Worship in the Book of Revelation
(Revelation 4, 13 & 14)
Swahili
Year:
2011
Quarter:
3
Lesson Number:
13
Utangulizi: Ufunuo ni kitabu chenye kustaajabisha! Sio tu kwamba kinatupatia makanisa, wageni, viumbe na mpambano lakini pia kinatuelezea kuhusu ushindi wa mwisho. Sijui kuhusu wewe, lakini ninaposhinda kitu maishani, huwa ninajisikia vizuri. Mungu hunipatia ushindi wangu na maarifa haya yananifanya nijisikie kumpa sifa! Fikiria ni kwa kiasi gani tutajisikia kusifu pale ambapo Mungu atatupa ushindi wa mwisho kabisa dhidi ya dhambi, kifo na majonzi! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone jinsi wale walio mbinguni wanavyofurahia hii ibada ya ushindi!
- Ibada ya Ufalme (Enzi)
- Soma Ufunuo 4:1. Fikiria kuhusu mpangilio huo. Mlango ulio wazi, sauti “kama ya baragumu,” ikitoa ukaribisho wa kutazama sinema kuhusu mambo yajayo. Je, utakubali?
- Soma Ufunuo 4:2. Je, ni nani aliyefanya sinema hii iweze kutizamwa? (Roho Mtakatifu!)
- Je, hii ndio thawabu unayotaka kuipokea?
- Yohana ndiye ambaye anatizama sinema (maono). Je, nini kilicho nyuma ya mlango? (“Kiti cha enzi kikiwa na mtu aliyekaa juu yake.”)
- Kwa nini Yohana anasema “mtu fulani (mmoja)” ameketi juu ya kiti cha enzi? Je, huyu ni mtu atokaye kwenye utunzaji wa nyumba aking’arisha kiti cha enzi? (Inaonekana kama ni kitu cha muda baada ya muda ya kile alichokiona Yohana. Huenda ni Mungu akiwa amekalia kiti cha enzi, lakini Yohana bado hajalijua hilo, na kwa hiyo hasemi jambo hilo. Hii inafanya kisa hiki kiwe cha kuaminika (inaongezea kisa hiki sifa)
- Soma Ufunuo 4:3-4. Kwa nini Mungu anakuwa na wazee ishirini na nne wakiwa wamekaa kwenye viti katika chumba chake cha kifalme? (Hii inathibitisha tena kwamba Mungu anataka kuishi pamoja na watu wake. Anatutaka tushirikiane naye katika utawala wake. Wanadamu wanaweza kuhitaji washauri, lakini Muumba wa Ulimwengu hahitaji. Pamoja na yote hayo, anachagua kuwa nasi ili tuweze kutawala pamoja naye.)
- Soma Ufunuo 4:5. Mara zote huwa ninafurahia masuala ya Mungu katika Biblia yanayohusisha “ngurumo.” Hakuna mwanadamu katika kipindi cha Yohana ambaye aliwahi kuona injini ya aina yoyote. Hawakujua chochote kuhusiana na umeme. Je, unadhani ni chanzo gani cha nishati alicho nacho Mungu chini ya uwezo wake mkubwa?
- Baini kuwa chanzo cha nishati kwa ajili ya hizi taa ni Roho Mtakatifu.
- Soma Ufunuo 4:6. Je, Mungu anapenda mwonekano wa aina gani? (Mwonekano wa maji! Hii inanipa uhakika kwamba mwonekano wa maji utakuwa sehemu ya mbingu.)
- Sasa tunaingia kwenye sehemu ya ibada. Soma Ufunuo 4:6-8. Hawa ni wageni wanaofurahisha kuangalia. Kwa nini unafikiri wana haya macho yote? (Hawakosi kuona kitu chochote!)
- Kwa nini hayo mabawa yote? (Wanaweza kwenda kwa haraka.)
- Chukulia mwonekano wa jumla wa hao viumbe wanne: simba, ndama, mwanadamu na tai. Je, hii inaashiria kitu gani? (Simba ni jasiri, ndama ni thabiti (ana nguvu) na ni mwaminifu, mwanadamu ana akili na tai ni mwepesi, mwenye mbio, anakwenda kwa haraka na ni mwadilifu.)
- Je, ni kwa jinsi gani kauli za hawa wageni zinamwelezea Mungu? (Mara tatu zinasema kwamba Yeye ni mtakatifu, na kisha zinatoa nyakati za vipindi vitatu. Mungu alikuwa mtakatifu kabla, ni mtakatifu sasa na atakuwa mtakatifu kesho (wakati ujao).)
- Chukulia taarifa hii yote kama rangi iliyopakwa kwenye karatasi ngumu. Je, tunaona picha gani? (Kwa vile wanamwelezea Mungu kwa sauti zao, kwa nini tusihitimishe kwamba wanamwelezea Mungu kwa mwonekano wao: Wakiona pote, wepesi kukabiliana na tatizo lolote, jasiri, thabiti/wenye nguvu, waaminifu, wenye akili, na waaminifu.)
- Je, hii inatufundisha nini kuhusu ibada mbinguni? (Niliangalia baadhi ya commentaries zilizopendekeza kwamba viumbe hawa waliwakilisha injili nne, viwango vinne vya makabila ya Israeli, au nguvu nne za asili. Inaonekana kuwa na mantiki zaidi kwamba yote haya yanaelezea tabia za Mungu. Ibada ni mambo yote kumhusu Mungu, sio kutuhusu sisi. Vipengele vyote vya ibada vinapaswa kujielekeza kumpa Mungu utukufu.)
- Kila mara unapoimba wimbo wa kitabuni au wimbo wa sifa, tafakari kuhusu hili: je, wimbo huu unanihusu zaidi kuliko vile unavyopaswa kumpa Mungu sifa?
- Kama miili ya wageni iliwakilisha tabia za Mungu, je, hiyo inatupendekezea nini kuhusu ibada? (Ibada sio tu kile tunachokisema, bali vile tunavyoishi.)
- Soma Ufunuo 4:9-11. Katika chumba cha enzi cha mbinguni, je, nini msingi wa wazee ishirini na nne kumpa Mungu sifa? (Ya kwamba Yeye ni Muumba (“kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote”). Kila kiti kiliumbwa kwa mapenzi ya Mungu na kila kitu kinaendelea kuwepo kwa mapenzi ya Mungu.)
- Je, hii inawaacha wapi wale wanaokana uumbaji na kuendeleza nadharia ya uibukaji? (Wanashambulia msingi wa mamlaka ya Mungu na msingi wenye mantiki wa kumpa Mungu “utukufu, heshima na uwezo.” Huu sio mjadala wa upole kati ya marafiki, huu ni mjadala unaochora msitari kwenye mchanga kati ya wale wanaoendeleza ibada kwa Mungu na wale wanaodhoofisha ibada kwa Mungu.)
- Ibada ya Mnyama
- Soma Ufunuo 13:1-4. Mnyama pia alikuwa na tabia za wanyama. Je, nini ulio msingi wa ibada kwa mnyama? (Uwezo. “Nani awezaye kufanya vita naye?” Alimpa mnyama mamlaka/uwezo.)
- Hebu fikiria kuhusu hili kidogo. Je, kuna tofauti gani kati ya msingi wa ibada kwa Mungu na ibada kwa mnyama? (Ibada kwa Mungu imejengwa kwenye tabia Yake (takatifu) na kwa kile alichokifanya na anachokifanya (uumbaji na mwendelezo wa ulimwengu). Ibada kwa mnyama imejengwa kwenye nguvu/uwezo ghafi (usio na ujuzi/uzoefu.)
- Soma Ufunuo 13:5-7. Kama ungekuwa unachagua kati ya ibada ya kweli na ya uongo, je, ungeangalia ishara gani? (Mashambulio kwenye jina la Mungu, mbingu, malaika, na kwa wafuasi wa Mungu.)
- Je, unayasikia wapi mambo kama haya hivi leo?
- Je, ni rahisi kuchanganya aina hizi mbili za ibada? (Baadhi ya watu wanataka kuhoji kwamba mambo yaya ni magumu/tatanishi. Je, hili linaweza kuwa gumu/tatanishi kwa kiasi gani? Ama umwabudu Mungu Muumba au umshambulie yeye, mbingu, malaika, na wafuasi wa Mungu. Ama ibada yako imejengwa kwenye tabia na mibaraka ya Mungu, au imejengwa kutokana na kulazimishwa (kwa nguvu). Haionekani kuwa ngumu/tatanishi kivile kwangu!)
- Soma Ufunuo 13:1-4. Mnyama pia alikuwa na tabia za wanyama. Je, nini ulio msingi wa ibada kwa mnyama? (Uwezo. “Nani awezaye kufanya vita naye?” Alimpa mnyama mamlaka/uwezo.)
- . Wito wa Mwisho wa Kuabudu
- Soma Ufunuo 14:6-7. Je, ujumbe wa kwanza wa wito wa mwisho kwa wale walio duniani kuhusu kuabudu ni upi? (“Injili ya milele.”)
- Je, sehemu ya kwanza ya huu wito ni ipi? (Kumcha Mungu na kumtukuza.)
- Je, hiyo inamaanisha nini? (Ni wito wa utii na sifa (kusifu).)
- Je, haya mambo mawili yanahusianishwa? (Tunampa Mungu utukufu kwa kuzifuata njia zake.)
- Je, hiyo inamaanisha nini? (Ni wito wa utii na sifa (kusifu).)
- Je, sehemu ya pili ya huu wito ni ipi? (“Saa ya hukumu yake imekuja.”)
- Je, hiyo inamaanisha nini? (Ni wito wa kutubu kwa sababu muda (“saa”) ya hukumu ya Mungu ni sasa.)
- Je, sehemu ya tatu ya huu wito ni ipi? (Kumwabudu Mungu kwa kuwa Yeye ni Muumba.)
- Je, sehemu ya kwanza ya huu wito ni ipi? (Kumcha Mungu na kumtukuza.)
- Soma Ufunuo 14:8. Je, ujumbe wa pili wa wito wa mwisho kuhusu ibada ni upi? (Mpinzani wako ameshindwa. Wakristo wanapaswa kupeleka ujumbe wa injili kwa ujasiri kwa sababu “Babeli, ule mji mkubwa” umeanguka!)
- Soma Ufunuo 14:9-11. Je, ujumbe wa tatu wa wito wa mwisho kuhusu ibada ni upi? (Ni onyo. Muda wa kufanya uchaguzi ni sasa. Hatma iko juu – uzima wa milele au ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji.)
- Soma Ufunuo 14:12. Kama huwa unasoma masomo haya mara kwa mara, unayafahamu mambo haya. Umesikia ujumbe wa malaika watatu. Kama umefanya uamuzi sahihi, je, ushauri wa malaika wa mwisho kwetu ni upi? (Endelea kuwa mwaminifu. Vumilia kwa upole.)
- Je, nini kinachojumuisha uaminifu, uvumilivu na ustahimilivu? (Haki kwa imani “Endelea kuwa mwaminifu kwa Yesu,” na kuwa na mtazamo wa utii.)
- Rafiki, je, huyu ni wewe? Je, umekubali wito wa kumchagua Yesu kuwa Bwana wako? Je, umetubu dhambi zako na kukubali kafara ya Yesu kwa ajili (niaba) yako? Je, unaishi maisha yanayompa Mungu utukufu? Je, unainua sauti yako kumsifu Muumba wako? Je, u na mtazamo wa utii wa unyenyekevu kwa mapenzi ya Mungu? Kama sivyo, kwa nini usifanye uamuzi huo hivi leo? Hukumu tayari i hapa. Uovu umeangushwa. Mungu analeta sura za mwisho za historia ya hii dunia kwenye mwisho wake.
- Soma Ufunuo 14:6-7. Je, ujumbe wa kwanza wa wito wa mwisho kwa wale walio duniani kuhusu kuabudu ni upi? (“Injili ya milele.”)
- a Lijalo: Tutaanza somo zuri ajabu linalohusu injili katika Wagalatia!