Somo la 8: Chagua Uzima

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kumbukumbu la Torati 30, Warumi 6, Yakobo 1, Mwanzo 2 & 3
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
4
Lesson Number: 
8

Somo la 8: Chagua Uzima

(Kumbukumbu la Torati 30, Warumi 6, Yakobo 1, Mwanzo 2 & 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Hivi karibuni George Barna amechapisha utafiti wa kizazi cha Milenia. Hawa ni watu walio katika umri wa miaka ya ishirini na thelathini. Matokeo yanakatisha tamaa sana. Asilimia 35 tu ndio wanaodai kumwamini Mungu wa Biblia. Asilimia 41 hawajui kama Mungu yupo, hawajali kama yupo, au hawaamini kwamba yupo. Asilimia 74 wanaamini kuwa dini zote zina thamani sawa. Kati ya hao wenye umri kati ya miaka 18-24, asilimia 2 pekee ndio wanaoamini katika mtazamo wa Biblia juu ya ulimwengu! Cha kufurahisha, asilimia 5 pekee walisema kuwa maisha yao ni mazuri na hawana haja ya mabadiliko. Kama ungewauliza “kuchagua uzima,” je, utakuwa unazungumzia jambo lile lile? Huenda hapana. Tatizo kubwa ni kwamba vijana hawa wanaonekana kutokuwa na elimu ya Biblia (na huenda elimu ya mambo mengine mengi.) Hebu tuone kama Biblia ina msaada wowote katika kuwaelimisha watu juu ya suala la “kuchagua uzima.”

  1.    Kuzijua Amri
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 30:11-13. Ni rahisi kiasi gani kuzijua amri za Mungu? (Kifungu hiki kinasema kuwa sio vigumu. Amri za Mungu zinapatikana kwa wingi ili tusiwe na kisingizio cha kutozijua.)
      1.    Unadhani ni kwa nini vijana wa Kimarekani wako nyuma sana kwenye elimu inayohusu amri za Mungu? Unapendekeza tufanye nini ili tuwasaidie kuamini kuwa ni muhimu kuzijua amri za Mungu? (Kumbuka kwamba asilimia 5 pekee ya kizazi cha Milenia kinaamini kuwa maisha yao ni mazuri. Hoja ya kwamba kumtii Mungu huboresha maisha yako ni hoja ya muhimu.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 30:14. Ni kwa jinsi gani neno la Mungu li karibu yetu? Ni kwa jinsi gani li katika vinywa vyetu na katika mioyo yetu?
      1.    Je, hii inaweza kuwa kweli kwa kizazi cha Milenia? (Soma Warumi 10:6-8. Vizazi vya zamani vinatakiwa kufanya jambo hili kuwa la kweli kwa kutangaza neno la Mungu.)
  1.   Kuchagua Uzima
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 30:15. Jambo gani limewekwa mbele yetu linalomua kama tutaishi au tutakufa, kuwa wema au waovu?
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 30:16-18. Hii inajibuje swali la awali? (Amri za Mungu zinaleta utofauti. Tukizitii, “tunaishi na kuongezeka. Tusipozitii, “hatutaishi kwa muda mrefu” na “hakika tutaangamia.”)
      1.    Unapendekeza kuwa tuwaendeeje vijana na ukweli huu? (Vipo vitabu vya kila namna na watu walio na kanuni chache rahisi kwa ajili ya kuboresha maisha. Dhana ya kupokea mabadiliko muhimu machache kwa ajili ya kuboresha maisha yako ndio dhana ya sasa. Tunapaswa kuikumbatia dhana hiyo.)
      1.    Kitu gani kinaingilia kati kampeni kama hiyo? (Kutoelewa lengo la Amri Kumi. Hii ndio mada ninayoendelea kuisisitiza katika masomo haya. Mungu hakuwapatia wanadamu Amri Kumi ili kuhalalisha kutuua, alizitoa kwetu ili kuboresha maisha yetu. Kuhubiri kwamba amri hizo huboresha maisha, na wakati huo huo kuhubiri wokovu kwa njia ya Yesu pekee, husaidia kufanya ujumbe wa jumla kuwa bayana.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 30:19. Je, uchaguzi huu mmoja umewekwa mbele ya watu wote?
      1.    Watu wangapi hawaelewi kuwa wanafanya uamuzi huu?
    1.    Ongezea Kumbukumbu la Torati 30:20. Soma Kumbukumbu la Torati 30:19-20. Ni kitu gani hasa ambacho Mungu anakiahidi kwetu endapo tutatii na kung’ang’ania kwake? (Kwamba tutapata uzima sisi na uzao wetu. Tutaishi maisha marefu.)
      1.    Utaona kwamba “uzima” na “wingi wa siku” vinaonekana kuwa vitu viwili tofauti. Unahitimisha nini kutokana na hili? (Hii sio tu ahadi ya kuishi kwa muda mrefu, bali pia ni ahadi ya kuishi maisha mazuri. Pia ninaamini Mungu anafikiria uzima wa milele.)
      1.    Kifungu kinazungumzia kukaa katika nchi aliyopewa Ibrahimu. Je, hiyo inamaanisha kuwa ahadi hii si kwa ajili yetu? (Ilikuwa mahsusi kwa wale ambao Musa alikuwa anawaelezea, lakini pia haya ni maadili yasiyo na ukomo wa muda.)
    1.    Soma Warumi 6:15-16. Je, kuna mahali pa muafaka (middle ground) linapokuja suala la kuchagua uzima au mauti?
      1.    Utaona kwamba kifungu cha 16 kinaonekana kuzungumzia kuwa utii hujielekeza kwenye “haki” badala ya maisha mazuri tu. Una maoni gani? Je, nimekuwa nikikupotosha?
    1.    Soma Warumi 6:17-21. Vifungu hivi vinazungumzia fedheha, kifo, utakaso, na mwisho wa utakaso, uzima wa milele. Je, huu ni uthibitisho zaidi kwamba Amri Kumi hazikutolewa tu ili kuboresha maisha yetu? (Manufaa ya kuzishika Amri Kumi sio tu kwamba maisha yetu yanaboreshwa, bali pia tunakuwa watu bora. Tunafanana zaidi na Bwana wetu.)
    1.    Soma Warumi 6:22-23. Hii inazungumzia nini kuhusu kuupata uzima wa milele (au mauti ya milele)? (Inasema kuwa uzima wa milele ni “karama ya Mungu ... katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Hii inathibitisha kile nilichokuwa nikikihoji – uzima wa milele ni karama, haupatikani kutokana na utii wetu. Kutoipokea karama ndio sababu ya kuupoteza uzima wa milele. Hata hivyo, vifungu hivi vinaonesha kuwa utii kwa Mungu ni muhimu kwa ajili ya maisha bora kwetu, na kwa wale wanaotuzunguka.)
    1.    Soma Yakobo 1:23-24. Hii inaashiria kuiangalia sheria “kwa umakini.” Kitu gani kinapaswa kutokea kimantiki ikiwa tutaangalia kwa umakini? (Hatuondoki. Badala yake, kujifunza sheria kunatufanya tutambue kuwa tunatakiwa kufanya mabadiliko maishani mwetu.)
    1.    Soma Yakobo 1:25. Ni nini matokeo ya kujifunza sheria kwa umakini na kufanya mabadiliko tunayoona kuwa yanatakiwa kufanyika? (Kwa mara nyingine, inatuambia kuwa tutabarikiwa.)
  1. Miti Miwili
    1.    Soma Mwanzo 2:8-9. Miti gani miwili ipo “katikati ya bustani?” (Mti wa ujuzi wa mema na mabaya, na mti wa uzima.)
      1.    Kwa nini Mungu aweke miti miwili karibu-karibu?
    1.    Soma Mwanzo 3:22-24. Je, wanadamu waliumbwa ili waishi milele? (Inaonekana sivyo. Walitakiwa kuendelea kula matunda ya mti wa uzima ili waendelee kuishi.)
      1.    Soma Ufunuo 22:2. Tunaona nini katika Yerusalemu Mpya? (Mti mwingine wa uzima.)
        1.    Kwa nini uko pale? (Ili tuweze kuponywa na kuishi milele.)
    1.    Hebu tuzungumzie jambo hili. Kushindwa kwa Adamu na Eva kumtii Mungu kunatufundisha nini kwenye jambo dogo la kujizuia kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya? (Waliumbwa wakiwa wakamilifu. Hawakuwa na mwelekeo wa dhambi. Hawakukabiliana na jaribu gumu. Hawakujaribiwa nyakati zote wala hawakujaribiwa kwenye maeneo mengi. Nadhani fundisho ni kwamba tutakuwa wapumbavu kama tunadhani kuwa tunaweza kuishi bila kutenda dhambi. Yesu alitumwa ili kutuokoa kutokana na sababu hii hii.)
      1.    Unapata fundisho gani kutoka kwenye ukweli huu kwamba uchaguzi wa Adamu na Eva ulileta tofauti kubwa sana kwenye mustakabali wao wa siku zijazo?
      1.    Unapata fundisho gani kutoka kwenye ukweli kwamba uzima wa milele uligeukia kwenye kuendelea kula matunda ya mti mmoja wa busatani? (Haya yote ni suala la uchaguzi. Inathibitisha tena kuwa kufanya chaguzi sahihi, uamuzi unaoendana na Amri Kumi, una athari kubwa kwenye mustakabali wetu wa siku zijazo.)
      1.    Vijana wanakabiliana na vikwazo gani katika kujifunza mafundisho haya? (Hawaamini suala la Uumbaji. Hawamwamini Mungu wa Biblia.)
    1.    Rafiki, tunatakiwa kujichunguza kwanza. Je, tumedhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kufanya chaguzi sahihi? Je, tunashawishika kuamini kuwa hizi zinaleta utofauti katika ubora wa maisha yetu? Mara tunapoweka vipaumbele vyetu kwa usahihi, tunaweza kufanya nini ili kuwafundisha vijana juu ya umuhimu wa chaguzi hizi? Je, utatumia muda wako kutafakari maswali haya kuhusu kuchagua uzima?
  1.   Juma lijalo: Geuza Mioyo Yao.