Somo la 8: Kuhudumu Kama Yesu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Luka 15, Mathayo 9, Mathayo 25)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
3
Lesson Number: 
8

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, unakumbuka swali la zamani, “Yesu angefanya nini?” Mara zote nimekuwa na mashaka juu ya umuhimu wa swali hilo katika kutatua maswali yanayowakabili Wakristo. Hali aliyokabiliana nayo Yesu haifanani na hali ninayokabiliana nayo. Kwa upande chanya, nyakati zote alitenda matendo ya ajabu yasiyoyomithilika. Kwa upande hasi, alikuwa na hali ngumu, hususani katika upande wa majaribu. Swali zuri zaidi ni “Je, Yesu angetaka nifanye nini?” Hebu tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu jibu la swali hilo kwa kuzama kwenye somo letu la Biblia!

 

  1.    Ushirikishaji

 

    1.    Soma Luka 15:1-2. Je, malalamiko haya ni tatizo? Kwani wazazi wako hawakukwambia usichangamane na makundi mabaya ya watu? (Bila shaka huu ni ushauri mzuri. Lakini, ukosoaji wa viongozi wa Kiyahudi unaonekana kuwa tofauti. Walidhani kwamba Yesu alipaswa kuwabeza wale wasiotetea viwango sahihi.)

 

    1.    Soma Luka 15:3-4. Yesu anapouliza, “Ni nani kwenu,” anamaanisha nini? (Anamaanisha kwamba wasikilizaji wake wote watakubaliana naye.)

 

      1.    Je, unakubaliana kwamba ungekwenda kumtafuta mmoja aliyepotea? (Aliyepotea ndiye aliye mawazoni mwako zaidi.)

 

    1.    Soma Luka 15:5-6. Je, nawe utakuwa na mtazamo huo huo wa furaha pale unapopata kitu chako kilichopotea?

 

    1.    Soma Luka 15:7. Kwa nini mbingu zinajisikia furaha kwa “mwenye dhambi mmoja atubuye?” (Kwa kuwa 99 wameokolewa. Sasa wote wameokolewa.)

 

    1.    Yesu alielezea kisa hiki ili kujibu mashtaka yaliyotolewa dhidi yake katika Luka 15:1-2. Unalielewaje jibu la Yesu? (Alitumia muda wake na watoza ushuru na wenye dhambi ili kuwaongoa.)

 

      1.    Je, hii inamaanisha kwamba tunapaswa kuacha kufanya kazi na washiriki wenzetu wa kanisa na kutumia muda wetu wote kuwatafuta waliopotea?

 

      1.    Yesu alitumia kiasi gani cha muda na wanafunzi wake tofauti na muda alioutumia na wasioamini? (Yumkini alitumia muda mwingi zaidi na wanafunzi wake.)

 

        1.    Tunapaswa kuhitimisha nini kutokana na hili? (Mfano wa Yesu wa kondoo aliyepotea ni jibu kwa swali moja, na si jibu kwa maswali yote.)

 

      1.    Kuna tofauti gani kuu kati ya Yesu na viongozi wa Kiyahudi? (Viongozi wa Kiyahudi walijitenga na wadhambi. Yesu aliwashirikisha wadhambi.)

 

  1.   Kipaumbele Kwanza

 

    1.    Soma Mathayo 9:1-2. Unadhani kwa nini “watu” walimleta mwenye kupooza kwa Yesu? (Walitaka Yesu amponye ugonjwa wake wa kupooza.)

 

      1.    Je, Yesu alifanya hivyo? (Hapana. Alimsamehe mwenye kupooza dhambi zake.)

 

    1.    Soma Mathayo 9:3-4. Shtaka gani linatolewa dhidi ya Yesu? (Kwamba anakufuru kwa sababu anadai kuwa na uwezo wa Mungu.)

 

    1.    Soma Mathayo 9:5-6. Kwa nini Yesu alimponya mwenye kupooza? (Alimponya ili kujibu mashtaka ya kukufuru.)

 

      1.    Je, hiyo inamaanisha Yesu hakumponya mtu yule kwa kuwa tu alikuwa mwenye kupooza?

 

      1.    Unadhani kwamba bila shtaka la kukufuru Yesu angemponya mtu huyu?

 

    1.    Soma Mathayo 9:7-8. Kisa hiki kinatuambia nini kuhusu vipaumbele vya Yesu? (Alijali zaidi afya ya kiroho ya mtu huyu kuliko afya yake ya kimwili.)

 

      1.    Je, hiyo ndio njia uliyofundishwa? Je, kanisa lako linashughulikia mahitaji ya mwili ya wadhambi kabla ya kushughulikia mahitaji yao ya kiroho?

 

    1.    Soma Mathayo 9:35. Unahusisha umuhimu gani kwenye mpango ambao kazi za Yesu zinaorodheshwa?

 

    1.    Soma Mathayo 9:36. Nini kiliwafanya makutano “wachoke na kutawanyika?” Je, walikuwa wanashambuliwa kimwili? Kwa nini kutokuwa na mchungaji kunatajwa? (Walikuwa na uongozi hafifu wa kiroho. Walifundishwa mambo yanayohusu torati yaliyowafanya wajisikie kuchoka na kutawanyika.)

 

      1.    Je, unazijua hisia hizi?

 

      1.    Nilipokuwa kijana mdogo ninakumbuka kusoma chapisho lililotaarifu kwamba ninapaswa kuishika torati ili niweze kuokolewa. Chapisho hilo halikusema hivyo moja kwa moja, bali lilisema kuwa kama nilikuwa na dhambi hata moja niliyoipenda basi nilikuwa nimepotea. Mwitiko wangu wa masikitiko ulikuwa ni kwamba ikiwa wokovu ulikuwa mgumu kiasi hiki, kwa nini basi kujihangaisha kuutafuta? Kwa nini nisijifurahishe “katika dhambi kwa kitambo” ikiwa kivyovyote vile nitapotea? Nadhani “nilichoka na kutawanyika.” Una maoni gani?

 

      1.    Kwa upande mwingine, niliwahi kuwa na rafiki aliyesema kwamba si vibaya kushiriki kwenye kile nilichodhani kuwa ni dhambi mbaya kwa kuwa “Mungu atanisamehe.” Sikutilia shaka msamaha wa Mungu, lakini nilitilia shaka kama huu ulikuwa mtazamo sahihi. Je, unadhani mtu huyu alikuwa “amechoka na kutawanyika?”

 

    1.    Soma Mathayo 9:37-38. Inamaanisha nini kuwa na “watenda kazi” “mavuno” na “kuchoka na kutawanyika?” (Lazima inamaanisha kuwafundisha injili. Kuwasaidia kuelewa haki kwa imani na sababu ya Mungu kutupatia torati.)

 

      1.    Sasa swali la msingi: Unapaswa kuhudumuje kama Yesu? (Kipaumbele cha kwanza ni kushiriki injili na waliochoka na kutawanyika. Kama Roho Mtakatifu anatia nguvu uwezo wangu (wako) usio wa kawaida ili kuwaponya watu, fanya hivyo pia!)

 

    1.    Je, Yesu aliwahi kufundisha somo la mapishi? Je, aliwahi kufundisha somo la usimamizi wa fedha?

 

      1.    Kama jibu lako ni “hapana,” kwa nini Wakristo wanafundisha masomo ya aina hii kama sehemu ya kuwafikia watu kiroho? (Hii ni mojawapo ya sababu kwa nini ninadhani swali la, “Je, Yesu angetaka nifanye nini?” ni bora zaidi kuliko kuliko swali la “Yesu angefanya nini?” Somo la mapishi ni njia isiyo ya mwujiza ya uponyaji mwili. Kufundisha usimamizi wa fedha ni njia isiyo ya mwujiza ya kuwafanya watu wasichoke na kutawanyika.)

 

  1. Mambo Yasiyo ya Kipaumbele Kwanza?

 

    1.    Soma Mathayo 25:31-33. Yesu anaelezea tukio gani? (Ujio wake wa Mara ya Pili na hukumu ya mwisho.)

 

    1.    Soma Mathayo 25:34-36. Hebu subiri kidogo! Inawezekanaje hukumu ikajengwa juu ya matendo? Hivi punde tumegundua kwamba kushiriki injili na wengine ndio wajibu wetu wa kwanza, kifungu hiki kinasema kugawa chakula na kinywaji ndio wajibu wetu wa kwanza (na pekee?). Unaelezeaje kotokuwiana huku?

 

    1.    Soma Mathayo 25:37-39. Je, wale waliookolewa hawana uelewa wa Biblia? Inawezekanaje wasiwe na ufahamu wa Mathayo 25? Inawezekanaje wasijue uhusiano kati ya kuwasaidia masikini na kumsaidia Yesu?

 

      1.    Visa vya Yesu kuwalisha makutano havionekani kuhusiana na hali ya kiuchumi ya wasikilizaji. Je, injili zinaweka kumbukumbu ya Yesu kuwapatia masikini chakula, maji wenye kiu, nguo kwa walio uchi, au kuwatembelea wafungwa?

 

        1.    Je, huu ni mfano mwingine wa kwa nini “Je, Yesu angefanya nini?” ni swali hafifu?

 

    1.    Soma Yohana 6:53-56. Yesu anahusianisha chakula na kinywaji gani na uzima wa milele?

 

    1.    Soma Yohana 4:34-35. Chakula gani kinahusianishwa na “mavuno?”

 

    1.    Soma Yohana 6:26-27. Chakula gani ni bora kuwa nacho?

 

    1.    Soma Wagalatia 3:22-24. Kifungo kibaya kabisa ni kipi?

 

      1.    Ni kwa jinsi gani haki kwa imani pekee inakuweka huru dhidi ya kifungo hiki?

 

    1.    Je, unadhani kauli za Yesu katika Mathayo 25 ni za kiishara? (Ikiwa unakubaliana, hiyo inaendana na dhana ya kwamba kushiriki injili na wengine ndio wajibu wetu wa kwanza. Kwa kuongezea, inaimarisha fundisho la haki kwa imani.)

 

      1.    Ikiwa kauli za Yesu kuhusu kugawa chakula, kinywaji, na kuwatembelea wafungwa ni mambo ya kiishara, je, hii inaelezea sababu ya wenye haki kuchanganyikiwa kuhusiana na swali?

 

    1.    Soma Luka 3:11. Je, Yesu anawajali wale ambao kiuhakisia hawana chakula? (Ndiyo. Pendekezo langu kuhusu uelewa sahihi wa Mathayo 25 haituondolei wajibu wa kuwapenda wanadamu wenzetu. Hata hivyo, linafafanua jinsi tunavyopaswa kushuhudia na mada ya msingi ya ushuhudiaji wetu.)

 

    1.    Rafiki, Yesu anakutaka ushiriki injili na wengine.  Je, kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, utashiriki na wengine kile ambacho Yesu amekutendea?

 

  1.   Juma lijalo: Kujenga Mtazamo Unaoongoa.