Somo la 7: Baragumu Saba

Error message

 • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
 • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 8-11
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
1
Lesson Number: 
7

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Juma hili tunaingia kwenye mhuri wa saba! Katika Ufunuo 6 tuliona kwamba Yesu alifungua mihuri sita ya kwanza. Juma lililopita, katika Ufunuo 7 tulijifunza juu ya watu wa Mungu waliotiwa mhuri. Waliotiwa mhuri ni wale waliochagua kumfuata Yesu. Juma hili Yesu anatufungulia mhuri wa saba ili tuweze kuujifunza. Kwa nini Mungu anatupatia taarifa kwa kufuata mpangilio huo? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kama tunaweza kupata jibu la swali hilo na tufumbue maana ya mhuri wa saba na baragumu saba!

 

 1.    Mhuri wa Saba, Baragumu Saba

 

  1.    Soma Ufunuo 8:1. Unadhani kwa nini kuna ukimya mbinguni kwa muda wa nusu saa mara mhuri wa saba ulipofunguliwa? (Tutajifunza kwamba unahusisha mambo ya kutisha. Huenda mbingu zimeshtuka kwa uelewa huu.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:2. Ni wapi hapo awali tuliwaona malaika saba? (Soma Ufunuo 1:20. Hawa malaika saba walikuwa na ujumbe maalumu kwa makanisa saba.)

 

   1.    Baragumu saba ni kitu gani? (Soma Ufunuo 1:10. Sauti ya Yesu inafanana na baragumu. Hii inaashiria kwamba kila mmojawapo ya malaika saba ana ujumbe aliopewa na Mungu.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:3. Uvumba unawakilisha nini? (Maombi ya watakatifu.)

 

   1.    Unadhani kwa nini hilo limebainishwa kwa umahsusi? (Kwenye mhuri wa sita tuliishia kwenye habari ya waovu kujificha kwenye mapango (Ufunuo 6:15-17), kwa kuwa waliamini mwisho wa dunia ulikuwa umekaribia. Wenye haki, kinyume chake, wanayapeleka maombi kwa Mungu ili awalinde kwenye hizi nyakati za kutisha.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:4-5. Kwa nini kutupa juu ya nchi chetezo chenye uvumba, kinachohusisha maombi yetu? (Kitabu cha robo hii kinanukuu maoni ya Kiyahudi kuhusu huduma za hekaluni. Mwisho wa huduma ya kafara ya kila siku kuhani alichukua uvumba na kuutupa ardhini, ambapo makuhani saba walipuliza baragumu saba.)

 

   1.    Chukulia kwamba hilo ni sahihi. Kwa nini tuwe na ishara hiyo katika kipindi hiki cha njozi ya Yohana? (Kwa kuwa tulijadiliana kwamba wafuasi wa Mungu walitiwa mhuri katika sura ya mwisho ya kitabu cha Ufunuo, hii inaweza kuonesha kufungwa kwa mlango wa rehema. Kafara zimekwisha. Wanadamu ama wanaokolewa kwa neema au wamehukumiwa kwa matendo yao.)

 

 1.   Baragumu

 

  1.    Soma Ufunuo 8:6-7. Mvua ya mawe na moto ni muunganiko usio wa kawaida. Hii inaashiria nini? (Soma Kutoka 9:25-26. Hii inaashiria kwamba hii ni hukumu kutoka kwa Mungu.)

 

   1.    “Vilivyotangamana na damu” inatuambia nini? (Watu wanakufa kutokana navyo.)

 

   1.    Matokeo yake duniani ni yapi? (Theluthi ya nchi imeteketea.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:8-9. Kwako jambo hili linafanana na nini? (Volkano kubwa inalipuka ikiwa na madhara makubwa sana.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:10-11. Kwako jambo hili linafanana na nini? (Hili ni anguko la kimondo kikubwa! Kinayatia maji sumu.)

 

  1.    Soma Ufunuo 8:12. Nini kimetokea hapa? (Sehemu ya jua letu inazima. Kwa kuwa jua hutoa mwanga kwa ajili ya mwezi, matokeo yake ni kwamba mwanga wa mwezi pia umepungua.)

 

   1.    Utakumbuka kwamba tumeona rejea nyingine kwenye Ufunuo kuelezea ishara za mambo yasiyokwenda sawa katika anga na sayari zake. Huu ni mfano mwingine.

 

  1.    Soma Ufunuo 8:13. Je, hii inaonekana kana kwamba mambo yatakuwa mazuri? (Hapana! Mtoa maoni mmoja aliziita baragumu tatu zinazofuata kuwa “baragumu za ole.”)

 

  1.    Soma Ufunuo 9:1-4. Hebu tuliangalie hili. Hii inaonekana kama anguko jingine la kimondo. Lakini, kwa nini kimondo kipewe ufunguo? (Soma Isaya 14:12 na Luka 10:16-18. “Nyota” iangukayo kutoka mbinguni ni Shetani. Sidhani kama hiki ni kimondo.)

 

   1.    Soma Ufunuo 20:1-3. Shetani anahusikaje na “kuzimu?” (Shetani anakaa kuzimu kwa muda wa miaka elfu moja.)

 

   1.    Soma Ufunuo 20:7-8. Ilinganishe na Ufunuo 9:2-4. Je, maelezo haya ya aina mbili tofauti yanafanana?

 

   1.    Angalia tena Ufunuo 9:4. Rejea ya “mhuri” inatuambia nini kuhusu muda wa jambo hili? (Inafuata maelezo ya Ufunuo 7, na hiyo inaniambia kuwa inafuata kufungwa kwa mlango wa rehema.)

 

    1.    Soma Kutoka 9:26. Hii inatuambia nini kuhusu mapigo ya Misri? (Si yote yaliwatesa watu wa Mung.)

 

  1.    Soma Ufunuo 9:4-6. Nani anayewatesa wale wasio na mhuri wa Mungu? (“Nzige wa moshi” watokao kuzimu. Hii inaonekana kama vile ni malaika walioanguka – wale waliomchagua Shetani kama kiongozi wao.)

 

  1.    Soma Ufunuo 9:7-11. Unahitimisha nini kutokana na ukweli kwamba hawa nzige wa moshi/nge wana sura zinazofanana na wanadamu na “mfalme” wao ni “malaika wa kuzimu?” (Hii ni dalili nyingine kwamba hawa ni malaika walioanguka.)

 

  1.    Soma Ufunuo 9:12-17. Utakumbuka kwamba hawa ni wale wasiotiwa mhuri. Wanakufaje? (Kwa “moto, moshi na kiberiti.”)

 

   1.    Soma Ufunuo 20:9-10. Hawa maadui wa Mungu wanakufaje? (Kwa moto na kiberiti.)

 

  1.    Soma Ufunuo 9:20-21. Waovu waliosalia wanaathirikaje na haya mapigo ya kutisha? (Wanaendelea na matendo yao maovu, kana kwamba hakuna kilichotokea.)

 

 1. Kitabu

 

  1.    Soma Ufunuo 10:1-4. Hapo kabla tulimwona nani akiwa ameshikilia kitabu? (Ufunuo 5 & 6 inasimulia kwamba Yesu alifunua gombo. Maelezo haya yanaonekana kana kwamba huyu ni Yesu.)

 

  1.    Soma Ufunuo 10:5-7. Baragumu ya saba ni ipi? (Ni hitimisho kwenye pambano kati ya wema na uovu.)

 

  1.    Soma Ufunuo 10:9-11 na uilinganishe na Ezekieli 2:9-3:3. Inamaanisha nini “kula” gombo? (Inamaanisha kula kile ambacho Mungu amekielezea na kisha kukishiriki na watu wengine.)

 

   1.    Kwa upande wa Yohana, ulaji ni mtamu, lakini gombo linabadilika na kuwa chungu mdomoni mwake. Yesu aliutazamaje ufunuaji wake wa gombo lililotiwa mhuri? (Mbingu yote ilifurahi!)

 

    1.    Unadhani Yohana anazitazamaje baragumu? (Yohana anaelezea nyakati za kutisha.)

 

 1.   Mashahidi wawili

 

  1.    Soma Ufunuo 11:1-2. Je, hii inaonekana kama mwendelezo wa Ufunuo 9-10? (Hapana. Sura hizo zinaonekana kama mwisho wa dunia. Hii inaonekana kama maelezo ya hekalu la duniani.)

 

  1.    Soma Ufunuo 11:3. Katika kifungu cha 2 na 3 tunaona rejea ya “miezi 42” na “siku 1,260.” Hizi ni nyakati zinazofanana. Unadhani jambo hili ni la kiishara? (Kipindi hiki kinachofanana pia kinapatikana katika Danieli 12:7, Ufunuo 12:6 na Ufunuo 12:14.)

 

   1.    Soma tena Danieli 7:25 na Danieli 12:7. Ikiwa “wakati” ni mwaka, basi hii ni miaka 3.5, au siku 1,260. Unadhani hii inazungumzia siku halisi? (Soma Daniel 12:9. Danieli anaambiwa kuwa huu ni unabii utakaoeleweka katika siku za mwisho. Ikiwa ilimaanisha tu “siku,” basi mara moja maana itakuwa dhahiri.)

 

  1.    Soma Ufunuo 11:3-4 na Ufunuo 11:7-11. Kwa ujumla, kipindi cha miaka 1,260 kinawakilisha kipindi cha magumu kwa watu wa Mungu. Mashahidi hawa wawili ni akina nani ambao pia wanaitwa mizeituni miwili na vinara viwili? Wanatoa ushuhuda kwa Mungu katika kipindi kigumu, wanauawa kisha wanafufuliwa. (Ikiwa kipindi hiki kinawakilisha zaidi ya miaka elfu moja, basi hawa si wanadamu. Kuwaita “mizeituni” na “vinara” inaashiria zaidi kwamba wao si wanadamu. Hata hivyo, rejea ya Ufunuo 11:8 kuhusu “mizoga yao” inaonekana kama vile wao ni wanadamu. Wanasheria wanarejea “mwili wa sheria,” hivyo imani kwamba mashahidi wawili ni Agano la Kale na agano Jipya la Biblia inaleta mantiki. Shetani anaendeleza vita ya kutisha dhidi ya imani kwa neno la Mungu.)

 

  1.    Rafiki, mwisho wa nyakati umefunuliwa kwako ili uweze kuupitia. Je, ungependa kuyaepuka mapigo haya na mauti ya milele? Kwa nini usichague upande wa ushindi sasa hivi kwa kuutoa moyo wako kwa Yesu?

 

     Juma lijalo: Shetani, Adui Aliyeshindwa.