Somo la 5: Mawakili Baada ya Edeni
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: “Wakili” si neno linalotumika sana siku hizi. “Wakala,” “mwakilishi,” “mwajiriwa” au “meneja” ndio maneno yanayotumika zaidi. Lakini je, maneno hayo yanaakisi maana kamili ya kuwa wakili? Muhimu zaidi kwa ajili ya malengo yetu, je, yanaakisi maana ya Kibiblia ya kuwa wakili wa Mungu? Kwa mara nyingine tena hebu tujikite kwenye neno la Mungu ili tujifunze zaidi juu ya lengo la Mungu kwetu kama mawakili!
- Mawakili wa Mwanzo
-
- Soma Mwanzo 1:27. Tunajifunza jambo gani la kupendeza kuhusu wanadamu katika kifungu hiki? (Kwamba Mungu alituumba kwa sura na mfano wake!)
-
-
- Unadhani hiyo inamaanisha nini? Nini umuhimu wake? (Mungu anataka tufanane na yeye. Mungu ametupatia zawadi ya pekee na utambulisho wa pekee.)
-
-
- Soma Mwanzo 1:28. Uhusiano wetu na uumbaji mwingine wote uliosalia ukoje? (Sisi ni watawala juu ya wanyama wote. Tunatakiwa kuitiisha nchi (dunia).)
-
-
- Wangekuwepo wanadamu wangapi kwa mujibu wa mpango wa asili wa Mungu? (Tunaambiwa “kuijaza nchi.”)
-
-
- Soma Mwanzo 1:29-30. Tulikuwa na chakula maalum? (Ndiyo – mboga za majani na matunda.)
-
-
- Je, chakula chetu kilikuwa cha hali ya juu kuliko chakula cha wanyama? (Ndiyo – wanyama walipewa “mimea ya kijani” kwa ajili ya chakula chao.)
-
-
- Hebu tulia kidogo na utafakari nafasi na wajibu ambao Mungu alitupatia. Unavielezeaje? (Mungu alitufanya kuwa watawala wa nchi. Kama jinsi alivyokuwa Mtawala wa Ulimwengu, alitufanya kuwa watawala wadogo juu ya nchi na kila kilichomo.)
-
-
- Je, utauchukulia uwakili huu kama wajibu au upendeleo wa pekee?
-
-
-
- Unapofikiria kuhusu uelewa wa jumla wa kuwa wakili, je, wajibu aliotupatia Mungu unaonekana kuwa mkubwa zaidi? (Nadhani ni mkubwa zaidi. Tunayo mamlaka makubwa na upendeleo mkubwa.)
-
-
- Soma Mwanzo 2:15-17. Hapa tuna majukumu gani ya kiuwakili?
-
-
- Mungu aliweka ukomo kiasi gani kwa kile wanachoweza kula wanadamu?
-
-
- Soma Mwanzo 2:19-20. Hapa tunaona majukumu gani ya kiuwakili?
-
-
- Hii inazungumzia nini juu ya uhusiano kati ya wanadamu na wanyama? (Kumpatia Adamu haki ya kutoa majina inaonyesha kwamba kwa dhahiri alikuwa mtawala wa wanyama.)
-
-
- Hebu tuingize kile tulichokigundua kutoka Edeni kwenye swali la kile ambacho Mungu anatutaka tukifanye kama mawakili. Je, kuwa wakili wa Mungu ndio kazi ambayo ungetaka kuwa nayo – ikiwa tunaweza kuitumia Edeni kama matakwa na maelekezo ya kazi yetu? (Ndiyo!)
-
-
- Unapendelea nini katika kazi ya kuwa wakili wa Mungu? ( Mamlaka. 2. Uhusiano na Mungu – kufanana na Mungu. 3. Mungu haonekani kuhitaji faida kubwa. Kati ya miti yote, tunapata kula katika miti yote isipokuwa miti miwili. Anachoonekana kukihitaji Mungu ni urafiki/ushirika. 4. Tunapata kuishi na kufanya kazi mahali pazuri. Na, kazi yetu ni ya ngazi ya umeneja, si ya kuchosha mwili.)
-
- Uwakili Baada ya Edeni – Fedha
-
- Soma Mwanzo 3:16. Maelekezo ya kazi yamebadilikaje kwa Eva?
-
-
- Je, sehemu ya kazi katika ngazi ya umeneja imebadilishwa? (Adamu aliumbwa kwanza, lakini hapakuwepo na dalili katika maelezo ya uumbaji kwamba hawakuwa sawa. Hata hivyo, Eva hakumtumaini Mungu katika suala la mamlaka yake (angalia, Mwanzo 3:4-6), na baada ya hapo Mungu alipunguza kiwango chake cha mamlaka.)
-
-
-
- Unadhani kwa nini Mungu alikifanya kitendo cha kuzaa kuwa kichungu? (Katika uwezo wake wa kendeleza na kuzaa watu wengine, Eva alikaribia sana kufanana na muumbaji wake, Mungu. Eva hakuamini kwamba Mungu alikuwa amemfanya kufanana naye (angalia, Mwanzo 3:4-6), hivyo Mungu akaufanya wajibu wake kama muumbaji mwenza kuwa jambo asiloweza kulisahau.)
-
-
- Soma Mwanzo 3:17-19. Maelekezo ya uumbaji yamebadilikaje kwa Adamu?
-
-
- Unadhani kwa nini Mungu amefanya kitendo cha Adamu kuzalisha chakula kuwa kigumu sana? Kwa nini hiyo adhabu mahsusi? (Ukiangalia Mwanzo 3:6 na 1 Timotheo 2:14, inaonekana kwamba Adamu alichukua uamuzi wa kumsaidia Eva badala ya kumsaidia Mungu. Hivyo, Mungu akafanya uamuzi kwamba katika siku zijazo, kumsaidia mkewe na familia yake kutamfanya aizingatie njia aliyoichagua.)
-
-
-
- Je, bado unataka kazi ya kuwa wakili? (Bado ni kazi ya kupendeza – Mungu anaonekana kutupatia mamlaka makubwa sana juu ya uumbaji wote uliosalia. Kwa mujibu wa kile tulichokisoma hadi kufikia hapa, Mungu hadai faida ya kifedha katika uwekezaji wake. Anachokitaka tu ni manufaa ya muda (Mwanzo 2:2-3), na kwa kiasi kikubwa manufaa hayo yanaonekana kuwa baraka kwa ajili yetu.)
-
-
- Soma Malaki 3:7-10. Hebu tuchukulie matumizi ya jumla ya matakwa haya kwetu leo. Unafikiria nini, kama wakili, kuhusu “mgawanyiko” kati yako na Mungu? (Hili ni jambo kubwa! Si jambo la kule Edeni kwenye matunda ya miti, lakini bado ni jambo kubwa! Mungu anadai asilimia 10 pekee – nasi tunapata asilimia 90.)
-
- Soma Malaki 3:10-11. Sasa hebu niambie juu ya mtazamo wako wa makubaliano hayo? (Hii inatuahidi kwamba tunarejeshewa “huwezi kuhifadhi vyote” – kwa hakika lazima kurejeshewa huku kuwe ni zaidi ya asilimia 10! Tafadhali naomba unipatie hii kazi ya uwakili! Ama kwa hakika bado hatujajadili kiasi cha dhabihu (sadaka) ambacho hakijabainishwa.)
- Uwakili Baada ya Edeni - Kiroho
-
- Soma Wakolosai 2:2-3. Mungu anataka tuwe na nini? (Kufahamu kwa hakika.”)
-
-
- Kishawishi gani, tena, kiliwasilishwa mbele ya Eva? (Soma tena Mwanzo 3:5 – aliahidiwa maarifa makubwa.)
-
-
-
- Angalia tena Wakolosai 2: Kiini cha kufahamu kwa hakika ni kipi? (Kuelewa siri ya Yesu na kile alichotutendea.)
-
-
-
-
- Je, sisi ni mawakili wa hizo taarifa?
-
-
-
- Soma 1 Wakorintho 4:1-2. Kutokana na kile tulichojifunza, lipi lililo “jambo la siri” la Mungu lililo la muhimu kuliko yote? (Yesu ni nani! Kile alichowatendea wanadamu!)
-
-
- Unadhani inamaanisha nini kuwa “mwaminifu” kwa kile tulichokabidhiwa?
-
-
-
- Unadhani inamaanisha nini kuwa mwaminifu kwa “mambo ya siri ya Mungu?” (Jambo lile lile alilokuwa akilifanya Paulo – kushiriki habari za Yesu na wale ambao hawakumjua.)
-
-
- Soma Mathayo 22:39. Hii inaashiria uwakili wa namna gani? (Tumepewa karama (zawadi) ya kupendwa na Mungu. Tumepewa zawadi ya uzima wa milele kutokana na upendo wa pekee na kafara ya Yesu. Tunapewa wito wa kushiriki upendo huu na watu wengine.)
-
-
- Hapa Mungu anaashiria “mgawanyo” au “mapato” ya aina gani? (Huu unaonekana zaidi kuwa mgawanyo ulio sawa. Tunampenda jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe, sio zaidi na sio kidogo.)
-
-
-
-
- Unadhani Mungu alidhamiria tuweke tarakimu au asilimia kwenye huu mgawanyo? (Hapan Kwa fedha zetu au muda wetu tunaweza kuweka tarakimu. Kwa upendo, hususani aina ya upendo tunaojifunza kwenye “siri ya Mungu” (Yesu), wajibu unaonekana kukamilika kabisa.)
-
-
-
- Soma Waefeso 6:13-17. Aina gani ya uwakili usio wa kifedha unaashiriwa hapa?
-
-
- Kwa nini kumtumia mpiganaji kama kielelezo cha uwakili wetu? (Soma Waefeso 6:11-12. Sisi ni mawakili kwa Bwana ambaye yuko kwenye pambano dhidi ya “nguvu za dunia hii ya giza” na “majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”)
-
-
-
- Ikiwa tupo kwenye pambano, je, hiyo haizungumzii jambo muhimu juu ya namba nadhifu na kamili tulizozijadili hapo awali kuhusu wajibu wetu wa kupewa manufaa ya kifedha na muda? (Wakati fulani, Mungu alitoa namba za kiwango cha chini na kuelezea mfumo wake wa urejeshaji. Lakini, hiyo inaonekana kuakisi sakafu (sio dari) kwa kile ambacho Mungu anakitafuta kwa mawakili wake.)
-
-
- Rafiki, Mungu ametupatia kazi kubwa! Kama mawakili wake, tunayo mamlaka makubwa na fursa kubwa. Mungu hatarajii tupate manufaa makubwa kwa vigezo vya kifedha kutokana na uwakili wetu. Hata hivyo, anatarajia kwamba tutaakisi upendo wake na tutasalia kuwa waaminifu kwake. Je, utakubali, sasa hivi, kazi ya Mungu?
- Juma lijalo: Sifa (Alama) za Wakili.