Safari ya Wana wa Israeli na Ibada: Kumfahamu Mungu
Utangulizi: Amri Kumi zinaanza na kauli kwamba hatupaswi kuwa na miungu mingine mbele za Mungu wetu. Kwa ujumla nimekuwa nikifikiria kuwa ibada ya sanamu (ambayo ilikuwa ni suala kubwa katika Biblia) ilikuwa ni upumbavu. Kwa nini mtu yeyote yule aabubu kitu walichokifanya kwa mikono yao? Kama suala hili ni la kipumbavu, kwa nini Mungu anajihusisha nalo sana? Kwa nini miungu ya bandia inaelezewa kwenye amri yake ya kwanza? Je, miungu ya kale si kitu chochote, au ni ya kilaghai/kitapeli? Kama Shetani alitaka kuwa kama Mungu, je, inawezekana kuwa malaika walioanguka ndio miungu ya uongo ya kale? (Angalia Ufunuo 14:11.) Kama miungu ya uongo sio kipande cha ubao/mti, bali kiumbe chenye busara, je, inajaribu kutufanya tusimwabudu Mungu kwa usahihi? Je, inajaribu kuiba/kuharibu ibada yetu? Kama ndivyo, hii inaelezea kwa nini Mungu wetu analipa suala hili kipaumbele. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu kuona kile inachotufundisha kuhusu ibada ya kweli na ya uongo!
I. Kijiti Kinachowaka Moto na Ibada
A. Soma Kutoka 3:1-3. Mungu anavuta nadhari ya Musa (usikivu wa Musa)! Kwa nini Mungu anamwingilia Musa kwa kutumia njia hii? (Alimtaka Musa afikiri kuwa hili ni jambo alilopaswa kulitafakari.)
B. Soma Kutoka 3:4. Je, nawe ungejibu kama Musa alivyojibu? (Kwa hakika Musa alishtushwa na sauti – kwa hakika alikuwa pale.)
C. Soma Kutoka 3:5-6. Hebu tuchunguze hili kwa muda kidogo kuona kile tunachoweza kujifunza kuhusu ibada. Kwa nini Mungu anamwambia Musa kuvua viatu vyake? (Mungu ni mtakatifu hivyo hiyo inafanya mahali panapomzunguka kuwa patakatifu.)
1. Kwa nini Musa alitakiwa kuwa mbali? (Tunaweza kupakaribia mahali patakatifu, lakini hatuwezi kumkaribia zaidi Mungu mkamilifu.)
2. Je, ujumbe wa jumla kuhusu ibada ni upi? (Mungu huja kimiujiza – kijiti kinachowaka moto. Anafanya sehemu za kawaida kuwa takatifu. Tunaweza tu kumsogelea, lakini hatupaswi kumkaribia zaidi.)
D. Soma Yohana 13:3-5. Je, unaelezeaje kutoka kwa Mungu ambaye unavua viatu vyako mbele zake, kwenda kwa Mungu ambaye anaosha miguu yako?
1. Je, asili ya Mungu imebadilika?
2. Je, asili ya ibada imebadilika?
3. Soma Waebrania 4:14-16 na Warumi 5:10. Je, mafungu haya yanapendekeza kitu gani?
a. Je, yanapunguza utukufu wa Mungu?
II. Ndama wa Dhahabu na Ibada
A. Soma Kutoka 32:1-4. Je, inawezekana kwetu sisi hivi leo kuwa wapumbavu kiasi hicho na wachukizaji kiasi hicho kwa Mungu?
1. Je, ni kitu gani kwenye haya mafungu kinatoa chukizo kubwa kabisa kwa Mungu? (Kwamba kazi zenye uwezo kubwa wa Mungu zinahusishwa na kitu kilichotengenezwa kwa mikono ya mwanadamu.)
a. Je, huwa unahusisha mafanikio yako na bidii yako ya kazi na maarifa yako badala ya uwezo wa Mungu?
B. Soma Kutoka 32:17-20. Je, hivi ndivyo tunavyoweza kuitambua ibada ya uongo – uimbaji, kucheza, na muziki wa sauti ya juu?
C. Soma Kutoka 15:20-21. Je, hivi ndivyo tunavyoweza kutambua ibada ya kweli – uimbaji, kucheza, na ngoma?
D. Soma 1 Mambo ya Nyakati 15:27-29. Je, hivi ndivyo ambavyo tunaweza kutambua ibada ya kweli kwa wale walio na moyo wa Mungu (1 Samweli 13:14) – kupiga kelele, muziki wa sauti ya juu, vyombo vya muziki vya kugonganishwa, vyombo vya muziki vilivyotengenezwa kwa uzi/ugwe, na kucheza? (2 Samweli 6:14 inaongezea taarifa zaidi kwamba huu haukuwa mchezo uliozuiliwa au wa kimapokeo. Daudi “alicheza mbele za Mungu kwa uwezo wake wote.” Hii ni ibada ya Mfalme Daudi.)
E. Tunahitajika kuchukulia kwa umakini hitimisho la ibada ya Mfalme Daudi yenye kucheza kwa uchangamfu sana. Soma 2 Samweli 6:20-22. Nini asili ya mjadala kuhusu ibada ya Daudi kwa Mungu?
1. Nini nafasi ya Mikali, mke wa Daudi wa kifalme? (Analalamika kuwa Daudi “anakosa adabu,” hana haya/ni hayawani na hana heshima. Anatenda kama mtumishi wa kawaida. Baini kuwa hii ni kabla ya sanduku la agano, alama ya uwepo wa Mungu.)
2. Nafasi ya Mungu ni ipi? (Kwamba ibada isiyo na heshima na kumsherehekea Mungu ni sahihi. Mungu alimchagua Daudi na atamfurahia/anamsherehekea Mungu wake hata kama inaonekana kutokuwa na heshima na udhalilishaji/ufedheheshaji.)
3. Sasa, rafiki, je, hii inaonekana kama mjadala wa sasa dhidi ya ibada? Je, umesikia kwamba “kucheza, muziki wa sauti ya juu, kuimba, kupiga kelele na mkanganyiko wa ujumla” ni alama ya ibada ya sanamu?
F. Hebu tusome jibu la Mungu kuhusu suala hili. Soma 2 Samweli 6:23. (Mikali alikuwa tasa baada ya kumshambulia Daudi kwa ibada isiyokuwa na heshima.)
1. Je, umewahi kuwa kwenye nyumba ya ibada “tasa?”
2. Je, umewahi kuwa kwenye huduma ya ibada iliyo kavu kama vumbi? Kila mtu ana nywele za rangi ya kijivu, nyeusi au nyeupe (kama mimi!), na hakuna mtu anayeonekana kusherehekea, kusherehekea kwa dhati, kile Mungu alichowafanyia?
3. Je, laana ya Mikali imo ndani ya nyumba yako ya ibada?
G. Watu wana maoni makali sana kuhusiana na hii mada. Maoni yetu yanatakiwa kujengwa kwenye msingi wa Biblia – hususan pale ambapo yako wazi sana. Hata hivyo, kuna mantiki ya kawaida katika hili. Angalia watoto wako. Je, wote wanaweza kukupenda na kukuheshimu?
1. Je, unataka wakusalimuje? Kwa vichwa vyao vikiwa vimeinamishwa na midomo yao imefumbwa? Au, matabasamu ya furaha na kicheko, na furaha ya dhahiri?
H. Shetani ameona, na kabla hajaasi, hata alikuwa sehemu ya ibada ya utukufu zaidi kwa Mungu. Kama Shetani anataka kuwa kama Mungu, kama anataka kuabudiwa, je, ni aina gani ya ibada Shetani ataihamasisha/ataitia moyo? (Itakuwa na mantiki kwamba kama Shetani anataka kuabudiwa kama Mungu, atataka kuhamasisha aina ya ibada anayopewa Mungu. Isipokuwa kama baadhi ya vipengele vya ibada ya kipagani vinakiuka kwa wazi sheria ya Mungu, hii inapendekeza kuwa kile kilichotokea kwa ndama wa dhahabu wa Haruni badala yake kinaweza kuonekana kama ibada ya kweli (ingawa ni sawa na lengo baya la ibada).)
III. Miungu wa Kisasa na Ibada
A. Soma Kutoka 20:4-6. Je, unamfahamu mtu mmoja aliye na sanamu sehemu ya nyuma ya nyumba yake na ayayoiabudu? (Kamwe sijawahi kuona hilo, hata mara moja, maishani mwangu mwote hapa Marekani.)
1. Je, mojawapo ya kishawishi cha Shetani chenye mafanikio makubwa sana kimezeeka? Je, ulikuwa tu ni mtindo unaopita?
2. Je, nini ishara ya ibada ya sanamu? (Sanamu ni kitu kinachotengenezwa na wanadamu. “Tunakisujudia” na kukiabudu.)
a. Je, inamaanisha nini kuiabudu sanamu? (Tunaipatia fedha zetu, muda wetu, heshima yetu na tunapokea ushauri wake.)
3. Nilipokuwa ninasoma “Miungu ya Kimarekani,” (kitabu nisichokipendekeza) mojawapo ya mungu wa kisasa alikuwa ni televisheni. Televisheni, kuonyesha umuhimu wake, alisema (hii inanukuliwa kutokana na kumbukumbu baada ya kukisoma kitabu hicho) “Familia zinakusanyika kunizunguka, zinatoa muda wao, zinanipa usikivu wao, na zinatii maneno yangu.” Wow! Hiyo ilishika nadhari/usikivu wangu. Je, ibada yetu ya sanamu imejongea kutoka nyuma ya nyumba hadi sebuleni?
IV. Ibada ya Ufunuo
A. Soma Ufunuo 5:13-14 na Ufunuo 19:1-7. Je, ni matamanio yako makubwa kuungana na haya maneno ya sifa na kumwabudu/kumsujudia Mungu?
B. Rafiki, kama unataka kuwa sehemu ya hili kundi, kwa nini usimsifu Mungu kwa mkazo huo hivi sasa? Kwa nini usipige kelele na kupaza (Ufunuo 19:1) sifa zako kwa Mungu? Kwa nini usimsifu kama unavyomaanisha, na sio kama unajiandaa kulala kidogo siku ya Sabato mchana?
V. Juma Lijalo: Sabato na Ibada.