Uhuru Katika Kristo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Wagalatia 5:1-15)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
3
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Mojawapo ya mibaraka mikubwa kabisa kwangu ni kuishi maisha yangu yote mahali ambapo tuna uhuru wa kisiasa na kiuchumi. Katika kipindi chote cha maisha yangu, sehemu kubwa ya dunia hii imekuwa huru kiuchumi na kisiasa. Uhuru huo umepunguza kiwango cha umasikini na njaa ulimwenguni kote. Hivi karibuni nilisoma makala iliyobainisha kwamba umasikini wa kutupwa ulipungua kwa zaidi ya asilimia 80 kutoka mwaka 1970 hadi mwaka 2006 na unaendelea kupungua. Sina hata chembe ya shaka mawazoni mwangu kwamba uhuru wa kisiasa na kiuchumi una uhusiano wa karibu na utokomezaji wa umasikini. Je, uhuru gani mwingine unahusianishwa na kuyafurahia maisha bora? Kwa hakika upo uhusiano na uhuru wa dini. Katika somo letu la leo, Paulo anatuasa tuangalie kwa makini uhuru wa kiteolojia. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

 

  1. Uhuru

 

    1. Soma sehemu ya kwanza ya Wagalatia 5:1. Kwa nini Yesu alituweka huru? (Paulo anasema, “ni kwa ajili ya kuwa huru.”)

 

      1. Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Lazima imaanishe kwamba angalao Mungu anayo mawazo makubwa sana juu ya uhuru.)

 

      1. Ifikirie Biblia kwa ujumba. Yesu ametuwekaje huru? (Adamu na Eva walipotenda dhambi, tulihukumiwa mauti ya milele. Angalia Warumi 5:14. Yesu alituweka huru dhidi ya adhabu yetu ya kifo.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:1 yote. Paulo anamaanisha “kongwa lipi la utumwa?” Je, anazungumzia utumwa wa dhambi? (Paulo anazungumza kwa kurudiarudia juu ya watumwa na utumwa katika kitabu cha Wagalatia sura ya 4. Anazungumzia juu ya utumwa wa kuwa chini ya sheria.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:2-3. Hii inabainishaje anachokimaanisha Paulo anapoandika kuhusu utumwa? (Paulo anasema kwamba anazungumzia juu ya tohara na “torati yote.”)

 

      1. Kwa nini Yesu “hatufaidii neno” ikiwa tunawajibika kuitimiza torati yote? (Tunapomkiri Yesu kwa njia ya ubatizo, tunakufa pamoja naye na tunafufuka pamoja naye na kuingia kwenye uzima wa milele. Ikiwa unajaribu kuokolewa (kupata wokovu) kwa kuishika sheria, unakuwa umeipuuza kafara ya Yesu kwa ajili (niaba) yako.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:4. Hadhi yetu maishani ikoje ikiwa “tunatengwa na Kristo?” Tuna tumaini gani ikiwa tuko kwenye hiyo hali? (Tumepotea! Tupo chini ya hukumu ya wale ambao lazima, lakini hawawezi, waitimize “torati yote.”)

 

      1. Tuchukulie kwamba wewe ni mtu mwema sana. Wewe ni bora kuliko watu wengi unaowafahamu. Unaweza usiwe na vishawishi katika maeneo fulani maishani mwako, lakini je, hali hiyo ipo kwenye maeneo yote yanayogusa maisha yako?

 

 

      1. Nilipokuwa kijana (rika la umri wa kubalehe), mtu mzima aliniuliza pamoja na marafiki wangu endapo tulikuwa na uhakika kwamba tumeokoka? Lilikuwa swali zuri sana, na nina uhakika mtu huyu alijiona kwamba anautangaza Ufalme wa Mungu kwa kuuliza swali hilo. Tatizo ni kwamba mtu huyu hakuwa mwaminifu katika mambo madogo madogo – na alikuwa ananishauri nifanye vitendo visivyo vya uaminifu ili niweze kujiwekea akiba kutokana na malipo madogo madogo. Je, unaweza kuona jinsi utii katika mambo yote ulivyo mgumu sana hata kwa watu wema?

 

    1. Soma Wagalatia 5:5. Nani atupatiaye mtazamo wa kuitazamia haki kwa furaha? Nani aliye wakala anayeshughulika na kuileta haki maishani mwetu? (Roho Mtakatifu!)

 

    1. Soma Wagalatia 5:6. Imani inajielezeaje kwa njia ya upendo?

 

      1. Hebu tutafakari jambo hili kidogo. Mungu anataka kutupatia uhuru. Je, imani na upendo vinahusiana? (Ikiwa tunampenda mtu fulani, tungependa awe huru. Paulo anaanza kujenga hoja yake kwa dhana ya kwamba imani huleta matokeo fulani maishani mwetu.)

 

  1. Kuuingilia Ukweli

 

    1. Soma Wagalatia 5:7-8. Je, kuna mwanaridha yeyote asomaye somo hili? Inamaanisha nini “kumzuia” mwanaridha? (Ninachukulia inamaanisha kukaa kwenye msitari wako wa kukimbilia na kisha kuondoka ili usiweze kukimbia. Njia yako imezibwa.)

 

      1. Paulo anaposema “kushawishi huku” hakukutoka kwa Mungu, anamaanisha nini? Mungu “haingilii” msitari wetu wa kukimbilia? (Tunafahamu kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo kwamba Mungu anatupatia uhuru wa kuchagua. Watetezi wa habari ya wokovu kwa njia ya matendo walikuwa wanajaribu kuuminya uhuru wa Wagalatia.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:9. Tunatakiwa tume makini kiasi gani kulinda hoja dhidi ya kutangaza kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo? (Paulo anasema ina madhara yanayopenya taratibu lakini kwa hakika – yanapenya kanisa zima.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:10. Haiwezekani Paulo awe anaandika kumhusu Shetani, kwa sababu Paulo anamjua. Lazima hiyo imaanishe kuwa Paulo anamzungumzia mtu. Jambo gani linawatokea watu wanaotangaza na kuunga mkono kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo? (“Watachukua hukumu yake.”)

 

      1. Unadhani adhabu ya fundisho hilo ni ipi?

 

      1. Binafsi nina mashaka kama mtu yeyote unayemfahamau atasema kwamba “Nitakwenda mbinguni kutokana na matendo yangu, achana na habari za Yesu.” Lakini, je, umewahi kuambiwa kuwa ikiwa huishiki sheria utapotea?

 

    1. Soma Wagalatia 5:11-12. Kwa dhahiri baadhi ya watu “wanaounga mkono tohara” walianzisha uvumi kwamba Paulo anakubaliana nao. Paulo anatoa sababu gani kuthibitisha kwamba uvumi huo ni wa uongo? (1. Ikiwa Paulo alikubaliana na tohara, asingekuwa anapata mateso. 2. Hawezi kuwa anatangaza tohara na wakati huo huo anatangaza kile ambacho Yesu alitutendea msalabani. 3. Anao mtazamo wenye uhasama dhidi ya kundi la watu wanaounga mkono tohara.)

 

  1. Utii na Ukweli

 

    1. Soma Wagalatia 5:13. Ikiwa siwezi kuutumia uhuru wangu, je, niko huru kweli? (Ndiyo, unaweza kuchagua. Paulo anasema, “Chagua kwa busara.”)

 

 

      1. Je, kuna utumwa dhambini?

 

      1. Hebu tufikiria jambo hili kidogo. Paulo anatuambia “tusiifuate asili ya dhambi (tusiufuate mwili)” na kisha anatuambia “tutumikiane kwa upendo.” Kwa nini mambo hayo yanakinzana? Kwa nini anayabainisha yaonekane kukinzana? (Dhambi nyingi zinahusisha ubinafsi. Unataka kutoa mimba kwa sababu kwa ubinafsi unajipendelea kuliko mwanao ambaye hajazaliwa. Unataka kufanya uasherati, kwa sababu unajipendelea dhidi ya mwenzi wako na mwenzi wa mwenzako, na watoto wote wanaohusika hapa. Unaiba kwa sababu kwa ubinafsi unajipendelea dhidi ya miliki ya mali za mtu mwingine.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:14. Je, unakubaliana na kauli hii? (Soma Mambo ya Walawi 19:18 na Mathayo 22:37-40. Paulo hakutunga jambo hili. Mambo ya Walawi na Yesu wanakubaliana.)

 

      1. Muda mfupi uliopita nimeandika kuwa “dhambi nyingi zinahusisha ubinafsi” kwa sababu nilidhani kwamba dhambi nyingine zinaweza zisiwe hivyo. Ikiwa sheria yote imejengwa juu ya kuwapenda watu wengine kama tunavyojipenda, basi lazima dhambi zote zihusishe ubinafsi. Je, unaweza kufikiria dhambi isiyohusisha ubinafsi?

 

      1. Je, hii inamaanisha kwamba kujipenda ni sawa? (Ndiyo! Ila tu tusijipende kupitia mgongo wa mtu mwingine.)

 

    1. Soma Wagalatia 5:15. Tatizo mahsusi la Wagalatia ni lipi? Je, wanatakiwa kuwa wala mbogamboga (vegetarians)?

 

      1. Nilidhani tatizo lilijikita kwenye mtazamo wao wa wokovu. Kwa nini Paulo anaibua suala hili? (Lazima iwe kwamba sio tu kuwa hawakubaliani na hali halisi, bali tatizo ni jinsi wanavyoenenda katika kutokubaliana.)

 

        1. Je, unawafahamu watu kama hawa? Hawawezi kutokubaliana jambo fulani bila kumshambulia mtu anayehusika?

 

    1. Rafiki, je, unataka kuwa huru? Paulo anatuambia kwamba neema hutupatia uhuru wa kiteolojia. Sisi si watumwa chini ya hukumu ya sheria. Lakini, wakati huo huo, Paulo anatuambia kuwa tufanye uchaguzi kwa umakini na tutende yale mambo ambayo yanaonesha upendo kwa watu wengine. Je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie kuibua na kuendeleza mtazamo wa upendo ndani yako?

 

  1. Juma lijalo: Kuishi kwa Roho.