Msingi wa Umoja

(Waefeso 4, Warumi 14)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
4
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Kutokuwepo kwa umoja kunaweza kuleta maumivu! Katika mkutano wa makambi mwishoni mwa juma lililopita, rafiki wangu alinirushia mpira. Nilikimbia ili kuudaka, na mara nilipokuwa ninajiandaa kuushika kwa mikono, mguu wangu ulinasa ardhini. Badala ya kuangukia uso, nilitegesha bega, nikaanguka chini, nikabiringika na kusimama – bado nikiwa nimeushika mpira. Lilikuwa jambo zuri sana kwa mtu mzee kama mimi. Lakini, palikuwepo na hitilafu ya umoja. Mguu wangu uliniangusha, na bega langu la kushoto lilipitia uzoefu wa nguvu isiyo ya kawaida isiyohusiana na suala la kuchapisha maneno kutumia bao bonye (keyboard)! Usiku ule ulikuwa mchungu! Bado napitia uzoefu wa matokeo mabaya yaliyotokana na tukio lile. Hebu tuchimbue kile Biblia inachotufundisha kuhusu umoja katika mwili wa Kristo!

 

 1.    Upole, Unyenyekevu, Upendo

 

  1.    Soma Waefeso 4:1. Mfungwa ni nani? (Paulo! Katika mfululizo wetu wa masomo uliopita kwenye kitabu cha Matendo tulijifunza jinsi Paulo alivyowekwa kizuizini mara kwa mara kule Rumi. Kitabu cha Matendo kiliishia kwa Paulo kuwa kizuizini.)

 

  1.    Soma Waefeso 4:2. Ni kwa jinsi gani kuwa mtumwa kunakufanya uwe mpole na mvumilivu?

 

   1.    Paulo anasema kuwa jambo gani linapaswa kuwafanya wasomaji wake wawe na “unyenyekevu wote na upole” na “wavumilivu?” (“Kuchukuliana kwa upendo.” Paulo anatuambia kuwa hili linaendana na kuishi maisha “yanayostahili wito tulioitiwa.”)

 

   1.    Hebu tuchimbue jambo hili. Upendo unakufanyaje kuwa mnyenyekevu, mpole na mvumilivu?

 

   1.    Katika makuzi yangu, wazazi wangu walilalamika kwamba niliwatendea vyema marafiki na wageni kuliko nilivyowatendea wanafamilia wangu. Kwa kuwa naijua familia yangu, sikupaswa kuwa kwenye ubora wa tabia yangu. Hivyo, nilikuwa na unyenyekevu, upole na uvumilivu mdogo kwa wale niliowapenda! Je, hilo ni kweli kwako pia? (Ikiwa ni kweli, basi huenda ilithibitisha kuwa upendo wa wazazi wangu ulivumilia tabia yangu mbaya.)

 

   1.    Binafsi ninaona kwamba unapompenda mtu, unayafikiria mambo mema kwake. (Unataka kuendeleza uhusiano wenu, hivyo unakuwa mvumilivu zaidi, mpole na mnyenyekevu kuliko vile unavyokuwa na wageni kabisa.)

 

  1.    Soma Waefeso 4:3. “Umoja wa Roho” ni nini? (Huyu ni Roho Mtakatifu. Huu ni umoja unaotokana na Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu.)

 

  1.    Soma Waefeso 4:4-6. Kwa nini umoja ni matokeo ya Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu? (Paulo anabainisha kuwa mambo kadhaa tofauti-tofauti yanatufanya tuwe wamoja katika Roho Mtakatifu. “Mambo” haya yana mtazamo mmoja. Lakini zaidi ya hayo, tunaunganishwa na Mungu “aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”)

 

   1.    Hebu tujiulize maswali magumu. Je, hivi ndivyo vigezo ambavyo Roho Mtakatifu analeta umoja – ubatizo, Utatu, na Ukristo? Ikiwa ndivyo, je, tunaweza kutokubaliana kwenye masuala mengine? (Ukitafakari nyuma kuhusu somo letu la hivi karibuni la Kitabu cha Matendo, utakumbuka mkutano uliobainishwa kwenye Matendo 15 ambapo kanisa lilikutana kutatua suala la tohara kwa Mataifa. Huo ulikuwa mtafaruku mkubwa katika kanisa la awali.)

 

    1.    Je, tohara inabainishwa kwenye vifungu hivi kama jambo ambalo Mungu analeta umoja? (Hapana. Hiyo inaniongoza kuhitimisha kwamba Roho Mtakatifu anapaswa kuleta umoja kwenye mambo tofauti na yale yaliyobainishwa kimahsusi.)

 

  1.    Hebu turukie chini na tusome Waefeso 4:11-13. Je, tunaweza kuona baadhi ya vipengele vya kanisa ambavyo hatupaswi kutegemea umoja? (Hatuunganishwi sote kwenye matabaka ya kazi zetu. Tunafanya kazi pamoja, lakini si kila mmoja, kwa mfano, “anapewa” kazi ya uchungaji.)

 

   1.    Tunaelezeaje aina hii ya umoja? (Tuna kazi na nafasi tofauti tofauti kanisani, lakini tunafanya kazi pamoja. Paulo anaelezea mahali pengine kwamba huu ni sawa na umoja kwenye mwili wa mwanadamu. Angalia 1 Wakorintho 12.)

 

   1.    Eneo gani mahsusi la umoja linatajwa? (“Umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu.”)

 

    1.    Je, hiyo inamaanisha kuwa tunaweza tusikubaliane kwenye baadhi ya maeneo, kama vile nani anapaswa kuwa mchungaji?

 

   1.    Hebu tuangalie tena kauli ya kufurahisha sana katika Waefeso 4:13. “Tutakuwa wakomavu.” Ukiongezea ukomavu kwenye unyenyekevu, uvumilivu, upendo na upole, je, bado mifarakano itakuwepo? (Hiyo inapunguza uwezekano wa mifarakano. Nadhani mantiki ya Kiyunani “imekamilika.” Hivyo, “ukomavu” sio tu jambo la mtazamo, ni kuongezeka kwa uelewa wa mapenzi ya Mungu.)

 

   1.    Kanisani kwangu leo kuna ukinzani juu ya uamuzi wa mchungaji gani anaweza kuwekewa mikono. Niko mbali na ukweli kwamba kila lililoandikwa kuhusu mada hii linaakisi unyenyekevu au ukomavu. Unadhani unyenyekevu unawezaje kusaidia kutatua tatizo hili? Je, inamaanisha kuwa mara zote mshiriki wa kanisa anapaswa kutii mamlaka kamili ya kanisa? Je, hicho ndicho unyenyekevu unachokihitaji?

 

 1.   Uanuwai na Umoja

 

  1.    Soma Warumi 14:1-4. Ni kwa jinsi gani unyenyekevu na upendo unawajibika kwenye “masuala yenye mgogoro?” (Tusiwadharau wale tusiokubaliana nao. Sisi sote ni watumishi wa Mungu, na Mungu pekee ndiye anayeweza kuwahukumu watumishi wake.)

 

  1.    Soma Warumi 14:13-18. Umoja unahifadhiwaje kwenye mazingira ambayo tuna mgogoro wa dhahiri kuhusu uhalali wa chakula fulani? (Kila mtu anatakiwa kufanya uamuzi wake mwenyewe.)

 

  1.    Soma Warumi 14:22-23. Paulo anapendekeza kwamba tuuendelezeje umoja? (Kwa kubaki na mawazo yetu nafsini mwetu!)

 

   1.    Unawezaje kutimiza hilo? Tabia gani itahitajika? (Kwa dhahiri utahitajika unyenyekevu! Mtu mwenye majivuno atakuwa na uhakika wa kuelezea kile anachokiamini. Upendo ni kizuizi cha kuelezea mawazo yako. Roho Mtakatifu atabadili mioyo yenu.)

 

   1.    Je, Paulo anatuomba tutoe mawazo yetu? (Hapana. Hatuambii tukubaliane na kile watu wote wanachokubaliana nacho. Badala yake, anasema kuwa baki na mawazo yako nafsini mwako.)

 

  1.    Je, wazo hili la kwamba sote tunaweza kuwa na mawazo tofauti, lakini tuna umoja kwa sababu tunafunga vinywa vyetu, ni sehemu ya muhimu ya jibu kwa umoja wa kanisa? (Soma tena Warumi 14:1. Linatakiwa kuwa suala “lenye mgogoro.” Sidhani kama hiyo inamaanisha kuwa kila mgogoro unapozuka tunatakiwa kufunga vinywa vyetu. Badala yake, nadhani wazo hilo linazungumzia suala ambalo Biblia hailizungumzii kwa wazi.)

 

 1. Familia ya Kanisa

 

  1.    Soma Waefeso 5:21. Hii inafanyaje kazi? Umewahi kupitia uzoefu wa “kumnyenyekea” mtu mwingine kwenye makutano ya barabara, au wakati ukitembea ukumbini, na kuwa wapole ikamaanisha kuwa hakuna yeyote kati yenu aliyeweza kupiga hatua? Mimi na mke wangu tunafanya hivi mara zote tunapokuwa tunapata chakula. Tunatofautiana kwenye kile akipendacho mwingine. (Kiuhalisia, hamuwezi kuwa na ukubali wa pamoja la sivyo tutabaki na njaa, au kamwe hatutaweza kuvuka kwenye makutano ya barabara. Lazima Paulo atakuwa anazungumzia kuhusu mtazamo.)

 

  1.    Soma Waefeso 5:22-24. Je, hii inafafanua Waefeso 5:21? Je, inamaanisha kuwa waume na wake wanyenyekeane, lakini ili kuhakikisha kwamba kweli tunakula, ninachukua uamuzi wa mwisho?

 

  1.    Soma Waefeso 5:25-27. Tunahitaji mjadala kuhusu maana ya Paulo kuhusu kunyenyekea. Ikiwa waume wanatakiwa kuwa kama Yesu alivyokuwa kwetu, hiyo inamaanisha kuwa waume wanatakiwa kuwapendelea wake zao zaidi ya kujipendelea wao wenyewe maishani mwao. Hiyo ni maana isiyo ya kawaida ya kunyenyekea. Naweza kusema kuwa Yesu alijitoa kwetu, na si kinyume chake. Unasemaje?

 

  1.    Soma Waefeso 5:28. Mojawapo ya fundisho la muhimu kabisa la Kibiblia kuhusu ndoa linapatikana hapa: “Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.” Je, tunaweza kutafsiri jambo hili katika kutatua mifarakano ya kanisa? “Ayapendaye mamlaka ya kanisa hujipenda mwenyewe?” Au, je, inapaswa kuwa “Aupendaye umoja wa kanisa hujipenda mwenyewe?” Dhana iliyopo ni kwamba kunyenyekea huleta baraka. Je, hiyo ni sahihi?

 

  1.    Soma Waefeso 5:29-33. Je, inaonekana ajabu kwako kwamba lazima mume “ampende” mke wake, na kwamba lazima mke “amstahi” muwe wake? (Binti wangu anazungumzia jambo hili – anataka mume ambaye anaweza kumtii. Kama unampenda mumeo, lakini unadhani kuwa yeye ni zuzu, uwezekano wa ndoa yako kuwa njema ni mdogo. Ama kwa hakika, unapaswa kuepuka kuoa au kuolewa na mtu yeyote usiyemheshimu, kutokana na kunyenyekeana ambako Paulo anakushadadia.)

 

   1.    Utaona kwamba kifungu cha 32 kinaita jambo hili “siri kubwa.” Hiyo inaashiria nini kuhusu uelewa wetu wa kunyenyekea kwenye ndoa na kanisani? (Inamaanisha kuwa suala linatatiza.)

 

  1.    Rafiki, ikiwa umoja kanisani una utata, je, utamwomba Roho Mtakatifu akupatie karama za unyenyekevu, upendo na uvumilivu ili uweze kuelewa jinsi tunavyopaswa kujitoa ili kuutimiza umoja?

 

 1.   Juma lijalo: Uzoefu wa Umoja Katika Kanisa la Awali.