Maneno ya Busara kwa Familia

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mithali 5, 13 & 31)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
2
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Familia zinashambuliwa. Tafsiri ya ndoa na familia inabadilika kwenye utamaduni mpya. Shinikizo la utamaduni mpya linawafanya wenzi wafanye kazi kwa bidii kiasi kwamba muda wa kukaa na familia unapungua. Hata pale familia inapokuwa pamoja, wanakuwa wanatizama televisheni na simu na si kuongea wao kwa wao. Dhana iliyopo ni kupenyeza kanuni za Biblia kwa watoto wako. Kiasi gani cha muda kinatumika katika kutimiza azma hiyo? Utamaduni pia unahamasisha kutokuwepo kwa uaminifu kwenye ndoa. Hebu tuchimbue maneno ya busara ya Biblia katika kulinda familia dhidi ya utamaduni mpya!

 

  1. Uaminifu

 

    1. Soma Mithali 5:1. Nani anayezungumza? (Hii imeandikwa kwa mfumo wa baba akizungumza na mwanaye.)

 

    1. Soma Mithali 5:2. Kuyasikiliza maneno haya na kuyafanyia kazi kutatufanyia nini? (Itatusaidia kuwa na busara na kuyahifadhi maarifa.)

 

      1. Inamaanisha nini kuilinda busara? (Nadhani inamaanisha kwamba utafanya uchaguzi wa busara.)

 

      1. Inamaanisha nini kwa midomo yako kuhifadhi maarifa? (Watoto wako watakusikiliza juu ya kile unachowaambia kwenye mada fulani.)

 

      1. Unadhani kwamba ushauri huu ni mahsusi kwa ajili ya jinsi (gender) fulani? (Lugha inaashiria hivyo, lakini nadhani ushauri hauko hivyo.)

 

    1. Soma Mithali 5:3. Je, unavutiwa na mwanamke malaya? (Ndiyo!)

 

    1. Soma Mithali 5:4. Je, mwisho wa uhusiano wako utakuwa wa kufurahisha kama mwanzo wa uhusiano huo? (Hapana, utakuwa mchungu.)

 

      1. Rejea ya upanga wa makali kuwili inatuambia nini? (Tutaumizwa vibaya sana.)

 

    1. Soma Mithali 5:5-6. Je, mtu anayetamani kufanya ngono na wewe anadhani kwamba anafanya kitendo kibaya? (Hafikirii juu ha hilo. Anaangalia raha ya muda huo, na si maisha kwa ujumla.)

 

      1. Kama mtu anayetafuta kufanya ngono angeyafikiria maisha, mtu huyo angehitimisha nini? (Mwisho wa ngono ni uchungu na mauti.)

 

    1. Soma Mithali 5:7-8. Njia bora ya kuepuka matatizo ni ipi? (Kaa mbali kabisa.)

 

 

      1. Je, hicho ndicho kitamaniwacho na asili ya moyo? (Mtu ambaye si mwenzi wako anapokuambia kuwa umependeza au una mvuto wa kimapenzi (sexy), kauli hiyo inaamsha nafsi yako. Haya ndio mambo ambayo watu wengi wanapenda kuyasikia. Unataka kutumia muda wako na mtu anayekusifia.)

 

        1. Hitimisho la dhahiri kwa wanandoa ni lipi? (Msifie mwenzi wako! Sifa kutoka kwa watu wengine haitakuwa na maana sana.)

 

    1. Soma Mithali 5:9-11. Kilichoanza kama kiamshi kikubwa cha nafsi sasa kinaishiaje? (Unapoteza mali yako. Maisha yako yanaishia kwenye maombolezo. Nafsi yako inazama.)

 

      1. Kwa nini maisha yako yanaishia kwenye maombolezo? (Nyama yako na mwili wako vimeangamia. Ngono imejikita kwenye nyama yako na mwili wako. Huna mvuto tena.)

 

    1. Soma Mithali 5:12-14. Anguko kuu ni lipi? (Kufuata ushauri. Kukubali kukemewa.)

 

    1. Soma Mithali 5:15-19. Tunapaswa kuelekeza usikivu wetu kwa nani? (Kwa wenzi wetu!)

 

      1. Soma tena Mithali 5:19. Kifungu hiki kinamwambia nini mwenzi japo si moja kwa moja? (Usiende. Usiseme kwamba, nimeoa/nimeolewa. Haijalishi jinsi ninavyoonekana, ninavyovaa, au ninavyoenenda.)

 

      1. Mara ngapi umeona vitendo vya ngono vinavyomhusisha mtu mwenye sura mbaya kuliko mwenzi anayekataa kwa dharau? (Hii inatokea kwa sababu wito wa kufurahisha nafsi hupofusha. Lakini, bado unatakiwa kujitahidi kuendelea kuvutia.)

 

      1. Ubinafsi ni wa muhimu kiasi gani katika kutokuwa na uaminifu kwenye ndoa? (Kitabu cha Mithali kinabainisha juu ya kushindwa kufuata ushauri. Ujumbe mkuu wa Biblia ni kujikana nafsi. Mwenzi asiye mwaminifu anasema, ninajipendelea zaidi kuliko mwenzi wangu na familia yangu. Kwa kadri tunavyozidi kuzeeka, kujikana nafsi kunahusika na mazoezi na chakula bora.)

 

    1. Soma Mithali 5:21-23. Mungu anathibitisha kwamba anaona mambo yote. Anatazamaje kitendo cha kutokuwa na uaminifu kwenye ndoa? (Anakiita ujinga mkubwa.)

 

      1. Ni vigumu kwetu kutathmini matendo yetu kiuhalisia. Unaweza kuona kwa nini Mungu anakiita sio tu Mkubwa, bali ujinga Mkubwa? (Kwa mtazamo wa mali huo ni ujinga. Kwa mtazamo wa uhusiano wako na watoto wako huo ni ujinga. Kwa mtazamo wa kuishi maisha ya amani huo ni ujinga. Pia kinaweza kuhatarisha kazi yako. Mungu yuko sahihi!)

 

  1. Wazazi na Watoto

 

    1. Soma Mithali 13:22. Je, kifungu hiki kinasema kuwa kama wewe ni mtu mwema utawaachia urithi wanao na wajukuu wako? Kwamba hili ndilo lengo ikiwa unataka kuitwa mwema? Au, kifungu hiki kinasema kuwa matokeo ya asili kutokana na utiifu kwa Mungu ni kujikusanyia fedha za kutosha kwa ajili ya kusaidia familia yako kwa vizazi viwili? (Nadhani ni maana ya pili. Mungu anambariki mtu mwema. Mdhambi ataupoteza utajiri wake kwa wenye haki.)

 

      1. Utakumbuka kwamba hivi punde tumejadili hasara za kifedha zinazotokana na kutokuwa na uaminifu kwenye ndoa? Je, hiyo ni sehemu ya sababu ya mtu mwema kuwa na fedha nyingi za kuacha kama urithi?

 

 

    1. Soma Mithali 13:25. Unawezaje kuhakikisha kuwa watoto wako wanalishwa chakula vizuri? (Mungu atawatafuta wale walio waaminifu!)  

 

      1. Inamaanisha nini kuwa mwaminifu? (Soma Mithali 27:23-27. Kitabu cha Mithali kinahusianisha uaminifu na uwajibikaji. Kinafundisha kwamba tunapaswa kuwa waangalifu kwenye biashara zetu, kwa sababu utajiri (mali) hauna dhamana ya kuendelea kuwepo. Kwa mkulima, kila mwaka ni mpya.)

 

    1. Soma Mithali 13:24. Utaona kwamba malezi ya aina mbili yanabainishwa: fimbo na nidhamu. Yana maana mbili. Moja inaweza kumaanisha fimbo kiuhalisia na nyingine inamaanisha kumrudi mtoto. Unadhani kwa nini maneno hayo mawili yalitumika?

 

      1. Soma Mithali 29:1. Si jambo la kawaida katika baadhi ya maeneo kumchapa mtoto. Mke wangu, mwalimu mstaafu wa shule ya msingi na mtaalamu wa nidhamu, anabainisha kwamba kuna njia bunifu nyingi za kurejesha nidhamu bila kumchapa mtoto. Tunatakiwa kujali kitu gani ikiwa hatuwalei watoto wetu vizuri kuwa na nidhamu? (Watakapotoka na kwenda duniani, wataangamizwa. Kwenye mjadala juu ya uchapaji, hili ni jambo la muhimu kuzingatiwa.)

 

      1. Hebu turejee nyuma na tuangalie tena Mithali 13:24. Nia ya kuwaadhibu watoto wako ni ipi? (Upendo. Kama unamchapa mtoto wako kwa sababu una hasira, unakuwa umepoteza kabisa maana ya kuadhibu. Adhabu sahihi inahamasishwa na upendo, si hasira.)

 

  1. Mke

 

    1. Soma Mithali 31:10-12. Hapo awali tulisoma vifungu ambavyo kwa mahsusi vilizungumzia uaminifu wa mume. Tuliviangalia kwamba vinahusika kwa wenzi wote wawili. Hii inatuambia nini kuhusu mke mwaminifu? (Anamtendea mumewe wema na si mabaya. Mumewe humwamini kikamilifu.)

 

    1. Soma Mithali 31:13-15. Unaweza kumwelezeaje mke wa aina hii? (Mchapakazi! Mwenye bidii ya kazi. Kwa hakika huyu si mwanamke mvivu.)

 

    1. Soma Mithali 31:16-18. Fursa sawa kwa wote haikuwa sehemu ya utamaduni wakati jambo hili lilipoandikwa. Hii inatupatia fundisho gani kuhusu wanawake wanaofanya kazi zilizo nje ya utamaduni wa kawaida? (Mimi si mtaalamu wa utamaduni wa kipindi hicho, lakini ninaamini kwamba kumiliki vitu, kununua vitu, kupanda shamba la mizabibu, na kufanya biashara - zote hizo zilikuwa ni shughuli ambazo kwa ujumla ziliachwa kwa wanaume. Biblia, kwa mara nyingine, inaenda kinyume na utamaduni mpya!)

 

    1. Soma Mithali 31:21-22. Hapo awali tulijadili jinsi ambavyo matokeo ya uadilifu kazini ni kuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto wako. Vifungu hivi vinasema kuwa mama anawezaje kuchangia kwenye usalama wa watoto wake? (Matokeo ya mama mwenye bidii ni kuwavika watoto wake mavazi mazuri.)

 

 

      1. Kwa wale mnaodhani kuwa Biblia inahamasisha mavazi ya kawaida, mavazi ya aina gani yanasifiwa hapa? (Kitani safi, nguo nyekundu na mavazi ya urujuani vyote vinaashiria mavazi ya gharama. Kuna mjadala unaoendelea kuhusu kama nguo nyekundu inapaswa kueleweka kama nguo yenye kuhifadhi joto mara mbili zaidi. Lakini, mantiki ya jambo hili haiwezi kupotoshwa: mama na watoto wamevaa vizuri.)

 

      1. Tunapaswa kuielewaje 1 Timotheo 2:9-10 na 1 Petro 3:3-4? (Petro anatuambia kuwa tabia yako, na si kile unachokivaa, ndio inayopaswa kuwa urembo wako wa kweli. Tukichukulia kwamba hakuna ukinzani miongoni mwa vifungu vya Biblia, hiyo itamaanisha kwamba kuvaa mavazi mazuri si jambo baya, lakini lisichukuliwe kama msingi wa kutathmini thamani yako binafsi.)

 

    1. Rafiki, je, unaona mada kuu katika kile ambacho Biblia inakizungumzia kuhusu familia? Nadhani mada hiyo ni uaminifu kwa Mungu, kujikana nafsi, bidii katika kazi yetu, na upendo baina yetu. Mambo haya yanaweka mazingira ya amani katika familia. Ukiona kwamba familia yako haifikii viwango hivi, kwa nini usimwombe Mungu akusaidie ili ufikie ubora huu?

 

  1. Juma lijalo: Wimbo wa Kifalme wa Mapenzi