Roho Mtakatifu na Kuishi Maisha Matakatifu
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mojawapo ya mibaraka mikubwa katika safari yangu ya kiroho ni pale nilipotambua kwamba nimeokolewa kwa neema pekee. Nimewaona watu wanaohangaika na utii wakidhihirisha furaha kuu pale walipoielewa neema kwa mara ya kwanza. Wanajisikia huru! Hatari kubwa ni kutoelewa sababu ya utii. Mungu hatupatii wito wa kuwa watii kama sehemu ya jaribu. Hakususii utii uwe mzigo. Badala yake, utii hutuletea mibaraka maishani mwetu na kumpatia Mungu utukufu. Mungu anawatafuta wafuasi wanaotaka kumtii, wale ambao mioyo yao inatamani mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani na mbinguni. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!
- Sababu ya Kuishi
-
- Katika Kumbukumbu la Torati 28 Mungu anatoa kanuni rahisi ya maisha. Mtii Mungu ili ubarikiwe. Usimtii Mungu nawe utalaaniwa. Soma Kumbukumbu la Torati 30:1-3. Kifungu hiki kinachukulia dhana gani? (Kwamba watu wa Mungu wamepata mateso kwa sababu ya kutokutii, lakini Mungu atawapatia maisha mazuri katika siku zijazo ikiwa watakuwa watiifu.)
-
- Soma tena Kumbukumbu la Torati 30:2. Mungu anatamani utii wa namna gani? (Utii kwa “moyo wako wote na kwa roho yako yote.”)
-
-
- Unadhani inamaanisha nini kutii kwa “moyo wako wote na kwa roho yako yote?”
-
-
-
-
- Ikiwa utii unakukera, endapo utii ni mzigo kwako, je, hicho ndicho anachokitamani Mungu? (Hapan)
-
-
-
-
-
- Ikiwa utii unakera, tunapaswa kufanya nini, kuacha kujaribu kuwa watiifu?
-
-
-
- Je, umewahi kufanya kazi kwa bidii ili kupata jambo fulani? Ikiwa ndivyo, kwa nini? (Ujira ulistahili kazi hiyo. Nakumbuka siku moja nilikuwa nimekaa kwenye maktaba ya sheria na kuangalia nyasi za kijani na mwanga wa jua nje kupitia dirishani. Ingekuwa heri kama ningekuwa nimekaa nje nikifurahia mwanga wa jua! Lakini, nilijua kuwa endapo nitaendelea kutia bidii, badala ya kucheza, nitakuwa mwanasheria katika kipindi chote cha maisha yangu.)
-
-
- Je, huo ni mfano wa utii unaokubalika? Inawezekana isiwe rahisi, lakini unataka kufanya hivyo kwa sababu ya thawabu kuu utakayopata?
-
- Sababu (Nia) ya Upendo
-
- Soma 1 Petro 1:3-5. Tumaini la Mkristo ni lipi? (“Urithi usioharibika, usio na uchafu wala usionyauka.” Hii ni motisha ile ile ambayo tumeijadili hivi punde – maisha yenye baraka.)
-
- Soma 1 Petro 1:6-7. Hii ni habari mbaya kuhusu maisha yenye baraka. Vifungu hivi vinatuambia kuwa mambo gani yanaweza kututokea wakati tukimfuata Yesu? (Mateso kwa njia ya majaribu.)
-
-
- Sababu ya mateso haya ni ipi? (Tunapewa sababu mbili. Kwanza, kwamba kuwa waaminifu kwa njia ya mateso inaonesha kuwa tunanuwia kwa dhati kumfuata Yesu. Pili, matokeo ya mateso ni “kumsifu Mungu, kumpa utukufu na kuwa watii” tunapomtafakari Yesu.)
-
-
-
- Hivi karibuni tulijifunza kitabu cha Ayubu. Mada moja kubwa ya kitabu cha Ayubu ilikuwa ni kwamba kanuni za kawaida kuhusu utii na mibaraka hazitimii mara zote. Kwa nini? (Kwa sababu uovu upo katika hii dunia. Shetani anataka kutudhuru.)
-
-
- Soma 1 Petro 1:8-9. Jambo gani linatuhamasisha kuwa watiifu? (Upendo kwa Mungu na lengo letu la imani.)
-
-
- Kwa nini tunahamasishwa na upendo? (Tunarejea kwenye fungu la kwanza tulililosima katika kitabu cha Petro: Yesu anatupatia uzao mpya kwa njia ya kifo na ufufuo wake. Kile ambacho Yesu ametufanyia kinatufanya tumpende. Alituokoa kutoka mautini na kwenye hukumu ya haki kwa dhambi zetu.)
-
-
- Fikiria kile ambacho tumekijadili hivi punde. Sababu mojawapo ya utii ambayo Mungu ametupatia ni kufurahia maisha ya baraka. Sababu ya pili, na ya asili ya utii ni kwamba Yesu alitupenda na alikufa ili kuyafanya maisha yajayo yawezekane kwetu. Ukiunganisha hizi sababu mbili, je, zinaendana na wito wa kumtii Mungu kwa moyo wetu wote na kwa roho yetu yote?
- Wajibu wa Roho Mtakatifu
-
- Soma 1 Timotheo 1:8. Je, hii inamaanisha kwamba kuna matumizi yasiyo sahihi ya sheria?
-
- Soma 1 Timotheo 1:9-11. Hebu tunyambulishe vifungu hivi. Paulo anasema kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki. Je, kutumia sheria kwa watu wenye haki itakuwa ni matumizi ya sheria yasiyo sahihi?
-
-
- Sheria imetungwa kwa ajili ya nani? Inatumika kwa nani kwa usahihi? (“Wavunjaji wa sheria na waasi, makafiri na wenye dhambi, wanajisi na wasiomcha Mungu….”)
-
-
-
- Mara kwa mara watu wanataka kubishana juu ya kile kinachomaanishwa kwa “sheria.” Sheria gani inarejewa hapa? (Kwa kiwango cha chini kabisa, sheria hiyo inarejea Amri Kumi kwa sababu kwa mahsusi kabisa inarejea mambo yaliyoagizwa yasitendwe katika Amri Kumi.)
-
-
- Tuchukulie kwamba angalao katika hatua za awali unakubaliana na mimi hadi hapa tulipofikia. Ikiwa wewe ni mtu ambaye una motisha kubwa ya kuwa mtiifu kwa sababu unampenda Yesu na unataka kuishi maisha ya furaha, je, ni jambo gani hasa unalolitii? Ikiwa wewe ni mwenye haki, basi kuitumia sheria kwako haitakuwa jambo sahihi ya sheria hiyo, je, ni sawa?
-
- Soma Wagalatia 5:13-14. Kifungu hiki kinasema kuwa Wakristo wanapaswa kutii nini na hawapaswi kutii nini? (Hatupaswi “kujiingiza kwenye mambo ya dhambi.” Kwa upande mwingine, tunapaswa “kutumikiana kwa upendo.”)
-
- Soma Wagalatia 5:16-17. Ikiwa unatamani kumtii Mungu kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, je, unatakiwa kufanya nini? Hii inahusianaje na Roho Mtakatifu? (Kuna vivutio viwili katika maisha ya Mkristo. Kivutio cha kwanza ni kuishi kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu. Kivutio cha pili ni kuishi kwa mujibu wa tamaa ya asili yetu ya dhambi.)
-
-
- Unafahamu kile ninachokizungumzia? Je, umepitia uzoefu wa huu ukinzani?
-
-
- Soma Wagalatia 5:18. Hii inaendana na kile tulichokisoma muda mfupi uliopita katika 1 Timotheo 1:9 kwamba sheria haikutungwa kwa ajili ya wenye haki. Ni kwa jinsi gani wenye haki, wale wanaoongozwa na Roho Mtakatifu, hawafungwi na sheria?
-
- Chukulia kwamba ulikuwa na wazazi wazuri, lakini hawakuwa nawe mara zote ulipokuwa katika umri wa kubalehe (teenager). Jambo gani lingekuwa jema zaidi: kutokuwepo kwa wazazi na uwepo wa orodha ya sheria zao; au wazazi wako kuwa pamoja nawe na kuweza kukupatia mwongozo maishani mwako?
-
-
- Je, “wazazi wako kuishi nawe na kukupatia ushauri” ndicho kinachomaanishwa kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu?
-
-
- Watu wenye dhamira njema watasema “Mungu ametupatia wito wa kuishika sheria yake.” Nadhani hili ni jambo gumu, lakini kutokuelewa mapenzi ya Mungu kulikopitiliza. Kwa nini? Kwa sababu lengo ni dogo sana, na kiwango ni cha chini sana. Jiulize, kwa nini Yesu alisema katika Mathayo 5:21-22 na Mathayo 5:27-28 kwamba Amri Kumi zinakataza mauaji na uzinzi, lakini mchakato wa fikra ni wa muhimu na wa kutisha? Hasira na tamaa ya kufanya uzinzi pia vinakinzana na mapenzi ya Mungu. Mungu ana lengo kubwa zaidi kwa ajili ya watu wake, na lengo hilo ni kuishi maisha yanayoongozwa na Roho wa Mungu. Tunatakiwa kumwomba Roho Mtakatifu akae ndani yetu ili aziongoze fikra zetu na matendo yetu.
- Kutambua Tofauti Iliyopo
-
- Ni vigumu kiasi gani kuelezea kama unaishi maisha yanayoongozwa na Roho au maisha yanayoongozwa na Shetani au maisha yanayoongozwa na asili yako ya dhambi? Mojawapo ya mambo mazuri kuhusu sheria ni kwamba ina ubayana wa aina fulani. Je, tunaweza kufurahia ubayana huo tunapoishi maisha yanayoongozwa na Roho?
-
- Soma Wagalatia 5:19-21. Je, haya ni maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu? (Hapana. Matendo haya ni matokeo ya kuishi kwa mujibu wa asili yetu ya dhambi.)
-
- Soma Wagalatia 5:22-23. Tofauti na orodha ya awali kuwa mbaya na hii orodha kuwa nzuri, je, unaona tofauti gani nyingine ya muhimu? (Kwa ujumla orodha ya kwanza ni ya matendo. Sio kikamilifu, lakini kwa kiasi kikubwa. Orodha ya pili ni ya mitazamo.)
-
-
- Unaweza kuona kwa nini sheria ni ya muhimu kwa mtu anayeabudu sanamu? Unafanya hivyo wakati kitendo hicho kipo kwenye orodha ya masuala ya kisheria yasiyotakiwa kutendwa. Vipi ikiwa lengo lako ni upendo, furaha na amani? Je, sheria inakusaidia katika mambo hayo? (Hapana. Haya ni maelezo mengine yanayohusu kuwaambia Wakristo kuwa sababu ya kuishika sheria inahafifisha lengo la Mungu kwa ajili ya maisha yetu. Njia pekee tutakayokuwa na upendo, furaha na amani ni kuwa na Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu na kuyaongoza matendo yetu!)
-
-
- Soma Wagalatia 5:24-25. Mambo gani yanatakiwa kusulubiwa? (Mawazo mabaya na tamaa. Utaona kwamba kifungu hakikusema “matendo mabaya.” Lengo hilo ni la chini sana!)
-
- Rafiki, je, utamwomba Roho Mtakatifu akae ndani yako na kuyaongoza mawazo na tamaa zaho? Jambo hilo linaweza kuhitaji kujitoa kwa dhati, lakini utampa Mungu utukufu na kuishi maisha ya furaha zaidi!
- Juma lijalo: Roho Mtakatifu na Tunda la Roho.