Somo la 8: Elimu na Ukombozi
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mtazamo wa watu wengi juu ya Mungu ni kwamba yeye ni Baba yetu. Kama ulikuwa na baba mzuri, kama ilivyokuwa kwangu, basi mtazamo huu ni wa msaada sana. Mtazamo mwingine, unaoweza kuwa wa msaada zaidi kwa wale ambao hawakuwa na baba wazuri, ni kwamba Mungu ni mwalimu wetu. Kwa hakika kila mtu angalao alikuwa na mwalimu mmoja mzuri. Somo letu juma hili limejikita kwenye mada ya Mungu kama Mwalimu wetu. Mungu atatufundisha mambo ya aina gani? Je, ni mambo ya kiroho pekee? Hebu tuzame kwenye Biblia yetu na tujifunze zaidi!
- Kama Mwalimu Wetu
-
- Soma Mwanzo 1:26. Kamwe hatujawahi kumwona Mungu. Unadhani Mungu alimaanisha nini aliposema kuwa atatufanya “kwa mfano wetu, kwa sura yetu?” (Unapowafikiria viumbe hai wengine ambao waliumbwa, hakuna kiumbe hata mmoja anayefikiria kama sisi au, kwa kiasi kikubwa, anayefanana na sisi. Ninahisi hicho ndicho ambacho Mungu alikuwa anakizungumzia.)
-
-
- Mjadala wa “kutawala” unaongezea nini kwenye uelewa wetu wa kile ambacho Mungu alikimaanisha? (Kuwatawala wanyama kunamaanisha kuwa fikra yetu ni ya hali ya juu kuliko fikra yao.)
-
-
-
- Mungu anapoandika kuwa tuliumbwa kwa mfano wake, alikuwa anajaribu kutufundisha nini?
-
-
- Soma Mwanzo 1:27. Kifungu hiki kinahabarisha kuwa wanadamu waliumbwa “mwanamume na mwanamke” na hii ni kwa mfano wa Mungu. Unalielewaje jambo hili?
-
-
- Kwa ujumla wanaume na wanawake wanaonekana kufanana, lakini kuna tofauti za muhimu. Mungu anafanana na tofauti ipi? (Kimwili, Yesu alizaliwa kama mwanaume. Maana ya msingi, ninaamini, ni kwamba kwa pamoja, mwanaume na mwanamke wana uwezo wa kuzaliana – kuumba uhai mpya. Huo ni uakisi wa Mungu Muumbaji wetu.)
-
-
- Soma Mwanzo 5:3. Ingawa hatuna uhakika Mungu alimaanisha nini aliposema kuwafanya wanadamu kwa mfano wake, je, unafahamu kwa uhakika ilimaanisha nini kwa Sethi kuzaliwa kwa “sura” ya Adamu na “kwa mfano wake?”
-
-
- Je, tunapaswa kusoma lugha hii, tunayoielewa wazi, kule kwenye lugha tuliyoisoma katika Mwanzo 1:26? Je, hii inafunua maana ya Mwanzo 1:26? (Nadhani hiyo ndio sababu ya kurudia lugha ile ile. Tunapofikiria jinsi tunavyofanana na wazazi wetu, vivyo hivyo tunafanana na Mungu kwa namna hiyo hiyo.)
-
-
-
-
- Je, hiyo ni sahihi? Tunafahamu kuwa hatukaribii kufanana na Mungu kiakili, kiuwezo, na kimamlaka. Watoto wanajilinganisha na wazazi wao. Je, tunapaswa kujilinganisha na Mungu?
-
-
- Mwalimu wa Mfano
-
- Soma Isaya 11:1. Je, kifungu hiki kinahusu kilimo cha bustani? (Soma Warumi 15:11-12. Hii inabainisha kuwa Isaya anamzungumzia Yesu. Kama una mashaka, soma muktadha mpana katika Warumi 15:8-13.)
-
- Soma Isaya 11:2. Je, Roho wa Mungu anapatikana kwa ajili yetu? (Soma Yohana 14:26. Yesu anasema kuwa atampeleka Roho Mtakatifu ili atufundishe.)
-
- Angalia tena Isaya 11:2. Roho ya hekima na ufahamu ni ipi? Je, unayo?
-
-
- Je, hekima ni sawa na ufahamu? (Hapana. Ufahamu ni kuzijua kweli. Ni kuufahamu uhalisia. Hekima ni kufanya uchaguzi sahihi ili kupata matokeo bora yanayotokana na kweli zilizopo.)
-
-
- Angalia tena Isaya 11:2. Roho ya ushauri na uweza ni ipi? Je, unayo?
-
-
- Kwa nini ushauri na uweza vinatajwa kwenye sentensi moja? Je, maneno haya yanahusiana kwa namna fulani? (Ushauri ni kutoa mawaidha. Uweza ni uwezo wa kufanyia kazi ushauri wako. Hali bora ni pale unapofahamu nini cha kufanya na una ujasiri na uwezo wa kutenda.)
-
-
- Angalia tena Isaya 11:2. Roho ya maarifa na ya kumcha Bwana ni ipi? Je, unayo?
-
-
- Je, “maarifa” ni kujirudia tu kwa “ufahamu?” (Kuunganisha “maarifa” na “kumcha” inaashiria kuwa kifungu hakizungumzii ufahamu wa jumla wa mazingira ya aina mbalimbali, bali uelewa maalumu wa Mungu. Dhana iliyopo ni kwamba tunamjua Mungu na tunachukua uamuzi wa kuenenda kwa namna inayoendana na uelewa wetu wa mapenzi yake. Hii inanikumbusha maneno yaliyopo kwenye Sala ya Bwana “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”)
-
-
- Soma Isaya 11:3. Hebu tuendelee na njia ya kile ambacho mfano wa Yesu unatufundisha. Maneno “furaha” na “kumcha” mara nyingi hayapatikani yakiwa pamoja. Inamaanisha nini “kufurahi katika kumcha Bwana?” (Unafurahia kumtii Mungu.)
-
-
- Unaweza kulielezea jambo hilo? Kwa muktadha mwingine wowote ule, je, unafurahia kuheshimu kitu fulani? (Ninamiliki gari lenye uwezo mkubwa sana. Ninaheshimu kwamba uwezo wote huu unaweza kuniingiza kwenye matatizo, licha ya hayo bado ninaufurahia uwezo huo. Ufahamu wangu mzuri kabisa ni kwamba ninafurahia uhusiano wangu na Mungu mwenye upendo na uwezo mkuu.)
-
-
- Hebu tuangalie nusu ya pili ya Isaya 11:3. Je, kwa kawaida huwa unachukua uamuzi bila kuwa na taarifa za kina? Inamaanisha nini kuchukua uamuzi unaopuuzia unachokiona na unachokisikia? (Hii haijengi uamuzi usiojengwa juu ya taarifa za kina. Bali, kinachomaanishwa ni kwamba tunachukua uamuzi unaojengwa kutokana na uelewa wetu wa mapenzi ya Mungu badala ya mwonekano wa mambo au hoja za ulimwengu.)
-
- Soma Isaya 11:4. Kwa mara nyingine, hii inamzungumzia Yesu, lakini tunayaangalia mafundisho kwa ajili ya maisha yetu. Ni nini ulio msingi wa kuchukua uamuzi tunaouona hapa? (Hii inathibitisha mjadala wetu wa awali kwamba haki ya Mungu, na si hisia zetu, ndio kipimo cha hukumu.)
-
-
- Tunajaribiwaje, kama wanadamu, kutenda vinginevyo? (Masikini na wanyonge hawawezi kutusaidia. Tunapaswa kufanya uamuzi kwa haki, bila kujali kama tumenufaika binafsi.)
-
-
- Angalia tena sehemu ya mwisho ya Isaya 11:4. Hapo kabla tulizungumza kuhusu kutii, badala ya kumwogopa Mungu. Je, tumehafifisha isivyostahili uoga halisi? (Mara zote hicho ndicho huwa ninakijali tunapotafakari mada hii. Hii inabainisha kuwa Mungu ananena (“fimbo ya kinywa chake”) na anawaua waovu. Pambano kati ya wema na uovu ni suala zito. Mungu sio tu kwamba ni Baba yetu mpendwa wa mbinguni, na Yesu kaka yetu mpendwa, hii inatuambia kuwa Yesu atatekeleza hukumu kwa waovu.)
-
-
-
- Kwa kuwa tunatafuta mifano inayofundisha kwa ajili ya maisha yetu, je, tunapaswa pia kufuata tabia ya Mungu kwenye mfano wa kipengele cha hukumu? (Kwa dhahiri, hatupaswi kumuua mtu yeyote, lakini ninadhani tuna mambo ya kujifunza hata katika hiki kipengele cha tabia ya Yesu.)
-
-
-
- Soma 1 Wafalme 4:29-30. Je, huu ni uthibitisho wa kile ambacho tumekuwa tukikijadili – kwamba Mungu atatupatia hekima na ufahamu?
-
-
- Kama umesema, “ndiyo,” unadhani hili linatokeaje? Je, Mungu ananena tu na Sulemani anaipokea? Au, unadhani kuwa inaendana zaidi na mambo tuliyoyajadili awali, kwamba hili ni suala linalowezeshwa na Roho Mtakatifu tunapokabiliana na mambo mbalimbali maishani? (Tofauti halisi ni kwamba njia ya pili inatufanya tuendelee kutembea na Mungu. Hilo lilikuwa tatizo kwa Mfalme Sulemani.)
-
-
- Soma 1 Wafalme 4:31. Tunaishi katika siku ambazo elimu ina msukumo mkubwa kuelekea kwenye usawa. Baada ya mwaka wangu wa kwanza wa shule ya sheria, miongo kadhaa iliyopita, shule iliacha kupanga madaraja ya ushindi wa wanafunzi darasani. Hivi karibuni zaidi, watoto wangu walipokuwa sekondari (high school), wakati zawadi kwa washindi kimasomo zilipokuwa zinatolewa, mkuu wa shule alisema jinsi ambavyo wanafunzi wote walistahili zawadi. Tunapaswa kuhitimisha nini kutokana na uamuzi wa Mungu kumfanya Sulemani kuwa na hekima zaidi kuliko “watu wote?” (Mungu anaamini katika sifa njema kutokana na uaminifu. Sifa njema katika muktadha huu humpa utukufu Mungu na Sulemani.)
-
- Soma 1 Wafalme 4:32-33. Tunapaswa kutafuta aina gani za hekima? Je, ni hekima tu inayohusu haki? (Tunajifunza kuwa Sulemani aliandika nyimbo, alikuwa mtaalamu wa miti, maua, na aina zote za wanyama.)
-
-
- Hii inaashiria nini kwako kwa kuzingatia taaluma yako? (Tunapaswa kumwomba Mungu atufanye kuwa bora zaidi katika kile tunachokifanya! Tunapaswa kujitahidi kuwa bora zaidi!)
-
-
-
-
- Je, hili pia ni jambo ambalo Roho Mtakatifu atatuongoza?
-
-
-
-
-
- Mara kwa mara huwa ninasikia kuwa hatupashwi kung’ang’ana kuwa bora, bali kujitahidi kutenda kwa kadiri tunavyoweza. Ikiwa Roho Mtakatifu anatuwezesha, je, kweli “ubora wetu” ni mzuri vya kutosha?
-
-
-
- Rafiki, Mungu ana hamu ya kuboresha uelewa wetu na uwezo wetu. Je, utamwomba Roho Mtakatifu akuelimishe zaidi?
- Juma lijalo: Kanisa na Elimu.