Somo la 3: Kutoka Fumbo Hadi Ufunuo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Danieli 2)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
1
Lesson Number: 
3

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.                          

 

Utangulizi: Jirani wangu alikuwa amekaa kwenye bustani iliyo mbele ya nyumba yake akiwa ameegemea kizuizi. Aliegemeza kichwa chake mikononi mwake. Hili halikuwa jambo la kawaida hivyo nilimwendea na kumuuliza kuwa tatizo ni nini. Aliniambia anajihisi kama wingu jeusi lilikuwa linamfuata kwa sababu alikabiliana na mfululizo wa matatizo. Danieli na marafiki wake watatu wanaweza kuwa na malalamiko yanayofanana na ya jirani huyu. Wamechukuliwa mateka. Nchi yao na maisha yao ya kawaida yameharibiwa, na sasa wanakabiliana na adhabu ya kifo! Matatizo hayo ni mabaya na makubwa zaidi kuliko yale anayokabiliana nayo jirani wangu. Hebu tuzame kwenye somo letu na tuone jinsi ya kukabiliana na nyakati zilizo na “wingu jeusi” maishani!

 

  1.     Ndoto

 

    1.     Soma Danieli 2:1-3. Je, umewahi kuwa na ndoto iliyokuhangaisha? Je, ndoto ilikufanya upoteze usingizi?

 

      1.     Je, umewahi kutafakari kwamba ndoto yako ilikuwa ni ujumbe kutoka kwa Mungu?

 

      1.     Unadhani kwa nini Nebukadreza alihangaishwa sana na ndoto yake? (Unahitaji usingizi wako! Wafalme wanafahamu kwamba wao ni watu muhimu. Hivyo, lazima ndoto zao ziwe za muhimu. Maoni ya “New Bible Commentary” yanatuambia kwamba wafalme wa kale wa Mashariki ya Karibu waliamini kuwa miungu iliwapa ujumbe kwa njia ya ndoto.)

 

        1.     Je, Mungu wa kweli atampatia Nebukadreza ujumbe kwa njia ya ndoto? Kwa nini asimpe Danieli ndoto hiyo? (Soma Danieli 2:37. Mungu alimpa Nebukadreza uwezo, kwa nini asimpatie ujumbe pia? Endapo hii ingekuwa ndoto ya Danieli, Mfalme asingeizingatia hata kidogo.)

 

      1.     Nebukadreza aliwaleta wataalamu wa aina gani ili kutatua tatizo la ndoto yake?

 

      1.     Soma Kumbukumbu la Torati 18:9-12. Mungu ana maoni gani kwa “wataalamu” wa aina hii?

 

    1.     Soma Danieli 2:4. Je, ombi hili linaonekana kuwa na mantiki?

 

    1.     Soma Danieli 2:5-6. Nebukadreza ni bosi wa namna gani?

 

      1.     Je, ana wazimu tu? Au, kuna njia yoyote nyuma ya wendawazimu wake? Je, ombi lake linaleta mantiki yoyote kwako?

 

    1.     Soma Danieli 2:7-9. Nebukadreza anaelezea mantiki yake. Una maoni gani kuhusu mantiki yake? (Nebukadreza hawaamini washauri wake. Anadhani wanaweza kuwa na tabia ya kudanganya mambo. Kwa kuwa anapaswa kuwa na uwezo wa kuthibitisha kile alichokiota, anaamini hii ndio njia pekee ya kufahamu kama tafsiri ni sahihi. Kwangu hiyo inaleta mantiki.)

 

    1.     Soma Danieli 2:10. Je, matakwa ya Mfalme yanaleta mantiki kwa washauri wake? (Hapana! Wanajenga hoja kwamba madai haya hayajawahi kutokea na hayawezekani.)

 

      1.     Washauri wanajenga hoja gani wanaposema, “Hapana mfalme, pamoja na ukuu na uwezo wake wote, aliyewahi kudai jambo kama hili?” (Wanamwambia Mfalme kwamba hafanyi kazi yake vizuri.)

 

    1.     Soma Danieli 2:11. Tafakari jibu hili kwa makini. Je, kweli jambo hili ni nje kabisa ya uwezo wao? (Inaonekana hiyo ndio kazi yao, kumwambia Mfalme kile ambacho miungu inakisema.)

 

      1.     Tuchukulie kwamba Nebukadreza alikumbuka ndoto yake na kuwashirikisha washauri wake, kama walivyoomba. Wangefanya nini? (Inadhaniwa wangemwambia kile ambacho miungu imesema juu ya tafsiri na maana ya ndoto! Ubashiri wangu ni kwamba walikuwa na historia ndefu ya kufanya hivi. Hivyo, huku ni kukiri kwa dhati.)

 

  1.   Changamoto

 

    1.     Soma Danieli 2:12. Je, Mfalme ana hasira sahihi? Je, ana haki ya kukasirika? (Tafakari kile ambacho washauri wamemwambia hivi punde. Hawawezi kuwasiliana na miungu, licha ya uwakilishi wa nyuma kwenye masuala tofauti na hilo. Na wanamwambia kuwa si wao wanaoshindwa kufanya kazi yao kwa ukamilifu, bali mfalme ndiye asiyemudu kazi yake vizuri. Haya si mambo unayopaswa kuyasema ili kumfurahisha bosi wako!)
    2.     Soma Danieli 2:13-14. Ungefanyaje kama ungesikia amri ya Mfalme? Je, “busara na hadhari” vingekuwa njia ya kuelezea jibu lako? Au, je, “mhemko” ndio ungekuwa maelezo mazuri zaidi?

 

      1.     Tumejadili kama adhabu hii ilikuwa ya haki kwa washauri wa Mfalme, lakini je, Danieli na marafiki wake wamewahi kujigamba kwamba wanaweza kutafsiri ndoto? Je, wamewahi kumpotosha Mfalme?

 

      1.     Unapokuwa umetendewa isivyo haki kazini kwako, unapoadhibiwa kwa makosa ya wengine, je, unatawala hisia zako? Je, unakuwa na hekima?

 

    1.     Soma Danieli 2:15-16. Je, ungependelea kwenda mbele ya mfalme? Unakumbuka ile taarifa ya mwisho juu ya mtazamo wake? (Alikuwa “amekasirika na kughadhabika” na alitaka kuwaua wenye hekima. Nisingekuwa na hamu ya kwenda kwa mfalme!)

 

      1.     Utaona kwamba Danieli aliomba kupewa muda zaidi. Soma tena Danieli 2:8. Unadhani Danieli aliahidi kutafsiri ndoto? Ikiwa hakuahidi, basi alikuwa anafanya jambo lile lile ambalo Mfalme aliwatuhumu wenye hekima wengine kulifanya!

 

    1.     Soma Danieli 2:17-18. Ikiwa unadhani kwamba Danieli aliahidi kutafsiri ndoto, je, anajiamini mno? Hii inaonyesha kwamba bado Danieli hajui kama Mungu atamrehemu!

 

      1.     Danieli anafikiria nini kuhusu maombi ya pamoja katika kikundi? Unadhani kwamba maombi ya kikundi ni bora zaidi?

 

    1.     Soma Danieli 2:19. Mungu anaingilia kati na Danieli anamhimidi. Linganisha jinsi unavyoomba kwa nguvu kwa ajili ya msaada na jinsi unavyoomba maombi ya kuhimidi baada ya hapo?

 

    1.     Soma Danieli 2:20-23. Angalia aina ya uhimidi wa Danieli. Hii inaendanaje na tafsiri ya ndoto ya Mfalme? (Maelezo haya juu ya uwezo wa Mungu yanazungumza zaidi kuhusu udhibiti wa Mungu juu ya mambo yajayo (mustakabali).)

 

  1. Tafsiri

 

    1.     Soma Danieli 2:24-25. Kwa nini Danieli anakwenda kwa Arioko kwanza? Je, ana wasiwasi kwamba ataanza kuwaua marafiki wa Danieli? Je, Danieli anajaribu kuwaokoa wenye hekima wengine?

 

      1.     Kwa nini asiwaache hawa wenye hekima wengine wafe? Ikizingatiwa kwamba, hii ni sehemu ya sababu ambayo Mungu aliwatoa watu wa Kaanani. Angalia Kumbukumbu la Torati 18:9-12.

 

      1.     Unafurahi Arioko anapochukua sifa kwa jambo hili? Kwa nini Danieli hakusema, “Hiyo si kweli, nimekuja kwako, hukunifuata?”

 

        1.     Hii inatufundisha nini juu ya nyakati ambazo mabosi wetu wanachukua sifa kutokana na mawazo yetu?

 

    1.     Soma Danieli 2:26. Tafakari kwa makini jinsi ambavyo ungejibu swali hili endapo ungekuwa Danieli.

 

    1.     Soma Danieli 2:27-28. Je, hivi ndivyo ambavyo ungejibu? (Kamwe nisingejibu hivi. Neno langu la kwanza lingekwa “Ndiyo!” Jambo la mwisho ambalo ningelifanya ni kurudia maneno ya wenye hekima yaliyomfanya mfalme aamue kuwaua!)

 

      1.     Unadhani Danieli ni mwerevu kiasi cha kutambua hili?

 

        1.     Ikiwa ndivyo, kwa nini anaanza jibu lake kwa namna ya kipumbavu kabisa – kwa mujibu wa hekima ya kibinadamu? (Anachokilenga Danieli ni kumpa Mungu sifa badala ya kujipatia sifa yeye mwenyewe. Linganisha hili na njia aliyoitumia Arioko.)

 

    1.     Soma Danieli 2:29-30. Kwa mara nyingine, je, hivi ndivyo ambavyo ungejibu? (Daima Danieli anampa Mungu utukufu badala ya kujitukuza yeye mwenyewe. Kama ningekuwa mnyenyekevu ningejibu, “mimi si mwerevu zaidi ya wenye hekima wengine, lakini ninajua nani wa kumwomba.”)

 

      1.     Je, Danieli anasema ukweli kuhusu sababu ya fumbo kufunuliwa kwake? Je, si kwa sababu Danieli alimwomba Mungu ayaokoe maisha yake, na si kwa sababu Mfalme alikuwa mdadisi? (Tukio lote ni kubwa sana kuliko Danieli na marafiki wake. Huu ni ukweli mgumu kwa Wakristo kuukubali – mambo yote si kwa ajili yetu!)

 

    1.     Soma Danieli 2:31-32 na Danieli 2:37-38. Kwa nini Mungu aliipangilia ndoto kwa namna ya kumpa Nebukadreza utukufu wa juu kabisa? (Soma Danieli 2:46 & 48. Huu ni ukweli wa pili wa muhimu, ulioakisiwa katika Yakobo 4:10 na Luka 12:8. Tukimpa Mungu utukufu, kama alivyofanya Danieli, atatuinua na kututukuza. Athari za kupangilia ndoto kwa namna hii ilikuwa ni kumweka Danieli kwenye nafasi ya kumpa Nebukadreza heshima ya hali ya juu. Kumpa heshima bosi wako ni jambo zuri kwa ajili ya uhakika na usalama wa kazi yako!)

 

    1.     Sitakufanya usome Danieli 2:33-45, lakini unapaswa kusoma vifungu hivyo ikiwa hufahamu kisa hiki. Soma Danieli 2:44-45. Ni nini ulio “msingi” wa historia ya dunia? (Mungu mkuu wa Mbinguni atashinda katika historia na ataweka ufalme utakaodumu milele!)

 

    1.     Rafiki, tafakari jinsi siku ya Danieli ilivyogeuka kuwa. Alikuwa mwaminifu kwa Mungu, alimtumaini Mungu, alimpa Mungu utukufu. Matokeo yake ni kwamba Mungu alibadili kile ambacho kingeweza kuwa siku mbaya kabisa maishani mwake na kuwa kile ambacho kingeweza kuwa siku bora kabisa katika maisha yake. Je, utadhamiria kuwa mwaminifu kwa Mungu?

 

  1.   Juma lijalo: Kutoka Kwenye Tanuru Hadi Ikulu.