Somo la 14: Kuona Fahari Juu ya Msalaba
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Tunafikia mwisho wa somo letu la barua ya Paulo kwa Wagalatia kwa mwaka huu wa 2017. Kama ulikuwa nasi kwenye mfululizo wote wa masomo haya, ni matumaini yangu kwamba umekuwa na uelewa mzuri wa ujumbe wa Paulo wa kuhesabiwa haki kwa imani, na imani yake kwamba kwa uwezo na uongozi wa Roho Mtakatifu imani hubadili mtazamo wetu. Mabadiliko hayo yanatufanya tutake kuishi maisha yanayompa Mungu utukufu na kurahisisha safari yetu ya hapa duniani. Paulo anazo kweli chache muhimu anazotaka kushiriki nasi katika kuhitimisha kwake, hivyo hebu tuzame kwenye somo letu la mwisho la Wagalatia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Herufi Kubwa
-
- Soma Wagalatia 6:11. Kauli ya Paulo kuhusu kuandika kwa mkono wake mwenyewe inaashiria nini juu ya barua yake yote kwa Wagalatia? (Soma Warumi 16:22. Paulo alimtumia mwandishi (mweledi wa barua) kuandika barua zake. Hakushika kalamu yeye mwenyewe - isipokuwa sehemu tunayokwenda kujifunza hivi punde.)
-
- Angalia tena Wagalatia 6:11. Kwa nini Paulo anatuambia kuwa anaandika kwa “herufi kubwa?” (Huu ni uthibitisho kwamba Paulo mwenyewe aliandika hivi vifungu vichache vya mwisho.)
-
-
- Kwa nini Paulo anaandika kwa herufi kubwa? (Soma Wagalatia 4:15. Jibu rahisi kabisa na la dhahiri ni kwamba Paulo ana matatizo ya uoni hafifu. Si jambo geni kwa wasomaji walio na umri wa zaidi ya miaka arobaini kuelewa kwamba kuandika na kusoma maandishi madogo ni changamoto. Hata hivyo, wasomi wanapendekeza sababu nyingine za kutumika kwa herufi kubwa. Sababu hizi ni kwamba Paulo si mweledi sana kuandika kwa Kiyunani, au ana mwandiko mbaya, au kwamba barua kwa Wagalatia ni ndefu. Pendekezo la mwisho linageukia kwenye uelewa wa “herufi kubwa” kumaanisha “barua ndefu.” Nadhani suala la uoni hafifu ni jibu la dhahiri zaidi.)
-
- Maneno ya Kuhitimisha
-
- Soma Wagalatia 6:12-13. Kabla hatujaingia kwenye mjadala juu ya kinachomaanishwa hapa, maoni ya Paulo kuhusu “herufi kubwa” yana athari gani juu ya umuhimu wa sehemu hii ya waraka? (Paulo hakutia tu sahihi barua yake kwa Wagalatia, kimsingi aliandika kwa mkono sehemu tunayojifunza juma hili. Hiyo inaashiria kwamba hii sehemu ya hitimisho ni ya muhimu sana kwake, na hivyo inapaswa kuwa ya muhimu kwetu.)
-
-
- Hebu tujikite kwenye Wagalatia 6:12. Hamasa ya watu wanaounga mkono tohara ni ipi? (Wanataka waonekane wazuri na wanataka kuepuka mateso (maudhi).)
-
-
-
-
- Kuna shida gani na jambo hilo? (Kama kijana mdogo ataniuliza ikiwa mvuto wa mtu unapokutana naye kwa mara ya kwanza ni wa muhimu, kwa dhahiri nitamjibu kuwa, “Ndiyo.” Hata hivyo, kama tutakavyoona hapo baadaye kwenye somo hili, Paulo anatuambia tusijikite kwenye mambo ya nje.)
-
-
-
-
-
- Paulo anamaanisha nini anapozungumzia kundi la watu wanaounga mkono tohara wanaotaka “kuepuka maudhi kwa ajili ya msalaba wa Kristo?” (Kwa dhahiri, Wayahudi wa Israeli walikuwa wanawatesa (wanawaudhi) Wakristo. Tulianza somo letu la barua ya Paulo kwa kusoma wajibu wa Paulo (Sauli) katika mauaji ya Stefano kwa sababu ya ushuhuda wake wa Kikristo. Angalia Matendo 7:57-60. Hivyo, Wagalatia waliokuwa wanaunga mkono tohara walihamasika kutojiingiza kwenye matatizo na kundi la watu wa Yerusalemu.)
-
-
-
-
-
-
- Unauchukuliaje uhamasishaji kama huo? (Paulo anasema kwamba huo ni ubinafsi, kinyume na uelewa mahiri wa mapenzi ya Mungu, kwamba ndio unaowasukuma kuwa na msimamo wa kuunga mkono suala la tohara. Wanataka waonekane kuwa wanaendana na matakwa ya mamlaka ya Yerusalemu.)
-
-
-
-
-
-
-
- Je, unahatarisha (kwa kulegeza msimamo) imani yako ya dini ili kuepuka kushambuliwa na watu wengine?
-
-
-
-
- Soma Wagalatia 6:13. Hapa Paulo anamaanisha nini? Kwamba wale wanaounga mkono tohara ni wanafiki? (Sidhani kama hilo ndilo tatizo kubwa. Ikiwa mtu anajenga hoja kwamba kuishika sheria ndio ufunguo wa wokovu na mtu huyo hawezi kuishika sheria, basi kiuhalisia, kujaribu kuishika torati si suluhisho la dhambi.)
-
-
- Angalia lugha yake ya “kuona fahari katika miili.” Unapomshawishi mtu akubaliane na mtazamo wako, je, unajisikia fahari “kujivuna”? (Ndiyo, sote tunajisikia kutimiza jambo fulani tunapoweza kuwashawishi watu wengine juu ya mtazamo wetu.)
-
-
-
-
- Tatizo ni lipi hapa basi? (Wamemshawishi watu jambo lisilo na maan)
-
-
-
-
-
- Jambo hili linapaswa kuongozaje juhudi zetu za uinjilisti? (Tunatakiwa kuelekeza juhudi zetu kwenye mambo ya msingi zaidi – imani kwa Yesu na utoaji wake wa haki kwa imani.)
-
-
-
- Soma Wagalatia 6:14. Unaona fahari juu ya jambo gani? Mtu anapokuuliza jambo linalokuhusu, unasema nini kwanza?
-
-
- Paulo anaposema kwamba “ulimwengu umesulubishwa” kwake, unadhani anamaanisha nini? (Kusulubisha kitu inamaanisha kukiua. Anamaanisha kwamba ameufia ulimwengu na ulimwengu umemfia.)
-
-
-
-
- Kwa nini Paulo anatumia neno “kusulubisha” ikiwa tu anamaanisha “kifo?” (Ukweli ni kwamba Yesu aliushinda ulimwengu kwa njia ya mateso yake. Yesu aliishinda sheria ya dhambi iletayo mauti kwa wale wanaojenga imani yao kwa Yesu. Ndio maana Paulo anasema kuwa lengo lake ni kuona fahari msalabani.)
-
-
-
-
- Nilipokuwa ninakua, na hata sasa hivi, ninawasikia watu wakizungumzia kukaa mbali na ulimwengu. Hiyo inaendana na kile ambacho Paulo anakizungumzia hapa. Unadhani hiyo inamaanisha nini?
-
-
- Soma Wagalatia 6:15. Je, hiki ndicho anachokimaanisha Paulo kwa kuufia ulimwengu? (Nilipokuwa ninakua, kukaa mbali na ulimwengu ilikuwa dhahiri. Kuwa “watu wa pekee.” Ungeweza kumgundua na kumbainisha mshiriki wa kanisa wa kike kutoka kundini kwa sababu hakuwa amejiremba vipodozi vingi wala kuvaa vito kama vile hereni, au nguo zinazoendana na wakati (fasheni). Ukweli huu pia ulihusika kwenye madhehebu mengine katika kipindi hicho.)
-
-
- Je, hilo si wazo la kwamba unaweza kuona tofauti iliyopo ya tohara ya kisasa inayofanana na ya zamani? Tatizo lipo kwa nje, tunatofautiana na ulimwengu? (Paulo anatuambia kuwa kinachotutofautisha na ulimwengu ni kwamba tunaona fahari juu ya msalaba. Ulimwengu ni mbinafsi, na msalaba ni ishara na hatima ya kutokuwa na ubinafsi. Hiyo inaweza kuwa na athari kwenye kile tunachokivaa, tunachokiendesha na jinsi tunavyoishi. Lakini, jambo la muhimu si mambo ya nje, bali ni mtizamo. “Kinachojalisha ni uumbaji mpya.”)
-
-
- Soma Wagalatia 6:16. Paulo anabainisha kuenenda kwa “kanuni hii.” Anamaanisha kanuni gani? (Kanuni ya uumbaji mpya. Kanuni ya kwamba mambo ya nje si ya muhimu. Kanuni ya kutokuwa na ubinafsi.)
-
-
- Je, tutakuwa na amani ikiwa tutaifuata hii kanuni mpya? (Paulo anasema kuwa kundi la tohara linang’ang’ania msimamo wake kwa kiasi fulani ili kuepuka mateso (maudhi).)
-
-
-
- Ngoja nikuulize swali la uhalisia. Ikiwa moyo wako umeongolewa na kutokuwa na ubinafsi, je, utakuwa na amani ndogo au kubwa maishani mwako? Ikiwa moyo wako umeongolewa kiasi kwamba mambo ya nje hayana utofauti wowote, je, utakuwa na imani ndogo au kubwa?
-
-
-
- Je, utakuwa na rehema ndogo au kubwa ikiwa utayazingatia mambo ya nje kwa hali ya uchache?
-
-
- Soma Warumi 2:28-29. Paulo anaandika nini kuhusu mambo ya nje hapa?
-
- Soma Wagalatia 6:17. Kwa nini watu wasimtaabishe Paulo? Anayo chapa ya Yesu? (Soma 2 Wakorintho 6:4-5 na 2 Wakorintho 11:24-25. Kiuhalisia Paulo anazo alama za kuteswa kwake ikiwa ni matokeo ya kumshuhudia Yesu. Hahitaji tena mapigo zaidi. Na, anao uthibitisho unaoonekana mwilini mwake kuonesha kujitoa kwake kwa Yesu.)
-
- Soma Wagalatia 6:18. “Roho” yako ni ipi? (Paulo amekuwa akituhamasisha kuishi kwa mujibu wa maelekezo ya Roho Mtakatifu. Hivyo, anahitimisha kwa kusema kuwa ruhusu roho yako imsikilize Roho Mtakatifu. Pokea na kubali ujumbe huu wa neema unaotolewa na Yesu.)
-
- Rafiki, je, utaikubali na kuipokea neema leo? Je, utajitahidi kila mara kuishi kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu? Je, utajikita kwenye mambo ya msingi kutoka moyoni na si mambo ya nje? Kwa nini usichukue uamuzi huo sasa hivi?
Juma lijalo: Tutaanza mfululizo mpya wa masomo ya barua ya Paulo kwa Warumi.