Baraza la Yerusalemu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Matendo 15)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
3
Lesson Number: 
8

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Nyakati zinabadilika, lakini Mungu habadiliki. Je, kanisa linaruhusiwa kurekebisha au kuzikataa amri za Mungu? Jibu langu la dhahiri ni “Hapana!” Lakini, somo letu juma hili linaonesha kuwa jibu la dhahiri la “Hapana!” haliwezi kuwa sahihi mara zote. Hilo linamfanya kila mwanafunzi makini wa Biblia awe na dukuduku kidogo kwa sababu linahamisha msingi wa imani zetu kutoka kwenye mwamba wetu thabiti wa Biblia. Isipokuwa kwa jambo hili: Biblia ndio inayoashiria kuwa sheria zinaweza kubadilika. Hebu tuzame kwenye somo hili muhimu la Biblia na tuone kama tunaweza kuyaelewa kwa usahihi mapenzi ya Mungu!

 

 

  1. Tatizo

 

    1. Soma Matendo 15:1. Je, hii kauli ni ya kweli? Kumbuka kwamba katika kipindi hiki Biblia ilikuwa na Agano la Kale pekee. (Soma Mwanzo 17:9-10 na Mwanzo 17:12-14. Hii inabainisha dhahiri kwamba tohara inahusika kwa wageni na wasio “uzao” wa Ibrahimu. Kifungu kinasema kuwa watakaoshindwa kutahiriwa “watatengwa na watu wake” kwa sababu “wamevunja” agano na Mungu.)

 

    1. Soma Matendo 15:2. Kwa nini Paulo na Barnaba wasikubaliane na kauli hii ya dhahiri ya Biblia? (Kwangu hili linaonekana kama tatizo halisi. Tumejifunza kwamba kuwaokoa Mataifa ilikuwa ni mpango wa Mungu. Majuma mawili yaliyopita tulijifunza kuhusu Kornelio na nyumba yake kukubaliwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hakuna hata sehemu moja kwenye matukio yote hayo ambapo Roho Mtakatifu amezungumza kinyume na tohara. Hivyo, kipingamizi halisi ni kwamba kinaifanya kazi ya kuwaongoa Mataifa iwe ngumu zaidi.)

 

    1. Soma Matendo 15:3. Kwa nini Paulo na Barnaba wanasafiri kwenda Yerusalemu? (Wao ni mawakili wa Mataifa na wanapingana na tohara. Wanaelekea Yerusalemu kwa kuwa huko ndipo yalipo makao makuu ya kanisa. Ndiko walipoishi “mitume na wazee.” Lengo la hii safari ni kuwauliza kuhusu swali hili.)

 

      1. Kwa nini wauendee uongozi wa kanisa kufanya mashauriano (kuuliza) wakati Biblia iko wazi kwenye suala hili? (Kwa dhahiri, Paulo na Barnaba na waumini wa Antiokia hawakulitazama jambo hili kwa namna hiyo.)

 

      1. Ikiwa Paulo na Barnaba, na viongozi waliopo Antiokia, wana uhakika na mtazamo wao kuhusu tohara, kwa nini kuwasilisha suala hili kwa uongozi kule Yerusalemu?

 

  1. Makao Makuu ya Kanisa

 

    1. Soma Matendo 15:4. Uongozi unawapokeaje Paulo na Barnaba? (Unaonekana kuwa ukaribisho mzuri.)

 

    1. Soma Matendo 15:5. Kwa nini inaonekana kwamba Mafarisayo walioongoka pekee ndio wanaounga mkono torati? (Habari njema ni kwamba suala hili linazileta pamoja pande mbili kwa ajili ya mazungumzo. Habari mbaya ni kwamba hii inaashiria kuwa uongozi wa kanisa la awali haukuwa ukiunga mkono mtazamo wa tohara. Ninasema “habari mbaya” kwa sababu kundi linalounga mkono tohara linaonekana kuungwa mkono na Biblia.)

 

  1. Kuuchunguza Ushahidi wa Kibiblia

 

    1. Soma Yeremia 9:25-26. Jambo gani linamfikirisha Mungu hapa? (Watu wake wametahiriwa katika miili, na si kutahiriwa mioyo.)

 

      1. Je, hii inamaanisha kuwa tohara halisi haitoshi? (Ndiyo.)

 

      1. Je, hiyo inamaanisha kuwa tohara halisi si ya muhimu? (Haimaanishi hivyo. Badala yake, hitimisho lenye mantiki ni kwamba lazima mtu atahiriwe katika yote mawili, kimwili na kutahiriwa moyoni.)

 

    1. Soma Warumi 4:8-10. Hii inatuambia nini kuhusu kuokolewa? (Kwamba tohara si muhimu kwa ajili ya wokovu.)

 

      1. Kimsingi Paulo ni sehemu ya kundi la watu katika Matendo 15 wanaojenga hoja dhidi ya tohara!

 

    1. Soma Warumi 4:11-12. Tohara ni ishara ya nini? (Haki kwa imani.)

 

      1. Tuchukulie kwamba Paulo yuko sahihi kabisa kuhusu kipindi cha haki ya Ibrahimu na tohara yake. Tukubaliane kwamba Ibrahimu alitangazwa kuwa mwenye haki licha ya tohara. Ikiwa hakupitia njia ya tohara, je, Mwanzo 17 inasema kuwa jambo gani linapaswa kutokea? (Ibrahimu anapaswa “kutengwa” kama mtu asiye kwenye uhusiano wa agano na Mungu.)

 

      1. Baadhi ya watu wanajenga hoja kwamba kuwa kwenye uhusiano wa agano na Mungu ni tofauti na wokovu. Lakini, kama hilo ni kweli, kwa nini Mwanzo 17:14 inasema kuwa matokeo ya kushindwa kutahiriwa ni kwamba “unatengwa” na Mungu? Hilo linaweza kuelewekaje kwa namna nyingine tofauti na kupoteza wokovu?

 

    1. Hadi kufikia hapa unawezakuwa unauliza, “Bruce,unajenga hoja juu ya nini? Agano Jipya liko wazi kwamba tohara haihitajiki!” Lengo langu ni kukufanya uhitimishe kwamba tohara inahitajika, siamini kama inahitajika. Lengo langu ni kukufanya uone kwamba hoja ya Biblia juu ya Mafarisayo waongofu wanaoshadadia tohara ina nguvu, wakati hoja kinzani ni dhaifu tunapoangalia Agano la Kale pekee. Kwa nini hilo ni muhimu? (Hitimisho lisiloepukika kwangu, suhulisho nililolipenda sana, ni kwamba hoja madhubuti ya Biblia haipaswi mara zote kutatua swali.)

 

      1. Ikiwa hoja madhubuti ya Kibiblia haipati mashiko, tufikieje basi suluhisho la migongano muhimu kanisani leo? Hebu tuangalie jambo hilo katika sehemu inayofuata.

 

  1. Uamuzi

 

    1. Soma Matendo 15:6-9. Petro anajenga hoja gani katika kuipinga tohara? (Roho Mtakatifu amebainisha wazi kwamba Mataifa wanakubaliwa na Mungu.)

 

      1. Je, hilo ndilo swali? (Hapana. Suala ni endapo, baada ya Mataifa kuwa Wakristo, lazima pia watahiriwe?)

 

    1. Soma Matendo 15:10-11. Hapa Petro anajenga hoja gani? (Kwanza anajenga hoja kuwa tohara ni mzigo, nira. Hiyo ndio hoja halisi tuliyoijadili hapo awali.)

 

      1. Je, amri ya Mungu inapaswa kupuuziwa kwa kuwa tu ni mzigo?

 

    1. Hebu tuangalie tena Matendo 15:11. Hapa Petro anajenga hoja gani mpya, na inahusikaje na suala la mzigo? (Petro anajenga hoja kwamba Yesu analeta utofauti. “Mzigo” hauwezi tu kuwa tohara kirahisi namna hiyo, kwa kuwa Wayahudi walikuwa wametahiriwa. Sheria ndio iliyokuwa mzigo.)

 

      1. Hili jambo ni la muhimu sana kiasi kwamba hatutakiwi kutolielewa vizuri. Yesu analetaje utofauti? Anabatilishaje maelekezo ya moja kwa moja ya Mungu? (Yesu alitimiza matakwa ya sheria kwa niaba yetu. “Twaamini kwamba tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Yesu.”)

 

    1. Kabla hatujaendelea na hoja zilizotolewa dhidi ya tohara kwenye huu mkutano wa Matendo 15, elezea jinsi hoja hii kuhusu neema inavyotumika kwenye amri nyingine za Mungu? (Kamwe hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa kile alichotutendea Yesu pekee.)

 

      1. Bado suala hili linaacha swali kuhusu jinsi tunavyopaswa kuishi. Mataifa hawakuhitajika kutahiriwa ili waweze kuokolewa. Lakini je, wanatakiwa kutahiriwa kama kitendo cha utii kwa Mungu? Kama hawatakiwi kufanya hivyo, je, kanisa linapaswa kuacha kujenga hoja za kutetea amri nyingine za Mungu? (Kwa kuangalia suala hili katika mtazamo wetu wa sasa, tunajumuisha Agano Jipya kwenye Biblia. Ni dhahiri kwamba ubatizo, na si tohara, ndio ishara mpya ya uhusiano wetu na Mungu. Wakolosai 2:11-12.)

 

      1. Mojawapo ya masuala yenye changamoto kubwa leo kwenye Kanisa la Kikristo ni ngono za jinsia moja. Wale wanaoamini kwamba wao ni wasenge watajenga hoja kwamba kuachana na uhusiano wa kingono ya jinsia moja ni mzigo mkubwa – huenda mkubwa kuliko tohara. Je, kanisa linapaswa kuliangalia jambo hili kama linavyoiangalia tohara? (Sidhani. Sababu kubwa ni kwamba mahusiano ya kibasha (kisenge) sio tu kwamba yanalaaniwa katika Agano la Kale (Mambo ya Walawi 20:13), lakini pia katika Agano Jipya (Warumi 1:24-27) – hata baada ya msalaba, baada ya kifo na ufufuo wa Yesu. Hata hivyo, kama ilivyo kwa tohara, ni kweli kwamba hakuna anayeokolewa kwa kuachana na ngono ya jinsia moja. Hiyo “kazi” ya kuacha jambo fulani inastahili zaidi kuliko kazi nyingine yoyote ile linapokuja suala la kuokolewa kwa matendo yetu.)

 

    1. Soma Matendo 15:13-18. Yakobo anajenga hoja gani dhidi ya kundi linalounga mkono tohara? (Anajenga hoja ya Kibiblia. Anasema kuwa injili inayokwenda kwa Mataifa ni utimilifu wa unabii. Anabainisha kuwa miujiza inayotendwa miongoni mwa Mataifa iliyotaarifiwa na Barnaba na Paulo inathibitisha jambo hili.)

 

    1. Rafiki, ushauri (maoni) wa viongozi wa mwanzo wa Kanisa ulikuwa ni kuwaweka huru Mataifa dhidi ya wajibu wa kutahiriwa. Tunajifunza nini leo kutokana na hilo? (Tunatakiwa kutafakari mabishano yanayotokea kanisani kwa umakini mkubwa. Kwa kuwa tu kundi moja linatumia kauli ya dhahiri ya “asema Bwana” si mwisho wa mjadala. Tunatakiwa kuona mahali ambapo Roho Mtakatifu anatuelekeza. Tunatakiwa kuangalia kwa ukamilifu jinsi Biblia inavyolizungumzia jambo linalohusika. Tunatakiwa kukiri kwamba sisi sote tunaokolewa kwa neema pekee.)

 

      1. Je, uko pamoja na jambo hili?

 

Juma lijalo: Safari ya Pili ya Kimisionari.