Somo la 9: Geuza Mioyo Yao
Somo la 9: Geuza Mioyo Yao
(Kumbukumbu la Torati 4, Mathayo 3 & 4, Matendo 2 & 17, Warumi 1)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Inamaanisha nini “kutubu?” Hili ni jambo ambalo nimelifikiria kwa kina, lakini sikumbuki kuliandikia kwa umahsusi. Kama tunatakiwa “kutubu” dhambi mahsusi, je, hiyo sio hoja kama ile ya wokovu kwa njia ya matendo? Kama utashindwa kutubu, au ikiwa unakosa jambo la kulitubia, au hauko makini vya kutosha katika kutubu kwako, basi umepotea. Kama sitendi jambo fulani kwa usahihi, nimepotea! Hebu tuigeukie Biblia na tuone kile inachotufundisha kuhusu toba!
- Yesu na Toba
-
- Soma Mathayo 3:1-2. Yohana anamaanisha nini anaposema kuwa “Ufalme wa Mbinguni umekaribia?” (Anazungumzia kuhusu Yesu kuja duniani.)
-
-
- Ikiwa tuko sahihi kuhusu Yohana kusema kuwa Yesu anakuja, inaleta mantiki gani kwa Yohana kutoa wito kwa watu kutubu? Kwa nini asiseme, “Mjitayarishe?” “Mumtazame,” “Muwe makini?” Au, jambo linalofanana na hilo? (Kwa dhahiri Yohana hawaambii wasikilizaji wake kukiri dhambi zao. Bali, anawataka wawe tayari kwa ajili ya jambo jipya.)
-
-
- Soma Mathayo 4:17. Sasa Yesu anasema jambo lile lile kama alilolisema Yohana Mbatizaji – angalao wanakubaliana! Lakini, ni jambo gani hasa wanalokubaliana nalo? Je, Yesu anasema “tubuni” kwa sababu nipo hapa?
-
-
- Ikiwa ndivyo, unadhani wasikilizaji wake wanapaswa kutubu juu ya jambo gani? (Kwa mara nyingine, hili halionekani kushughulika na dhambi mahsusi. Yesu anawaambia wabadili fikra zao kwa sababu yupo hapa duniani. Wote wawili, yaani Yohana na Yesu wanasema kuwa hili ndilo jambo jipya litakalowafikirisha watu.)
-
-
- Soma Marko 1:14-15. Hapa tuna taarifa za kina zaidi. Badiliko gani linahusisha toba? (Kuiamini injili.)
-
-
- Ni imani gani wanayopaswa kuitubia? Wanaacha imani gani ili kuiamini injili? (Ifikirie ile hadhara. Waliamini katika mfumo wa kafara, mfumo wa hekalu. Kwa dhahiri hii haihusiani na dhambi mahsusi, bali inahusu namna mpya ya kuangalia mambo. Kwa umahsusi, sasa Mwanakondoo wa Mungu amekuja kutimiza ishara ya mfumo wa hekalu.)
-
-
- Soma Matendo 2:36-38. Hili ndilo hitimisho la hubiri la Petro siku ya Pentekoste. Hapa kutubu kunamaanisha nini? Kumbuka kwamba wengi wa wale waliokuwepo hawakuwa na sehemu katika mateso ya Yesu kwani walikuwa wamesafiri hadi Yerusalemu kwa ajili ya Pentekoste.
-
-
- Dhambi gani zinasamehewa hapa? (Ubatizo, kama tulivyojadili majuma mawili yaliyopita, ni njia ambayo tunaungana katika maisha makamilifu ya Yesu, kifo chake kwa ajili yetu, na ufufuo wake katika uzima wa milele. Petro anazungumzia kuhusu uelewa mpya wa jinsi ambavyo wanadamu wanabadilika kutoka kwenye mauti ya milele na kuingia kwenye uzima wa milele.)
-
-
- Soma Matendo 17:22-23. Paulo anafanya nini hapa? (Anapeleka injili kwa Wayunani/Wagiriki ambao kwa dhahiri hawajui jambo lolote kumhusu Yesu.)
-
- Soma Matendo 17:24-29. Jambo gani ni tofauti kumhusu Yesu ikilinganishwa na miungu ya Wayunani inayojulikana?
-
- Soma Matendo 17:30-31. Toba inamaanisha nini kwa watu hawa wa Athene? (Inamaanisha kujifunza taarifa mpya na kuachana na fikra zako za kale.)
-
- Hebu turejee nyuma kidogo na tutafakari njia zote ambazo tumeona toba imetumika pale inapohusiana na Yesu. Unaelewaje maana ya neno “toba?” (Ingawa dhambi inahusika, msamiati huo hauhusiani kivyovyote vile na dhambi mahsusi. Unahusiana kwa hali zote na kubadili namna ya kufikiri habari za Mungu na wokovu.)
- Kumbukumbu la Torati na Toba
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 4:25. Je, hawa ndio watu wanaopaswa kuwa na ufahamu mkubwa zaidi? Yaani, ni watu ambao kwa hali ya kawaida hawazielewi njia za Mungu? (Hapana. “Wamezeeka” katika mfumo uliopo.)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 4:26-28. Ni nini ulio mustakabali wa kugeuka na kuacha kumtumikia Mungu kwa makusudi na kujiingiza kwenye tabia za kipumbavu? (Mambo hayakuendei vizuri. Angalia jinsi Musa anavyoshughulika na kiwango cha upumbavu wa maamuzi haya. Unageuka na kuacha kumwabudu Mungu mkuu wa mbinguni na kuabudu kitu ulichokitengeneza ambacho hakiwezi kutekeleza mambo ya kawaida kabisa – kama vile kuona, kusikia, kula, na kunusa.)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 4:29-31. Je, lipo tumaini kwa watu wanaofanya maamuzi ya kipumbavu linapokuja suala la uhusiano wao na Mungu? (Ndiyo! Mungu atukuzwe!)
-
-
- Tumaini linageukia wapi? (Linamgeukia Mungu. Kumtafuta Mungu, kumchunguza, kumpata, na kumtii.)
-
-
-
-
- Utatumia neno gani kwa badiliko hili la mtazamo na matendo? (Vipi kuhusu “toba?” Unabadili mwelekeo wako wa maisha. Unaamua kwamba matendo ya kipumbavu hayakusaidii, na unaamua kumtumikia Mungu aliye hai.)
-
-
-
- Angalia tena Kumbukumbu la Torati 4:31. Utaelezeaje kwa ufupi ufafanuzi huu wa Mungu? (Yuko tayari wakati wote kukuchukua – Mungu wa rehema.)
-
- Itakuwa vyema kupitia kwa haraka haraka Kumbukumbu la Torati 28 & 29. Katika sura hizi Mungu anaelezea kwa kina manufaa ya kumfuata na hatari ya kufuata miungu mingine. Soma Kumbukumbu la Torati 30:1-3. Mungu anatafuta nini ndani yetu? (Anatutaka tumtii “kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.”)
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 30:9-10. Matokeo ya utii kwa Mungu ni yepi? (Mungu “atakufanya uwe na wingi wa uheri.”)
-
- Hebu turejee tena nyuma kidogo kwa ajili ya mjadala mdogo. Mungu anamfanya Musa aweke mbele yetu njia tofauti-tofauti za maisha. Mungu anajadili uwezekano kwamba katika hatua za awali tutafanya maamuzi yasiyo sahihi. Unadhani kutubu kunamaanisha nini katika muktadha huu? (Kuchagua njia sahihi kwa ajili ya maisha yetu.)
-
-
- Mantiki na vitu tuvipendavyo ni vya muhimu kiasi gani kwa namna ambayo Mungu anaweka mbele yetu chaguzi zetu? (Huu ni wito wa dhahiri wa kutumia mantiki nay ale tuyapendayo. Mungu anasema “Je, unataka kufanya chaguzi za kipumbavu? Je, unataka kuishi maisha mazuri? Acha kufanya maamuzi ya kipumbavu na anza kunichagua Mimi nawe utaishi maisha mazuri.)
-
- Matumizi Halisi Maishani
-
- Soma Warumi 1:15-16. Paulo anasema kuwa anahubiri nini? (Injili.)
-
-
- Sababu ya kuhubiri injili ni ipi? (Inaangazia namna ya wanadamu kuokolewa, kuishi maisha ya milele.)
-
-
- Soma Warumi 1:18-20. Adui wa injili ni nani? (Wasio na haki wanaoikandamiza kweli ya Mungu.)
-
- Soma Warumi 1:21-23. Matokeo ya kuukandamiza kweli ya Mungu ni yepi? (Wanadamu wanakuwa wapumbavu. Hawamtii Mungu, wanawatii ndege na wanyama.)
-
- Soma Warumi 1:24-27 na Warumi 1:29-32. Nini kinafuata baada ya kumkataa Mungu kama Muumbaji wetu, na kuacha kumtii na kumshukuru? (Dhambi za aina zote.)
-
- Hebu kwa mara nyingine turejee tena nyuma kidogo na tutafakari toba maana yake ni nini. Mjadala huu katika kitabu cha Warumi unatuambia nini kuhusu toba? (Toba si suala la kufuatilia dhambi zako na “kuzitubu.” Badala yake, toba inahusu kuigeukia imani kwa Mungu mkuu wa mbinguni na kuachana na mtazamo unaomkataa Mungu na kukubali mbadala wa kipumbavu.)
-
-
- Je, toba haihusiani kabisa na dhambi za mtu? (Hapana, kwa sababu Paulo anatuambia kwamba kuwa na ukweli usio sahihi, kuwa na mtazamo mbaya kuhusu Mungu unatuanzishia mtelezo wa kuingia dhambini.)
-
-
-
- Je, “mtelezo” wa Paulo (au kuingia dhambini) unaleta mantiki? Je, unawafahamu watu ambao ni wasengenyaji au wanaotamani ambao awali hawakuwa wasenge? Ikiwa ndivyo (sina hakika kama jibu ni “ndiyo,”), unaelezeaje kile anachokiandika Paulo? Au, hatuelewi tu sura hii ya kwanza ya kitabu cha Warumi? (Hii inaingia kwenye kiini cha kuikataa dhana ya kwamba toba inarejelea juhudi endelevu za kufuatilia na kutubu kila dhambi kama kigezo cha wokovu. Paulo anatuambia kuwa kama tukimkataa Mungu, basi katika hali ya kawaida mfululizo wa mambo ya kutisha utafuatia. Wakristo wasio wasenge/mabasha pia wanajihusisha kwenye dhambi zilizoorodheshwa. Paulo anasema kuwa anatamani, angalia Warumi 7:8.) Jibu la dhambi ni la kiulimwengu – hakikisha uko kwenye njia sahihi ya kumwamini na kumtumaini Mungu. Kama uko nje ya huo msitari, basi unatakiwa kutubu.)
-
-
- Soma Mathayo 6:12. Hii ni sehemu ya sala aliyoifundisha Yesu. Hii inazungumzia nini kuhusu kuomba msamaha? (Toba ni badiliko la mwelekeo wa fikra zako. Hata hivyo, bado tunapaswa kumwomba Yesu msamaha wa dhambi.)
-
- Rafiki, je, una taswira pana na sahihi ya kumwelewa Mungu? Ikiwa sivyo, basi tubu na umkiri Yesu na Muumbaji wako na Mwokozi wako. Kwa nini, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, usifanye hivyo sasa hivi?
- Juma lijalo: Kumbuka, Usisahau.