Sabato na Ibada
Utangulizi: Fikiria talaka ya kutisha inayowahusisha watoto. Mama anamchukia baba, akijihisi kuwa yupo kwenye ushindani naye, na akitaka kufuta kumbukumbu yake kutoka mawazoni mwa watoto. Mambo gani mabaya sana mama anaweza kuyafanya ili aweze kumuumiza/kumsononesha/kumtia uchungu baba? Kitu cha kwanza kinaweza kuwa kujaribu kumzuia baba ili asiweze kuwaona wanawe. Pili, anaweza kuwaambia watoto kwamba baba hakuwapenda au hata hakuwajali. Tatu, anaweza kuwaambia kuwa yeye sio baba wao. Malengo ya baba ni kinyume chake tu: kusisitiza ukweli kwamba yeye ndio baba yao, kwamba anawapenda na kuwajali watoto wake, na kwamba anataka kuwa anawaona wanawe mara kwa mara. Sasa chukulia pambano kati ya Mungu na Shetani. Je, haileti mantiki kwamba Shetani atakuwa na malengo sawa na ya huyu mama? Shetani anatutaka tuamini kwamba Mungu hatupendi au hatujali, Mungu sio baba wetu, na hatupaswi kujali sana kuhusu kukutana na Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kujifunza zaidi kuhusu masuala mahsusi!
- Uumbaji wa Sabato
- Soma Mwanzo 1:26-27. Je, hii inatufundisha nini kuhusu uhusiano wetu na Mungu? (Kwa kiwango fulani, tumeumbwa kufanana na Mungu.)
- Je, uhusiano wetu na uumbaji wote uliosalia ni upi? (Tumeumbwa ili kuutawala uumbaji wote uliosalia.)
- Je, unadhani ni kwa nini Mungu aliamua kwamba wanadamu wautawale uumbaji wote uliosalia? (Hii inasisitiza wazo la kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Kutokana na huu mfumo wa mahusiano, tunaanza kuona sehemu ya jinsi gani tunafanana na Baba wetu wa Mbinguni.)
- Soma Mwanzo 1:26-27. Je, hii inatufundisha nini kuhusu uhusiano wetu na Mungu? (Kwa kiwango fulani, tumeumbwa kufanana na Mungu.)
- Soma Mwanzo 2:1-3. Je, sababu ya Mungu ya kuiumba Sabato ni ipi? (Alimaliza uumbaji wake. Kazi ya Mungu yenye uwezo mkubwa ilikamilika.)
- Je, Mungu alitamka nini kuhusu Sabato? (Ilibarikiwa na ilikuwa takatifu.)
- Je, inamaanisha nini kuifanya siku kuwa “takatifu?” (Mungu aliitakasa siku.)
- Hebu tuyaweke haya pamoja. Je, kuna uhusiano gani kati ya uumbaji wa Mungu wa wanadamu na Sabato? (Jumamosi ni siku maalum, siku takatifu, siku ambayo tunakumbushwa kwamba Mungu ni Muumba wetu.)
- Soma Kutoka 20:8-11. Mungu anaposema “Ikumbuke siku ya Sabato,” je, anarejelea kitu gani? (Hii ni rejea ya dhahiri ya kisa cha uumbaji katika kitabu cha Mwanzo.)
- Kwa nini Mungu anatuambia tufanye kazi kwa siku sita? (Kwa mara nyingine tena hii ni rejea yenye ufahamu fika wa siku sita za uumbaji wa Mungu.)
- Kwa nini tunaambiwa tusiwafanyishe kazi wanyama wetu siku ya Sabato? (Sio tu kwamba Mungu anatuambia vitu vyote vinastahili pumziko la Sabato, bali anasisitiza wazo kwamba tunatakiwa kuutawala uumbaji.
- Kiungo cha Sabato na Ibada
- Soma Mwanzo 1:1. Je, Mungu anajitambulishaje kwetu? (Anajitambulisha kama Muumba.)
- Unadhani ni kwa nini hili ni jambo la kwanza kabisa Mungu anatuambia kutoka kwenye Biblia yake?
- Soma Mwanzo 1:1. Je, Mungu anajitambulishaje kwetu? (Anajitambulisha kama Muumba.)
- Soma Ufunuo 14:7. Je, msingi wa Mungu wa kudai ibada yetu ni upi? (Kwamba yeye ni Muumba wetu.)
- Kwenye Biblia ya Nave, mafungu 104 ya Biblia (chini ya “Muumba” yakianzia kwenye kitabu cha Mwanzo hadi cha Ufunuo ambapo Mungu ama moja kwa moja, au kupitia kwa wanadamu, anayapatia madai yake umuhimu kuhusu mamlaka yake kwetu kwenye ukweli wa Uumbaji wake. Je, unahitimisha nini kuhusu fikra ya Mungu kutokana na hili? (Tunajifunza kuwa madai ya mamlaka ya Mungu yenye unyofu, mepesi na ya msingi dhidi ya wanadamu ni kazi yake ya uumbaji. Mungu anawaambia wanadamu: “Nimewaumba, kwa hiyo mnapaswa kunitii.”)
- Kumbuka utangulizi wetu kuhusu mwanamke aliyetalikiwa aliyetaka kufuta kumbukumbu ya watoto kumhusu baba yao? Kwa nini ni muhimu kwa Shetani kuishambulia ibada ya Sabato? (Inatimiza malengo mawili yenye mantiki ya Shetani ambapo hata sisi tuliweza kuyabaini. Kwanza, kwa vile Sabato ni kumbukumbu ya kila juma ya siku sita za Uumbaji wa Mungu, inaondoa hii kumbukumbu ya kila juma kwamba Mungu alituumba na kwa hiyo ana mamlaka juu yetu. Pili, kwa kuwa Sabato ni muda wa muhimu wa kujifunza, kumsifu na kumwabudu Mungu, kutokuijali/kiupuuza Sabato kunapunguza muda wetu wa kukutana na Baba wetu wa Mbinguni.)
- Je, Shetani anafanya nini katika kufanya wanadamu wasahau kwamba Mungu ni Muumba wao? (Watu wengi sana hawaamini tena kwamba uumbaji wa siku sita unahusika kiusahihi kabisa kuhusu chanzo cha wanadamu. Wengi wanaamini kuwa wanadamu walitokea kwa bahati tu na kutokana na uasilia wa mambo. Wengi wanaamini kuwa wanadamu hawana madai ya ubora zaidi dhidi ya wanyama, na kwamba hatuna mamlaka ya kuwatawala. Wakristo wengi, hata wale wenye kumcha Mungu sana, hawaijali Sabato ya siku ya saba.)
- Umuhimu wa Sabato
- Wengi wanasema, “Ili iweje? Kile ulichokisema hivi punde kuhusu umuhimu wa Sabato sio kizuri vya kutosha. Naweza kumwamini Mungu hata kama siamini kisa cha uumbaji au utunzaji wa Sabato.” Kama unadhani kuamini maelezo ya kitabu cha Mwanzo kuhusu Uumbaji na Sabato kunaleta tofauti, elezea kwa nini? (Kwanza, kama maelezo sio ya kweli, inamaanisha kuwa Mungu hakutuambia ukweli kuhusu chanzo cha wanadamu. Kama hivyo ndivyo, basi Mungu hasemi ukweli kuhusu mamlaka yake juu yetu. Mwisho, kama Mungu hasemi ukweli kuhusu chanzo chetu (kwa sababu anatia chumvi uwezo wake), hiyo inapendekeza kuwa Mungu wetu anapungukiwa uwezo.)
- Je, tuna uhakika hili linaibua swali kuhusu utovu wa uaminifu wa Mungu? Je, Mungu anaweza tu kuwa anaelezea kisa chenye ishara, akitupatia aina fulani ya fumbo kubwa muhimu? (Tunaposoma Ufunuo, tunajua tunasoma kuhusu ishara. Kitambu cha Mwanzo kipo mahsusi zaidi kuhusu masuala yenye kinagaubaga. Haileti mantiki kukichukulia kuwa kisa chenye ishara – hususan kisa kuhusu mageuko/mabadiliko!)
- Soma Wakolosai 1:15-18. Je, Mtume Paulo aliamini katika Uumbaji? (Ndiyo.)
- Je, Paulo anamrejelea nani katika hili fungu? (Yesu.)
- Je, tumaini lako la muhimu sana kama Mkristo ni lipi? (Mbingu. Unatumaini kuwa Yesu atakuchukua wewe na wale unaowapenda Mbinguni.)
- Je, ni kiungo gani kinachofanywa na haya mafungu kati ya Uumbaji na tumaini letu la mbingu? (Yesu ana “mamlaka ya juu kabisa” dhidi ya Uumbaji na mauti. Kama Yesu hana uwezo wa kutosha wa kuumba nchi (dunia) na vilivyomo, kwa nini tuamini kuwa ana uwezo wa kutosha kukishinda kifo? Paulo anaonyesha kwamba hizi imani zinaungana.)
- Hebu tuchukulie pale tulipo sasa. Sabato inaunganishwa na Uumbaji, mamlaka ya Mungu, na uwezo wa Mungu wa kutufufua kwa ajili ya uzima wa milele!
- Uhuru Kutoka Utumwani
- Soma Kumbukumbu la Torati 5:15. Kwa nini Biblia inatoa sababu mbili tofauti kwa ajili ya Sabato?
- Soma Warumi 6:15-18. Nini kilichotuweka huru kutoka kwenye utumwa wa dhambi? (Yesu ametuweka huru kutoka kwenye utumwa wa dhambi kupitia kwenye maisha yake na kifo chake kwa ajili yetu. Tunamheshimu Mungu kwa sababu ya kile alichotutendea.)
- Je, unaweza kuona kiungo kati ya kumbukumbu ya Uumbaji na kumbukumbu ya wokovu wetu? (Mungu alitupatia uzima, na kisha akatupatia uzima wa milele.)
- Je, hii ina chochote cha kujihusisha na uwezo na mamlaka ya Mungu?
- Sabato na Ufufuo wa Yesu
- Soma Mathayo 28:1 na Mathayo 27:50-53. Yesu alipumzika kaburini siku ya Sabato, lakini hawa wengine kwa hakika walifufuliwa siku ya Ijumaa. Kama wewe ungekuwa Mungu Baba, na Mwanao ameuawa kinyama ilhali akishinda Super Bowl ya dunia, je, ungetaka kumweka mikononi mwako mara moja? (Hakika! Hakuna mzazi hata mmoja ambaye atataka kusubiri japo kwa sekunde moja kumfariji na kumpongeza mwanae.)
- Kwa nini Mungu alisubiri hadi kufikia hatua ya kumfufua Yesu uzimani? (Chukulia mjadala wetu hadi hivi sasa. Sabato ndio msingi wa kile ambacho Yesu alikifanya na anakifanya kwa ajili yetu. Hitimisho la kimantiki ni kwamba Yesu alipumzika siku ya Sabato! Kama jinsi Yesu alivyopumzika baada ya kazi yake kubwa ya Uumbaji, kwa hiyo alipumzika baada ya kazi yake kubwa ya ukombozi. Ni maelezo pekee ya kimantiki ya ucheleweshaji.
- Soma Mathayo 28:1 na Mathayo 27:50-53. Yesu alipumzika kaburini siku ya Sabato, lakini hawa wengine kwa hakika walifufuliwa siku ya Ijumaa. Kama wewe ungekuwa Mungu Baba, na Mwanao ameuawa kinyama ilhali akishinda Super Bowl ya dunia, je, ungetaka kumweka mikononi mwako mara moja? (Hakika! Hakuna mzazi hata mmoja ambaye atataka kusubiri japo kwa sekunde moja kumfariji na kumpongeza mwanae.)
- Rafiki, kama unaamini kuna pambano linaloendelea dhidi ya uwezo na mamlaka ya Mungu, kwa nini usiamue hivi leo kuonyesha utii wako kwa Mungu kwa kukubali maelezo yake ya Uumbaji na kukumbuka na kunukuu mamlaka yake kwa kuitunza Sabato?
- Juma Lijalo: Kufurahi Mbele za Bwana: Patakatifu na Ibada.