Somo la 4: Biblia – Chanzo Chenye Mamlaka cha Teolojia Yetu

Error message

Deprecated function: implode(): Passing glue string after array is deprecated. Swap the parameters in drupal_get_feeds() (line 394 of /home/krwester/gobibletranslations.org/includes/common.inc).
(Marko 7, Luka 16, Matendo 15)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
2
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Masomo yetu yote yamejengwa juu ya Biblia. Kila swali linaanza kwa kusoma kifungu. Si kila kanisa au kikundi cha kujifunza Biblia kina mtazamo wa namna hii. Nakumbuka kutembelea darasa la Shule ya Sabato ambapo wanadarasa walikuwa wamekaa kwenye mzunguko. Wote walikuwa na Biblia, zilizokuwa zimefungwa, na wote walikuwa na vitabu vya mwongozo wa kujifunza Biblia (“lesoni”) ambavyo vilikuwa vimefunguliwa. Wanadarasa walijibu maswali yaliyoibuliwa kwenye mjadala kutokana na kumbukumbu ya kile walichodhani kuwa kimeandikwa, na mara nyingi haikuwa kauli kutoka kwenye Biblia. Niliposoma kifungu cha Biblia na kupendekeza kwamba kinahusika kwenye mjadala, mwalimu alionekana kuona uvivu wa kufungua Biblia yake na kutafuta kifungu hicho! Hebu tuzame kwenye somo letu leo ili tujifunze zaidi kuhusu Biblia kama chanzo chetu chenye mamlaka juu ya kile tunachokiamini!

                

 1.     Desturi na Utamaduni

 

  1.     Soma Marko 7:1-4. Nani anayedhani kuwa wanafunzi wanafuata mtindo ulio bora? (Niko pamoja na viongozi wa Kiyahudi katika suala hili. Utaona kwamba “baadhi” ya wanafunzi hawakunawa mikono yao.)

 

  1.     Soma Marko 7:5. Ungejibuje swali hili? (Bila kuelewa muktadha kwa ukamilifu, ningewaambia wanafunzi, “Jamani ndugu zangu, mnapaswa kunawa mikono yenu.”)

 

   1.     Unadhani kwamba unawaji wa kimapokeo ni sawa na unawaji wa kawaida wa kunawa mikono?

 

   1.     Unadhani kwamba jambo la msingi waliloliwazia viongozi wa Kiyahudi ilikuwa ni usafi? (Uelewa wangu kutokana na kupitia baadhi ya wanamaoni ni kwamba viongozi wa Kiyahudi walikuwa wanatafuta kosa kwa Yesu, na walikuwa wanazungumzia jambo jingine tofauti na unawaji mikono.)

 

  1.     Soma Marko 7:6-8. Jibu la Yesu linaashiria nini kuhusu endapo mjadala unahusu usafi wa kawaida? (Yesu anazungumzia masuala ya kimaadili. Kwangu hiyo inaashiria kwamba viongozi wa Kiyahudi walikuwa hawazungumzii kuhusu masuala ya kawaida ya usafi.)

 

  1.     Hebu tuchunguze kifungu ambacho Yesu anakinukuu. Soma Isaya 29:13. Unayaelezeaje malalamiko ya Mungu kuhusu watu wake? (Wanasema mambo ambayo hawayamaanishi kabisa. Wanatengeneza sheria zao wenyewe.)

 

   1.     Hiyo inatufundisha nini juu ya nia halisi iliyo nyuma ya ukosoaji wa viongozi wa Kiyahudi? (Hili halikuwa suala lenye kutumia akili ya kawaida kuhusu vitendo vya usafi. “Mioyo” ya viongozi hawa ilikuwa mbali kabisa na Mungu. Badala yake, walizingatia zaidi juu ya utamaduni wa kibinadamu.)

 

   1.     Unaona “tamaduni gani za kibinadamu” katika ibada ya eneo lako? Umepitia tamaduni gani maishani mwako? (Nilikuwa katika shule ya sheria katika kipindi cha vuguvugu kali sala la upinzani wa tamaduni. Licha ya hayo, na kutokana na ukweli kwamba nilikuwa maskini, nilivaa tai kila siku. Nilipokuwa mwanasheria, nilivaa suti ofisini hata pale wanasheria wengine walipoacha kuvaa tai. Nilivaa suti kanisani kwa sababu nilidhani kwamba ikiwa nilimtii hakimu kwa kuvaa suti mahakamani, vivyo hivyo ninapaswa kumtii Mungu kwa kuvaa suti kanisani. Siku moja mtu mmoja alinipendekezea kwamba kitendo hiki kinaweza kuwakatisha tamaa wengine, ambao hawakuwa (hawakumiliki) suti, wasiende kanisani. Utamaduni wangu wa kufanya kazi ulikuwa tofauti na wa watu wengine.)

 

    1.     Je, kuvaa tai au suti kanisani ni “desturi ya kibinadamu?” (Biblia haishurutishi jambo hili. Badala yake nina uhakika kwamba kamwe Yesu hakuvaa suti wala tai. Badala yake, ninakumbuka kwamba baadhi ya Wakristo wa awali nchini Marekani walidhani kwamba kuvaa tai hakukuwa na mwonekano mzuri.)

 

    1.     Katika kanisa langu la sasa, viongozi wanavaa kaptura mbele ya kanisa. Unazungumziaje kitendo hicho? (Nina mashaka kama kweli nitavaa kaptura kanisani, lakini ninaamini mtazamo wangu ni suala la desturi ya kibinadamu.)

 

  1.     Soma Marko 7:9-13. Hebu tuiangalie “Korbani” kidogo. Kifungu kinaashiria kwamba Korbani ni kitu gani? (Kifungu kinaashiria, na maoni yanathibitisha, kwamba mtu anaweza kutangaza mali kuwa “Korbani” na kwa kufanya hivyo kungeizuia dhidi ya matumizi mengine. Hivyo, ungeweza kuwazuia wazazi wako wasinufaike na mali hii.)

 

   1.     Yesu anatuambia kwamba hii inakinzana na Biblia. Kwenye mjadala wetu wa awali kuhusu desturi na kile tunachokivaa kanisani, je, desturi inakinzana na Biblia?

 

   1.     Je, hii inaelekea kuunga mkono desturi zisizokinzana na Biblia?

 

 1.   Akili ya Kawaida (Common Sense)

 

  1.     Soma Luka 16:1-3. Kama ungekuwa unamshauri huyu meneja, ungemshauri nini juu ya mustakabali wake? Ungefanya nini endapo ungekuwa meneja huyu?

 

  1.     Soma Luka 16:4-7. Je, hivyo ndivyo ambavyo ungependekeza?

 

   1.     Ikiwa sivyo, kwa nini? (Huu sio uaminifu. Ni kumsaliti bwana wake. Meneja huyu anajisaidia moja kwa moja kwa mgongo wa bwana wake.)

 

  1.     Soma Luka 16:8. Habari hii imechapishwa vibaya? Kitendo hiki kinawezekanaje?

 

  1.     Soma Luka 16:9-10. Unaweza kuelezea jinsi hitimisho hili linalohusu umuhimu wa kuwa mtu wa kuaminika linavyoendana na kusifiwa na bwana?

 

   1.     Bwana alimsifia meneja kwenye jambo gani mahsusi? (Alitenda na kuenenda “kiuerevu.”)

 

    1.     Hiyo inamaanisha nini? (Alitumia akili ya kawaida.)

 

   1.     Unadhani inamaanisha nini kusema “mali ya udhalimu?” (Kinachothaminiwa na ulimwengu: fedha, ushawishi, uzuri na mamlaka.)

 

   1.     Tunaambiwa tufanyie nini mali zetu za duniani? (Tuitumie “kujifanyia marafiki.”)

 

    1.     Tunaambiwa tuwe maarufu? (Nadhani inamaanisha kujifanyia marafiki kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Hiyo inaendana na thawabu ya “kukaribishwa katika makao ya milele.”)

 

   1.     Unadhani mfano huu unatufundisha kuwa waaminifu? (Kutokana na kauli zilizopo katika vifungu vya 10-12, mfano huu hauhusu uaminifu.)

 

    1.     Hii, sasa, inatufundisha nini kuhusu kuwa watumishi wa Mungu wanaoaminika? (Kuwa werevu! Kutumia akili ya kawaida kama jinsi “wana wa ulimwengu” wanavyotumia akili ya kawaida kivitendo.)

 

    1.     Zingatia swali lililobainishwa: tunakuwa watumishi wa Mungu wasio waaminifu ikiwa hatutumii akili ya kawaida?

 

    1.     Je, tunakuwa watumishi waaminifu ikiwa tunatumia akili ya kawaida?

 

   1.     Hii inatusaidiaje kuelewa jinsi tunavyopaswa kuitafsiri Biblia? (Sidhani kama tunapaswa kufuata utamaduni uliozoeleka au “kilicho sahihi machoni mwa watu,” lakini tunapaswa kutumia akili ya kawaida katika jinsi tunavyoitafsiri Biblia na kuenenda kivitendo katika kile inachokisema.)

 

   1.     Uelewa tofauti kidogo wa mfano huu ni kwamba tunapaswa kutumia fedha zetu (mali) kwa mtazamo wa mustakabali wetu mbinguni.

 

 1. Roho Mtakatifu

 

  1.     Soma Matendo 15:1-2. Tohara ni “mila” au “desturi?”

 

  1.     Soma Mwanzo 17:9-10, Mambo ya Walawi 12:1-3, na Yohana 7:22-23. Vifungu hivi vinaashiria nini kuhusu endapo hii ndio desturi pekee?

 

  1.     Hebu tuendelee na kisa chetu. Soma Matendo 15:5-6. Unauchukuliaje uamuzi uliofanywa na kanisa la awali? Je, walikuwa wanajaribu kuyatafsiri Maandiko?

 

   1.     Je, viongozi wa kanisa la awali ni kielelezo kizuri kwetu leo kwenye suala la ufasiri wa Kimaandiko?

 

  1.     Soma Matendo 15:7-8. Petro anajenga hoja kwamba Roho Mtakatifu ana wajibu gani katika kuyaelewa Maandiko?

 

  1.     Soma Matendo 15:12-13 na Matendo 5:19-20. Viongozi wa kanisa waliuchukuliaje utendaji wa Roho Mtakatifu katika kutafsiri kile kilichoonekana kama kauli kinzani kabisa katika Agano la Kale? (Hili ni eneo nyeti sana. Hatutaki kuwakubali manabii wanaokinzana na Biblia kutokana na madai ya uongozi wa Roho. Kwa upande mwingine, ikiwa Roho Mtakatifu anaenenda katika nyanja nyingi kwenye kutangaza uelewa tofauti na wa Biblia, tunatakiwa kuwa makini.)

 

  1.     Rafiki, je, utajifunza kutofautisha kati ya mazoea, desturi na utamaduni, na kufundisha Biblia? Je, utatumia akili ya kawaida (common sense) katika mafundisho ya Biblia maishani mwako? Je, utautafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu katika kuyaelewa mapenzi ya Mungu maishani mwako? Kwa nini usijitoe kwa ajili ya mambo haya sasa hivi?

 

 1.   Juma lijalo: Kwa Maandiko Pekee - Sola Scriptura.