Somo la 4: Kumpenda Bwana Mungu Wako
Somo la 4: Kumpenda Bwana Mungu Wako
(Kumbukumbu la Torati 6, Waefeso 2)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, huwa unampenda mtu kirahisi? Je, utakuwa na mjibizo (react) gani kwenye amri ya kumpenda mtu? Upendo ni jambo gumu ambalo kwa ujumla linahitaji muda kulifanyia kazi! Kichwa cha somo letu juma hili kinatoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 6:5 kinachotuelekeza kumpenda Mungu kwa “moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.” Kwa mantiki unaweza kuuliza, “Inawezekanaje kwetu sisi kufanya hivyo?” Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone jinsi hilo linavyowezekana.
- Kufafanua Upendo Kwa Mungu
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 6:5 na Mathayo 22:37-38. Tunapaswa kuhitimisha nini pale ambapo Agano la Kale na Agano Jipya yana maelekezo yanayokaribia kufanana kabisa?
-
-
- Inamaanisha nini kumpenda Mungu “kwa moyo wako wote?”
-
-
-
-
- Kama ningekuambia kuwa moyo unachukuliwa kama kiini cha hisia za mwanadamu, je, hilo litakuwa la msaada? (Ninadhani linasaidia. Hii inatuambia kuwa na upendo wenye hisia kamili kwa Mungu.)
-
-
-
-
- Inamaanisha nini kumpenda Mungu “kwa roho yako yote?”
-
-
-
-
- Kama ningekuambia kuwa roho inachukuliwa kama kiini cha sifa na tabia ya kibinadamu, je, hilo litakuwa la msaada? (Ninadhani ni la msaada kwa sababu linaashiria kuwa lazima upendo kwa Mungu uteke hisia zako.)
-
-
-
-
- Inamaanisha nini kumpenda Mungu “kwa nguvu zako zote?” (Hii huuingiza mwili wa binadamu kwenye amri.)
-
-
- Soma Marko 12:30. Marko anaongezea nini katika hili? (Marko anaongezea “kwa nguvu zako zote.” Marko anajumuisha kauli ya Mathayo 22:37 ya “akili,” na kauli ya Kumbukumbu la Torati 6:5 ya “nguvu” pale alipotaja nguvu. Hivyo, anaonyesha kuwa hakuna mgogoro kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, hakuna hata tofauti ndogo.)
-
-
- Ukiangalia vigezo hivi vinne, moyo, roho, akili na nguvu, je, itakuwa haki kusema kuwa huu ni wito wa kujitoa kamili katika hisia zako, akili yako, sifa na tabia zako, na juhudi zako kwa kutumia nguvu zako?
-
-
-
-
- Je, unaweza huku kujitoa kamili kwa kuamua tu kufanya hivyo?
-
-
-
-
-
- Ikiwa sivyo, tunafanyaje ili jambo hili liwe na uhalisia?
-
-
- Mpango wa Kwanza wa Upendo – Wewe Tenda Tu
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 6:6-7. Hii inatufundisha nini kuhusu jinsi ya kujitoa kuwa na upendo kamili kwa Mungu kuwa jambo halisi? (Anza kuwafundisha watoto habari za Mungu tangu wakiwa wadogo. Tumia muda mwingi kufanya hivyo.)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 6:8-9. Hii inatufundisha nini kuhusu jinsi ya kujitoa kuwa na upendo kamili kwa Mungu kuwa jambo halisi? (Kuwa na ukumbusho wa mara kwa mara wa uhusiano wako na Mungu.)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 6:10-12. Hii inatufundisha nini kuhusu jinsi ya kujitoa kuwa na upendo kamili kwa Mungu kuwa jambo halisi? (Mungu anapotubariki, tunapaswa kuwa na shukurani. Lazima tuyahusishe mambo mazuri na Mungu.)
-
- Hadi kufikia hapa utakuwa unajiuliza, “Ni kwa jinsi gani kwa kutenda mambo kunabadili moyo wangu?” Je, una jibu kwa swali hilo? (Ninadhani tunabadili mitazamo yetu mara zote kwa kile tunachokitenda. Ulaji ni mfano mzuri sana. Kwa kula vitu fulani nyakati fulani unaweza kubadili wakati gani una njaa na ladha gani unapendelea.)
-
- Soma Malaki 3:10. Je hili ni jambo la “kutenda” kabisa: unatoa zaka yako na kupata baraka kubwa kabisa? (Ndiyo. Hii inaandikwa kama shauri la biashara. Hakuna haja ya hisia yoyote.)
-
- Soma 2 Wakorintho 9:7. Je, kuna mtu ameacha mazingaombwe na sasa watu katika Agano Jipya wanatoa kwa moyo wa ukunjufu? Hawalazimishwi? (Kwa mara nyingine, nadhani hii inaonyesha mwendelezo wa asili. Ulitii tu uliposoma kitabu cha Malaki, lakini matokeo yalikufanya ufanye uamuzi wa kutoa kwa moyo wa ukunjufu tena kwa kujitolea.)
- Mpango wa Pili wa Upendo – Kuvunjika Moyo Wako
-
- Soma Waefeso 2:1-2. Utakuwa na mjibizo (reaction) gani ukitambua kuwa utanyongwa katika kipindicha juma moja? Vipi kama ukitambua kuwa utakufa kutokana na ugonjwa wa saratani kabla ya mwisho wa mwaka? (Haya yatakuwa mambo ya kutisha kuyafahamu. Litakuwa jambo la kukatisha tamaa sana.)
-
-
- Kifungu hiki kinatuambia nini kuhusu kifo chetu kinachokaribia? (Kinazungumza nasi. “Tumekufa katika ... makosa na dhambi.”)
-
-
- Soma Waefeso 2:3. Je, ni Shetani ambaye tunapaswa kuwa na wasiwasi naye linapokuja suala la dhambi? (Sio jambo la msingi! Tunapaswa kuwa na wasiwasi juu yetu. “Tamaa za miili yetu na nia zetu” ndivyo hutufanya kwa asili kuwa “wana wa kuasi.”)
-
- Soma Waefeso 2:4-5. Je, bado hatima yetu ni kifo? (Hapana. Mungu alitufanya kuwa hai.)
-
-
- Kwa sababu gani? (Kwa sababu anatupenda.)
-
-
-
- Alitufanyaje kuwa hai? (Alituokoa kwa neema kwa njia ya Yesu Kristo.)
-
-
- Soma Waefeso 2:6. Ni jambo gani jingine ambalo Mungu ametutendea kwa njia ya Yesu? (Ametuketisha “katika ulimwengu wa roho.”)
-
- Soma Waefeso 2:7. Mungu ana mpango gani nawe kwa siku zako zijazo? (Atatuonyesha “wingi wa neema yake upitao kiasi.” Atakuwa mwema kwetu.)
-
- Soma Waefeso 2:8. Je, hili ni jambo la “kutenda?” (Hapana! Kifungu hiki kinatuambia kuwa “haikutokana na nafsi zenu.” Bali, ni “kipawa cha Mungu.”)
-
-
- Sasa, hebu turejee nyuma na tuangalie vile vifungu katika Kumbukumbu la Torati nilivyoashiria kuwa vinatuambia kufanya hivyo. Je, huo si uelewa sahihi wa vifungu hivyo?
-
-
-
- Vifungu tulivyovisoma hivi punde kwenye kitabu cha Waefeso vinatufundisha kuwa njia ya kumpenda Mungu kikamilifu ni ipi? (Sidhani kama “fanya hivyo tu” katika Kumbukumbu la Torati inatuelekeza kwenye taswira kamili ya upendo ambao Mungu anautaka. Bali, ninadhani hiyo ni njia ya mtu anayeanza. Tunaingia kwenye taswira kamili ya upendo katika kujibu upendo kamili ambao Mungu ametuonyesha. Ametukinga dhidi ya kifo fulani. Amebadili (substituted) maisha yaliyojaa utajiri na wema mbinguni – na aliyatenda yote hayo kama zawadi. Hilo linapaswa kubadili moyo wako!)
-
-
- Soma Waefeso 2:9. Hii inatuambia nini kuhusu njia ya matendo? (Haitupeleki pale tunapohitaji kuwepo.)
-
-
- Kuna kasoro gani na njia hiyo? Kwa nini njia hiyo inakataliwa? (Tutajivunia matendo yetu. Tutajisifia ukuu wetu.)
-
-
- Soma Waefeso 2:10. Hebu subiri kidogo. Sasa hii inatuambia kuwa Mungu alituumba kwa ajili ya “matendo mema” na kwamba “tunapaswa kuenenda nayo.” Matendo yalirejeshwaje kwenye taswira? (Mungu alituumba upya. Alituokoa kutoka kwenye mauti ya milele. Uelewa huo unabadili mioyo yetu, roho zetu, na akili zetu. Inatufanya tuchukue uamuzi wa kutumia miili yetu kwa ajili ya matendo mema.)
-
- Hebu tupitie Kumbukumbu la Torati kidogo. Soma Kumbukumbu la Torati 5:10. Tabia zipi zinafanana kwa watu wa Mungu? (Wanampenda Mungu na kuzishika amri zake. Moyo wa upendo kwa Mungu unatutia moyo kuzishika amri zake.)
-
-
- Je, hili ni tendo tu la upendo wa shukurani kwa upande wetu? (Hapana. Mahala fulani tunapata wazo kwamba utii ulikuwa jambo hasi. Mungu alitupatia amri zake ili kuyafanya maisha yetu yawe mazuri. Tunapouelewa upendo wake vizuri, tutaelewa kwa nini alitupatia mwongozo wa maisha.)
-
-
- Soma Waefeso 3:14-16. Jambo la msingi ni lipi tunaposogea kutoka kwenye kufanya uamuzi wa kupenda na kujongea kwenye matendo mema? (Roho Mtakatifu anatupatia nguvu na uwezo.)
-
- Soma 1 Yohana 4:19. Je, huu ni ufupisho sahihi wa hamasa yetu ya kuwa na huo upendo kamili wa Mungu ambao tumeujadili? (Huu ndio mpango wenyewe kwa ufupi.)
-
- Rafiki, je, leo utaanza safari ya upendo kamili kwa Mungu? Kwa nini usianze kwa kutenda tu mambo ambayo anayaamuru? Kwa nini usitafakari kile alichokutendea wewe na wale wote uwapendao? Ukifanya hivyo, utampenda kwa sababu alikupenda kwanza.
- Juma lijalo: Mgeni Katika Malangoni Yako.