Utakatifu wa Mungu
(1 Petro 1, Mwanzo 2, Ayubu 42, Luka 5)
Swahili
Year:
2012
Quarter:
1
Lesson Number:
5
Utangulizi: Biblia inatuambia kwa kurudia rudia kuwa Mungu ni mtakatifu. Je, hiyo inamaanisha nini? Hili sio suala linalomaanisha kufurahisha akili zetu tu, kwa sababu Mungu anatuamuru kwenye Agano la Kale na Agano Jipya la Biblia kuwa tuwe watakatifu kama jisi Mungu alivyo mtakatifu. (1 Petro 1:15-16; Mambo ya Walawi 11:44.) Kama hatuelewi kile kinachomaanishwa kwa Mungu kuwa mtakatifu, hatuwezi kuelewa lengo la muhimu maishani mwetu. Hetu tuone tunavyoweza kulibaini hili kwa mara nyingine tena kwa kuzama kwenye somo letu la Biblia!
- Wakati (Muda) Mtakatifu
- Soma Mwanzo 2:2-3. Hii inatuambia kuwa Mungu “aliifanya” Sabato kuwa takatifu. Je, muktadha huu unapendekeza kuwa utakatifu unamaanisha nini? (Kwanza kabisa, utakatifu unatoka kwa Mungu. Yeye ndiye mwanzilishi wake. Pili, kuwa takatifu ni kuwa tofauti na siku nyinginezo. Utabaini kuwa utakatifu na mibaraka vinaonekana kufanana. Siku takatifu ni siku iliyowekwa wakfu dhidi ya siku nyinginezo, siku maalum, siku iliyobarikiwa.)
- Soma Zaburi 86:8-10. Je, ni kipengele gani cha utakatifu wa Mungu kinachofanana na Sabato? (Mungu amewekwa wakfu. Hakuna mungu kama Bwana wetu. Yeye peke yake ndiye mkuu na mzuri ajabu.)
- Soma Kutoka 20:11. Je, uhusiano iliopo kati ya huu muda mtakatifu na Uumbaji ni upi? (Ni sherehe, ukumbusho wa uwezo wa ubunifu wa Mungu.)
- Kama haya mawazo kuhusu utakatifu wa Mungu pia yanahusika kwetu kwa namna fulani hivi, je, ni sehemu gani ya kitendawili cha utakatifu tunachoweza kukifahamu? (Utakatifu unatoka kwa Mungu pekee. Inamaanisha kuwa tumewekwa wakfu na kubarikiwa pia. Inamaanisha kuwa maisha yetu yanapaswa kuwa kama usherehekeaji wa uwezo wa Mungu na ubunifu wa Mungu.)
- Soma 1 Samweli 2:2. Tunapozama kwenye mjadala kuhusiana na utakatifu wa Mungu na lengo la utakatifu wetu, je, hii inatufundisha kitu gani cha muhimu? (Hatuwezi kufikia kiwango cha Mungu cha utakatifu. Hakuna hata mtu mmoja aliye kama yeye! Habari njema ni kwamba hatupaswi kukata tamaa pale ambapo utakatifu wetu mara kwa mara unaonekana kuwa kwenye matatizo.)
- Soma Kutoka 20:8-10. Je, ni kwa namna gani kuacha kufanya kazi kuna cha kujihusianisha na muda mtakatifu? (Ni wakati wa kujielekeza kwenye kile alichokiumba Mungu, sio vile tunavyovifanya. Hii inaonyesha kuwa utakatifu unatoka kwa Mungu, sio kwetu. Hatutengenezi/hatufanyi muda mtakatifu kwa kufanya jambo fulani.)
- Je, ni kipande gani kingine cha kitendawili kinaimarishwa na suala hili kuhusiana na sisi kuwa watakatifu? (Hatuwezi kujifanya wenyewe kuwa watakatifu.)
- Akili Takatifu
- Soma 1 Petro 1:13-16. Je, tumefanya makosa? Petro anatuambia tuwe watakatifu katika yote tuyatendayo. Je, hiyo inamaanisha kuwa tunaweza kuufanya/ku-uumba utakatifu?
- Angalia tena 1 Petro 1:13. Je, ni “tendo” gani linafanyika hapa? (Hakuna tendo lolote. Petro anatuambia tu kuwa tujielekeze kwenye zawadi ya neema ya Mungu. Zingatia/kuwa msikivu. Neema (utakatifu?) tunayoipokea “tunapewa,” hatuipati kwa juhudi zetu.)
- Vipi kuhusu 1 Petro 1:14, ambapo tunaambiwa kuwa “watiifu?” (Tunapojielekeza kwa Bwana wetu, tunajifunza zaidi kuhusiana na mapenzi yake. Kimsingi Petro anasema, “Mmejifunza, kwa hiyo msiishi kufuatana na matamanio yenu maovu.”)
- Soma 1 Petro 1:17-19. Je, matendo ni sehemu ya kuishi maisha matakaifu? (Ndiyo. Wakati ambapo hatuwezi kujifanya wenyewe kuwa watakatifu, Mungu anatutaraji tuishi maisha yanayoendana na kuwa watakatifu. Lengo la kwanza ni kuzingatia mapenzi ya Mungu. “Je, ninaweza kufanya jambo gani hivi leo ili kuuendeleza Ufalme wa Mungu, badala ya kukiendeleza chanzo cha dhambi?”)
- Je, kuishi kama “wageni” na “kwa hofu yenye utii” kuna nini cha kujihusisha na lengo letu la utakatifu? (Hatutakiwi kuridhika sana na maisha ya hapa. Sisi sio sehemu ya hii dunia. Sisi ni sehemu ya Ufalme wa Mungu. Kwa hiyo, “tunamhofu” (ikimaabisha heshima, inayohusiana na Mungu). Hatujihusishi na dunia ila kuuendeleza Ufalme wa Mungu.)
- Je, ni tofauti gani iliyopo ya kwamba tunafidiwa na kafara ya Yesu mwenyewe, badala ya malipo ya fedha? (Inafanya jinsi tunavyoishi maisha yetu yawe ya mtu binafsi. Yesu alilipa gharama kwa ajili ya dhambi zetu kwa kuyatoa maisha yake. Haliwezi kuwa suala la binafsi zaidi ya hapo. Tunahitajika kulichukua lengo la utakatifu na kulifanya kuwa suala la mtu binafsi.)
- Soma 1 Petro 1:20-21. Je, ni hoja gani unayoiona hapa kuhusiana na neema? (“Tunaamini katika Mungu” kupitia “kwake” – kupitia kwa kile Yesu alichotutendea pale msalabani na katika ufufuo wake.)
- Soma 1 Petro 1:22. Kwa wazi kabisa hii inaonyesha kuwa kile ambacho nimekuwa nikikifundisha ni makosa, sawa? Kinasema kwamba “tumejitakasa roho zetu kwa kuitii kweli.” Je, ni nini kinachoweza kuwa wazi zaidi ya hicho?
- Angalia sehemu iliyosalia ya hili fungu. Je, unaweza kusaga meno yako na kumpenda mtu ambaye unamwona kabisa kuwa hapendeki? Vipi kuhusu “upendo wa dhati” kutoka moyoni? (Sote tunafahamu kuwa upendo wa dhati wa “ndugu” unatoka tu kwenye moyo uliobadilishwa na Mungu. Moyo unaotambua kuwa Mungu alikufa kifo cha kutisha kwa ajili yetu, ni moyo unaojibu kwa shukrani na upendo. Upendo wa ndugu ni mwitikio kwa Mungu. Kwa hiyo Mungu, na sio mapenzi ya mwanadamu, ndicho chanzo cha upendo. Hata hivyo, ni kweli kwamba “tabia” ya utii (kinyume na “tabia” ya kutokutii) inasaidia katika njia ya kuuelekea utukufu.)
- . Utukufu Linganishi
- Sehemu kubwa ya kitabu cha Ayubu kinajumuisha maneno ya Ayubu akijitangazia kutokua na hatia ilhali marafiki zake wanasisitiza kuwa anaadhibiwa kutokana na dhambi zake. Suala la kuvutia linakuja pale ambapo Ayubu anatangaza kuwa anataka awe na Mungu chumbani na amfanye ajibu baadhi ya maswali yake kuhusu usawa na haki. Katika kitabu cha Ayubu sura za 40 & 41 Mungu anamtokea Ayubu na anamwambia kuwa watakuwa na “uendeshaji wa mashtaka,” lakini hali itakuwa ni kwamba Ayubu ndiye atakayekuwa akijibu maswali. Hebu tusome Ayubu 42:1-3. Je, jibu la awali la Ayubu kwa Mungu ni lipi? (Nilijibu nikiwa mpumbavu. Sikuelewa uwezo na utukufu wa Mungu.)
- Soma Ayubu 42:4-6. Je, utukufu na utakatifu wa Mungu vinatenda kitu gani kwa Ayubu? (Kutubu kwa unyenyekevu. Uelewa wa kwamba hatupo kwenye nafasi ya kuhoji haki na asili ya Mungu.)
- Je, hii inakubalianaje na mjadala wetu wa awali kuhusiana na kile kinachomaanishwa kwa kuwa mtakatifu? (Kuwa mtakatifu ni “kuwekwa wakfu.” Mungu “amewekwa wakfu” kutoka kwetu. Kamwe hatuwezi kuwa na tumaini la kuweza kuufikia utakatifu wa Mungu. Tunapokea zawadi ya utakatifu anayotupatia na kudhamiria kutembea kwenye njia inayotuelekeza kwenye utakatifu. Kutembea katika njia hiyo hakutegemeani na suala la kama tunaelewa matatizo yote maishani. Kile tunachokielewa ni kwamba Mungu wetu ni mkuu, mwenye upendo na mtakatifu.)
- Soma Luka 5:1-5. Hebu jiweke kwenye nafasi ya Petro. Je, mawazo yako kuhusu amri ya Yesu ni yapi? (Walikuwa wamekwisha safisha zana zao na vifaa vyao. Yesu anawataka wachafue zana zao ili kwamba waje waifanye kazi hiyo tena. Wanavua samaki usiku, na walikuwa wametia juhudi kubwa sana usiku kucha. Yesu anawaambia kufanya kazi ya ziada. Wao ni wataalam wa uvuvi, Yesu ni mhubiri. Wao wana maarifa makubwa kuhusiana na suala hili.)
- Soma Luka 5:6-8. Kwa nini hii inaonyesha kuwa Petro ni mdhambi? Alimtii Yesu? (Petro anatambua kuwa yeye sio mwerevu ambaye anajiendekeza kwa Yesu tu. Anatambua kuwa yupo mbele ya nguvu ya ulimwengu. Kitu kitakatifu kimekutana na kisicho kitakatifu na kitiifu, na utakatifu unahitaji utenganifu!)
- Soma Luka 5:10 (sehemu ya mwisho). Je, kwa nini Yesu asiogope? (Kwa sababu yupo kwenye utume wake kuwapatanisha Mungu Mtakatifu na wanadamu wadhambi. Safari yetu ya kuuelekea utakatifu ni ya “kuwavua watu,” kuuendeleza Ufalme wa Mungu.)
- Rafiki, je, utaufanya utakatifu kuwa lengo lako hivi leo? Je, malengo, maazimio, matamanio na matendo yako, yatajielekeza katika kuuendeleza Ufalme wa Mungu? Je, utafanya uchaguzi huo sasa hivi?
- Juma lijalo: Mungu Mtoaji wa Sheria.