Somo la 11: Watu Waliorudi Nyuma
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kuna ushauri mbaya unaoonekana kutapakaa siku hizi. Moyo wako ukikwambia kutenda jambo, basi unapaswa kulifanya. Hata kwa wale wanaotamani kumfuata Mungu, msitari tunaopaswa kuufuata maishani wakati mwingine ni vigumu kuuona. Tena ikizingatiwa kwamba, Yesu alituambia katika Marko 12:31 kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Hiyo inaweza kuonekana kama kuupa upendo kipaumbele. Lakini upendo wa kweli unahusisha utiifu kwa sheria ya Mungu. Hebu tuchimbue suala hilo tunapozama kwenye Biblia yetu na kujifunza zaidi!
- Kuwatenga Wageni
-
- Soma Nehemia 13:1-3. Jiweke kwenye nafasi kwamba uko ndani ya Yerusalemu wakati uamuzi huu ulipofanyika. Chukulia kwamba una marafiki walioshuka kutoka kwa Waamoni na Wamoabu. Wanataka kumwabudu Mungu pamoja nawe. Moyo wako ungekwambia ufanye nini? Kuwazuia marafiki wasimwabudu Mungu kwa sababu ya jambo lililotokea vizazi kumi (Kumbukumbu la Torati 23:3-6) vilivyopita?
-
-
- Vipi kama walikuwa wameoleana na familia yako na sasa mlikuwa mnavunja familia wakati kile tu walichokuwa wanakitaka ni kumwabudu Mungu?
-
-
- Hebu tujikite kwenye Nehemia 13:2. Ni nini sababu ya kuwatenga watu waliotokea kwa Waamoni na Wamoabu? (Kizazi chao hakikuleta chakula na maji wakati Waisraeli walipokuwa wanapita. Na walijaribu (bila mafanikio) kuleta laana kwa watu wa Mungu.
-
-
- Unadhani baadhi ya watu watasema kwamba hilo si jambo la dhati, kwa dhahiri si la dhati kiasi cha kuvunja familia na kuwazuia wale unaowapenda wasiabudu pamoja nawe?
-
-
- Soma Nehemia 13:4-5. Je, Eliashibu na Tobia ni marafiki? (Inaonekana hivyo kwa kuwa Biblia inasema walikuwa na “uhusiano wa karibu.”)
-
-
- Tobia anapewa chumba cha aina gani hekaluni? (Stoo.)
-
-
-
- Je, utamruhusu rafiki yako alale kanisani kwako ikiwa kanisa lina stoo ya ziada ambayo ilikuwa haitumiki?
-
-
- Soma Nehemia 13:6-8. Je, ni sahihi kufanya hivi? Kwa nini tu usimwombe Tobia aondoke kwa upole?
-
-
- Kwa nini amfukuze kabisa? (Tafsiri ya Biblia ya NIV kwenye Agano la Kale inatupatia ishara ya muhimu. Inatuambia kuwa Tobia alikuwa Mwamoni.)
-
-
- Soma Nehemia 13:9. Hii inatuambia nini kuhusu stoo ambayo Tobia alikuwa anaishi? (Itakuwa ilikuwa inatumika kutunza sadaka za nafaka.)
-
- Hebu turejee nyuma na tuangalie jinsi utakavyotumia maamuzi yote haya katika zama hizi. Je, ni sahihi kufanya uamuzi kwa moyo wako?
-
-
- Kuna mitafaruku mingi ya “moyo” siku hizi. Nchini kwangu, kuna suala la uhamiaji haramu. Hii pia inahusisha suala la nini cha kufanya kuhusu watoto wa wahamiaji haramu. Hii inahusisha aina hiyo hiyo ya suala la kizazi: watoto hawakutenda jambo lolote baya. Je, wanapaswa kuadhibiwa kwa kile walichokifanya wazazi wao?
-
-
-
-
- Utaona kwamba maamuzi anayoyafanya Nehemia yana vidokezo vikubwa vya kiroho. Je, hiyo inaleta utofauti tunapoyatumia mawazo haya kwenye masuala ya sasa?
-
-
-
-
- Kanisani kwangu kuna suala la kuwawekea wanawake mikono. Kwenye makanisa mengine kuna suala la kuwawekea mikono mabasha/wasenge (homosexuals). Unaona tofauti kati ya haya masuala ya kisasa na masuala ya zama za Nehemia? (Kwa kuzingatia kuwa yanahusisha hoja za “moyo,” tofauti na hoja zilizojengwa juu ya Maandiko, zote zinafanana.)
-
-
-
- Je, utawala wa sheria wa Mungu mara zote hutufunga?
-
- Sheria ya Mungu na Zaka
-
- Soma Nehemia 13:10-12. Tatizo ni lipi? (Walawi hawakuwa wakilipwa, hivyo walirejea na kuwezesha maisha yao kwa njia ya kilimo.)
-
- Zingatia Nehemia 13:11. Jibu la swali la Nehemia ni lipi? Unadhani kwa nini watu waliacha kutoa zaka? Unadhani hili linahusiana na mtafaruku wa Tobia? (Mojawapo ya maoni yanapendekeza kuwa neno la Kiebrania lililotumika hapa linapendekeza kuwa Nehemia alifungua aina fulani hivi ya mashtaka ya kisheria dhidi ya viongozi. Kwa kuwa mashtaka yake aliyalenga kwa viongozi, na si kwa watu, hii inaashiria viongozi walikuwa na makosa.)
-
-
- Ukiona matendo yasiyo sahihi kwa uongozi wa kanisa, je, hiyo inaathiri utayari wako wa kutoa zaka?
-
-
-
-
- Je, inapaswa kuwa hivyo? (Chochote kile ambacho viongozi wanaweza kuwa wamekifanya, ugumu unawaangukia Walawi. Jibu sahihi ni kuendelea kulitegemeza kanisa na kurekebisha uongozi.)
-
-
-
-
-
- Nehemia ni Gavana, hivyo ni kiongozi wa juu. Vipi kama kiongozi wa juu anawaunga mkono viongozi wanaojihusisha na tabia zisizofaa? Unapaswa kufanya nini?
-
-
-
- Soma Nehemia 9:38 na Nehemia 10:35. Unakumbuka mjadala wetu wa jambo hili? Tulikubaliana kwamba walisaini mkataba wa kumtii Mungu uliojumuisha kipengele cha makubaliano ya kulitegemeza hekalu! Hii inaashiria nini kuhusu uwezekano wa Nehemia kufungua aina fulani ya mashtaka ya kisheria dhidi yao? (Sasa hii inaleta mantiki kamili.)
-
- Soma Nehemia 13:13. Ni jibu gani jingine alilonalo Nehemia kwa ajili ya tatizo? (Anasafisha nyumba. Anawabadilisha viongozi wasiotunza ahadi zao.)
-
- Soma Nehemia 13:14. Nehemia anamwomba Mungu afanye nini kwenye hili ombi? (Kukumbuka uaminifu wake, na si matatizo ya sasa.)
-
-
- Kwa nini Nehemia adhani kuwa Mungu atamwajibisha katika hili? (Nehemia alikuwa msimamizi – ingawa hakuwepo mambo yalipoharibika.)
-
- Sheria ya Mungu na Sabato
-
- Soma Nehemia 13:15-16. Unaweza kulielezeaje tatizo hili? Sabato ilitendewa kama siku nyingine ya kazi. Walijihusisha na kazi za kawaida na biashara siku ya Sabato.)
-
- Soma Nehemia 10:31. Nini kimetokea kwenye hii ahadi ya dhati iliyowekwa miaka mitatu iliyopita? (Pia imevunjwa.)
-
-
- Hebu tujadili hili kidogo. Ni nini sababu ya kuandaa na kuuza chakula siku ya Sabato, na kuifanya kama siku yoyote ya kazi? (Unafanya kazi ili kujitegemeza.)
-
-
-
- Sababu ya Sabato ni ipi? (Kumwadhimisha Mungu kama Muumba wetu.)
-
-
-
- Unaona jinsi mambo haya mawili yanavyokinzana? (Sabato humwadhimisha Mungu kama Muumba na Mlinzi wetu. Hiyo si kazi yetu. Watu hawa walidhani kuwa kazi yao ndio iliyokuwa kiini cha uhai wao na si Mungu wao.)
-
-
- Soma Nehemia 13:17. Hapa Nehemia anamfungulia nani mashtaka? (Kwa mara nyingine, anawashtaki viongozi.)
-
- Soma Nehemia 13:18. Kwa nini Nehemia anarejea somo la historia? (Unakumbuka tulipojifunza Nehemia 9? Ilinukuu kutokuwa na uaminifu kwa mababu wao, kitendo kilichowafanya waingie mkataba wa kuwa waaminifu. Kwa mahsusi mkataba huo haukubainisha kufanya biashara siku ya Sabato. Nehemia 10:31.)
-
- Soma Nehemia 13:19-22. Nilidhani sote tumekubaliana kwamba mtu anabadilika kuanzia ndani hadi nje. Kanuni za nje kamwe hazibadili moyo wa mtu. Unaelezeaje jambo hili? (Huenda lengo la kwanza la Nehemia ilikuwa ni kubadili hali, badala ya kubadili mioyo.)
-
-
- Je, hii ndio sababu Wakristo wanaunga mkono sheria zinazolinda maadili? Au, je, hali ya Nehemia ni tofauti?
-
- Kuoleana (Ndoa ya Mseto)
-
- Soma Nehemia 13:23-25. Kiapo kilichoingiwa kwa sababu ya vipigo na kung’oa nywele ni kizuri kwa kiasi gani?
-
-
- Soma Nehemia 10:30. Hapo awali walikuwa wamekula kiapo cha mkataba kwenye suala hili hili!
-
-
-
- Ikiwa hili ni fundisho kwa ajili ya nidhamu ya kanisa, basi kwa dhahiri nimekuwa kwenye upande usio sahihi siku za nyuma. Unadhani hili ni fundisho kuhusu nidhamu kanisani? Vijana wanapojiingiza kwenye ndoa za mseto, au ngono bila ndoa, au kuwa na mtoto nje ya ndoa, je, ni sahihi kung’oa nywele (au jambo linalofanana na hilo katika zama za sasa)? (Tofauti moja ni kwamba Nehemia aliwakilisha mamlaka ya serikali. Alikuwa na mamlaka ya kuadhibu makosa.)
-
-
- Soma Mathayo 13:24-30. Je, hii inatufundisha jambo tofauti kuhusu matumizi ya mamlaka ya kanisa? (Kabla hujajibu, soma Mathayo 13:36-42. Kwa kuwa Yesu anaelezea kwamba “konde” ni ulimwengu, huu hauonekani kuwa ufananisho wa moja kwa moja. Hata hivyo, onyo kuhusu hatari ya kung’oa ngano unapong’oa magugu linaonekana kuwa na ufananisho wa moja kwa moja.)
-
- Rafiki, je, una tatizo la kuirudiarudia dhambi? Je, una kawaida ya kufanya uamuzi kwa moyo wako badala ya akili yako? Nehemia anatukumbusha kwamba utii ni muhimu kwa Mungu. Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akusaidie uwe na uelewa sahihi wa suala hili?
- Juma lijalo: Kukabiliana na Uamuzi Mbaya.
