Sakata la Yona
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Utafanya nini kati ya haya, kubashiri mafanikio ya kijeshi ya nchi yako au kumsaidia adui wa nchi yako? Isipokuwa tu kama huipendi nchi yako, jibu ni rahisi. Fikiria jinsi ambavyo kwa umaarufu unayatabiri mafanikio, na bila umaarufu jinsi unavyomsaidia adui. Maswali haya yanatupatia mwangaza wa somo letu juma hili kuhusu nabii Yona. 2 Wafalme 14:25 inatuambia kwamba Yohana alitabiri mafanikio ya kijeshi ya Israeli. Bila shaka ndio maana alikuwa shujaa wa taifa. Kisha Mungu alimwendea Yona huku akiwa na kazi tofauti kabisa ya Kimisionari. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!
- Utume
- Soma Yona 1:1-2. Jambo hili halionekani kuwa baya katika mtazamo wa mtu mzalendo, si ndio? Kuhubiri dhidi ya maadui wa nchi yako!
- Tatizo dogo ni lipi? (Yona anaambiwa kwenda Ninawi ili kuihubiria. Sio kukaa nyumbani Israeli na kuihubiri Ninawi.)
- Soma Yona 1:3. Unadhani kwa nini Yona alikimbia na kutoroka?
- Soma Yona 1:1-2. Jambo hili halionekani kuwa baya katika mtazamo wa mtu mzalendo, si ndio? Kuhubiri dhidi ya maadui wa nchi yako!
- Dhoruba/Tufani
- Soma Yona 1:4-6. Unaweza kuuelezeaje huo usingizi mzito? Dhoruba ni kali sana kiasi kwamba merikebu inaweza kuvunjika, lakini pamoja na yote hayo Yona ana uwezo wa kuendelea kulala! (Nadhani kitendo hiki kinaelezea msongo/shinikizo kubwa alilolipitia katika kufanya maamuzi ya kutoroka. Kwa sasa amechoka sana.)
- Soma Yohana 1:7-9. Je, mabaharia hawa ni watu wa dini? (Ndiyo. Wanaamini katika nafasi ya Mungu na si mambo yatokeayo kwa bahati.)
- Mustakabali wa imani ya Yona ukoje? (Bado anamwamini Mungu hata kama kwa sasa anamwasi Mungu.)
- Soma Yona 1:10-12. Unadhani lengo la Mungu ni lipi katika jambo hili? Kumwuua Yona? Kumzuia asikimbie?
- Jambo gani lilitokea kwenye uhuru wa uchaguzi tulioujadili katika somo la kwanza? Unakumbuka miti miwili, uchaguzi wa ubunifu na channel factors? (Huu ni uchaguzi mkubwa unaosababisha jambo fulani litokee!)
- Soma Yona 1:13-14. Unadhani mabaharia walifikiria kwamba jambo gani litatokea endapo wangemtupa Yona baharini? (Angekufa.)
- Je, mabaharia wako sahihi kuhusu mtu ambaye anawajibika kimaadili kwa kifo cha Yona?
- Je, wanampa Mungu mipaka? Wanafikiria nadharia kadhaa kumhusu Mungu?
- Je, ungekuwa na mtazamo wa shukrani kiasi hicho dhidi ya Yona endapo ungekuwa umepoteza mzigo wako?
- Soma Yona 1:15-16. Je, Yona ni mmisionari asiyekusudiwa? (Ndiyo! Anafanikiwa kuwaongoa mabaharia merikebuni.)
- Samaki
- Soma Yona 1:17 na Yona 2:5. Ikiwa Yona alitoroka kwa sababu ya hofu, hebu fikiria kitendo cha kutupwa baharini na kisha kumezwa na samaki mkubwa? Je, ingekuwa ni kitendo cha msaada kuwa na mwani uliozingwa kichwani mwako? (Lazima kitendo hiki kiwe cha kutisha.)
- Soma Yona 2:1-2. Yona ana hali mbaya kiasi gani? (Anadhani kuwa anaita kutoka kuzimu, “vilindi vya kaburi.”)
- Nilipokuwa mdogo niliambiwa kuwa endapo sitakuwa mtiifu kwa Mungu, hatasikiliza maombi yangu. Je, hali anayoipitia Yona inatufundisha nini? (Hata kama Yona yupo kwenye uasi, Mungu anamsikiliza na kumjibu!)
- Maombi ya Yona yaliyopo katika Yona 2:3-9 yanamfanya asifikirie kwamba atakufa, na kuwa na matumaini mema, na kuweka nadhiri mpya ya kumfuata Mungu. Endapo wewe ungekuwa Yona, je, ungependa Mungu akuelemee kiasi hiki ili uweze kufanya uchaguzi sahihi?
- Soma Yona 2:10. Matokeo gani yalitokana na maombi ya Yona na badiliko la moyo wake? (Anaokolewa kutoka tumboni mwa samaki ambaye alimwokoa kutoka kwenye tufani.)
- Ninawi
- Soma Yona 3:1-3. Je, Ninawi ni kivutio cha utalii? Inachukua muda wa siku tau kuangalia makumbusho yote na kuendesha kwenda mahali kote? (Maoni kadhaa yanasema kuwa Ninawi ilikuwa na mzingo wa maili 60. Ilichukua muda wa siku tatu kuweza kuutembelea na kuuzunguka mji yote.)
- Soma Yona 3:4. Ungejisikiaje endapo wewe ndio ungekuwa Yona? Wewe ni mgeni katika mji mkubwa unayepeleka onyo la kutisha kwamba utaangamizwa!
- Niliposoma kisa hiki hapo kabla, nilijifunza kwamba palikuwepo na sababu zilizomfanya Yoha awe na hofu. Washamu (wanaoishi Ninawi) ni watu katili. Walikuwa wakiwaangusha watu na kuangukia nguzo na mihimili yenye ncha kali. Waliwaweka watu hai kwenye kuta na kuwatia chapa. Je, wewe ungependelea nini, kumezwa na samaki au kuangushwa kwenye kitu kilichochongoka?
- Soma Yona 3:5-6. Unaelezeaje mambo haya? (Uwezo wa Roho Mtakatifu!)
- Unakumbuka swali lililohusu kufanya uchaguzi kati ya samaki na kitu kilichochongoka? Matokeo haya yanatufundisha nini? (Hatuhitajiki kufanya uchaguzi. Tunaweza kumtumaini Mungu ili tuweze kuwa waaminifu.)
- Soma Yona 3:7-9. Matokeo ya Yona kushirikiana na Mungu wa ajabu wa Mbinguni ni yapi? (Watu wa huu mji mkubwa wanamgeukia Mungu! Usifikirie tu athari za kiroho, bali pia fikiria athari za kisiasa. Washamu walikuwa taifa kubwa lenye nguvu katika kipindi kile. Walikuwa na hadhi ya uovu. Sasa wao ni wafuasi wa Mungu!)
- Soma Yona 3:10. Hii inatufundisha nini kuhusu tabia ya Mungu?
- Nabii Asiye na Furaha
- Soma Yona 4:1-2. Je, Yona ni nabii wa kweli? Je, Yona na Mungu wapo kwenye ukurasa mmoja linapokuja suala la upendo wa Mungu?
- Je, unadhani Yona anasema uongo kuhusu sababu yake ya kukimbilia Tarshishi?
- Kwa nini upendo na huruma za Mungu ndio viwe sababu ya kutoroka? (Yona aliwaambia kuwa uangamivu utatokea ndani ya siku arobaini. Endapo hautatokea, itamfanya aonekane kama nabii wa uongo.)
- Chukulia kwamba wewe ni Yona na kwamba unaeleza ukweli. Angalia tena Yona 3:4. Unawezaje kuelezea jambo hili ili kuepuka tatizo la kuwa nabii wa uongo? (Siku arobaini ziliwapa watu fursa ya kutubu – jambo ambalo walilitimiza. Yona angeweza kuongezea onyo la dhahiri kwamba walitakiwa kutubu.)
- Soma Yona 4:3-4 na usome tena Yona 2:2. Je, unadhani Yona anasema ukweli kuhusu kutaka kufa? Muda mfupi uliopita ametoka kumwambia Mungu amwepushe na kifo alipokuwa tumboni mwa samaki! (Nchini Marekani, tungemwita Yona kuwa ni “malkia wa vitimbwi” – mtu mwenye maigizo kupindukia.)
- Mungu anamwitikiaje malkia wa vitimbwi? (Mungu anaenenda naye kwa upole na anasemezana naye kimantiki.)
- Soma Yona 4:5. Yona anatarajia nini anaposubiria “kuona mji ule utakuwaje?” (Bado ana matumaini kuwa Mungu atauangamiza!)
- Soma Yona 4:6-9. Unaichukuliaje tabia ya Yona?
- Soma Yona 4:10-11. Mafungu haya yanazungumzia nini kuhusu mfumo wa elimu wa Ninawi? Je, hii inamaanisha kuwa watu 120,000 hawakujifunza kuhusu mkono unaozungumziwa? (Hii ni rejea inayowahusu watu walio wadogo sana kiumri kiasi kwamba Mungu hawawajibishwi kwa dhambi wanazozitenda. Ninawi ilikuwa na watu wadogo (wachanga) wengi.)
- Je, Mungu anawajali wanyama? (Ndiyo. Nadhani anachokimaanisha Mungu ni kwamba mnyama ni wa muhimu zaidi kuliko mzabibu wa Yona.)
- Kwa nini Yona anaujali sana mti, badala ya watu na wanyama? (Kwa sababu mti ulikuwa unamtendea Yona wema. Ulimpatia kivuli. Tunaona kwamba Yona ni mbinafsi.)
- Je, unaweza kumchagua Yona kuwa rafiki yako?
- Kwa nini Mungu alimchagua kuwa nabii wake?
- Kwa nini Mungu alimkimbilia na kumtafuta Yona?
- Kwa nini Mungu anajihusisha na Yona wakati Yona anapoonyesha kuchukia?
- Tafakari jambo hili kidogo. Yona anashindwa kutawala hisia zake. Yeye ni mbinafsi. Tabia yake ina dosari. Kisa chake kinabainisha wazi kuwa Washamu walioishi Ninawi walikuwa waovu. Je, hii inatuambia nini kuhusu Mungu wetu? (Mungu anatupenda na anatufuatilia na kutuandama hata pale tunapofanya mambo ya kutisha.)
- Rafiki, Mungu anakuhitaji! Mungu anakuhitaji licha ya dosari na kasoro zako! Kwa nini usifanye uchaguzi sasa hivi wa kumfuata Mungu anayeonesha kiwango kikubwa cha uvumilivu na upendo?
- Soma Yona 4:1-2. Je, Yona ni nabii wa kweli? Je, Yona na Mungu wapo kwenye ukurasa mmoja linapokuja suala la upendo wa Mungu?
- Juma lijalo: Wamisionari Uhamishoni.