Somo la 5: Toka Kiburi Hadi Unyenyekevu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Danieli 4)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
1
Lesson Number: 
5

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, ungependa kuepuka fedheha? Mimi ningependa kuiepuka! Kudhalilishwa hadharani ni mojawapo ya mambo mabaya kabisa kwa watu wengi. Inaumiza zaidi ikiwa una hadhi ya juu sana katika jamii yako. Biblia inaonya katika Mithali 16:18 kwamba “Kiburi hutangulia uangamivu; na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.” Somo letu la juma hili ni onyo kwetu. Hebu tuzame kwenye somo letu na tujifunze zaidi!

                

  1.     Habari Njema

 

    1.     Soma Danieli 4:1-3. Ni nani anayeandika sehemu hii ya kitabu cha Danieli? (Mfalme Nebukadreza!)

 

      1.     Je, ungetabiri kwamba angekuwa mwandishi wa Biblia?

 

      1.     Unadhani hiki ni kitu gani? (Ni tangazo la Mfalme kwa watu wote walio chini yake katika kila nchi.)

 

      1.     Utasema nini ikiwa mtu maarufu sana na mwenye nguvu duniani ameandika suala hili kumhusu Mungu? Hiyo ingekuwa zana kubwa ya uinjilisti, sawa?

 

  1.   Habari Zenye Kutia Wasiwasi

 

    1.     Soma Danieli 4:4-5. Maisha ya Nebukadreza yalikuwaje kabla hajaota ndoto? Maisha yake yalikuwaje baada ya kuota ndoto?

 

      1.     Ndoto ya awali ya Nebukadreza (Danieli 2:1) “ilimfadhaisha,” lakini ndoto hii “ilimuogofya.” Je, umewahi kuota ndoto iliyokuogofya?

 

        1.     Unadhani kwa nini ilimuogofya? (Alidhani inaweza kuwa inamuonya kuhusu jambo la kutisha litakalotokea katika siku zake zijazo.)

 

    1.     Soma Danieli 4:6-7. Unakumbuka kwamba kundi hili la wenye hekima hawakuweza kutafsiri ndoto ya kwanza ya mfalme (Danieli 2:10-12). Kwa nini Nebukadreza analeta ndoto kwa kundi lile lile kwa mara ya pili? Kwa nini asiende kwanza kwa Danieli? (Kuna uwezekano kadhaa. Kwanza, kwamba kwa mara nyingine wenye haki wa kipagani walipata upendeleo wa mfalme. Pili, kwamba kazi ya Danieli katika kipindi hiki ilikuwa ni ya kiutawala zaidi kuliko kutafsiri ndoto. Tatu, Danieli alikuwa safarini.)

 

    1.     Soma Danieli 4:8-9. Hii inaashiria sababu gani kwa ushauri wa Danieli kutotafutwa kwanza? (Matumizi ya neno “hatimaye” yanaashiria kwamba ilichukua kipindi fulani kabla Danieli hajaenda kwa mfalme. Hii inaunga mkono dhana ya kwamba alikuwa safarini.)

 

      1.     Kwa nini ucheleweshwaji huu ni jambo chanya? (Unaruhusu uwezo wa Mungu kudhihirishwa baada ya wengine kushindwa.)

 

      1.     Una maoni gani juu ya maelezo ya kwenye mabano kuhusu Danieli na jina lake la Kibabeli? Je, Danieli angeona fahari au angeudhika? (Danieli asingependa hili. Kwanza, Nebukadreza anamhusisha Danieli na mungu wa Kibabeli, na si Mungu wa kweli. Pili, Danieli anapaswa kuwa na “roho ya miungu watakatifu” ndani yake.)

 

        1.     “Roho ya miungu watakatifu” ni kitu gani? (Vyovyote vile miungu hiyo iwavyo, maelezo haya hayampi heshima Mungu wa Mbinguni. Inaonekana kwamba Nebukadreza anajaribu kuhusianisha uwezo wa Mungu na baadhi ya miungu yake.)

 

      1.     Unaweza kuona jambo lolote zuri kwenye rejea ya “roho ya miungu?” (Angalao anachokimaanisha Danieli kwamba ni Mungu, na si yeye binafsi, anayefunua ndoto kimemfikia mfalme. Angalia Danieli 2:27-28.)

 

      1.     Utaona kwamba Danieli ni “mkuu” wa waganga na Nebukadreza hana shaka juu ya uwezo wake kutafsiri ndoto. Hii inatupatia ishara gani ya ziada kuhusu sababu ya Danieli kuchelewa? (Hii inatoa uthibitisho zaidi kwamba lazima jambo fulani hivi kama safari lilisababisha Danieli achelewe. Mfalme anaonekana kupendelea uwepo wa Danieli.)

 

    1.     Soma Danieli 4:10-12. Kutokana na ukweli kwamba Nebukadreza alibadili ndoto iliyoelezewa katika Danieli 2 kuwa jambo lililomhusu kwa asilimia zote, unadhani kimantiki Nebukadreza alifikiria kwamba mti huu uliwakilisha nini? (Sina shaka kwamba Nebukadreza alidhani kuwa mti huu ulimuwakilisha yeye.)

 

    1.     Soma Danieli 4:13-14. Ikiwa ulidhani mti unakuwakilisha, je, ungeogopa pia?

 

    1.     Soma Danieli 4:15-16. Unadhani ilimaanisha nini kwamba kisiki cha shina na mizizi vilisalia? Unadhani “pingu ya chuma na shaba” inamaanisha nini? Unadhani ilimaanisha nini bado kuwa na akili, lakini kuendelea kuwa kama mnyama?

 

      1.     Angalia tena Danieli 4:7. Je, una maoni ya ziada juu ya sababu ya wao kushindwa kutafsiri ndoto? (Inaonekana dhahiri ndoto inahusu mustakabali wa kutisha wa Nebukadreza. Kama mimi ningekuwa wao ningesema, “Hebu tumwachie Danieli.”)

 

    1.     Soma Danieli 4:17-18. Utaona kwamba sehemu ya ndoto inaelezea kuwa inahusiana na utawala wa “falme za duniani.” Je, Nebukadreza ana sababu nzuri kudhani anaingilia kati dhana ya kwamba Mungu wa Mbinguni ni mwenye enzi? (Ndiyo. Hata sasa anarejelea “roho ya miungu watakatifu.”)

 

  1. Habari Mbaya

                           

    1.     Soma Danieli 4:19. Kwa nini Danieli anaogopa?

 

      1.     Kwa nini Nebukadreza anajaribu kumtuliza Danieli?

 

      1.     Je, hii inaonekana kama ni Nebukadreza yule yule aliye na tatizo la kudhibiti hasira? (Huenda hofu yake imetuliza hasira yake.)

 

    1.     Soma Danieli 4:20-22. Je, hofu ya kutisha ya Nebukadreza imethibitishwa?

 

      1.     Ikiwa Mungu anataka kumnyenyekeza Nebukadreza, kwa nini anatumia ndoto inayoanza kwa kuimarisha utukufu wa Nebukadreza?

 

    1.     Soma Danieli 4:24-26. Je, adhabu hii ina lengo mahsusi? (Ndiyo, kumshinikiza Mfalme Nebukadreza kumkiri Bwana.)

 

      1.     Nebukadreza anawezaje kumkiri Mungu wakati ana akili kama ya mnyama? (Lazima alikuwa na uwezo wa uamuzi huu. Ni vigumu kuelewa kwa nini itachukua miaka saba.)

 

        1.     Je, kuna maelezo mengine katika hili – kwamba kipindi hiki hakipo mikononi mwa Nebukadreza, bali kipo mikononi mwa Mungu? Je, tunapaswa kuhitimisha kwamba Mungu anaamini itachukua miaka saba? Je, kipindi hicho cha miaka saba ni cha muhimu?

 

    1.     Soma Danieli 4:27. Je, Nebukadreza anapewa nafasi nyingine?

 

      1.     Je, hii nafasi nyingine ni jambo ambalo Mungu ameliamrisha? Au, je, hili ni jambo tu ambalo Danieli anadhani linaendana na huruma za Mungu?

 

      1.     Hebu tuchimbue marekebisho anayoyapendekeza Danieli. Kwanza, anasema “Ukaache dhambi zako kwa kutenda haki.” Je, huo bado ni ushauri halali kwa ajili yetu leo? Je, matendo mema yanatuokoa?

 

      1.     Pili, anasema, “Ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini.” Ni nani ambaye kwa uwezekano mkubwa ndiye anayewakandamiza watu kule Babeli? (Nebukadreza. Baadhi ya maoni ya watu yanabainisha tatizo la watu kufanyishwa kazi kwenye miradi ya umma bila kulipwa.)

 

        1.     Je, hapa Danieli anawajibika kwa kiasi fulani kwa sababu yeye ni mtawala mkuu?

 

      1.     Je, hili ni onyo kwetu kuhusu kuwahurumia maskini na wanaokandamizwa?

 

      1.     Je, tuna sababu yoyote kuamini kwamba ushauri wa Danieli unahusiana na jambo analojishughulisha nalo Mungu kuhusu Nebukadreza?

 

    1.     Soma Danieli 4:29-31. Hivi punde tumejadili ushauri wa Danieli kwa mfalme. Nebukadreza anachocheaje adhabu ya kwenye ndoto? (Inaonekana kutohusiana kivyovyote vile na marekebisho anayoyapendekeza Danieli. Utakumbuka kwamba Danieli 4:26 alibainisha tatizo tofauti, kwamba Nebukadreza alitakiwa “kukiri kwamba mbingu ndizo zinazotawala.” Kwa mara nyingine Nebukadreza anadai kwamba yeye nyiye mwenye udhibiti.)

 

    1.     Soma Danieli 4:32-33. Unadhani kwa nini Nebukadreza anasikia sauti kutoka mbinguni? Lengo la adhabu lililobainishwa ni lipi?

 

  1.   Urejeshwaji

 

    1.     Soma Danieli 4:34. Kitu gani kimebadilika kuhusu mtazamo wa Nebukadreza? (Hii ni sababu zaidi ya kushangaa ushauri wa Danieli. Nebukadreza anafanya kwa usahihi kilichodhamiriwa kwenye adhabu – kumkiri Mungu mkuu wa Mbinguni.)

 

    1.     Soma Danieli 4:36-37. Ni nini matokeo ya kumpa Mungu utukufu?

 

    1.     Rafiki, yachunguze maisha yako. Je, unampa Mungu utukufu au unajitukuza mwenyewe? Kwa nini, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, usidhamirie kumpa Mungu utukufu katika kila jambo?

 

      Juma lijalo: Toka Ufidhuli Hadi Uangamivu.