Somo la 7: Mambo Muhimu Katika Kuwa na Umoja wa Familia
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unaamini kwamba familia ndio msingi wa jamii? Kama ni kweli, basi kama familia inasambaratika, taifa pia linasambaratika. Je, unaamini kwamba taifa lako linasambaratika? “Ufunguo” ni kitu kinachofungua mlango au siri. Hebu tufungue Biblia zetu na tuone kile ambacho Biblia inakifundisha kwamba ndizo funguo za kufungua siri za umoja wa familia!
- Kuufungua Msingi
-
- Soma Waefeso 2:11-12. Tatizo gani moja la umoja linaelezewa hapa? (Watu hawana tumaini na hawana Mungu. Kwa mahsusi kifungu hiki kinawaelezea watu wa Mataifa, lakini pia kinatumika kumwelezea mtu yeyote ambaye hajaongolewa.)
-
- Soma Waefeso 2:13. Suluhisho la tatizo hili la umoja ni lipi? (Yesu.)
-
-
- Yesu anatatuaje tatizo hili? (Kafara yake kwa ajili yetu msalabani.)
-
-
- Soma Waefeso 2:14-15. Hii inaonekana kuelezea suluhisho zaidi ya tatizo moja. Matatizo gani ya umoja yanatatuliwa? (Hizi ni sura mbili za tatizo moja. Upande mmoja ni kwamba Wayahudi walidhani kuwa walikuwa na hadhi ya juu kimaadili kuliko watu wa Mataifa, ukizingatia kwamba walipewa torati ya Mungu. Upande mwingine ni kwamba watu wa Mataifa hawakuifuata sheria, na Yesu aliitimiza torati kwa ajili yao, kama alivyofanya kwa Wayahudi.)
-
- Soma Waefeso 2:16. Yesu alitatua tatizo gani jingine la umoja? (Tatizo letu la umoja na Mungu. Sisi ni wadhambi na Yeye ni Mungu mtakatifu. Yesu alitupatanisha na Baba yake kwa kuyaishi maisha Yake makamilifu, kulipa adhabu ya mauti kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka kwenye uzima wa milele.)
-
- Soma Waefeso 2:17. Yesu anatupatia nini? (Tumaini.)
-
-
- Hebu tutafakari jambo hili. Ikiwa Yesu ni jibu kwenye mgongano kati ya Wayahudi na watu wa Mataifa, na kati yetu na Mungu wetu Mtakatifu, je, dhana zile zile zitakuwa zinatumika kwenye umoja wa familia? Hebu tuangalie jambo hilo katika sehemu inayofuata.
-
- Kufungua Upatanifu/Ulinganifu
-
- Soma Yohana 17:20-21. Mfano wa mwisho wa Yesu wa umoja ni upi? (Utatu Mtakatifu! Yesu anasema kuwa anatutaka tuwe “wamoja” kama yeye alivyo mmoja na Baba.)
-
-
- Utaona kwamba Yesu anasema, “hao nao wawe ndani yetu.” Hii inamaanisha nini? (Waumini wenza katika Yesu ni wamoja pamoja naye na Baba.)
-
-
-
- Utautumiaje ushauri huu kwenye familia? (Kipaumbele chetu cha kwanza ni badiliko la familia yetu. Kama wanafamilia wote wanamwamini Yesu, basi kanuni zile zile za umoja zinazotumika hapa zinapaswa kutumika kwetu. Inatumainiwa kwamba, matatizo yanayovuruga na kutenganisha familia yako ni madogo kuliko matatizo yanayoutenganisha ulimwengu.)
-
-
- Soma Wafilipi 2:1-2. Hatua inayofuata baada ya “kuungana na Kristo” ni ipi? (“Kuwa na mawazo mamoja, kuwa na upendo mmoja, kuwa na roho moja na kunia mamoja.”)
-
- Soma Wafilipi 2:3-4. Hili linaonekanaje kivitendo? (Tunafanya juhudi za kutokuwa wabinafsi.)
-
-
- Linganisha 1 Timotheo 5:8. Wafilipi 2:4 inapotuambia kuwa tusiyaangalie mambo yetu wenyewe, je, hiyo inamaanisha kuwa tunatakiwa kuwapa kipaumbele watu wengine kuliko familia yetu? (Kwanza tunaacha ubinafsi kwa familia yetu. Kwa kuanzia, tunapaswa kuihudumia familia yetu.)
-
-
- Soma Wafilipi 2:7-10. Maisha ya Yesu yanatupatia utambuzi wa kile inachomaanisha kutokuwa na uaminifu. Matokeo ya kawaida ya kutokuwa na ubinafsi ni yapi? Je, ni kwamba tunaendelea kutokuwa na kitu chochote? (Yesu ndiye mfano wetu. Biblia inatuambia kuwa Yesu “alimwadhimisha mmo na kumweka mahali pa juu.”)
-
-
- Kuwaambia watoto wako kwamba mara zote wanapaswa kuwapa kipaumbele watu wengine sio ujumbe unaovutia sana. Ujumbe wa Biblia ni kwamba hatimaye njia hii ina thawabu kubwa!
-
-
- Soma Waefeso 5:21. Je, hii ni dhana maarufu leo?
-
-
- Maneno ya mwisho ya “katika kicho cha Yesu” yanaongezea nini kwenye maana? (Uelewa wetu juu ya nia ya Yesu ya jinsi tunavyopaswa kuishi unaisisitiza amri hii.)
-
-
- Soma Waefeso 5:22-23. Je, huu ni mfano wa utiifu ambao tumekuwa tukiujadili?
-
- Soma Waefeso 6:1-3. Je, huu ni mfano wa utiifu ambao tumekuwa tukiujadili?
-
- Soma Waefeso 6:4. Je, hii inarekebisha wajibu wetu wa utiifu? Je, hii inarekebisha utiifu wa mke kwa mume?
-
- Soma Waefeso 6:5-8. Muktadha wa sasa wa jambo hili ni upi? (Matendo yetu.)
-
-
- Je, huu ni mfano mwingine wa utiifu ambao tumekuwa tukiujadili?
-
-
-
- Zingatia Waefeso 6:7. Rejea ni ipi? (Huduma yetu kwa Mungu.)
-
-
-
-
- Je, unaona kwamba uhusiano wetu na Yesu, na jinsi tunavyomwelewa, vinaimarisha dhana yetu ya utiifu?
-
-
-
- Soma Waefeso 6:8. Kwa mara nyingine, matokeo ya utiifu huu ni yapi? (Thawabu!)
-
- Soma Waefeso 6:9 na Waefeso 5:25. Katika kifungu cha awali, inaonekana kama kila mtu anakuwa mtiifu kwa mume na bosi. Je, hiyo ni kweli? (Hapana. Wote wanamheshimu Yesu. Mfano wa Yesu ni ule wa kujitoa kwa wengine. Kiuhalisia, huu ndio mzunguko wa utiifu.)
-
- Soma Waefeso 5:28. Kwa nini usianzie hapa? Kwa nini usiseme, “Ukimtii [mume wako, mke wako, wazazi wako, bosi wako] basi unajipenda mwenyewe?” Kwa nini usiseme kwamba kuna thawabu kubwa, hata sasa, kwenye njia hii?
- Mfano wa Mwanadamu
-
- Soma Ruthu 1:1-5. Ungejisikiaje kama ungekuwa Naomi?
-
- Soma Ruthu 1:6. Angalia jinsi hii ilivyoandikwa: Mungu alijitokeza kuwasaidia watu wake kwa kuwapatia chakula. Je, Mungu amemsahau Naomi? Je, Naomi anafukuzia msaada wa Mungu? (Tulianza kwa kujifunza kwamba uhusiano na Mungu ndio msingi wa umoja wa familia. Naomi ana sababu ya kutilia shaka kwamba Mungu anamtafuta.)
-
- Kisa kinaendelea kwa kusema kuwa watatu hao wanaendelea kuelekea Yuda, lakini Naoni anawaambia wakweze wawili kwamba wanapaswa kurejea makwao. Soma Ruthu 1:12-13 na Ruthu 1:20. Hii inathibitisha nini kuhusu mtazamo wa Naomi? (Mkono wa Mungu u “kinyume” naye. Maisha ya wanawake wote watatu ni “machungu.” Hata hivyo, Naomi anasema kuwa hali yake ni mbaya sana kwa sababu Mungu wake amemwangusha.)
-
- Soma Ruthu 1:14-16. Hii inatuambia nini kuhusu mtazamo wa Ruthu juu ya Mungu? (Anataka Mungu wa Naomi awe Mungu wake. Anakataa wito wa Naomi wa yeye kurejea kwenye miungu ya nyumbani kwao.)
-
-
- Hapo awali tulijadili suala la kutokuwa na ubinafsi. Je, Rutu hawi na ubinafsi? (Ruka vifungu kadhaa na usome Ruthu 1:9-10. Angalia hatari na matatizo yanayozungumziwa kwenye vifungu hivi. Hii inaonesha kwamba Ruthu alielewa hatari ya kuwa mgeni. Licha ya hayo aliamua kukaa na Naomi.)
-
-
-
- Hapo awali tulijadili suala la utiifu. Je, Ruthu anajitoa kwa Naomi? (Ruthu anajitoa kwa Mungu wa kweli. Hata hivyo inaweza kuonekana kwamba Ruthu anajitoa kwa Naomi kwa hisia kwamba atakubali kumsaidia katika siku zijazo.)
-
-
- Soma Ruthu 1:17-18. Nani, kati ya wanawake watatu, anautangaza umoja? Nani anayehimiza kwamba wanaendana licha ya tofauti ya utaifa? (Ruthu.)
-
-
- Hii inatuambia nini juu ya ukweli wa kile tulichojufunza hapo awali? (Naomi alipoteza imani yake kwa Mungu. Yeye ndiye anayesisitiza kwamba watatu hao wagawanyike. Ruthu anamkumbatia Mungu wa kweli na anauendeleza umoja wa familia.)
-
-
- Kisa kinaendelea na tunaona kwamba Mungu anambariki Ruthu kwa kumpa mume tajiri aitwaye Boazi. Hebu tusome kile kinachomvutia Boazi kwake. Soma Ruthu 2:10-12. Kivutio ni kipi? (Uaminifu wake kwa Naomi na Mungu. Boazi anaamini kwamba Mungu anashughulika kuwalipa watu kutokana na wema wao.)
-
- Rafiki, je, unaweza kuona kwamba kanuni tulizojifunza kuhusu umoja wa familia zinathibitishwa kuwa ni za kweli katika maisha ya Ruthu? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, akusaidie ufuate mifano hii ya kuwa na moyo wa ibada kwa Mungu, kujitoa kwa Mungu, na kutokuwa na ubinafsi?
- Juma lijalo: Msimu wa Malezi.