Somo la 3: Agano la Milele

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kumbukumbu la Torati 4-5 & 26
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
4
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Agano la Milele

(Kumbukumbu la Torati 4-5 & 26)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kwa haraka haraka, utakumbuka kwamba tulijifunza, katika masomo mawili ya kwanza, kwamba Musa alikuwa anatoa hotuba ya kuagana na watu waliokuwa na historia ya kutomwamini Mungu. Jambo hilo linaweza kutatuliwaje? Musa anaweza kusema nini ili kuwasaidia watu wa Mungu kumwamini zaidi? Kwa kuzingatia lengo hilo, hebu tuendelee na safari yetu kupitia kitabu cha Kumbukumbu la Torati!

  1.    Kutenda Jambo kwa Usahihi (Kupatia)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:1. Mungu anawataka watu wafanye mambo gani mawili? (1. Kusikiliza na kutii. 2. Kwenda na kumiliki kile ambacho Mungu amewapa.)
      1.    Musa anatoa sababu gani za watu kuwa wasikivu na watiifu? (Ili wapate kuishi.)
        1.    Neno la Kiebrania la kuishi halimaanishi tu kuwa hai, linamaanisha kuishi vizuri. Kustawi. Kuhuishwa (revived.) Hilo linazungumzia nini kuhusu uhusiano kati ya ubora wa maisha yako na utiifu wako? (Nia yetu ya kutii haipaswi kuwa ni ili twende mbinguni, bali inapaswa kuwa ni kuishi maisha mazuri ambayo Mungu anatuwazia. Aina hiyo ya maisha humtukuza Mungu.)
      1.    Kwa nini Mungu anataka watu waimiliki Kaanani? (Ili kuyafanya maisha yao yawe mazuri. Ni zawadi wanayotakiwa kuifumbata.)
      1.    Je, hivi ndivyo tunavyopaswa kuzichukulia Amri Kumi leo – kwamba Mungu ametupatia zawadi ili kuyaboresha maisha yetu?
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:2. Mungu anaonya dhidi ya mambo mawili. Ni mambo gani hayo? (Kuongeza neno kwenye amri zake na kupunguza neno kutoka kwenye amri zake.)
      1.    Lipi kati ya haya ni tatizo kubwa unaloliona duniani leo? (Kupunguza. Wapagani wanasena hatuna haja ya kujali amri za Mungu. Wanadamu wa kisasa wanapaswa kuchagua njia ambayo ni bora kwa ajili yao.)
      1.    Lipi kati ya haya ni tatizo kubwa unaloliona kanisani leo? (Kuongeza neno kwenye amri za Mungu.)
    1.    Soma Mwanzo 3:2-3. Eva anajibu swali la Shetani kuhusu kile ambacho yeye (na Adamu) hawapaswi kukitenda. Je, anakiuka Kumbukumbu la Torati 4:2? (Ndiyo. Hakuna mahala palipoandikwa kuwa aliambiwa asiguse tunda.)
    1.    Soma Mwanzo 3:6. Eva alifanya nini kabla hajala tunda? (Aliligusa.)
      1.    Jiweke kwenye nafasi yake. Kuna athari gani kwake kuligusa tunda pasipo jambo baya kumtokea? (Ilimtia moyo kula tunda. Ilimfanya Shetani kuaminika.)
      1.    Mara nyingi Wakristo wanaamini kuwa hakuna madhara kutunga kanuni “za kulinda” ili kuwasaidia vijana kuepuka kukiuka kanuni halisi. Je, Mungu anadhani kuwa hakuna madhara? (Kwa dhahiri hapana, kwa sababu Mungu anakataza kuongeza neno kwenye kanuni. Mungu hawazuii viongozi wa vijana (na wengineo) wasiseme kuwa wanadhani kwa kuacha mambo fulani-fulani ni jambo jema. Tatizo linatokea pale ambapo kwa uongo kiongozi anasema kuwa kiuhalisia jambo jema ni dhambi.)
      1.    Kwa nini Musa azungumzie kuhusu kutoongeza neno kwenye amri za Mungu kwenye ujumbe unaopaswa kuwasaidia watu kumtumaini Mungu vizuri zaidi? (Kuongeza amri ambazo Mungu hakuzidhiinisha husababisha kutotumaini.)
  1.   Mungu wa Papo Hapo
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:7. Je, umewahi kutafakari suala hili la kumfikia Mungu? Unapata ugumu kiasi gani kuwa na mazungumzo na mtu ambaye ni kiongozi wa juu serikalini? Vipi kuhusu kiongozi wa juu kanisani? (Mungu yu juu ya maafisa wote, na bado anafikika mara moja.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:8. Ni jambo gani jingine lililo jema kuhusu mfumo wa serikali ya Mungu? (Sheria zake zinatoa cheti chake chenyewe cha ustahili. Matokeo yake ni kuwepo kwa watu wema na si watu wabaya. Matokeo yake ni maisha bora, si maisha mabaya kupindukia.)
  1. Mungu wa Pekee
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:23. Agano linahusianaje na “sanamu ya kuchonga?” (Utakumbuka kuwa katika kitabu cha Kutoka 32:1-4, wakati bado Musa akiwa Mlima Sinai, watu pamoja na Haruni walitengeneza ndama wa dhahabu!)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:15-16 na Kumbukumbu la Torati 4:19. Unaelezeaje sehemu hii ya agano na Mungu? (Kutotumamini jambo jingine lolote lile.)
      1.    Tatizo la msingi ni lipi kwa mujibu wa Kumbukumbu la Torati 4:19? (Kuviinamia na kuvitumikia.)
    1.    Soma Kutoka 32:7-8. Tatizo ni lipi katika kiini cha kuabudu sanamu? (Watu walihusisha uwezo na baraka za Mungu na sanamu.)
      1.    Hili linahusianaje na kutumaini/kuamini?
      1.    Ninawasikia watu wakisema kuwa nyumba ya mtu au gari lake ndivyo mungu wake. Je, hilo linaweza kuwa kweli? (Ni hadi pale mtu huyo anapoweka tumaini la kiungu kwenye vitu hivyo.)
        1.    Vipi kuhusu fedha? Je, inaweza kuwa kijimungu? (Hii inaingia karibu zaidi na tatizo. Kama mtu anatumaini fedha zake kumlinda na kumsaidia, basi fedha inafanya kazi kama kijimungu katika kutoa ulinzi.)
        1.    Je, watu wanaabudu fedha – sehemu ya pili ya katazo?
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 4:32. Mungu anatoa madai gani kwamba tunapaswa kumtumaini? (Anauliza kama Mungu mwingine yeyote yule anaweza kuwaumba wanadamu.)
      1.    Hili linazungumzia nini kuhusu Wakristo wanaokuza na kutangaza nadharia ya uibukaji na mianzo (origins)? Je, wana mungu mwingine?
  1.   Mungu wa Agano
    1.    Tunapozifikiria Amri Kumi, tunafikiria kitabu cha Kutoka 20. Katika Kumbukumbu la Torati 5:6-21 Mungu anazitaja upya Amri Kumi. Soma dibaji ya huu utajaji upya wa Amri Kumi unaopatikana katika Kumbukumbu la Torati 5:1-3. Musa anaziitaje Amri Kumi? (Anaziita “agano nasi katika Horebu.”)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 5:22. Kwa nini Musa anabainisha kuwa Mungu “hakuongeza neno” kwenye “mbao mbili za mawe?” (Anasisitiza ujumbe uliotolewa katika Kumbukumbu la Torati 4:2.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 5:28-29. Mungu anasema kuwa manufaa ya kuzishika amri zake ni yepi? (Maisha ya watu yatakuwa mazuri.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 5:33. Mungu anatoa husianisho gani katika kuzishika Amri Kumi na wokovu? (Mungu hatoi husianisho kama hilo hapa. Anahusianisha tu ushikaji wa amri na maisha mazuri na marefu hapa duniani.)
      1.    Ikiwa agano hili, Amri Kumi, linahusu utii na maisha mazuri ya hapa duniani, wanadamu walifikiaje kulifanya lihusu wokovu?
      1.    Ikiwa kuzishika amri hutupatia wokovu, hilo linazungumzia nini kuhusu kumtumaini Mungu dhidi ya uabudu sanamu? (Kama tunaamini kuwa ushikaji wetu wa amri hutupatia wokovu, basi tumaanini kile tulichokifanya na si kile alichokifanya Mungu. Kutumaini kazi za mikono yetu kwa ajili ya hatima yetu ya milele ndio msingi wa uabudu sanamu. Ni tofauti kidogo na wapagani wanaojenga hoja kuwa wanapata kusema kilicho sahihi na kisicho sahihi.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 26:16-19. Kwa kuwa kimsingi agano ni mkataba, Mungu anawataka watu wake watoe ahadi gani? (Utiifu kwa moyo wa dhati. Tumaini.)
    1.    Angalia tena Kumbukumbu la Torati 26:19.  Mungu anatoa ahadi gani kwa wale wanaomtumaini na kumtii? (Atakutukuza. Atakufanya uwe maarufu. Utasifiwa. Utatukuzwa juu ya watu wengine wote. Utakuwa na uhusiano maalumu na Mungu.)
      1.    Je, hii inahusika kwa taifa la Israeli pekee, au hii pia ni ahadi kwa mtu mmoja mmoja?
      1.    Je, mataifa mengine yanaweza kuzifuata Amri Kumi za Mungu na kutarajia mafanikio kama hayo?
    1.    Rafiki, ninadhani hotuba ya Musa ya kuagana inatuelekeza kumwamini na kumtii Mungu. Je, unapenda maisha bora? Je, unapenda watu wakusifu na kukutamania? Kwa nini usifanye uamuzi, sasa hivi, kwamba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu utazitii amri za Mungu na kupuuzia amri za wanadamu?
  1.    Juma lijalo: Kumpenda Bwana Mungu Wako.