Somo la 7: Kushiriki Neno

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Yeremia 23, Mathayo 7, 2 Timotheo 4, Yohana 17)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
3
Lesson Number: 
7

 

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Tunapaswa kushirikije neno? Kanisa langu mahalia linajitahidi kuondoa vikwazo vyote kwa wageni wanaolitembelea. Tunawapatia eneo la karibu kuegesha magari yao, ikiwa wamevaa kikawaida hawatajisikia vibaya kutokuwa sehemu ya kanisa. Tunawapa zawadi, na kuwakaribisha kila mgeni kwa binafsi yake. Ninakubaliana na njia hii. Kwa upande mwingine, hivi karibuni nilikuwa ninajadiliana na mchungaji wangu kuhusu suala la ubaguzi wa rangi. Aliniambia kuwa ninapaswa kujisikia vizuri kwa sababu nilikuwa “mahali salama.” Nilimjibu kwamba mjadala wetu haupaswi kuwa juu ya “mahali salama.” Nilinukuu Mithali 27:17 kwamba “chuma hunoa chuma.” Njia ipi ya kushiriki neno la Mungu ni sahihi? Au, je, njia zote mbili ni sahihi kutegemeana na mazingira? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

 

  1.    Nyundo, Moto, Ngano

 

    1.    Soma Yeremia 23:28. Je, kunena neno la Mungu kwa uaminifu kunalinganishwa na makapi au ngano? (Kwa dhahiri kunalinganishwa na ngano.)

 

      1.    Unajisikiaje kwenye ulaji wa makapi dhidi ya ngano? (Kimojawapo kina ladha mbaya (kwa wanadamu) na kina virutubisho kidogo.)

 

      1.    Ikiwa neno la Mungu ni sawa na ngano, je, watu wanapaswa kuwa na mwitiko hasi wanapolisikia?

 

    1.    Soma Yeremia 23:29. Hapa neno la Mungu linalinganishwa na kitu gani? (Moto na nyundo ivunjayo mawe.)

 

      1.    Je, kwa upande wako hapo panaonekana kuwa mahali salama?

 

      1.    Hebu tutafakari kwa kina zaidi kuhusu jambo hili. Je, mwamba (jiwe) na nyundo ndio athari ambayo neno la Mungu linayo kwenye maisha yangu au maisha ya wale ambao ninazungumza nao?

 

    1.    Soma Yeremia 23:14. Nani angeweza kutumia moto na nyundo katika mazingira haya? (Wote wawili, yaani mzungumzaji na msikilizaji. Wazungumzaji (manabii) ni wazinzi na wanafiki – wanatembea katika uongo. Wakati huo huo, maneno yao yanahamasisha kutenda uovu, kiasi kwamba hakuna mtu anayeuacha uovu. Wote wawili wanaakisi Sodoma na Gomora.)

 

    1.    Soma Mathayo 7:3-4. Tunaona onyo gani kuhusu ushuhudiaji wa “nyundo na moto?” (Tunatakiwa kuwa makini kutokana na ukweli kwamba tayari nyundo na moto vimeshatumiwa katika maisha yetu.)

 

    1.    Soma Mathayo 7:5. Je, doa linapaswa kuondolewa? (Ndiyo, hili si onyo dhidi ya kutoa ushauri wa kuwaleta wengine karibu na Mungu, bali ni onyo dhidi ya kuwa mnafiki.)

 

      1.    Hebu tuchimbue kwa kina zaidi. Ikiwa neno la Mungu limekuwa nyundo na moto katika maisha yetu, uwezekano mkubwa ni kwamba mtazamo wetu utakuwaje katika kushiriki ukweli na watu wengine? (Tukitambua ugumu wa kutawaliwa na dhambi, moto wetu na nyundo yetu vitakuwa vya upole na huruma.)

 

    1.    Soma Mathayo 7:6. Je, Yesu amebadili mada? Ikiwa sivyo, inamaanisha nini kuacha kuwatupia lulu nguruwe? (Nadhani anatuambia kuwa hatupaswi kuwashuhudia baadhi ya watu. Matokeo ya kuwashuhudia ni kwamba tunashambuliwa.)

 

      1.    Hili linaonekana kuwa gumu! Linaonekana kukinzana na maelekezo yetu ya kawaida. Utaona kwamba sura hii inaanza (Mathayo 7:1) na onyo juu ya kuwahukumu watu. Je, hitimisho kwamba baadhi ni mbwa au nguruwe halihitaji hukumu?

 

      1.    Tutajuaje kwamba wakati fulani si wa kushuhudia? (Hapa ndipo tunapohitaji utambuzi wa Roho Mtakatifu.)

 

      1.    Unaposoma juu ya ushuhudiaji wa wanafunzi wa Yesu, ni mara ngapi walishambuliwa kwa kushiriki injili?

 

      1.    Je, hawakuzingatia kifungu hiki? Unaelezeaje jambo hili? (Soma Mithali 9:7-9. Hukumu iliyovuviwa na Roho ni ya muhimu. Ushauri huu unahusika pale tunapozungumza na mtu mmoja au wawili. Kuzungumza na makundi ya watu wengi ni jambo tofauti kabisa.)

 

  1.   Uvumilivu Wote

 

    1.    Soma 2 Timotheo 4:1-2. Inamaanisha nini kuwa tayari kufundisha injili “wakati ufaao na usiofaa?” Je, kuna wakati unaofaa kwa ajili ya kufanya uinjilisti? (Tunapaswa kujiandaa wakati wote “kulihubiri neno.”)

 

    1.    Hebu tujikite kwenye nusu ya pili ya 2 Timotheo 4:2. Maneno matatu yaliyotumika ni “karipia, kemea na kuonya.” Je, hii inaonekana zaidi kama moto, nyundo, au ngano? (Haya yote yanaonekana kama maneno yaliyokusudiwa kubadili tabia.)

 

      1.    Kwa mara nyingine, je, msisitizo mkubwa umewekwa kwenye kutengeneza “mahali salama?”

 

      1.    Miaka mingi iliyopita mtu mmoja kutoka katika kanisa la jirani alidhani kuwa njia yetu ya kuongoa roho ilikuwa salama mno. Alisema kwa majivuno kwamba wao “walihubiri injili kamili (isiyopindapinda).” Nilipouliza matokeo ya injili hiyo ni yepi, alikiri kwamba hawajamwongoa mtu yeyote kwa muda mrefu. Uzoefu wako ni upi katika uongoaji roho?

 

    1.    Huenda jibu la hayo maswali mawili ya mwisho limejificha kwenye sehemu ya mwisho kabisa ya 2 Timotheo 4:2. Tunapaswa kuwa na mtazamo gani katika kushiriki injili? (“Uvumilivu wote.”)

 

      1.    Unadhani kwa nini “mafundisho” yaliongezewa kwenye “uvumilivu wote?” (“Imani” ndio njia nyingine ya kufasiri “mafundisho.” Hiyo inaniambia kuwa katika njia yetu ya uvumilivu, hatutakiwi kuacha kile Biblia inachokisema. Kuna “injili kamili” ya kuhubiri, lakini tunaileta kwa uvumilivu wote. Hiyo inaashiria kwamba tunaitumia nyundo kwa wepesi.)

 

  1. Baraka Kutoka Kwenye Neno

 

    1.    Soma 2 Timotheo 3:15. Kujifunza Biblia kutakuboreshaje? (Kutakusaidia kuuelewa wokovu vizuri zaidi, njia ambazo kwazo tunaokolewa kutoka kwenye mauti ya milele. Kutakufanya uwe na hekima katika mtazamo huo.)

 

    1.    Soma 2 Timotheo 3:16-17. Ni kwa jinsi gani kujifunza Biblia kunayaboresha maisha yako kwa ujumla? (Kunakufanya uwe kamili, kunakuvika ili uwe tayari kwa kila tendo jema.)

 

      1.    Nilipokuwa mdogo niliambiwa kuwa kujifunza Biblia kutanihekimisha zaidi. Nilikuwa na tamaa ya kuwa na hekima na kufikiri kwa kutumia mantiki zaidi. Je, kifungu hiki kinatoa ahadi hiyo? (Hakisemi kuwa kujifunza Biblia kutaongeza akili yetu ya asili, lakini ninaamini hiyo kuwa kweli katika maisha yangu.)

 

    1.    Soma Yohana 17:13-15. Huyu ni Yesu akizungumza kuhusu wafuasi wake. Lengo la Mungu kwetu ni lipi? (Furaha.)

 

      1.    Lengo la Shetani kwetu ni lipi? (Chuki na uovu.)

 

        1.    Yesu amejiandaa kufanya nini kuhusu tishio hili? (Lengo lake ni “kutulinda na yule mwovu.”)

 

    1.    Soma Yohana 17:16-17. Kujifunza Biblia kunatufanyia nini kwa mujibu wa vifungu hivi? (Kunatutakasa “kwa ile kweli.” Biblia ndio chanzo cha ukweli wetu.)

 

      1.    Yohana 17:14 inatuambia ulimwengu “unatuchukia” kwa sababu sisi “si wa ulimwengu.” Hiyo inamaanisha kwamba hatukubaliani na ulimwengu. Je, umegundua kwamba sasa ulimwengu unatushutumu mara kwa mara kwa chuki?

 

        1.    Jibu la shtaka hilo ni lipi? (Ukweli wa Biblia. Hiyo itatuhakikishia tena na tena kwamba kupachikwa majina ni uongo. Ni jambo la kutarajiwa pale tunapomfuata Yesu.)

 

        1.    Hili ni jambo ambalo limekuwa bayana kwangu katika siku za hivi karibuni tu. Nilidhani kwamba Wakristo walioniambia ni kwa jinsi gani ulimwengu uliwachukia walipungukiwa uwezo wa kutawala hisia – mojawapo ya mbinu zinazofundishwa na Biblia. Siku hizi ninawasikia wapagani wakisema mambo ya kutisha kuhusu washiriki wa kanisa pale yasipokuwa na mantiki kabisa. Ni hivi karibuni tu wapagani walikuwa wanachoma moto bendera na Biblia kama sehemu ya maandamano. Kwa nini waandamanaji wachome moto Biblia?

 

          1.   Je, ni kwa sababu Biblia inawapa Wakristo ujasiri katika mitazamo yao? Kwa sababu inatupatia furaha?

    

    1.    Soma 2 Petro 1:2-3. Kujifunza Biblia (kumjua Mungu) kunatufanyia nini? (Kunatupatia neema na amani. Kunatukirimia “vitu vyote vipasavyo uzima na utaua.” Kunatuingiza kwenye “utukufu na wema.” Zungumzia kitabu cha pekee! Zungumzia ujumbe mzuri ajabu!)

 

    1.    Rafiki, sidhani kama Mungu anatupatia ujumbe wa “mahali salama.” Bali, anatupatia wito wa kushiriki ujumbe wa Biblia kwa uvumilivu wote. Kuielewa Biblia kunatupatia neema, amani, furaha, uhakika na ubora. Hatutatetemeka kupata usalama, tutafurahia kwa uwezo na urafiki wa Mungu mkuu wa mbinguni! Je, unayataka hayo? Kwa nini usitubu na kuamini sasa hivi?

 

  1.   Juma lijalo: Kuhudumu Kama Yesu.