Ghadhabu ya Elihu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ayubu 32 & 34)
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
4
Lesson Number: 
10

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Unadhani “hasira njema” ni ipi? Nadhani hii ni hasira ya dharau na kupuuzia hadhi na taratibu za Mungu. Hasira ya mara kwa mara huwa inaibuka kutokana na dharau dhidi yangu. Kwa mujibu wa uelewa wangu, hasira njema si mbaya na hasira ya mara kwa mara si nzuri. Je, unakubaliana na jambo hili? Waefeso 4:26 inasema, “Muwe na hasira, ila msitende dhambi.” Hiyo inaonekana kuashiria kwamba baadhi ya hasira si mbaya. Tumeona kwamba marafiki wa Ayubu wanajihusisha katika kile wanachoamini kwa uhakika kwamba kilikuwa ni hasira njema kwa sababu walidhani kuwa Ayubu alikuwa anamdharau Mungu pamoja na kubeza taratibu za Mungu. Juma hili tunaangalia hasira ya Elihu, mmojawapo wa marafiki wa Ayubu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza endapo hasira ya Elihu ni sahihi!

 

1)      Elihu ni Nani?

 

a)      Soma Ayubu 32:1. Kwa nini “marafiki” waliacha kuhoji kwa kuwa tu Ayubu alidhani kuwa yu sahihi? Je, unaacha kuhoji au kujibu kwa kuwa tu mtu unayebishana naye anadhani kuwa yu sahihi? (Kwa dhahiri walidhani kuwa haikuwa na maana yoyote kuendelea kubishana kutokana na mtazamo wa Ayubu.)

 

i)       Je, hili ni fundisho linaloweza kuboresha maisha – kwamba usibishane na watu ambao wana uhakika kuwa wako sahihi?

 

b)      Soma Ayubu 32:2. Je, utaiita hii kuwa ni “hasira njema?”

 

i)       Nimetoa ushauri kuwa hasira njema haina tatizo, je, una maoni gani?

 

ii)     Unakubaliana na mtazamo wa Elihu juu ya hoja za Ayubu? (Ayubu alikuwa anajihesabia haki na kuitia changamoto haki ya Mungu.)

 

iii)   Unadhani Elihu alirithi mtazamo wa hasira kutoka kwa baba yake? Ungejisikiaje endapo jina lako lingekuwa “Barakeli, Mbuzi?” (Ikiwa unashangaa, basi huu ni utani.)

 

c)      Soma Ayubu 32:3. Je, Ayubu amemkasirikia Ayubu peke yake? (Hapana! Pia amewakasirikia marafiki wengine watatu.)

 

i)       Utagundua kwamba Eluhu amekasirika kwa sababu marafiki “hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa.” Je, Elihu alikasirika kwa kuwa walimhukumu Ayubu, au kwa kuwa hawakupata sababu ya kumkanusha?

 

ii)     Kwa nini hawakuweza kumkanusha Ayubu? (Kwa sababu Ayubu alikuwa anasema ukweli.)

 

d)      Soma Ayubu 32:4-5. Tunajifunza nini kumhusu Elihu ambacho ni cha muhimu katika kufanya uamuzi kama kweli alipaswa kukasirika? (Elihu ni mdogo (kijana). Ikiwa mtu anaona kuwa baadhi ya hoja hazina maana, yumkini somo hilo linatokana na umri na uzoefu.)

 

 

2)      Mashtaka ya Haki ya Elihu

 

a)      Soma Ayubu 32:6. Kuna dhana gani hapa? (Kwamba Elihu ni mjuzi zaidi ya Ayubu. Uwezekano mkubwa ni kwamba hii si kweli, na bila shaka dhana hiyo inamkera Ayubu.)

 

b)      Soma Ayubu 32:7. Je, unakubaliana na kauli hii? Je wanadamu wanakuwa na busara zaidi wanapokuwa watu wazima (wazee)?

 

i)       Unadhani kweli kwamba Elihu anaamini katika dhana hii? (Nina mshaka kwa sababu anadhani kuwa ana ufahamu zaidi ya Ayubu na marafiki wazee.)

 

c)      Soma Ayubu 32:8-9 na Ayubu 32:18-19. Elihu anadhani kuwa ana nafuu gani licha ya umri wake mdogo? (Kwamba Roho Mtakatifu anayaongoza mawazo yake.)

 

i)       Je, unakubaliana kwamba kijana mdogo aliyejawa Roho Mtakatifu ana busara zaidi kuliko mzee? (Kwa uzoefu wangu, vijana wapumbavu huwa wana kawaida ya kuwa wapumbavu katika utu uzima wao. Hivyo, nakubaliana na Elihu kwamba si lazima umri uendane na busara. Kimsingi, ikiwa unayo fursa ya kupata hekima ya Mungu, basi hakuna hekima ya mwanadamu iliyo bora zaidi bila kujali umri.)

 

d)      Soma Ayubu 32:10. Kuna hatari gani kwenye madai ya Elihu kwamba anaongozwa na Roho Mtakatifu? (Anaweza asiwe sahihi. Anaweza kuwa anajidanganya.)

 

i)       Nakumbuka mzee mmoja wa kanisa mahalia aliyekuwa mhubiri mbaya sana. Sababu moja ya kuwa mbaya katika kuhubiri ni kwamba kwa dhahiri alikuwa hajiandai. Mara kwa mara, tulipokuwa tunakaribia kwenda mimbarani ili akahubiri, alikuwa ananiambia kuwa Roho Mtakatifu amemwambia abadilishe mada ya hubiri lake usiku wa kuamkia siku ya kuhubiri – na alitumia muda wote wa usiku kuandaa hubiri jipya. Unauchukuliaje ujumbe huo utokao kwa Roho Mtakatifu? (Baada ya jambo hili kutokea mara kadhaa, nilimwambia kuwa Roho Mtakatifu alifahamu kabla kile anachopaswa kukihubiri, na kulikuwa na uwezekano mdogo kwa Roho Mtakatifu kubadili mawazo yake usiku mmoja kabla ya hubiri.)

 

e)      Soma Ayubu 32:11-12. Elihu anajenga hoja kwamba sasa ni zamu yake kuzungumza. Kwa nini? (Alisubiri, wakubwa wake walishindwa, na sasa atafanya vizuri zaidi ya wakubwa wake.)

 

f)       Soma Ayubu 32:13. Je, unakubaliana na Elihu? Je, kuna ubaya wowote kumwacha Mungu amkane Ayubu, tukichukulia kwamba hicho ndicho kilichomo mawazoni mwa Mungu?

 

g)      Soma Ayubu 32:14. Tutarajie hoja za namna gani kutoka kwa Elihu? (Anasema kuwa atajenga hoja mpya. Ataona.)

 

h)      Ayubu 33 inaanza na hoja ya Elihu. Hebu tuendelee na hoja hiyo katika sura inayofuata. Soma Ayubu 34:5-6. Je, kauli hii ni sahihi juu ya nafasi ya Ayubu? (Ndiyo.)

 

i)       Soma Ayubu 34:7-9. Je, hizi ndizo hoja mpya alizoziahidi Elihu? (Ndiyo na hapana. Marafiki watu wazima (wazee) pia walisema kuwa Ayubu anastahili yale yanayomtokea. Nukuu ya Eliya kwamba Ayubu anauumbua (anamshusha hadhi) usawa wa Mungu kutenda haki ni mada iliyopitwa na wakati. Tofauti ni kwamba Elihu anataja dhambi mahsusi: kujihusisha na watu waovu.)

 

 

i)       Je, kuna ushahidi wowote wa hii dhambi mahsusi?

 

j)       Soma Ayubu 34:12-15. Je, unakubaliana na Elihu? Au, je, unakubaliana na Ayubu aliyesema kwamba Mungu anachekelea hila za waovu (Ayubu 10:3)? (Kwa dhahiri Elihu yuko sahihi.)

 

k)      Soma Ayubu 34:17-19. Utakumbuka juma lililopita Ayubu alikuwa na mashtaka kwamba marafiki watu wazima walimpendelea (walimtetea) Mungu (Ayubu 13:8). Elihu anasema kuwa Mungu ni hakimu mwadilifu atendaye haki. Je, Elihu pia anampendelea (anamtetea) Mungu? (Naam, hakika.)

 

i)       Je, kuna lolote tunaloweza kujifunza kwenye tuhuma za Ayubu kwamba marafiki hawa wanampendelea Mungu na si yeye? (Tunafahamu, kwa hakika, kwamba Elihu anazungumza ukweli wa jumla, hauhusiani na hali mahsusi ya Ayubu. Yumkini endapo marafiki wangeangalia namna ya kuwatetea wote wawili, yaani Mungu na Ayubu, wangeweza kufikia uamuzi unaokaribiana zaidi na uhalisia wa kilichokuwa kinamtokea Ayubu.)

 

l)       Soma Ayubu 34:35-37. Je, hapa Elihu anaibua hoja mpya? (Kwa hakika hiki ndicho ambacho marafiki wazee (wakubwa) wamekuwa wakikisema. Lazima Ayubu atakuwa alitenda dhambi kwa sababu anateseka. Ayubu anapokana kwamba dhambi yake imesababisha mateso yake, na anatia changamoto utendaji haki wa Mungu, basi marafiki wanajenga hoja kwamba Ayubu hamheshimu Mungu.)

 

i)       Kwa nini Elihu anasema kuwa ana hoja mpya, wakati anaona kuwa ama anarudia hoja za zamani au anatoa mashtaka ya uongo? (Elihu anadhani kuwa ana hasira njema, lakini uwezekano mkubwa ni kwamba Elihu anaonekana kujawa na majivuno yake mwenyewe.

 

m)   Elihu anaendeleza mashtaka yake kwenye sura tatu zaidi. Katika sura ya mwisho, Ayubu 37, Elihu anarekebisha hoja yake. Hebu tuiangalie. Soma 37:14-18. Je, umesikia hoja kama hizi hapo kabla? (Hii inaonekana kufanana sana na kile Mungu anachomwambia Ayubu kuanzia kwenye Ayubu 38. Kutokana na mada hii kwamba Mungu ni Mungu na Ayubu si Mungu, Elihu anasisitiza jambo ambalo marafiki wazee hawakulisisitiza.)

 

3)      Tafakari

 

a)      Soma Ayubu 1:6-12. Je, Ayubu anasema ukweli anaposema kuwa hastahili mambo yanayomtokea? (Naam, kwa maana ya kwamba kutenda makosa husababisha mateso. Hata hivyo, katika muktadha huu, kutenda mambo mema kulileta mateso.)

 

i)       Je, marafiki wanasema ukweli kwamba kutenda mambo mabaya huleta mateso? (Naam, ikiwa Kumbukumbu la Torati 28 inasema ukweli.)

 

ii)     Kwa hiyo, mambo yanawezaje kupinduliwa (kugeuzwa) vibaya kiasi hicho wakati kila mtu anasema ukweli? (Soma 1 Wakorintho 13:12. Hakuna mwanadamu hata mmoja aliyeona taswira yote.)

 

b)      Soma tena Ayubu 1:12. Je, uamuzi huu ni wa kujikinga? Je, ulimfanya Shetani akiri baadaye kwamba, “Nimekosea, ninaachana na uovu?”

 

i)       Je, kibali cha Mungu kumdhuru Shetani kilisababisha badiliko lolote chanya?

 

 

c)      Soma Isaya 45:9-11 na Warumi 9:21. Mafungu haya yanatufundisha jambo gani la muhimu? (Tunafahamu kwamba Mungu ana upendo wa hali ya juu sana kwetu kwa sababu alikufa kwa ajili yetu. Lakini, linapokuja suala la kuuendesha ulimwengu, tunatakiwa kumwachia Mungu. Kama ulivyokwishasoma kwenye masomo haya hapo kabla, maisha yetu hayatuhusu, yanamhusu Mungu na pambano linaloendelea ulimwenguni kote kati ya wema na uovu. Ingawa mateso ya Ayubu yanaweza kuonekana kukinzana na kanuni za Mungu, tunafahamu kwamba yalikuwa ya muhimu katika pambano kati ya wema na uovu. Tunafahamu ilikuwa muhimu kwa sababu ya faraja ambayo mfano wa Ayubu unatupatia tunapoteseka.)

 

d)      Rafiki, je, utakubali kumwachia Mungu auendeshe ulimwengu? Je, utaamua tu kumtumaini Mungu atende jambo sahihi?

 

4)      Juma lijalo: Kutoka Katika Upepo wa Kisulisuli.