Hukumu Dhidi ya Babeli

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ufunuo 17)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
1
Lesson Number: 
12

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Tulipojifunza kitabu cha Ufunuo 16 juma lililopita tulimaliza kwa maadui wa Mungu kukusanyika kwa ajili ya Pambano la Har-Magedoni. Juma hili tunatambulishwa mhusika mpya, “kahaba mkuu.” Vita na ngono, hii inaanza kuonekana kama kitabu cha riwaya cha kisasa. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi juu ya kile anachokifikiria Mungu kwa ajili ya mustakabali wetu!

 

  1.    Kahaba Mkuu

 

    1.    Soma Ufunuo 17:1-2 na Ufunuo 14:8. Kwa dhahiri kahaba mkuu si mwanamke mwema. Unadhani anawakilisha nini? (Anaonekana kufanana na Babeli Kuu. Kwa dhahiri haya ni mamlaka dhidi ya watu wa Mungu.)

 

      1.    Unadhani kubainishwa kwa jinsi yake kunatuambia jambo gani? (Hapo awali tulihitimisha kwamba mwanamke wa Ufunuo 12:1 alikuwa kwenye kundi linalomfuata Yesu. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa kwamba kahaba huyu anawakilisha mamlaka ya dini inayopingana na Mungu.)

 

      1.    Kifungu kinapobainisha kwamba kahaba mkuu anaketi juu ya maji mengi, hiyo inamaanisha nini? (Soma Ufunuo 17:15. Utakumbuka kwamba hapo awali tulijadili suala hili. “Maji mengi” yanamaanisha watu na “nchi” inamaanisha mahali wasipokaa watu. Haya ni mamlaka ya kidini yanayotenda kazi kwenye eneo lililojaa watu wengi.

 

      1.    Kahaba ana uhusiano gani na mamlaka za kidunia? (Amewavuta kwenye mtazamo wake. “Wamezini.” Hii inamaanisha kwamba hawana uaminifu kwa Mungu. “Mtu wa kawaida mtaani” pia ametekwa naye kwa sababu “amelevywa” kwa “mvinyo” wake. Hivyo, viongozi wa kidunia na watu wote kwa ujumla wanakubaliana na mtazamo wake wa kuwa kinyume na Mungu.)

 

    1.    Soma Ufunuo 17:3-4. Kwa nini usafiri jangwani (au nyikani) ili kumwona mwanamke aketiye juu ya maji mengi? (Unakumbuka mnyama wa baharini mwenye Pembe Kumi na mnyama aketiye juu ya nchi wa Ufunuo 13? Hii inaweza kuuzungumzia uhusiano wao, au inaweza kutuambia kwamba mwanamke anatenda kazi nje ya eneo lake la kawaida.)

 

      1.    Kahaba Mkuu anaonekanaje? (Mwenye mvuto! Tajiri! Anavaa mavazi yenye rangi za kifalme. Ana mapambo ya vito mengi yaliyo ghali na anatumia kikombe cha gharama kubwa kunywea. Kwa dhahiri ana fedha nyingi.)

 

      1.    Je, anapaswa kutembea kwa miguu ili kufika sehemu mbalimbali? (Hapana, anatumia mnyama mwekundu kusafiri.)

 

        1.    Je, tumeona safari yake kwa kutumia mnyama mwekundu hapo awali? (Hapana! Hii inaonekana kabisa kama “Pembe Kumi” za kale, Mnyama wa Baharini wa Ufunuo 13.)

 

        1.    Tulipojifunza Pembe Kumi katika Ufunuo 13, tulihitimisha kwamba iliwakilisha Rumi ya Kipagani na Kipapa. Nikapendekeza kwako kwamba Mnyama wa Nchi Kavu wa Ufunuo 13 kwa pamoja aliwakilisha mamlaka za Kiislamu, wapagani, na Wakrisho (nchini Marekani na kwingineko) ambao hawakujifunza Biblia zao. Wanaunganisha nguvu zao Shetani anapoigiza ujio wa Yesu Mara ya Pili. Angalia 2 Wathesalonike 2:1-12. Je, kahaba mkuu ni sawa na Mnyama wa Nchi Kavu? (Hiyo inawezekana – lakini inazungumzia (inarejea) kipindi ambacho wapagani, Waislamu, na Wakristo wa juu juu wanapoyafanya mawazo yao ya kidini ya kumkana Mungu kuwa ya muhimu.)

 

        1.    Ikiwa Kahaba Mkuu ndiye Mnyama wa Nchi Kavu, kwa nini apande juu ya Pembe Kumi? (Inaonesha utiifu wa mamlaka zote za kidini kuungana katika kuwapinga watakatifu wa Mungu.)

 

        1.    Je, Kahaba Mkuu kufanya safari kwa “kupanda mnyama” inamaanisha tu kwamba hana haja ya kutembea kwa miguu? (Hapana. Hii inamaanisha kuwa anamdhibiti mnyama wa Pembe Kumi. Anaelekeza matumizi ya uwezo wake.)

 

    1.    Soma Ufunuo 17:5-6. Kwa nini jina la Kahaba Mkuu linaanza kwa “Siri?” (Nadhani hii ni ishara kwamba huenda tusiwe sahihi kwa ukamilifu wote. Si dhahiri kuelewa jambo hili, ni ngumu kulielewa.)

 

      1.    Maelezo ya Kahaba Mkuu kama “mama” yanatusaidiaje katika kumwelewa kuwa yeye ni nani? (Yeye ni chanzo, “mama,” wa mamlaka zote zinazowafanya watu wasiwe waaminifu kwa Mungu. Yeye ni chanzo cha machukizo yote.)

 

      1.    Fikiria jambo hilo kidogo. Hiyo inatusaidiaje katika kumwelewa Kahaba Mkuu kama kielelezo? (Hii haiwezi kuwa shirika au hata dini ya dhahiri. Hii ni falsafa ya kidini inayoyaunganisha kwa mkazo makundi na mashirika yote yanayowakilishwa na Kahaba Mkuu.)

 

        1.    Una maoni gani juu ya hiyo falsafa ya kidini? (Maoni yangu ni haya: imani kwamba maisha bila Mungu sio tu kwamba yanawezekana, bali pia ni ya hali ya juu. Huu ni mtazamo wa “kiroho” au wa “kimaadili” unaokinzana na mafundisho ya Mungu.)

 

      1.    Je, hii falsafa ya kidini ni jambo tunaloweza kulipuuzia? (Hapana. Itatuua endapo itapewa fursa.)

 

  1.   Kahaba Mkuu Aelezewa

 

    1.    Soma Ufunuo 17:7. Je, tumepitia uchanganuzi wote huu bila kuwa na faida yoyote? Je, sasa malaika anataka kutuelezea “siri” hii?

 

    1.    Soma Ufunuo 17:8-9. Je, hiyo imekutatulia siri (fumbo)? (Hii inaonekana kufanana na mjadala wetu uliotangulia kwa sababu tumehusianisha Pembe Kumi na mjadala wetu wa awali wa Ufunuo 13. “Milima saba” pia inaendana na mjadala wetu wa awali kwa sababu Rumi imejengwa juu ya milima saba.

 

      1.    Si kwa haraka kihivyo. Mnyama huyu anapanda kutoka “kuzimu.” Kwani Pembe Kumi hazikuibuka kutoka baharini katika Ufunuo 13:1? Je, kuzimu ni kitu kingine tu? (Tulipoangalia Ufunuo 9:11 tulihitimisha kwamba Malaika wa Kuzimu ni Shetani. Ilionekana kwamba Kuzimu ni jahannamu. Katika Ufunuo 20 tutajifunza kwamba Shetani anafungwa kuzimu. Huenda kupanda kutoka kuzimu inamaanisha kwamba aliibuka kutoka kwenye falsafa za Kishetani.)

 

      1.    Kuna tatizo jingine kubwa. Ingawa tafsiri ya Biblia ya NIV (pamoja na tafsiri nyingine) zinaitafsiri hii kama “vilima,” inaonekana ni sahihi zaidi kuitafsiri kama “milima.” Hiyo inaufanya utambulisho wa Rumi kuwa tatanishi zaidi. Unadhani “milima saba” inaweza kumaanisha nini? (Hii inaturejesha nyuma kwenye mjadala tuliokuwa nao tulipoona kwa mara ya kwanza Pembe Kumi zinainuka kutoka baharini katika Ufunuo 13. Hapo awali tuliona joka linalomwakilisha Shetani, na joka hilo lilikuwa na vichwa saba. Wakati huo, nilipendekeza kwamba hiyo ilimaanisha kuwa joka alikuwa mwerevu. Lakini, tangu wakati huo nimetafakari juu ya dhana ya kwamba “mlima” unarejelea eneo la kiushawishi hapa duniani. Kwa mfano milima inaweza kuwa sheria, burudani, biashara, serikali, nk. Hivyo, badala yake hii inaweza kumaanisha kuwa ushawishi wake wa Kishetani unahusisha maeneo mengi maishani yaliyo ya muhimu na yenye ushawishi.)

 

    1.    Soma Ufunuo 17:10-13. Je, hii inaielezea siri kwa kina zaidi kwako? (Kuna maelezo mengi kwa wafalme hawa na falme hizi. Hata hivyo, hadi kufikia hapa tumekuwa tukijadili kuwa Pembe Kumi ni mamlaka ya kidini na ya kidunia zilizounganishwa pamoja, na hii inaleta mantiki.)

 

  1. Ushindi

 

    1.    Soma Ufunuo 17:14. Nani anayeshinda kwenye pambano dhidi ya Pembe Kumi? (Mungu wetu! Upande wetu!)

 

    1.    Soma Ufunuo 17:16-18. Tunaona ushindi gani mwingine? (Kuna mapambano miongoni mwa wapinzani wa Mungu. Pembe Kumi na Kahaba Mkuu wana ugomvi. Pembe Kumi na mnyama wanamshambulia kahaba.)

 

      1.    Hebu tutafakari jambo hili. Ikiwa Kahaba Mkuu ni nguvu zilizoungana pamoja zinazohusika kwenye ujio bandia wa Yesu Mara ya Pili, hiyo inaashiria nini juu ya mustakabali (wa siku zijazo)? (Ulimwengu wote utakapoamini kwamba mkombozi wa imani na dini zote amekuja, na kwamba muunganiko wa nguvu za kidini unageuka na kuwa kinyume na watu wa Mungu, muda unakuja ambapo tabia yake ya kweli itadhihirishwa. Katika hatua hii patakuwepo na uasi wa ndani kwa ndani.)

 

      1.    Utaona kwamba Kahaba Mkuu pia anahusianishwa na mji. Je, tunapaswa kuelewa kwamba kwa wakati huu Kahaba Mkuu anayo makao makuu kwenye mji mmoja mkubwa hapa duniani? (Soma Ufunuo 16:19. Hii ni rejea ya awali juu ya “mji mkuu” na pia inazungumzia uangamivu wake. Tunapaswa kuelewa kwamba Kahaba Mkuu anayo makao makuu.)

 

    1.    Rafiki, muda wa kuwa tayari ni sasa! Kuwa mwanafunzi makini wa Biblia ili usiweze kudanganywa na Kahaba Mkuu.

 

     Juma lijalo: Nayafanya Yote Kuwa Mapya.