Somo la 8: Huru Kupumzika

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Marko 2, 1 Wafalme 18
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
3
Lesson Number: 
8

Somo la 8: Huru Kupumzika

(Marko 2, 1 Wafalme 18)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Mara ngapi mtu amekujia kwa ajili ya msaada, na ukatambua kuwa jambo fulani haliko sawa? Kile wanachodhani kuwa wanakihitaji sicho ambacho kiuhalisia kinahitajika. Kwa mfano, mtu anakujia (kwa mara nyingine) kukopa fedha. Kile ambacho hasa mtu huyo anakihitaji ni bajeti, kujidhibiti, au kazi nzuri. Somo letu juma hili linaangalia visa viwili kwenye Biblia vinavyoelezea juu ya kuangalia chanzo cha mambo yanayotusumbua maishani. Kugundua chanzo ni muhimu katika kupata pumziko la kweli. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Mwenye Kupooza
    1.    Soma Marko 2:1-3. Unadhani kipaumbele cha kwanza cha Yesu kilikuwa ni kipi: kufundisha (kuhubiri) au kuponya? (Lazima mahubiri yake ndio yaliyokuwa kipaumbele chake cha kwanza. Uponyaji ulitokana na huruma yake kwa watu wanaoteseka na tamaa yake ya kuwavuta watu kwenye mahubiri yake.)
    1.    Soma Marko 2:4. Unachukuliaje pale kipaumbele chako cha kwanza kinapoingiliwa na vipaumbele vya watu wengine?
      1.    Fikiria unahubiri na ghafla panatokea kelele kubwa zinazotokana na kutoboa paa. Hii inafuatiwa na mwanguko wa kitu kwako na kwa watu unaowahubiri. Utakuwa na mwitiko gani ikiwa unajaribu kuhubiri wakati kitendo hiki kinaendelea?
        1.    Je, utawachukulia watu wanaobomoa paa kuwa watu wasiojali wala kuwafikiria wengine na mafidhuli?
      1.    Jiweke kwenye nafasi ya marafiki wa mtu mwenye kupooza. Je, ungeliangalia kundi la watu na kufanya uamuzi wa kurudi kesho?
        1.    Kitu gani kiliwahamasisha kusonga mbele?
        1.    Je, unawachukulia kama watu wasiojali wengine na mafidhuli? Au, unawachukulia kama watu wenye upendo, wenye kujali, na watu wa muhimu katika kumsaidia rafiki yao?
        1.    Watu wa kanisani kwako wanapokuwa wanateseka, je, mtazamo wako ni ule wa “hetu turudini kesho” au “hebu tutoboe tundu kwenye paa sasa hivi?”
    1.    Soma Marko 2:5. Yesu aliitikiaje kitendo hicho? Je, alikereka kwa ushenzi wao?
      1.    Hebu rudi nyuma kidogo na utafakari kitendo cha utoboaji na hubiri la Yesu. Je, utoboaji ni jambo jema kwa kile kinachofuatia? (Ndiyo. Ulifanya usikivu wa watu ujielekeze kwenye kile alichokisema na kukifanya Yesu kwa yule mtu aliyepooza. Utoboaji ulikuwa baraka kwenye utume wa Yesu.)
      1.    Yesu alijenga hitimisho lake kwenye kitu gani (kifungu cha 5) juu ya imani “yao?” (Matendo yao.)
      1.    Kifungu kinamrejelea nani kinaposema, “imani yao?”
    1.    Tatizo ni kwamba mtu huyu amepooza. Jiweke kwenye nafasi ya marafiki. Umetoka tu kufanya kazi na aibu ya kutoboa paa mbele ya umati huu mkubwa. Badala ya kumponya rafiki yako, Yesu anasema, “Umesamehewa dhambi zako.” Utajisikiaje?
      1.    Unadhani kwa nini Yesu anazungumza kuhusu dhambi? (Soma Yohana 9:1-3. Utambuzi wa kawaida ulikuwa ni kwamba ugonjwa ulisababishwa na dhambi. Kwa dhahiri, baadhi ya magonjwa yalisababishwa na dhambi. Kama ugonjwa wa mwenye kupooza ulisababishwa na dhambi au kama alidhani tu kuwa ulitokana na dhambi, kwa dhahiri dhambi yake ndilo jambo lililomhangaisha kwanza. Yesu alishughulika na mzizi wa kilichomhangaisha zaidi mwenye kupooza.)
    1.    Soma Marko 2:6-7. Je, walimu wa sheria wako sahihi? (Ndiyo. Mungu pekee ndiye anaweza kusamehe dhambi.)
      1.    Marko ana ujumbe gani kwetu?
    1.    Soma Marko 2:8-9. Jibu kwa swali la Yesu ni lipi? Kitu gani ni rahisi?
      1.    Kama umejibu “Dhambi zako zimesamehewa,” je, una uhakika?
    1.    Soma Marko 2:10-12. Endapo walimu wa sheria wasingekuwa wanafikiria kwa kina, je, mwenye kupooza angeponywa?
    1.    Je, inaleta mantiki kuamini kwamba kila anayeponya pia anaweza kusamehe dhambi? (Ni kweli kwamba uponyaji hutokana na uwezo wa Mungu. Lakini si kila anayeponya ni Mungu. Ninadhani Yesu alikuwa anajenga hoja tofauti. Wakosoaji walikuwa wanasema, “Hii ni hewa yenye joto (na yenye makufuru). Mtu yeyote anaweza kusema jambo lolote.” Yesu anaonesha kuwa maneno yake yana nguvu. Anaposema kuwa ninaweza kusamehe dhambi, wanatakiwa kuyachukulia maneno yake kwa dhati.)
  1.   Eliya
    1.    Soma 1 Wafalme 18:21-24. Je, hili ni jaribu la haki?
      1.    Kwa nini Eliya anasema kuwa yeye pekee ndiye nabii wa Mungu? (Sio haki kwa viwango vya wanadamu kwa Eliya kuwa kinyume na watu 450. Hii inaashiria uwezo wa Mungu. Pia inasema jambo fulani kuhusu mtazamo wa Eliya.)
    1.    Soma 1 Wafalme 18:27-29. Je, huu ni mjadala wenye heshima? Je, Eliya anawahurumia manabii wa uongo? Unauchukuliaje mtazamo wake?
    1.    Soma 1 Wafalme 18:36-38. Ungejisikiaje kama ungekuwa Eliya?
    1.    Soma 1 Wafalme 18:40 na 1 Wafalme 18:45-46. Unaelezeaje juu ya mtazamo tofauti dhidi ya Mfalme Ahabu na manabii wa uongo? Kwani Ahabu si mfadhili wao?
      1.    Unauelezeaje mtazamo wa Eliya?
    1.    Soma 1 Wafalme 19:2-3. Hili linawezekanaje? Anawezaje kuogopa kitu chochote?
      1.    Utaona kwamba kituo chake cha kwanza ni Yuda. Mwana maoni mmoja alibainisha kuwa kama suala halisi lilikuwa ni woga juu ya uhai wake, Eliya angekuwa salama kule Yuda ambapo Yehoshafati angemlinda dhidi ya Yezebeli. Kumwacha mtumishi wake na kuendelea kukimbia kuelekea jangwani inamaanisha kuwa tatizo ni jambo fulani la ndani zaidi.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:4. Unadhani Eliya anamaanisha nini anaposema “yatosha?” (Amekuwa na mgogoro wa kutosha. Amechoka kupambana.)
      1.    Je, umewahi kujisikia hivi: kuchoka sana, sonona, au suala la afya ya akili lenye kufanana na hayo lisiloleta mantiki yoyote?
      1.    Je, anafanana na yule mwenye kupooza kwa maana ya kwamba tatizo halisi haliko bayana?
    1.    Soma 1 Wafalme 19:6. Mungu anashughulikaje na aina hii ya tatizo la akili? (Anaonesha kuwa anajali. Anampa Eliya vitu ambavyo ni kinyume na kumwacha afe.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:7-8. Nini kinafuata baada ya kuponya aina hii ya tatizo? (Kumtafuta Mungu. Mungu anamsaidia katika juhudi hizi.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:9-10. Malalamiko makuu ya Eliya ni yapi? (Yuko peke yake.)
      1.    Je, hiyo ni kweli? (Alikuwa mpweke dhidi ya makuhani wa Baali.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:11-12. Mungu ana ujumbe gani kwa Eliya katika kielelezo hiki? (Kwamba Mungu ndiye mdhibiti wa mambo yote ya asili. Eliya anaweza kujisikia mpweke, mtu mmoja dhidi ya kila mtu, lakini Mungu anayedhibiti mambo ya asili yuko upande wake.)
      1.    Inamaanisha nini kwamba Mungu “hakuwamo” kwenye upepo, tetemeko la nchi, au motoni?
      1.    Je, hii inahusiana na moto uliyoila ile kafara? (Ndiyo! Mungu ana uwezo na mambo ya kutisha kabisa pamoja na udhihirishaji wa utukufu kutokana na uwezo wake. Eliya anahangaika kwamba Mungu amemwacha peke yake dhidi ya maadui wa Mungu. Mungu anamwonesha Eliya kwamba njia za Mungu hazitokani na nguvu changa.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:13-14. Je, Eliya anauelewa ujumbe wa Mungu? (Sidhani kama anauelewa kwa sasa.)
    1.    Soma 1 Wafalme 19:15-17. Mungu anafanyaje kazi? (Hahitaji moto ushuke kutoka mbinguni. Hahitaji watu wengi kuwa upande wake. Yupo tu ndani ya udhibiti wake.)
      1.    Hebu tujikite kwenye 1 Wafalme 19:16. Eliya alitoa maombi gani mawili binafsi? (Alisema, “yatosha” na kwamba alitaka kufa. 1 Wafalme 19:4.)
        1.    Mungu anajibuje ombi la Eliya la kuondolewa majukumu? (Anajibu kwa kumpatia mrithi.)
        1.    Mungu anajibuje ombi la Eliya la kutaka kufa? (Soma 2 Wafalme 2:11. Sasa Eliya ana umri wa maelfu ya miaka!)
        1.    Hii inatuonesha nini kuhusu Mungu wetu?
    1.    Rafiki, Mungu anajua mambo ya ndani katika hali na mazingira yanayokukabili. Anakujali, yeye ndiye mdhibiti, na atakusimamia na kushughulikia mambo yako. Je, utamtumaini leo?
  1. Juma lijalo: Mahadhi ya Pumziko.