Matengenezo: Kuponya Mahusiano Yaliyovunjika
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mara nyingine umoja ni jambo gumu! Miaka mingi iliyopita nilikuwa kwenye kikao ambacho uongozi wa kanisa letu mahalia ulikuwa unakutana na mwenyekiti (rais) mpya wa konferensi pamoja na mchungaji wetu mpya. Nikiwa kama Mchungaji Mlei, mimi ndiye niliyekuwa kiongozi wa kanisa mahalia. Mwenyekiti mpya wa konferensi alimuuliza kila mzee wa kanisa juu ya maoni yake kulihusu kanisa. Mzee mpya aliyekuwa amechaguliwa alisema kuwa mambo yalikuwa yanakwenda vizuri, isipokuwa tu kwamba kulikuwa na tatizo kwenye teolojia yangu na kwamba uongozi wa kanisa ulikuwa na tatizo la ubaguzi. Wazo langu la harakaharaka lilikuwa ni kwamba umoja ungeendelea kuhifadhiwa endapo ningesimama na kumkaba! Mimi pamoja na yeye kamwe hatukuwahi kujadiliana kuhusu teolojia. Mzee huyu alikuwa amehamia kutoka kanisa jingine, na ingawa alikuwa kwenye kundi la jamii ya watu wa hali ya chini, tulimchagua kuwa mzee wa kanisa ndani ya mwaka mmoja – tendo lisilo la kawaida kwa kundi la wabaguzi! Shambulio hili lisilotarajiwa na lisilo la haki dhidi ya hadhi/sifa yangu na dhidi ya uongozi wa kanisa lilisababisha hisia mbaya moyoni mwangu. Je, tunapaswa kufanya nini mambo kama hayo yanapotokea? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Utatuzi wa Migogoro
- Soma Mathayo 18:15. Hebu turejee kwenye kisa changu kilichopo kwenye utangulizi. Ubaguzi ni dhambi. Kama huyu mzee mpya alidhani kuwa viongozi wengine pamoja na mimi tulionyesha ubaguzi dhidi yake kutokana na asili yake, je, wajibu wake ulikuwa ni upi? (Kwa mujibu wa hili fungu, alipasa kunijia. Au, angeleta wazo lake kwenye kikao cha wazee wa kanisa.)
- Je, sababu ya kumwendea mtu binafsi ukiwa na hoja zako ni ipi? (mara kadhaa huwa tuna mitazamo tofauti. Mara nyingine huwa hatufahamu habari kamili. Fungu hili linasema kuwa kushiriki hoja zako na mtu mwingine kunakusaidia kuelewana na mshiriki mwenzako wa kanisa.)
- Soma Mathayo 18:16. Je, hii inaashiria kuwa asili ya tatizo lililopo ni ipi? (Hii inaashiria kuwa baada ya kukutana kwa awali, utakuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na ukweli wa mambo.)
- Je, faida ya kuwahusisha watu wengine wachache ni ipi? (Kama washiriki wengine wa kanisa wangesema kuwa, “Bruce, tunaliona tatizo,” ningewachukulia kwa dhati kabisa. Kwa upande mwingine, kama huyu mzee mpya angewatafuta watu wengine ambao walikuwa na mawazo kama yake, nina shaka kama angempata mtu hata mmoja.)
- Je, kulikuwa na hasara gani kwa upande wangu (ambaye nilikuwa mlengwa wa yale malalamiko) wa kuyaleta yale malalamiko mara ya kwanza kabisa mbele ya mwenyekiti mpya wa konferensi na mchungaji mpya? (Je, unajibuje mashambulizi kama hayo? Je, utajibu kuwa, “Mimi sio mbaguzi na kwamba tunakubaliana na teolojia yangu?” Badala yake nilichokisema ni kwamba, “Sijawahi kuyasikia haya malalamiko hapo kabla, na ninadhani yanaweza kuwa yanaibuka kutokana na tofauti za kimtazamo.”)
- Soma Mathayo 18:17. Je, hatua ya mwisho katika mchakato wa upatanisho ni ipi? (Kuliacha kanisa lifanye maamuzi juu ya jambo linalohusika.)
- Hebu tuliangalie suala hili kwa mujibu wa mtazamo wa mzee mpya. Kwa nini kanisa linaachiwa kufanya maamuzi? Je, kura kama hiyo itakuwa ya haki? (Soma Mathayo 18:18. Hii inatuambia kuwa kanisa linabeba mamlaka ya Mungu. Kama mashaka haya yangekuwa ya kweli, Mungu angeyashughulikia. Kama mashtaka yalikuwa ya uongo, basi Mungu angeyashughulikia pia.)
- Soma Mathayo 18:19-20. Je, Yesu ametoka nje ya mada? (Hapana. Wazo la kuzungumza na watu wengine na la kuomba na watu wengine kuhusiana na suala fulani ni jambo la msingi sana. Kamwe sikuwahi kuelewa jinsi teolojia ya huyu mzee mpya ilivyotofautiana na teolojia yangu. Kwa uelewa wangu, hakuna mtu mwingine yeyote yule aliyewahi kuushutumu uongozi wa kanisa kwamba una ubaguzi. Huenda asilimia arobaini ya washiriki wa kanisa letu walitoka kwenye tabaka la chini, na uhuishaji wa suala la kijamii ilikuwa sehemu ya msingi ya kuakisi kwetu upendo wa Mungu.)
- Soma Mathayo 18:15. Hebu turejee kwenye kisa changu kilichopo kwenye utangulizi. Ubaguzi ni dhambi. Kama huyu mzee mpya alidhani kuwa viongozi wengine pamoja na mimi tulionyesha ubaguzi dhidi yake kutokana na asili yake, je, wajibu wake ulikuwa ni upi? (Kwa mujibu wa hili fungu, alipasa kunijia. Au, angeleta wazo lake kwenye kikao cha wazee wa kanisa.)
- Msamaha
- Soma Mathayo 18:21. Tukio hili lilitokea miaka mingi iliyopita, lakini ukweli kwamba bado ninalikumbuka inaonyesha kuwa linauma na kwamba pengine nina tatizo kwenye suala la msamaha. Je, unadhani kuwa Yesu amebadili mada? (Hapana. Yesu bado anazungumzia jinsi ambavyo Wakristo wanavyotendeana.)
- Huyu mzee kijana kamwe hakuwahi kuniomba msamaha. Je, hiyo inajalisha? (Utabaini kuwa Petro anauliza suala la msamaha kwa wale wanaokukosea, sio kwa wale wanaoomba kusamehewa.)
- Soma Mathayo 18:22. Je, tunapaswa kuwa na kijitabu kidogo na kuweka alama kuwa mara ngapi tunamsamehe mtu fulani? Ningekuwa na wakati mgumu kuhesabu hadi 77.
- Je, Yesu na Petro wanakubaliana kwamba kuna ukomo kuhusu idadi ya msamaha tunaopaswa kumsamehe mtu, na kwamba wanatofautiana tu kwenye usahihi wa idadi?
- Soma Mathayo 18:23-25. Je, suala hili linaendana na mjadala uliotangulia? Je, msamaha unahusika hata kwenye fedha?
- Soma Mathayo 18:26-27. Angalia tofauti iliyopo kati ya ombi la rehema na jibu la mfalme. Je, hiyo inaashiria nini? (Mfalme alimpa zaidi ya kile alichokiomba. Haikuwa rehema tu, ulikuwa ni msamaha.)
- Utabaini kuwa mdeni hakuomba kusamehewa, lakini bado aliupokea msamaha. Kwa nini?
- Soma Mathayo 18:28. Je, mwenendo huu una mantiki? Almanusura familia nzima ya mdeni iuzwe utumwani kwa sababu malofa kama hawa hawakuwa wakilipa kile walichodaiwa!
- Soma Mathayo 18:29-33. Je, jibu sahihi kwa swali la mfalme ni lipi? (Ndiyo, alipaswa kuwa na rehema.)
- Hebu tusimame kidogo na tutafakari kila tulichokijadili hadi sasa. Ninaghafirishwa na mzee mdogo anayetilia shaka teolojia yangu na kuniita mbaguzi mbele ya ofisa mpya wa kanisa nisiyemfahamu. Je, ninapaswa kukumbuka jambo gani? (Ninapaswa kukumbuka kwamba Yesu aliitwa majina na kudhihakiwa kwa sababu ya dhambi yangu. Kama Yesu anaweza kunisamehe, ninawezaje kushindwa kusamehe kosa dogo kama hilo?)
- Je, jambo hili linatoa nuru gani ya ziada kwenye mjadala kati ya Yesu na Petro kuhusu idadi tunayopaswa kusamehe? (Yesu hazungumzii idadi mahsusi. Je, mtu gani anayesoma hili somo ameombwa kusamehe zaidi ya Yesu alivyotusamehe?
- Hebu tusimame kidogo na tutafakari kila tulichokijadili hadi sasa. Ninaghafirishwa na mzee mdogo anayetilia shaka teolojia yangu na kuniita mbaguzi mbele ya ofisa mpya wa kanisa nisiyemfahamu. Je, ninapaswa kukumbuka jambo gani? (Ninapaswa kukumbuka kwamba Yesu aliitwa majina na kudhihakiwa kwa sababu ya dhambi yangu. Kama Yesu anaweza kunisamehe, ninawezaje kushindwa kusamehe kosa dogo kama hilo?)
- Soma Mathayo 18:34-35. Wow! Je, mdeni ambaye hakusamehe aliishia pabaya? (Ilikuwa ni wakati wake kuuzwa utumwani. Sasa anapelekwa gerezani na kuteswa.)
- Je, hii inamaanisha kuwa Baba wetu wa mbinguni mwenye upendo atatutesa kama hatusamehi wengine? (Soma 1 Yohana 4:19-21. Hili ni mojawapo kati ya mafungu mengi linalosema kwamba umuhimu wa kuwa Mkristo ni kuwapenda wengine. Tusipouakisi upendo hatujaukubali upendo wa Yesu na tumepotea.)
- Je, hii kauli ya “mpelekeni kwa watesaji” inatufundisha kuwa huyu Mfalme alikuwa na msamaha mmoja ndani yake, na si misamaha saba mara sabini, au hata misamaha saba? (Jambo tunalotakiwa kulifahamu kuhusu visa ni kwamba si kila sehemu inalenga kufunza/kufundisha. Dhana ya kisa ni kwamba tunapaswa kuwasamehe watu wengine kwa sababu ya msamaha mkuu wa Mungu kwetu. Dhana sio kwamba Mungu anatutesa tunapotenda dhambi mara mbili.)
- Soma Mathayo 18:21. Tukio hili lilitokea miaka mingi iliyopita, lakini ukweli kwamba bado ninalikumbuka inaonyesha kuwa linauma na kwamba pengine nina tatizo kwenye suala la msamaha. Je, unadhani kuwa Yesu amebadili mada? (Hapana. Yesu bado anazungumzia jinsi ambavyo Wakristo wanavyotendeana.)
- . Kuutambua Upendo
- Soma Ufunuo 3:19. Kile tulichojifunza hadi sasa kinaweza kutufanya kudhani kuwa wajibu wetu wa upendo unatufanya tusamehe tu. Je, fungu hili linaleta jambo gani kwenye huu mjadala? (Mara nyingine upendo hukemea na kuadabisha. Lazima tusamehe, lakini upendo sio jambo la kijinga kama ile kauli ya “sawa tu, hakuna tatizo” pale ambapo matatizo mazito yanaposhughulikiwa kikamilifu.)
- Soma Filemoni 1:1. Ngoja niwape utangulizi mfupi. Filemoni alikuwa mmiliki wa watumwa aliyebadilishwa na Paulo kuingia kwenye Ukristo. Filemoni alikuwa na mtumwa mmoja aliyeitwa Onesimo aliyetoroka na kuishi na Paulo ili amsaidie Paulo.
- Soma Filemoni 1:8-11. Je, ombi la Paulo kwa Filemoni ni lipi? (Amsamehe Onesimo kwa kumtoroka.)
- Kwa nini Filemoni amsamehe Onesimo? (“Ninakusihi kwa ajili ya upendo.”)
- Soma Filemoni 1:12-16. Je, Paulo anataka nini? (Anataka Filemoni amrejeshe Onesimo ili amsaidie Paulo.)
- Je, masuala ya msingi yamefichika hapa? Je, Filemoni hapaswi kumsamehe Onesimo kwa ajili ya upendo? Je, utumwa si kinyume na sheria ya upendo? Vipi kama unasema, “Sote tunapaswa kupendana sisi kwa sisi: kwa hiyo upendo hukomesha utumwa, upendo humsamehe Onesimo, na upendo humwacha Onesimo amsaidie Paulo pale ambapo Paulo yupo gerezani?” (Filemoni alikuwa na maslahi ya mali kwa Onesimo. Upendo si wizi. Suala linafanywa kuwa gumu zaidi na njia ya Paulo inatufundisha kuwa lazima tuwe na utambuzi jinsi tunavyoutumia msamaha na usuluhishi.)
- Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je, upendo ni jambo lisilowezekana kwako? Je, kushindwa kwako kuukumbatia upendo wa ajabu wa Mungu kunakufanya ushindwe kuwasamewe wengine? Kwa nini usimwombe Mungu akusamehe upungufu wako wa upendo, akupatie upendo zaidi, na aufungue moyo wako kwa wale waliokukosea?
- Juma lijalo: Ahadi ya Uamsho: Utume wa Mungu Wakamilika.