Somo la 13: Pumziko la Mwisho
Somo la 13: Pumziko la Mwisho
(Luka 21, Mathayo 24, Ufunuo 14)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kwa sasa inaonekana kwamba nchini Marekani uhuru wetu uko chini ya shambulio lisilo la kawaida. Ubashiri wangu ni kwamba popote pale ulipo hapa duniani hisia ni hizo hizo. Serikali mbalimbali zimechukua hatua madhubuti kupunguza uhuru binafsi kuhusiana na virusi vya UVIKO 19. Ingawa Biblia haisemi chochote nilichokiona kuhusiana na Wakristo kukabiliana na matatizo yanayohusiana na virusi hivyo, nimewasoma baadhi ya Wakristo wanaoelezea mtazamo kuwa kitendo cha hivi karibuni cha serikali kugandamiza haki kinaweza kuwa dalili ya mateso katika wakati wa mwisho. Je, hii inatuelekeza kwenye “pumziko la mwisho?” Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi kuhusu matukio yanayotuelekeza kwenye ujio wa Mara ya Pili!
- Ishara za Mwisho
-
- Soma Luka 21:5-7. Wanafunzi wanauliza maswali gani mahsusi? (Wanauliza kuhusu ishara na muda wa kuangamizwa kwa Yerusalemu.)
-
- Soma Mathayo 24:1-3. Wanafunzi wanauliza maswali gani kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mathayo? (Mathayo anaunganisha maswali mawili: 1. Yerusalemu itaangamizwa lini? 2. Ishara za ujio wa Mara ya Pili (mwisho wa dunia) ni zipi?)
-
-
- Kwa nini wanafunzi wanamwendea Yesu faraghani? (Itakuwa walidhani kuwa hii ni taarifa ya ndani (si taarifa kwa umma).)
-
-
- Soma Mathayo 24:4. Je, Yesu yuko sahihi kujali suala hili? (Tunaliona hili kwenye tofauti iliyopo kwenye maelezo yaliyotolewa kati ya Luka na Mathayo. Mathayo anaingiza mkanganyiko mkubwa zaidi kwa namna anavyoandika jambo hili.)
-
- Hebu turejee kwenye maelezo ya Luka kwa kuwa mpangilio wake ni mkubwa zaidi. Pitia kwa haraka haraka Luka 21:10-15 na usome Luka 21:16-19. Yesu anamwelezea nani hapa? (Anawaelezea wanafunzi. Maelezo mfanano ya Mathayo yanafanya iwe vigumu kutofautisha matukio ya nyakati za mwisho.)
-
- Katika Luka 21:20-24 kwa umahsusi Luka anaelezea kuangamizwa kwa Yerusalemu. Kisha anageukia wakati wa mwisho. Soma Luka 21:25-26. Hebu tuvunjevunje jambo hili. Tunaona ishara gani kutoka baharini? (Dunia iko hatarini kutokana na nguvu ya bahari.)
-
-
- Je, hilo ndilo jambo tunaloliona sasa? (Sitaingia kwenye masuala ya kuongezeka kwa joto duniani, nilipokuwa kijana mdogo wanasayansi walikuwa wanatabiri kuganda kwa dunia. Lakini, wengine wanatabiri kuwa kiwango cha maji kitaongezeka.)
-
-
-
- Je, umesoma chochote kuhusiana na ishara kwenye falaki (galaxies) - kundi la nyota na sayari ikiwemo yetu - na mwisho wa nyakati? (Nilipokuwa mdogo, baadhi ya walimu wangu walikuwa wakionyesha ishara angani zilizokuwa zikionekana katika eneo la New England nchini Marekani. Hilo linaonekana kutofikiriwa kwa kina pale unapotafakari kuwa Yesu anatoa unabii kwa ajili ya ulimwengu wote.)
-
-
- Soma Ufunuo 14:6-7. Je, hii ni sehemu ya ujumbe wa wakati wa mwisho? (Nadhani ndiwo kwa sababu unarejelea saa ya hukumu ya Mungu.)
-
-
- Amri ya kwanza ya huu ujumbe wa hukumu ni ipi? (Kumcha, kumsujudu, na kumtukuza Mungu Muumbaji.)
-
-
- Hebu turejee kwenye Luka 21:25. Je, kuna ishara kwenye falaki kwamba Mungu ni Muumbaji wetu? (Kwa sasa ushahidi wa kisayansi ni mkubwa kuliko wakati wowote ule katika historia. Kuna ushahidi mkubwa kuwa falaki zilianza wakati mahsusi. Kuna vipengele vingi muhimu maishani (pamoja na falaki) ambavyo sasa vinaeleweka vizuri. Haiwezekani kwamba mambo yote haya yalitokea kwa bahati. Kama alivyosema mtaalamu maarufu wa astrofizikia (sayansi ya hali ya nyota kikemikali na kimaumbile) ambaye pia hamwamini Mungu: “Tafsiri ya kawaida ya kweli zisizoepukika inaashiria kuwa akili ya hali ya juu inakubaliana na fizikia, pamoja na kemia na baiolojia, na kwamba hakuna nguvu zisizoeleweka zinazostahili kuzungumziwa kwenye mambo ya asili.” Kama unataka kujifunza zaidi, fanya utafiti kwa kuandika maneno “the fine-tuned universe” kwenye mtandao.)
-
- Angalia tena Luka 21:26. Ishara za namna gani zinawafanya watu wauogope mustakabali wao? (Huu ni unabii mahsusi kabisa – wanaastrofizikia wataona jambo lisiloenda vizuri katika falaki (galaxies) kitakachohatarisha mustakabali wa ulimwengu.
-
- Soma Luka 21:27-28. Luka anatuambia tufanye nini tunapoanza kuona ishara hizi? (Tuwe makini! “Changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu!”)
-
- Soma Mathayo 24:23-26. Tunaona ishara gani zinazokomea hapa duniani? Ishara ambazo zinaweza kuwadanganya Wakristo makini? (Ishara kuu na maajabu. Mambo ya kushangaza na kustaajabisha yako mbele yetu!)
-
-
- Tunapaswa kufanya nini na taarifa kama hizi za watu wanaodai kuwa wao ndio Kristo? (Hatupaswi kufanya chochote. Kifungu kinasema kuwa tusiwafuatilie.)
-
- Maana ya Ishara
-
- Soma Mathayo 24:36. Je, tunaweza kubashiri Yesu atakuja lini? (Kifungu hiki kinasema kuwa hakuna ajuaye.)
-
- Soma Mathayo 24:32-33. Kama hatuwezi kujua Yesu atakuja lini, kwa nini tuwe makini kwa kuzingatia ishara? (Siku na saa hazitafahamika, lakini tunaweza kujua kuwa ujio wa Mara ya Pili u “karibu.”)
-
- Soma Luka 21:29-32. Hii ni habari mfanano ya Luka kuhusiana na maelezo ya mtini. Anabainisha kipindi kipi? (Kwamba tunapoona ishara katika bahari na mbinguni, “kizazi hicho hakitapita hata hayo yote yatimie.” Hii inasaidia kuweka ukomo wa juu kwenye muda wa ujio wa Mara ya Pili.)
-
- Soma Luka 21:33. Tunaweza kuwa na uhakika kiasi gani kuhusiana na huu unabii wa Yesu? (Anatupatia hakikisho kuu.)
- Ujio wa Mara ya Pili
-
- Soma Mathayo 24:27, Mathayo 24:30 na Luka 21:27. Kipimo cha asidi kwa ajili ya kutambua ujio wa kweli wa Yesu wa Mara ya Pili ni kipi? (Ujio wa Yesu Mara ya Pili utawajia! Hatuhitaji uthibitisho wowote kutoka kwa mtu yeyote, tutamwona Yesu sisi wenyewe – na wote watamwona Yesu kwa wakati mmoja.)
-
- Soma Luka 21:34-35. Tunapaswa kufanya nini ili kujiweka tayari?
- Ujumbe
-
- Hapo kabla tuliangalia Ufunuo 14:7 kwa sababu ujumbe ule unaendana na uthibitisho mkubwa wa kisayansi wa Mungu Muumbaji. Unadhani malaika wanatoa ujumbe huu au hili ni jambo ambalo tunatakiwa kulitoa?
-
- Soma Ufunuo 14:8. Kuna tatizo gani kwa Babeli? (Inatangaza na kushadadia uasherati.)
-
-
- Mama kwa mara Mungu anazungumza kwenye Biblia kuhusu watu wake kutokuwa waaminifu kwake, na kulinganisha kitendo hicho na uzinzi. Angalia Yeremia 3:6-9. Nadhani hiyo ni moja ya maana zake. Unadhani kifungu hiki kinapaswa kusomwa kwa mapana zaidi? (Tunaona ongezeko la idadi ya wale wanaomkataa Mungu kabisa. Na, tunaona ongezeko la wale wanaopotosha kanuni za ngono kama zilivyoelezewa kwenye Biblia.)
-
-
-
- Kifungu kinamaanisha nini kinaposema kuwa mtangazaji na mhimizaji wa huu uzinifu “ameanguka?” (Watakatifu wameshinda, adui yao ameshindwa.)
-
-
- Soma Ufunuo 14:9-11. Je, hii ni taswira ya jahannamu kwa wale wanaopokea alama ya mnyama? (Ni vigumu kudhania kuwa hicho ndicho kinachoelezewa kwa sababu hiki kinatokea “mbele ya [malaika na Yesu].” Je, Yesu na malaika watawaangalia wapotevu wakiwa wanateswa milele?
-
-
- Unadhani kauli ya kwamba “hawana raha mchana wala usiku” inamaanisha nini? (Mfululizo wetu wote wa masomo haya umekuwa ukizungumzia juu ya kuingia kwenye pumziko ambalo Yesu ametupatia. Wamelikataa pumziko hili.)
-
-
- Soma Ufunuo 14:12. Watu wenye alama wanalinganishwa na kundi hili. Kitu gani kinatukinga dhidi ya kupokea alama ya mnyama? (Imani ya Yesu na kuzishika amri zake.)
-
-
- Tunazishikaje amri na kuwa na imani ya Yesu? (Soma Warumi 8:1-4. Yesu aliishika sheria kikamilifu kwa niaba yetu. Tunalikubali hili kwa imani na kutembea kulingana na mwongozo wa Roho Mtakatifu.)
-
-
- Soma Ufunuo 14:13. Kifungu hiki kinasema nini kuhusu wenye haki na pumziko?
-
- Je, tunatakiwa hadi tufe ili kuwa na pumziko? (Hapana. Soma Wafilipi 4:6-7. Yesu anatupatia amani sasa hivi. Ametupatia maonyo kuhusu mambo yajayo ili tuweze kuwa na amani kuyahusu.)
-
- Rafiki, Yesu ametupatia habari za kina kuhusu jinsi ulimwengu utakavyoisha. Je, utamwamini kuhusu mustakabali wetu? Je, utapumzika kwa ujasiri kutokana na uelewa huo?
- Juma lijalo: Tutaanza mfululizo mpya kuhusu kitabu cha Kumbukumbu la Torati.