Mamlaka ya Paulo na Injili
(Wagalatia 1, Matendo 15)
Swahili
Year:
2011
Quarter:
4
Lesson Number:
2
Utangulizi: Juma lililopita tulijifunza kwamba Paulo aliitegemea elimu yake ya thamabi na bora kabisa na mamlaka yake ya zamani ya kisheria katika kujitetea dhidi ya mashtaka ya kuvunja sheria yaliyoletwa mbele yake. Juma hili tutaona kwamba kwa mara nyingine tena Paulo anajitetea – na anatoa madai ya kustaajabisha sana. Je, aina hii ya utetezi inatuambia kitu gani? Inatuambia kuwa Paulo anaamini kwamba changamoto kubwa zimeibuliwa kwa faida ya uaminifu wake. Je, unajisikiaje pale ambapo mtu anaposhambulia uaminifu wako au hadhi yako? Ni ngumu sana, sawa? Je, unadhani ni kwa nini Paulo yu chini ya hilo shambulizi kubwa? Hebu tuzame kwenye somo letu la Wagalatia na kuona kama haya mashambulizi yanathibitika!
- Mamlaka ya Paulo
- Soma Wagalatia 1:1-2. Ni kwa jinsi gani kiongozi wako wa kidini alipatikana kwa ajili ya kuongoza kundi lako? (Kwa kawaida, wanadamu (wakiongozwa na Roho Mtakatifu) walifanya mchakato wa kumpata.)
- Je, Paulo anasema nini kuhusu wito wake? (Haukutokana na wanadamu.)
- Kwa nini Paulo anasema “si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu?” je, “wala kutumwa na mwanadamu” inaongezea kitu gani? (“Commentary” ya Jack Sequeira inasema kwamba maadui wa injili walikuja kwenye kanisa la Galatia (kanisa lililoanzishwa na Paulo) na kuwaambia washiriki kwamba Paulo “alijichagua mwenyewe.” Hakuwa na mamlaka ya kweli kwenye mafundisho yake. Kwa hiyo, kwenye lugha yake ya “wala kutumwa na mwanadamu” Paulo anasema “sikujichagua mimi mwenyewe.”)
- Je, ni nani aliyeupa mamlaka/aliyeidhinisha ujumbe wa Paulo? (Anasema ni “Yesu Kristo na Mungu Baba!"
- Hebu turukie mbele na kusoma Wagalatia 1:11-12. Je, madai ya Paulo hapa ni yapi? (Kwamba Yesu mwenyewe ndiye aliyemfundisha.)
- Je, kwa nini tunapaswa kumwamini Paulo? Yesu tayari alikuwa amesharejea mbinguni!
- Kama tukiviondosha vitabu vilivyoandikwa na Paulo kutoka kwenye Biblia, huenda tukawa na mtazamo tofauti wa wokovu. Kwa kawaida Yesu huwa anarejea kitu fulani kinachohitajika kufanywa na mtu ili aweze kuokolewa. (Angalia, kwa mfano, Mathayo 5:17-20; Mathayo 25:34-36; Mathayo 19:21.) Najua kwamba kauli hizi zinazoonekana kupingana na neema zinaweza kuelezewa, ila nina mashaka kama watu wengi wanaweza kujaribu kuelezea bila maandiko ya Paulo kuhusu neema. Hii inamaanisha kuwa swali la wapi Paulo alipata wazo lake ni jambo la muhimu sana – hata hivi leo.
- Je, kwa nini tunapaswa kumwamini Paulo? Yesu tayari alikuwa amesharejea mbinguni!
- Soma Wagalatia 1:15-20. Je, hii inaathiri vipi uaminifu wa Paulo? (Kwa ujumla huwa sipendezwi pale ambapo mtu anakana kwamba hadanganyi! “Kweli kabisa, hicho ndicho kilichotokea!” Kinachompatia Paulo uaminifu ni kwamba anatoa undani (maelezo ya kina) wa mafunzo yake – Alikuwa Arabuni kwa miaka mitatu akipokea mafunzo kutoka kwa Yesu.)
- Je, unadhani Yesu alitumia muda wa miaka mitatu akiwa na Paulo – kwa haraka haraka muda huo huo alioutumia Yesu na wanafunzi wake? (Kwa hakika hatujui. Paulo hadai kwamba Yesu alikuwa akimfundisha muda huu wote.)
- Soma Matendo 9:10-15. Nani aliyendika kitabu cha Matendo? (Tunaamini Luka ndiye aliyekiandika, sio Paulo. Kwa hiyo, Luka ameshawishika, kutokana na taarifa kutoka kwa Anania, kwamba Paulo alichaguliwa kipekee na Mungu ili ashiriki injili na watu wa Mataifa.)
- Soma 2 Petro 3:15-16. Je, mwanafunzi (mfuasi) Petro anasema nini kuhusu maandiko ya Paulo (zaidi ya kwamba ni magumu kuyaelewa kwenye baadhi ya sehemu)? (Kwamba maandiko ya Paulo yanatokana na busara ambayo Mungu alimpa Paulo, na kwamba yapo kwenye kiwango cha “Maandiko mengine,” na kwamba kuyapuuzia au kuyapindisha inamaanisha upotevu wa wokovu.)
- Je, hii inatuambia nini kuhusu mamlaka ya Paulo? (Kwamba viongozi wa kanisa wa mwanzo, Luka na Petro, walikubali kauli za Paulo kuhusiana na chanzo cha mamlaka yake. Nasi tunapaswa kuzikubali.)
- Hebu turejee kwenye swali letu la msingi: unadhani ni kwa nini mamlaka ya Paulo hayakustahili shambulizi kama hilo? (Kama shetani alitaka kutia muhuri ujumbe wa neema, basi Paulo ndio angekuwa mlengwa wake mkuu.)
- Je, neema (haki kwa imani pekee) ni ya muhimu? (Kinyume na baadhi ya Ukristo, dini zote za dunia zinategemea matendo. Hiyo inapaswa kutuambia kitu muhimu kuhusu mpambano kati ya wema na uovu.)
- Kabla hatujaondoka kwenye hiki kipengele, hebu tusome Matendo 1:6. Mara zote nimekuwa nikifikiri kuwa hili swali, lililowasilishwa kwa Yesu mara tu alipokuwa akirejea mbinguni, lazima lilikuwa la kusikitisha. Wafuasi wake bado wanaonekana kuchanganyikiwa kuhusu utume wa Yesu. Je, inawezekana kwamba kutokana na muktadha wa hili swali, Yesu alitafakari tena suala la kutumia msingi wa mvuvi wa zamani kuiendeleza injili, na kuamua kwamba ataongezea mwanateolojia mwerevu, mwenye elimu kubwa kwenye kundi lake kuu?
- Soma Wagalatia 1:1-2. Ni kwa jinsi gani kiongozi wako wa kidini alipatikana kwa ajili ya kuongoza kundi lako? (Kwa kawaida, wanadamu (wakiongozwa na Roho Mtakatifu) walifanya mchakato wa kumpata.)
- Injili
- Tukiwa sasa tumeshaafikiana kuhusu mamlaka ya Paulo, hebu turejee kwenye Wagalatia 1:1. Je, Paulo anamwelezea Yesu kwa namna gani? (“Aliyefufuka kutoka katika watu.”)
- Kwa nini? (Hili ndilo suala kuu kwenye dhana ya wokovu kwa neema. Aidha tunaishi au kufa kutokana na sheria, au tunaishi au kufa kwa kuyakubali maisha, kifo na ufufuo wa Yesu kwa niaba (ajili) yetu. Sehemu ya muhimu sana katika hili (kwa Yesu na kwetu) ni sehemu ya ufufuo!)
- Soma Wagalatia 1:3-5. Hebu tusiruke kwa haraka haraka maneno tunayoyaona mara zote. Je, inamaanisha nini kuwa na “neema na amani,” na kwa nini Paulo aseme maneno haya badala ya “utajiri na uzuri?” (Neema, kwa mara nyingine tena, ndio tiketi yetu ya kuelekea kwenye uzima wa milele. Hii inatupatia amani na Mungu. Yesu anafufuliwa kutoka katika wafu, kwa hiyo tuna neema na amani vinavyopatikana kwetu.)
- Soma Wagalatia 1:6-7. Je, ni nani anayeachwa? (Paulo anaonekana kujinukuu yeye mwenyewe. Yeye ndiye aliyewaleta kwenye neema.)
- Je, tatizo ni lipi? (Wanaigeuka injili.)
- Fikiria kuhusu hili kidogo. Ninapofikiria kuhusu kupotea, wazo langu ni kwamba Shetani atanizamisha sana dhamnini kiasi kwamba sitajali tena kuhusu uhusiano wangu na Mungu. Paulo anaonekana kuonya kuhusu tatizo tofauti – tatizo ambalo wanaopaswa kuwa wafuasi wa Mungu wanatuelekeza kwenye injili ya uongo “iliyopotoshwa.” Je, hiyo injili ya uongo inaweza kuwa ipi?
- Soma Matendo 15:2-6. Je, Matendo inaandika nini kama tatizo la injili ya uongo? (Kwamba watu wa Mataifa lazima watahiriwe na kutii sheria ya Musa.)
- Je, kuna tatizo gani la kutahiriwa au maelekezo ambayo Mungu alimpa Musa? Je, hapo zamani Mungu alitoa ushauri mbaya?
- Soma Matendo 15:7-11. Petro anasimama na kutoa hoja kwenye mtazamo wa Paulo. “Commentary” moja niliyoisoma ilisema kwamba (Matendo 15:5) “sheria ya Musa” ilikuwa inarejea sheria ya mapokeo badala ya Amri Kumi. Je, kutatua swali hilo ni muhimu?
- Petro na Paulo wanasema kwamba kile kinachotakiwa kwa ajili ya wokovu ni imani pekee. Watu wenye injili ya uongo wanasema kwamba kile kinachohitajika kwa ajili ya wokovu ni imani pamoja na kitu kingine. Ukiifanya hii kuwa kanuni ya kimahesabu: Wokovu = Imani + X. Je, suala ni kuwa “X” inasimama badala ya kitu gani? Au, je, suala ni kama kiukweli wokovu unahitaji “X”?
- Kama suala ni “X” inasimamia kitu gani, basi tunahitajika kuamua kama “X” ni Amri Kumi au sheria ya kimapokeo. Lakini, endapo suala ni kama kweli tunahitaji “X”, bila kujali kuwa “X” itakuwa kitu gani, basi kutafuta utambulisho wa “X” ni upotezaji wa muda.
- Soma Wagalatia 1:8-9. Je, ni jambo baya kiasi gani kuhubiri injili ya uongo? (Uzima wa milele upo mashakani.)
- Baada ya mjadala wa hili suala, Yakobo anasimama na kutoa uamuzi wa kanisa la awali. Soma Matendo 15:19-20. Kwa jinsi ninavyolielewa hili, tohara na sheria ya Musa havipo tena, kuachana na ulaji wa vyakula fulani na usafi wa masuala ya ngono bado vipo. Je, hii ni “X” mpya? Je, kanuni ya wokovu sasa ni Imani + X, X ikiwa imeelezewa kwenye fungu la 20? (Pitia kwa haraka haraka 1 Wakorintho8. Hapo, Paulo anatoa hoja kwamba wale tu “ambao dhamiri zao ni dhaifu” wanaacha kula nyama zilizotolewa kwa sanamu. Kauli za Paulo katika 1 Wakorintho 8, na akili ya kawaida kabisa, vinatuambia kuwa ulaji wetu na masuala ya usafi wa ngono haviwezi kuwa “X” mpya. Tohara, sheria ya Musa, Amri Kumi, ulaji sahihi na usafi wa masuala ya ngono, vyote ni mambo mema. Maelekezo haya yalitoka kwa Mungu ili kuyabariki maisha yetu na kutusaidia kuenenda katika njia Zake. Lakini, hakuna hata moja kati ya hizo iliyo kwenye sehemu ya kanuni ya wokovu. Kuvifanya viwe sehemu ya kanuni ya wokovu ni injili ya uongo.)
- Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je, unakubali kwamba ujumbe wa Paulo ulitoka kwa Yesu? Je, unaamini katika wokovu kwa imani pekee? Au, je, unaiendeleza injili ya uongo kwamba toba na imani katika Yesu vinahitajika kuongezewa kwa kiwango cha “X” – kivyovyote vile tunavyoweza kuielezea hii “X”? Mimi ni mtu ambaye ni mshindani. Ninapenda kupata ushindi na ninachukia kushindwa. Lakini, linapokuja suala la wokovu, asili yangu ya ushindani inahitajika kutupwa jalalani. Hakuna kitu chochote, kwa hakika kabisa hakuna kitu chochote ninachokifanya (ikijumuisha kuandika haya masomo) kilaleta tofauti yoyote kwenye wokovu wangu.
- Tukiwa sasa tumeshaafikiana kuhusu mamlaka ya Paulo, hebu turejee kwenye Wagalatia 1:1. Je, Paulo anamwelezea Yesu kwa namna gani? (“Aliyefufuka kutoka katika watu.”)
- Juma lijalo: Umoja Katika Injili.