hivi leo? (Ndiyo. Kwa kiasi ambacho hii inarejea Wayahudi, hakika huo ni ukweli. Kwa kiasi ambacho hii inarejea “Wayahudi wa kiroho” (Wakristo), bado ni ukweli.)
- Soma Mika 5:9. Je, tumaini letu limejengwa juu ya nini? (Ya kwamba Mungu atatuokoa! Ya kwamba tutainuliwa!)
- Soma Mika 5:10-11. Je, inakuwa ni msaada kwa kiasi gani kwa Mkobozi wetu kuangamiza magari yetu ya kukokotwa na farasi na maeneo yetu tuliyojizatiti vizuri? Hiyo inaonekana kama vile ambavyo “mtu mbaya” atakavyofanya! (Magari ya kukukotwa na farasi yalikuwa ni zana za hali ya juu za kijeshi. Maeneo muhimu yaliyojizatiti ndo yalikuwa ulinzi wa kijeshi. Mungu anasema kwamba nitaangamiza kila kitu mnachokitegemea – kitu ambacho ni tofauti na mimi.)
- Soma Mika 5:12-14. Kwa nini vitu hivi vinaangamizwa? (Kwa mara nyingine, hivi ndio vitu tunavyovitegemea badala ya kumtegemea Mungu.)
- Soma Mika 5:15. Kwa nini, katikati ya tangazo la tumaini, tunaona uangamivu? (Soma Mika 6:8. Mungu anawatafuta wale walio waaminifu! Anawatamani watu watakaotembea pamoja naye.)
- Soma Mika 7:18-19. Je, tumaini la wadhambi ni lipi? (Mungu atazika dhambi zetu “chini ya nyayo” na kuzitupa “katika vilindi vya bahari.”)
- Kwa nini hilo ni muhimu? (Soma Ufunuo 12:10-11. Shetani anatushtaki. Yesu anaahidi kuzika dhambi zetu.)
- Rafiki, Mungu wetu ni Hakimu na Mkombozi. Tunatakiwa kuyatilia maanani majukumu yote. Tunapoitegemea miungu mingine na kutotii, tunaweza kuitarajia hukumu. Lakini, hukumu huja na tumaini. Tumaini lililojengwa kwa Mungu atakayetusamehe na kutuokoa na kufuta dhambi zetu. Je, utadhamiria hivi leo kumtumaini Mungu na kuishi kwa mujibu wa neno lake?
- Juma lijalo: Kuutumaini Wema wa Mungu (Habakuki).