“Mbinguni” Duniani
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Juma lililopita tulijifunza juu ya hekalu la Mungu mbinguni. Tulijifunza kuhusu kiti cha enzi cha Mungu, washauri wake na kitovu cha udhibiti wa ulimwengu. Juma hili tunajifunza juu ya nakala (vivuli). Katika nakala hizo, kile tulichojifunza juma lililopita hakionekani kufanana na tutakachojifunza juma hili. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kwa nini Mungu aliruhusu tutengeneze “nakala” za hekalu, patakatifu pa mbinguni, aliyatengeneza mangapi, na maana ya mambo yote haya!
-
Ujenzi wa Nakala
- Soma Kutoka 25:1-8. Mungu anaomba sadaka kutoka kwa watu wake kwa ajili ya kujenga patakatifu pake hapa duniani. Kwa nini anafanya hivyo? (Anatutaka tuwe sehemu ya hili jukumu.)
- Soma Kutoka 25:9 na Waebrania 8:4-5. Je, tunajifunza nini kuhusu patakatifu pa duniani na patakatifu pa mbinguni? (Patakatifu pa duniani panajengwa (ni sampuli ya) baada ya patakatifu pa mbinguni.)
- Soma Waebrania 8:5-6. Patakatifu papi palipo bora zaidi? (Hii inatuambia kuwa jambo linaloendelea mbinguni ni bora zaidi! Ukweli kwamba patakatifu pa duniani palijengwa baada ya patakatifu pa mbinguni unaonesha kwamba patakatifu pa mbinguni palitangulia kuwepo. Utagundua kwamba Waebrania 8:5 inapaita patakatifu pa duniani kuwa “nakala” ya patakatifu pa mbinguni – kwa namna fulani hivi panawakilisha patakatifu halisi.)
- “Nakala” ni neno linalofurahisha. Je, mtu anaweza kujifunza nini kwako kutokana na kivuli chako?
- Je, ni kitu gani mtu asichoweza kujifunza kwako kutokana na kivuli chako?
- “Nakala” ni neno linalofurahisha. Je, mtu anaweza kujifunza nini kwako kutokana na kivuli chako?
- Nakala ya Yesu
- Soma Yohana 2:13-16. Je, Yesu anapaelezeaje patakatifu pa duniani? (“Nyumba ya Baba yangu.”)
- Je, Yesu alikuwa na madai gani kuhusu uhusiano wake na Mungu? (Yesu ni Mwana wa Baba. “Nyumba ya Baba yangu.”)
- Je, Yesu anadai kuwa na mamlaka gani juu ya nyumba ya Baba Yake? (Yeye ni Mwana.)
- Soma Yohana 2:17-18. Utabaini kwamba viongozi wa Kiyahudi hawakulicheka jambo hili, badala yake walitaka uthibitisho zaidi kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Je, wanahitaji uthibitisho gani? (Ishara.)
- Soma Yohana 2:19-20. Je, unafikiria nini juu ya ishara ya Yesu aliyoitoa? (Cha ajabu, watu hawaonekani kutilia shaka kwamba uthibitisho huu unahitaji hekalu kuvunjwa. Badala yake, wanadhani kwamba ni upuuzi kuamini kuwa hekalu linaweza kujengwa upya kwa siku tatu.)
- Soma Yohana 2:21-22. Je, kimsingi Yesu alimaanisha nini? (Kwamba atafufuka kutoka kaburini katika kipindi cha siku tatu.)
- Je, Yesu anaurejea mwili wake kuwa ndio hekalu la Mungu? Je, hii inamaanisha kuwa nakala ya pili ya hekalu sasa ilikuwepo duniani? Je, palikuwepo na mahekalu mawili, hekalu la jengo na hekalu la Yesu mwenyewe?
- Je, tunawezaje kulichukulia hekalu la jengo na Yesu mwenyewe kama “nakala” za hekalu la mbinguni? (Hekalu la mbinguni ndimo anamokaa Mungu. Mungu alimwambia Musa (Kutoka 25:8) amfanyie patakatifu pa duniani “ili nipate kukaa kati yao.” Yesu ni Mungu. Katika mahekalu yote matatu, yaani, hekalu la mbinguni, hekalu la Yerusalemu, na Yesu mwenyewe, tu na uwepo wa Mungu.)
- Soma Yohana 2:13-16. Je, Yesu anapaelezeaje patakatifu pa duniani? (“Nyumba ya Baba yangu.”)
- . Nakala ya Kanisa
- Soma 1 Wakorintho 3:5-9. Paulo anahitimisha huu mjadala juu ya jukumu la ushirikiano kwa kauli inayosema kuwa walimu ni “watenda kazi wenza” pamoja na Mungu, na kanisa ni “shamba” na “nyumba” ya Mungu. Je, ni kwa namna gani sisi tu shamba na nyumba?
- Soma 1 Wakorintho 3:10-13. Je, tunaona majengo gani hapa? (Kundi linalounda kanisa.)
- Je, wajenzi ni wapi? (Walimu wa Biblia.)
- Je, walimu wengine wa Biblia ni bora kuliko wengine? (Wengine wanajenga kwa kutumia “majani.”)
- Je, wajenzi ni wapi? (Walimu wa Biblia.)
- Soma 1 Wakorintho 3:16-17. Je, hekalu gani linarejewa hapa? (Kristofor Westermeyer, ambaye anaratibu wafasiri wa haya masomo, alibainisha kosa nililolifanya miezi kadhaa iliyopita nilipokuwa nikiandika juu ya hili fungu. Nilidhani kuwa lilikuwa likiwarejea watu, lakini Kris alidhani kuwa linarejea kanisa. Hii inanipa fursa ya kurekebisha kosa. Hapa analirejea kanisa kama hekalu.)
- Je, ni kwa namna gani kanisa ni hekalu?
- Kama kanisa ni hekalu, je, nalo ni nakala nyingine ya hekalu la mbinguni?
- Hebu tufikirie jambo hili kidogo. Tunalo hekalu mbinguni. Tunalo hekalu duniani. Tunaye Yesu na tunalo kanisa. Vyote ni mahekalu. Soma Mathayo 27:50-52. Je, hii inaashiria nini kuhusu hekalu la duniani? (Kupasuka kwa pazia kunaashiria kwamba hekalu halipo tena. Kazi iliyokuwa ikiendelea kwenye hekalu la duniani ilikuwa ikielezea ujio wa jukumu la Yesu. Yesu alipokufa kama Mwana-kondoo kwa ajili ya dhambi zetu, hekalu la duniani lilipoteza umuhimu wake.)
- Je, kanisa limechukua jukumu la kuwa hekalu la Mungu hapa duniani?
- Je, kanisa linapaswa kujihusisha juu ya kushikilia umuhimu wake?
- Nakala Yako
- Soma 1 Wakorintho 6:19-20 na 2 Wakorintho 6:16. Je, hapa hekalu ni lipi? (Sisi ndio hekalu la Mungu.)
- Kwa namna moja hili linaonekana kuwa jambo la kushangaza: Yesu, hekalu la Yerusalemu, Kanisa, na sasa wewe na mimi tu mahekalu. Je, jambo la asili linaloyafanya haya mahekalu yote ni lipi? (Mungu yu ndani yao.)
- Je, umewahi kusikia juu ya mitindo katika Biblia? Ninaposikia mambo kama hayo, mwitikio wangu wa jumla ni kwamba “ili iweje?” Jambo pekee ninalolichukulia kuwa la thamani kwenye hoja juu ya mitindo ni kwamba Mungu ana uchangamano na ni wa kisasa. Je, hili wazo kwamba tunayo mahekalu mengi duniani ndilo linalomaanisha kuwa “ili iweje?”
- Je, uelewa juu ya Mungu kuwa ndani ya hekalu la mbinguni unatutendea nini? (Angalao mambo mawili. Unatuambia kuwa Mungu ndiye mdhibiti! Usawa kati ya hekalu la duniani na hekalu la mbinguni unatuambia kuwa Mungu alikufa ili atuokoe na anatufanyia upatanisho mbinguni sasa hivi. Mungu alibuni makao yake ili kuakisi kazi yake kwetu.)
- Je, uelewa juu ya kanisa kuwa ni hekalu unatutendea nini? (Mungu anatamani kuwa nasi kwa namna iliyopangiliwa. Kanisa linapaswa kuakisi mapenzi ya Mungu.)
- Je, uelewa kwamba sisi ni mahekalu unatutendea nini? (2 Wakorintho 6:17 inatuambia kuwa tunapaswa kuakisi mapenzi ya Mungu. Tunapaswa kutengana na uovu.)
- Je, kuna masomo makuu tunayoweza kujifunza juu ya haya mahekalu? (Mungu anataka kuishi pamoja nasi. Makao yake yamebuniwa huku akituwazia. Anatutaka kumfanyia mahali ili aishi pamoja nasi. Alikuja duniani katika mfuno wa mwanadamu ili aishi pamoja nasi. Alimpeleka Roho Wake Mtakatifu ili aishi pamoja nasi. Tamanio la Mungu kuwa nawe pamoja na mimi linanipatia faraja na hamasa katika hii dunia iliyojaa changamoto nyingi.)
- Soma 1 Wakorintho 6:19-20 na 2 Wakorintho 6:16. Je, hapa hekalu ni lipi? (Sisi ndio hekalu la Mungu.)
- Nakala Zilizounganishwa
- Soma Ufunuo 7:9-10. Je, hapa ni wapi? (Mbele ya kiti cha enzi cha Mungu katika hekalu la mbinguni.)
- Je, mustakabali wa “nakala” ni upi? (Zipo hapa! Tupo hapa. “Kanisa” lipo pale. Yesu yupo pale. Hata hivyo, ninashawishika kumrejea Yesu kama “nakala.”)
- Soma Ufunuo 7:11-12. Kitu cha asili na nakala vinapoungana, je, kitu gani kinatokea? (Vinamsifu Mungu. Vinampa Mungu utukufu.)
- Soma Ufunuo 7:15-16. Je, tunafanya nini katika hekalu la mbinguni? (Tunapata fursa ya kumtumikia Mungu! Tunakuwa kama makuhani wa hekalu la duniani.)
- Soma Ufunuo 7:17. Je, Yesu yupo wapi? (Yupo “katikati ya kiti cha enzi!”)
- Je, uhusiano wetu na Yesu ukoje? (Anatuongoza maishani na katika furaha. Ufunuo 7:15 inatuambia kuwa “atatanda hema yake” juu yetu.)
- Rafiki, patakatifu pa mbinguni na nakala zake duniani vinaonesha kwamba Mungu anatamani kuwa pamoja nasi. Anatamani kuishi ndani yetu. Hatimaye, anatamani kutufanya tuishi pamoja naye kwenye hekalu la mbinguni. Je, ungependa jambo hilo? Kwa nini usimwombe Yesu aishi ndani yako sasa hivi, na kukufanya kuwa hekalu hapa duniani?
- Soma Ufunuo 7:9-10. Je, hapa ni wapi? (Mbele ya kiti cha enzi cha Mungu katika hekalu la mbinguni.)
- Juma lijalo: Kafara.