Somo la 9: Nyakati za Kupoteza

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Marko 5, Yohana 11)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
2
Lesson Number: 
9

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, umewahi kutafakari kuwa maisha ni kama mlima? Je, kadiri unavyopata uzoefu na kile ufanyacho, na kadiri sifa zako na wigo wako wa marafiki unavyopanuka, mambo yanazidi kuwa bora? Nini kinachotokea unapofika kileleni mwa mlima na kuanza kutazama chini? Kwa baadhi ya watu, maisha ni kama safu za milima na wana uzoefu unaojirudia wa kutizama chini. Hebu tuchunguze kile Biblia inachokisema kuhusu namna ya kukabiliana na safari ya kushuka kutoka mlimani.

 

  1. Yairo

 

    1. Soma Marko 5:21-22. Ni jambo gani unaloweza kunieleza kuhusu Yairo?

 

      1. Je, yeye ni mtu aliye kileleni? Au, angalau anayeelekea kileleni?

 

      1.  Je, Yairo anaonesha mienendo kama ya mtu aliye kileleni? (Hapana. Anaanguka chini ya miguu ya Yesu.)

 

    1. Soma Marko 5:23. Kuna upotevu mkubwa zaidi ya kufiwa na mtoto? (Hakika Yairo anatizama kuelekea chini ya mlima.)

 

    1. Soma Marko 5:24. Je, Yesu amekubali kumtibu binti Yairo? Je, mambo yote yatakuwa sawa sasa?

 

    1. Soma Marko 5:25-26. Mwanamke huyu yupo sehemu gani ya “mlima?” Je, Yupo juu au chini? (Yupo chini – kutokana na sababu nyingi. Kwanza alikuwa najisi kwa mujibu wa Walawi 15:19 & 25. Yeyote ambaye angemgusa naye angekuwa najisi. Hata wale ambao wangegusa kitu ambacho amegusa angekuwa najisi, Walawi15:22. Pili, hili limekuwa endelevu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Ametumia fedha zake zote kwa matabibu, na tatizo lilikuwa linazidi kuongezeka.)

 

    1. Soma Marko 5:27-29. Mwanamke huyu yupo sehemu gani ya “mlima” kwa sasa? (Hakika anaelekea kileleni.)

 

      1. Kuna fundisho gani kwetu kuhusu kupoteza?

 

    1. Soma Marko 5:30-32. Je, umewahi kuwa na haraka, na mtu fulani mbele yako katika msururu wa magari anafanya jambo fulani la kipuuzi? Unajisikiaje pale unapokawizwa bila sababu?

 

      1. Unafikiri Yairo anajisikiaje kwa sasa? Binti yake yupo kwenye hatua ya kifo. Muda ni wa msingi na Yesu amesimama kwa sababu zinazoonekana kuwa za kipuuzi - hata wanafunzi wake wanahoji hili!)
         
    1. Soma Marko 5:33-35. Endapo ungekuwa Yairo, je, kwa sasa ungekuwa na hasira na huzuni isiyohimilika?

 

  1. Je, Yesu hana vipaumbele? Kwa nini asimfanye binti Yairo kuwa kipaumbele chake? Mwanamke huyu amekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na miwili, ni tofauti gani ingeletwa na siku moja?

 

    1. Hebu tujikite kwenye Marko 5:34. Nini kilichomponya mwanamke? (Imani.)
      1. Ni kitu gani kinamjia juu yake sasa? (Amani.)

 

      1. Kwa nini yeye ana amani na Yairo anakuwa na siku mbaya kuzidi zote katika maisha yake?

 

    1. Soma Marko 5:35-36. Linganisha na Marko 5:33. Utaona kwamba hofu ya Yairo imekuwa badala ya hofu ya mwanamke. Kwa nini?

 

    1. Soma Marko 5:37-42. Tafakari hasira na kuchanganyikiwa ambako Yairo alihisi kwa kumwona Yesu akipoteza muda na mwanamke ambaye jambo lake wala halikuwa la dharura. Je, Yesu anachelewesha jambo hilo sasa?

 

      1. Tafakari nyakati ambazo Yesu hakujibu maombi yako?

 

      1. Soma Yohana 11:21 na Yohana 11:32. Ni Kipi haswa ambacho Martha na Mariamu wanamweleza Yesu?

 

      1. Ni kipi kingezuia hisia za kukata tamaa, kuchanganyikiwa na hasira? (Soma tena Marko 5:36. Rafiki, hili ndilo jibu.)

 

    1. Hebu tujadil jinsi kisa hiki kinavyoweza kutumika katika upotevu wetu au upotevu wetu unaoweza kujitokeza katika maisha yetu. Muda ni wa muhimu kiasi gani?

 

      1. Baada ya Yesu kumfufua binti Yairo, je, kukawia kwake awali kulileta tofauti yoyote?

 

      1.  Vipi kuhusu wewe? Endapo Yesu atasubiri mpaka marejeo yake mara ya pili kuwaponya wale uwapendao, kukawia huko kutaleta tofauti yoyote.

 

      1.  Je, tunaweza kuelezea sababu ya Yesu kuchagua kumtibu mwanamke mwenye tatizo la damu papo kwa papo, lakini akachelewesha muujiza ya binti Yairo?

 

  1. Je uamuzi wa Yesu katika suala hili ni jambo ambalo tunaweza kulihoji?

 

  1. Lazaro

 

    1. Soma Yohana 11:1-3. Ni kipi Mariamu na Martha walikitarajia kutoka kwa Yesu?

 

      1. Kwa nini walilitarajia? (Yesu alimpenda Lazaro.)

 

    1. Soma Yohana 11:4-6. Awamu hii Yesu anachelewa na siyo kwa sababu anasaidia mgonjwa mwingine. Kwa nini Biblia inasema alichelewa? (Kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Utaona kwamba Yesu anathibitisha kuwa anampenda Lazaro na dada zake.)

 

      1. Hebu tulijadili hili. Kuzorota kwa afya ya Lazaro kunaleta utukufu kwa Mungu. Je, huo ni uwezekano kwenye maisha yako na maisha ya wanafamilia wako – Mungu anaruhusu mambo yazorote kwa ututkufu wake?

 

    1. Soma Yohana 11:7 na Yohana 11:17-20. Unadhani kwa nini Mariamu hakutoka nje kwenda kumlaki Yesu? (Nafikiri alikuwa hajafurahishwa na Yesu. Alikuwa amemwangusha.)

 

    1. Soma Yohana 11:21-24. Je, Martha hana furaha na Yesu? (Ndio, tulitazama kifungu hiki hapo awali.)

 

      1. Je, Martha alihitaji kususbiri mpaka ufufuo kuja kumwona Lazaro tena?

 

    1. Soma Yohana 11:25-27. Kwa nini Yesu anakazia kuwa yeye ni Masihi ambaye angetoa uzima wa milele? (Ni matukio kama haya ambayo yanajaribu imani yetu. Martha alikuwa na hakika kuwa Yesu angemponya rafiki Yake, Lazaro. Alikuwa amewaponya wengi asiofahamiana nao! Angalia Yohana 11:37. Yesu aliposhindwa kufanya hili lilikuwa jaribu kubwa sana kwake.)

 

    1. Soma Yohana 11:38-44. Kwa sasa unafahamu vizuri kisa hiki. Niambie endapo kama unaafiki uamuzi wa Yesu kuamua kuchelewa?

 

      1. Endapo unaafiki, unadhani inaweza kuwa hivyo kwa kila kisa katika maisha yako ambapo Yesu hakuonekana kukusaidia? Je, kadiri muda utakavyozidi kusonga, mapenzi ya Mungu yatakuwa bayana kwako?

 

    1. Ruka hadi chini na usome Yohana 11:53. Ufufuo wa Yesu unasababisha viongozi wa Kiyahudi kuamua kuwa lazima wamuue Yesu. Unadhani kuwa Yesu alielewa kitakachotokea kama matokeo ya ufufuo wa mtu maarufu hivyo?

 

      1. Kama umejibu, “ndiyo,” sasa soma Yohana 11:4. Je, sehemu ya “utukufu” wa ufufuo wa Lazaro, ni kifo na ufufuo wa Yesu?

 

      1. Kama unaafiki, hilo linatufundisha nini kuhusu upendo wa Yesu kwetu? Hilo linatufundisha nini juu ya kumwamini Yesu? (Yesu alimpenda Lazaro, Mariamu na Martha. Walipata shida na walikatishwa tamaa, lakini Yesu aligeuza huzuni zao kuwa furaha. Muhimu zaidi, Yesu hakujiepusha na mateso, ili kwamba wote tuweze kufufuliwa siku ya mwisho!)

 

    1. Rafiki kama unaangalia chini ya “mlima” katika maisha, kama unakabiliana na changamoto ambazo unajua Mungu anaweza kuzitatua, natumaini unaona kwamba Mungu ni wa kutumainiwa. Anakupenda! Je, unaweza kuchagua kumwamini Bwana tu, bila kujali kitakachotokea?

 

  1. Juma lijalo: Nyakati Ndogo za Taabu.